TIME ya Januari 12, 2004 |
Tishio hili haliko Tanzania peke yake bali liko ulimwenguni kote Hata hivyo viwango vya kuathirika huweza kutofautiana toka nchi moja na nyingine lakini haipo nchi iwezayo kudai iko salama na tishio la ugonjwa huu.
Ugonjwa huu hauna tiba ila zipo dawa za kumfanya mgonjwa kuishi kwa matumaini na kupunguza athari zitokanazo na ugonjwa huu.
Pamoja na dawa hizi wagonjwa wengi tunashindwa kufuata masharti ya kudhibiti kikamilifu athari zitokanazo na ugonjwa huu katika miili yetu.
HII NI KUTOKANA NA KUTOJUA ATHARI za ugonjwa huu kwetu PILI KUTOJUA NJIA SAHIHI ZA KUDHIBITI ATHARI HIZI.
Sasa hivi wagonjwa wa sukari tunadanganywa sana na watu kuhusu tiba na kupoteza maelfu ya pesa pasipo na mafanikio.Njia sahihi ni kutumia dawa za hospitali za kuzuia athari zitokanazo na ugonjwa huu toka kwa waganga wa mahospitali. Tiba mbadala sahihi haswa haswa ni vyakula na mazoezi kusaidia hizi hizi za mahospbinitalini katika kudhibiti athari zitokanazo na ugonjwa huu.
Dawa za hospitalini ziko katika makundi makuu matano.
1.Kwanza zipo za kuchochea kongosho kuzalisha isulin zaidi (Sulfonylureas).
2. Pili ni (Meglitinides) hizi nazo kama kundi la kwanza huishajiisha kongosho kuzalisha insulin
zaidi
3.Kundi la tatu ni (Biguanides) Hizi hulikataza ini kutoa sukari (glucose) nyingi na husisimua misuli
kutumia sukari zaidi kutoka katika damu.
4.Kundi la nne linaitwa (Thiazolidinediones) Hizi ni dawa za hivi karibuni tu ambazo huiwezesha
insulin kusukuma (gulucose) sukari na mafuta kuingia katika misuli kwenda kuzalisha nishati
mwilini.
5.Kundi la tano ni (Alpha -Glucosidase Inhibitors) hii hufannyia kazi kwenye utumbo mwembamba
kuzuia mikate na vyakula vya wanga kubadilishwa kuwa sukari (glucose)
Pili ni vema kujipima kiasi chako cha sukari katika damu ili kujua kupanda na kushuka kwa sukari katika mwili wako.
Dalili ziashiriazo kuwa na ugonjwa huu za awali ni hizi:
1.Kukojoa mara kwa mara hasa usiku.
2.Kuona kwa mawengewenge, Macho kupoteza uoni wake wa kawaida.
3.Kuwa na kiu kali isiyoisha.
4.Kuwa na njaa kali kama ya mtoto.
5.Kupoteza uzito kusiko kwa kawaida kwa kipindi kifupi.
6.Kuwa na vidonda visivyopona haraka.
7.Mwili kuchoka kwa hali isiyo ya kawaida.
8.Kupoteza hamu ya tendo la ndoa.
9.Kiuno kuuma hasa ukitaka kusimama.
10.Miguu na mikono kufa ganzi hasa nyakati za asubuhi.
11.Kutopata usingizi mapema na ukilala hutaki kuamka na uamkapo unakuwa umechoka sana.
12.Kupata choo kigumu na huwa hakipatikani kwa wakati wa kawaida.
13.Uzito wa mwili kuongezeka sana na huku huli sana.
Dalili za ugonjwa huu ni nyingi mno ila za msingi ni hizi hapo juu.Tukiwa wagonjwa wa sukari tunapaswa kushirikiana na kubadilishana uzoefu na njia za kudhibiti athari zake.Hili hakika ni muhimu kulipata kutoka kwa kila mmoja wetu.KUMBUKA UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHDIFU.
Niligundua nina ugonjwa huu toka mwaka 1997 lakini sikuwa na dalili nilizoeleza hapo juu.Tatizo la awali kwangu lilikuwa kuongezeka uzito na kuvimba miguu.Hali hii iliniogopesha nikajihisi nina tatizo la moyo au figo hivyo nikawaona madakitari na ndipo nilipobainika kuwa nina ugonjwa wa kisukari.
Nilianza kusoma maandiko mbalimbali ya ugonjwa huu na ndipo nilipo kutana na gazeti la TIME la Januari 12, 2004 gazeti hili lilieleza kwa kina juu ya ugonjwa huu. Waandishi wa makala haya ni Christine Gorman na Kate Noble..Makala yao yalikuwa na kichwa kilichosema " Why so many are gating Diabetes" Ikiwa na maana KWANINI KISUKARI KINAWAKUMBA WENGI. Lilikuwa ni swali lilotaka majibu.Humo walieleza kuwa kisuksri hakijapatiwa dawa kamili na haijulikani kwa hakika kwanini watu wanakiugua.
Maelezo ya tafiti mbali mbali yalionesha nini chanzo yalitolewa na nini kifanyike kuzuia kupata ugonjwa huu yalitolewa pia.
Mtindo wa maisha , mazingira na urithi vilielezwa kuwa ni sababu kubwa za mtu kupata ugonjwa huu.Kwa kawaida kisukari si ugonjwa wa kuambukiza.Ni ugonjwa ambao mwili unashindwa kutumia sukari kama inavyotakiwa.
Kisukari ni ugonjwa ambao unaweza kutambulika kwa namna kuu nne.
1. Kwanza ni kwa njia ya kuangalia kiwango cha sukari katika damu.Kiwango sahihi kisizidi
m/moll 7 kabla ya kula chochote ndani ya saa 8 hadi 10, Kitaalamu upimaji huu huitwa FBG
(Fasting Blood Suger).Kwa kawaida mwili ukiwa hauna tatizo katika kutumia sukari baada ya
muda huo lazima sukari katika damu iwe katika kiwango sahihi.Sukari ikiwa zaidi ya kiwango
hicho lazima mwili una shida katika kubadili sukari katika damu kuwa nishati.
2. Kipimo cha pili cha kujua mtu ana sukari au hana ni (GTT) Glucose Tolerance Test. Kikawaida
m/moll za mtu asiye na kisukari ni chini ya 7. Kipimo hiki ni baada ya kula na kutumia sukari,
Kama baada ya kula na kutumia sukari kiwango cha sukari katika damu kitaonekana kuwa sukari
katika damu ni kati ya 7 na 11 m/moll muhusika atakuwa si mwenye kisukari.
3. Namna ya tatu ya kujua kuwa mtu ana sukari ni kwa njia ya kuona jinsi 'insulin' inavyogoma
kufungua 'cell' ili ipokee sukari kutoka katika damu ikazalishe nishati. Insulin ni homoni
izalishwayo na kongosho ifanyayo kazi kama ufunguo wa kufungua mlango.Yaweza ikawa nyingi
na ya kutosha lakini ikagoma kufungua au ikawa kidogo ikawa haitoshi.Wenye uhaba wa insulini
mara nyingi ni wale wa aina ya kwanza ya kisukari na wenye nyingi iliyogoma ni wale wa aina ya
pili ya kisukari.Kipimo hiki ni kigumu kidogo katika kupima kisukari kwani sukari ya mgonjwa
yaweza kuwa sawa lakini insulini haipo kabisa ama ipo lakini imegoma kufanya kazi.Kipimo hiki
kinaitwa (IR) Insulin Resistance.
4 .Namna ya nne ni kuisha kwa sukari mwilini. Hali hii inaitwa (hypoglysomia) Sukari mwilini ikiwa
chini ya ' mill moll' nne (4) ni hatari hivyo inatakiwa kupandishwa haraka kwa kumpatia mgonjwa
kitu cha sukari haraka ili kuipandisha.Wagonjwa wengi wa sukari hupoteza maisha sukari yao
ikishuka sana zaidi ya hapo.
Namna ya kudhibiti ongezeko la sukari ni KUACHA mazoea mabaya ya kunywa pombe kali na za kupitiliza, kula nyama choma kwa wingi, kula chips mayai, kunywa soda sana, kuvuta sigara, kula vyakula viyeyushwavyo haraka tumboni, kutofanya mazoezi na kutunza unene, Ndiyo, wapo wembamba na wana kisukari lakini hatari kubwa ya kupata kisukari iko kwa watu wanene zaidi.
Pata maelezo zaidi toka katika clip yangu hii fupi ya dakika saba tu na naomba maoni yako
0 comments: