Showing posts with label Habari za Ndani ya Jiji. Show all posts
MWANAMME NI KAZI
Katika utafiti wa hivi karibuni, watafiti wamegundua kwamba, wanawake wanawapenda wanaume wasio waoga na mashujaa kuliko wale waoga. Ushujaa wa wanaume ni kigezo kikubwa kwa wanawake kuwapenda marafiki wa kiume wa muda mrefu na muda mfupi. 

Hii inamaanisha kwamba katika urafiki wa kawaida na wa kimapenzi na wa kindoa, wema au ukarimu ulionekana kwamba ni kigezo cha kawaida tu na sio kipaumbele chao.

Tukirudi kwa mababu zetu wa kale walioishi mapangoni, wanawake waliwapenda wanaume shujaa ambao wangeweza kujitoa muhanga kuwalinda wao na watoto wao. Mwanaume ambaye alikuwa na uwezo wa kujitoa muhanga alionekana kuwa na uwezo wa kuwinda bila hofu na kuzama porini kutafuta chakula kwa Ajili ya familia au kutafuta dawa kwa ajili ya matibabu kwa familia yake.

Kikubwa hapa ni ulinzi na usalama. Na hili linawafanya wanawake wengi kuwapenda mabaunsa kwa sababu hih hii ya ulinzi na usalama
Mwanaume mwenye nazo anaonekana kupendwa lakini hapa swala si fedha yake, bali anaonwa kama ndiye anayeweza kuilinda familia. Ukikuta wanawake wanavutiwa na wanaume wenye fedha, usishangae, kwani bado wanaongozwa na  haja yao kuu ya  kuhakikishiwa usalama wao.

Kwa kifupi ni kwamba kinachotafutwa na wanawake ni  amani nausalama.

Siku hizi  fedha imechukua nafasi katika kujihakikishia usalama wetu. Kila kitu siku hizi ni pesa na ndio maana wanawake kwa dhana ile ile ya kujihakikishia usalama wanavutiwa na wanaume wenye nazo.

Sio kwa sababu ya tamaa...... La hasha, ni kutaka kuwa na uhakika na maisha yake na familia yake.
Mwanamume akikosa sifa ya fedha ataangaliwa kwa ujasiri  na uchakarikaji.Kwa haya mwanamke anajua kwamba kwa kushirikiana naye mbeleni maisha yatakuwa mazuri na salama.
Ikitokea kwa mfano kaolewa na mwanaume mzigo au siku hizi huwaita "Dead alive" au mwanaume suruali, jukumu la kutafuta hulishika mwenyewe kwa sababu hamna jinsi na mara nyingi hufanikiwa kuzikamata kwa sababu anafanya hivyo kwa nia na dhamira ya kujihakikishia usalama.
Kama vile wanaume wanavyokosea kuoa kwa kutopiga hesabu zao vizuri katika kuoa vivo hivyo wanawake nao hukosea kwa kudanganyika na zile sifa za mwanaume za muda mfupi bila kuchunguza vizuri zaidi. 

Wapo ambao wakigundua kwamba mwanaume aliyeolewa naye ni mvivu na asiyejali familia anafungasha na kuondoka, lakini wapo ambao wanatafuta suluhu na kuamua kushika hatamu za kuendesha nyumba hawa ni wale wanaoogopa kufanya makosa kwa mara ya pili yaani kuondoka na kuangukia kwa mwanaume mwingine mwenye sifa zisizopendeza. Hawa wanakubali matokeo na kuamua kusimama kama wao, hawayumbishwi na huwakubali wenzi wao kama walivyo.

Wanawake wa aina hii mara nyingi kufanikiwa sana tofauti na wale wanaojipweteka na kubaki wakilalamika. Lakini naomba niseme kuwa wanawake kwa kiasi kikubwa ni mashujaa hawawezi kukaa na kuangalia familia ikianguka kwa sababu mwanaume hawawajibiki. Wengi sana tena kiasi cha kutosha husimama na kushika nyumba kwani wanajua kwamba nyumba ikianguka mara nyingi lawama huwaendea wao.

Pia mwanamke huvutiwa na mwanaume anayejali usalama wa wazazi na ndugu  zake Mwanamke yuko tayari kumpenda mume mwingine nje ya ndoa kama huyu mume ataonesha  upekee katika kuwa chukua wazazi wake.

Kwa mfano wapo wanaume wengi hali zinapokuwa ngumu huzikimbia familia zao na kuzitelekeza hata kwa miaka kadhaa, lakini wakirudi wanakuta familia ipo mbali kimandeleo na watoto wana hali nzuri. Hao ndiyo huitwa wanawake wa shoka. Lakini maendeleo hay0 huwa hayaji hivi hivi, yuko mwanamume aliyependwa badala ya aliyeikimbia familia.

Kwa hiyo swala la uelewa,umaridadi, utanashati katika siyo sifa zinazotazamwa na wanaume bali ni ulinzi na upendo, 

Kwa wanaume vigezo ni utii, na matunzo mazuri. Vitu hivi kwao ni muhimu katika swala zima la kutafuta mwenza. 
TIME ya Januari 12, 2004 
Ugonjwa wa sukari umekuwa tishio siku hizi. Ugonjwa huu haushambulii wazee, watoto au vijana tu  bali makundi yote haya yamekuwa yakisumbuliwa na ugomjwa huu.


Tishio hili haliko Tanzania peke yake bali liko ulimwenguni kote Hata hivyo viwango vya kuathirika huweza kutofautiana toka nchi moja na nyingine lakini haipo nchi iwezayo kudai iko salama na tishio la ugonjwa huu.

Ugonjwa huu hauna tiba ila zipo dawa za kumfanya mgonjwa kuishi kwa matumaini na kupunguza athari zitokanazo na ugonjwa huu.

Pamoja na dawa hizi wagonjwa wengi tunashindwa kufuata masharti ya kudhibiti kikamilifu athari zitokanazo na ugonjwa huu katika miili yetu.

HII NI KUTOKANA NA KUTOJUA ATHARI za ugonjwa huu kwetu  PILI KUTOJUA NJIA SAHIHI ZA KUDHIBITI ATHARI HIZI.

Sasa hivi wagonjwa wa sukari tunadanganywa sana na watu kuhusu tiba na kupoteza maelfu ya pesa pasipo na mafanikio.Njia sahihi ni kutumia dawa za hospitali za kuzuia  athari zitokanazo na   ugonjwa huu toka kwa waganga wa mahospitali. Tiba mbadala sahihi  haswa haswa ni vyakula na mazoezi kusaidia hizi  hizi za mahospbinitalini katika kudhibiti athari zitokanazo na ugonjwa huu.

Dawa za hospitalini ziko katika makundi makuu matano.
1.Kwanza zipo za kuchochea kongosho kuzalisha isulin zaidi (Sulfonylureas).
2. Pili ni (Meglitinides) hizi nazo kama kundi la kwanza huishajiisha kongosho kuzalisha insulin
    zaidi
3.Kundi la tatu ni (Biguanides) Hizi hulikataza ini kutoa sukari (glucose) nyingi na husisimua misuli
   kutumia sukari zaidi kutoka katika damu.
4.Kundi la nne linaitwa (Thiazolidinediones) Hizi ni dawa za hivi karibuni tu ambazo huiwezesha
   insulin kusukuma (gulucose) sukari na mafuta kuingia katika misuli kwenda kuzalisha nishati
   mwilini.
5.Kundi la tano ni (Alpha -Glucosidase Inhibitors) hii hufannyia kazi kwenye utumbo mwembamba
   kuzuia mikate na vyakula vya wanga  kubadilishwa kuwa sukari (glucose)

Pili ni vema kujipima kiasi chako cha sukari katika damu  ili kujua kupanda na kushuka kwa sukari katika mwili wako.

Dalili ziashiriazo kuwa na ugonjwa huu za awali ni hizi:
1.Kukojoa mara kwa mara  hasa usiku.
2.Kuona kwa mawengewenge, Macho kupoteza uoni wake wa kawaida.
3.Kuwa na kiu kali isiyoisha.
4.Kuwa na njaa kali kama ya mtoto.
5.Kupoteza uzito kusiko kwa kawaida kwa kipindi kifupi.
6.Kuwa na vidonda visivyopona haraka.
7.Mwili kuchoka kwa hali isiyo ya kawaida.
8.Kupoteza hamu ya tendo la ndoa.
9.Kiuno kuuma hasa ukitaka kusimama.
10.Miguu na mikono kufa ganzi hasa nyakati za asubuhi.
11.Kutopata usingizi mapema na ukilala hutaki kuamka na uamkapo unakuwa umechoka sana.
12.Kupata choo kigumu na huwa hakipatikani kwa wakati wa kawaida.
13.Uzito wa mwili kuongezeka sana na huku huli sana.

Dalili  za ugonjwa huu ni nyingi mno ila za msingi ni hizi hapo juu.Tukiwa wagonjwa wa sukari tunapaswa kushirikiana na kubadilishana uzoefu na njia za kudhibiti athari zake.Hili hakika ni muhimu kulipata kutoka kwa kila mmoja wetu.KUMBUKA UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHDIFU.

Niligundua nina ugonjwa huu toka mwaka 1997 lakini sikuwa na dalili nilizoeleza hapo juu.Tatizo la awali kwangu lilikuwa kuongezeka uzito na kuvimba miguu.Hali hii iliniogopesha nikajihisi  nina tatizo la moyo au figo hivyo nikawaona madakitari na ndipo nilipobainika kuwa nina ugonjwa wa kisukari.

Nilianza kusoma maandiko mbalimbali ya ugonjwa huu na ndipo  nilipo kutana na gazeti la TIME la Januari 12, 2004  gazeti hili lilieleza kwa kina juu ya ugonjwa huu. Waandishi wa makala haya ni Christine Gorman na Kate Noble..Makala yao yalikuwa na kichwa kilichosema "  Why so many are gating Diabetes" Ikiwa na maana KWANINI   KISUKARI KINAWAKUMBA WENGI. Lilikuwa ni swali lilotaka majibu.Humo walieleza kuwa kisuksri hakijapatiwa dawa  kamili na haijulikani kwa hakika  kwanini watu wanakiugua.

Maelezo ya tafiti mbali mbali yalionesha nini chanzo yalitolewa na nini kifanyike kuzuia kupata ugonjwa huu  yalitolewa pia.

Mtindo wa maisha , mazingira  na urithi vilielezwa kuwa ni sababu kubwa za mtu kupata ugonjwa huu.Kwa kawaida kisukari si ugonjwa wa kuambukiza.Ni ugonjwa  ambao mwili unashindwa kutumia sukari kama inavyotakiwa.

Kisukari ni ugonjwa  ambao unaweza  kutambulika kwa namna kuu nne.
1. Kwanza ni kwa njia ya kuangalia kiwango cha sukari  katika damu.Kiwango  sahihi  kisizidi
    m/moll 7  kabla ya kula chochote ndani ya saa 8 hadi 10, Kitaalamu upimaji huu huitwa  FBG
  (Fasting Blood Suger).Kwa kawaida mwili  ukiwa hauna tatizo katika kutumia sukari baada ya
   muda huo lazima sukari katika damu iwe katika kiwango sahihi.Sukari ikiwa zaidi  ya kiwango
   hicho lazima mwili una shida katika kubadili sukari katika damu kuwa nishati.

2. Kipimo cha pili cha kujua mtu ana sukari  au hana ni  (GTT) Glucose Tolerance Test. Kikawaida
    m/moll za mtu asiye na kisukari ni chini ya 7.  Kipimo hiki ni baada ya kula na kutumia sukari,
    Kama baada ya kula na kutumia sukari  kiwango cha sukari katika damu kitaonekana kuwa sukari
    katika damu ni kati ya 7 na 11 m/moll muhusika  atakuwa si mwenye kisukari.

3. Namna ya tatu ya kujua kuwa mtu ana sukari ni kwa njia ya kuona  jinsi 'insulin' inavyogoma
    kufungua 'cell' ili ipokee sukari kutoka katika damu  ikazalishe nishati. Insulin ni homoni
    izalishwayo na kongosho ifanyayo kazi  kama ufunguo wa kufungua mlango.Yaweza ikawa nyingi
    na ya kutosha lakini ikagoma kufungua au ikawa kidogo ikawa haitoshi.Wenye uhaba wa insulini
    mara nyingi ni wale wa aina ya kwanza ya kisukari na wenye nyingi  iliyogoma ni wale wa aina ya
   pili ya kisukari.Kipimo hiki ni kigumu kidogo  katika kupima kisukari kwani  sukari ya mgonjwa
   yaweza kuwa sawa lakini insulini haipo kabisa  ama ipo lakini imegoma kufanya kazi.Kipimo hiki
   kinaitwa (IR) Insulin Resistance.

4 .Namna ya nne ni kuisha kwa sukari mwilini. Hali hii inaitwa (hypoglysomia) Sukari mwilini ikiwa
    chini ya ' mill moll' nne (4) ni hatari hivyo inatakiwa kupandishwa haraka kwa kumpatia mgonjwa
    kitu cha sukari haraka ili kuipandisha.Wagonjwa wengi wa sukari hupoteza maisha sukari yao
    ikishuka sana zaidi ya hapo.

Namna ya kudhibiti ongezeko la sukari ni KUACHA mazoea mabaya ya kunywa pombe kali na za kupitiliza, kula nyama choma kwa wingi, kula chips mayai, kunywa soda sana, kuvuta sigara, kula vyakula viyeyushwavyo haraka tumboni, kutofanya mazoezi na kutunza unene, Ndiyo, wapo wembamba na wana kisukari lakini hatari kubwa ya kupata kisukari iko kwa watu wanene zaidi.



Pata maelezo zaidi toka katika clip yangu hii fupi ya dakika saba tu na naomba maoni  yako


MWANZA Secondary School  view
FORM FOUR NATIONAL EXAMINATION RESULT FOR SECONDARY SCHOOL EDUCATION IS OUT.


 To get OVERALL results for  private centers  and secondary schools  Click here


For Mwanza secondary school click here


For QT click here

Mwanza Secondary School overall performance.

i). DISTINCTION = 9 MERIT = 29 CREDIT = 47 PASS = 100 
    FAIL = 47.

 ii).Registered 262,  Absent 6, Sat  256, Withheld 24, 
     NO-CA 0,  Clean 224.

iii)The school is under CENTRE POSITION OF
    CATEGORY(REGION WISE) CENTRE 
     WITH 40 CANDIDATES OR MORE

iv).Total passed candidates -185,

v).Regional position         60/174.
  
vi). National position         521/2322 
Kiongozi wa CCM  kata,
akimkaribisha mgombea kwa tiketi
ya CCM, mama Mtalo kunadi
sera zake na kuomba kura
Uchanguzi wa mwenykiti wa mtaa Sweya ulioahirishwa  kutokana na kufariki Bw. Pius Masome aliyekuwa mmoja wa wagombea kiti hicho kupitia CCM utarudiwa hapo Jumapili ijayo ya tarehe 8, Februari 2015.

Marehemu Bw. Pius alikuwa kasimama kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM na mgombea mwenanzake Bw. Fred alisimama kwa tiketi ya CHADEMA.

Kwa bahati mbaya Bw. Pius aliugua siku chache kabla ya uchaguzi
na siku hiyo uchaguzi ukifanyika alifariki akiwa katika matibabu hospitali ya Bugando kipindi kura zikiendelea kupigwa.

Siku ya Jumapili ya tarehe 1, Februari 2015 CHADEMA ndio walioanza kulipanda jukwaa na kuanza kunadi sera zao na siku iliyofuata ya Jumatatu tarehe 3,Februari 2015 CCM  walilipanda jukwaa kuziweka wazi sera zao.



Hakika safari hii wana Sweya wamekumbwa na changamoto la aina yake tofauti na awali linalotokana na mabadiliko waliyoyafanya wana CCM ya kumsimamisha mgombea mwanamke.

Kwa kura za awali  CHADEMA ilikuwa ikiongoza zidi ya CCM katika mtaa huu wa Sweya na walishinda nafasi zote za wajumbe wa mtaa.

Tunachojiuliza ni kumbwa mabadiliko haya yatabadili mwelekeo na msimamo wa wana Sweya wengi waliowapa CHADEMA ushindi wa wajumbe wa serikali ya mtaa?

Bw. Reverian Mtalo akimnadi mgombea  wa CCM ambaye pia ni mkewe alisema, anaweza na ameridhia uamuzi wake huo.

"Mke wangu amekua kiongozi katika ngazi mbalimbali kwenye vikundi vya kina mama, vya kijamii na vya kidini na aliponijulisha nia yake hii ya kugombea nafasi hii ya uenyekiti wa mtaa sikuwa na  wasiwasi wala shaka yeyote,juu ya uamuzi wake huu na nilimruhusu na naamini anaweza" alisema Bw, Mtalo.  
Bw, Mtalo akimnadi mkewe.
Shangwe na nderemo zilirindima kiwanjani humo pale Bw, Mtalo alipouliza swali,"Wanawake mnaweza hamuwezi?"

Kikundi cha wacheza ngoma na maonesho ya sarakasi kiliingia uwanjani na kuonesha maonesho, ambayo yalizikonga nyoyo za wasikilza kampeni kisawasawa.
Kikundi cha burudani 'kikijimwayamwaya' kweye kampeni hizi

Ukweli ni kwamba kampeni zinaonesha wagombea wa pande zote kuiva kisiasa na kutambua kile wanachokitaka kwani pande zote walimalizia kwa kuomba wananchi kuwapa kura za ndiyo.

Kilichobakia ni uamuzi wa wana sweya ni nani kati ya wagombea hawa kawashawishi kisera na wala sio malumbano ambayo wanaona hayana masilahi kwao.
Wana Sweya wakimsikiliza mgombea wa CCM  kwa makini

Baadhi ya wana Sweya walisikika wakidai kuwa wanataka kiongozi wa watu, mchapa kazi na mwenye sera zenye mashiko na suala la Chama si msingi MKUU kwao.

MV  TEMESHA
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli leo hii Jumatano ya tarehe 9 julai 2014, majira ya saa tatu asubuhi azindua  kivuko kitakachofanya kazi kama daladala ya kusafirisha abiria kupitia majini kwa lengo la kukabiliana na msongamano wa magari jijini hapa kutokana na kuwa na njia moja tu ya kuingia na kutoka katika  jiji hili. 

Kivuko hiki kijulikanacho kwa jina la MV TEMESHA injini yake ina 'horse power' kubwa ambayo itakiwezesha kwenda kasi  na  kuweza kubeba kwa wakati mmoja mzigo wa tani 65 ambao ni sawa na abiria 80 na magari madogo madogo sita.
Kikundi cha Ngoma kikitoa Burudani katika Uzinduzi huu
Kivuko hiki ambacho uzinduzi wake unafanywa leo hii hapa Sweya, Nyegezi nje kidogo ya jiji la Mwanza kinatarajiwa kufanya safari zake kuanzia wiki ijayo ambazo  zitanzia Luchelele, kupitia Sweya, Butimba, mkuyuni, Igogo, Mjini hadi Kirumba, lengo likiwa ni kupunguza foleni za magari jijini hapa cha kufurahisha zaidi ni kwamba, imedaiwa wanafunzi watasafiri bure alimradi tu wawe na vitambulisho.

Dk.John Pombe Magufuli Akiteta na Wenyeji wake

Kabla ya ufunguzi wa kivuko hiki Dk.John Pombe Magufuli alitoka katika kukagua mradi wa barabara ya kutoka Usagara hadi Kisesa mkoani humu kwa lengo lile lile la kupunguza msongamano wa magari katika jiji hili. Barabara hii ni ya urefu wa kilometa 16.7 na inajengwa kwa kiwango cha lami. 

Barabara hii na kivuko hiki hakika vitawezesha ufikaji katika kona yeyete ile katika jiji hili kwa wepesi zaidi.

Habari toka wizara hii zimeeleza pia kwamba kesho, Waziri huyu ambaye ni mmoja wa Mawaziri wanopigiwa mfano miongoni mwa Mawaziri  wachache wachapaka kazi na hodari katika nchi hii ataenda mkoani Mara kukagua barabara ya Makutano - Nata na Mugumu yenye urefu wa kilomita 50.  
Mkuu wa mkoa akitoa neno katika ufunguzi huu
Aidha kesho hiyo hiyo anatarajiwa kuzindua kivuko kingine cha MV MARA  huko Mkoani Mara kitakachofanya safari zake kati ya Iramba na Majita na baada ya uzinduzi huu atafanya mkutano wa hadhara eneo la mwibara ikiwa ni sehemu ya kufanya ukaguzi wa mradi wa barabara ya Nyamuswa- Bunda-Kisorya. na Nansio yenye urefu wa kilomita 51.

Imedawa pia kuwa serikali katika azma yake ya kupunguza kero za usafiri kwa wananchi wake inatarajia kuanzisha kivuko kingine kama hivi huko jijini Dar es salaam kitakachofanya safari kati ya Dar es salaam na Bagamoyo.
Wananchi wakibadilishana hili na lile kabla ya uzinduzi
Kweli hizi ni juhudi za wazi za serikali hii ya awamu ya nne katika kuwajali wananchi wake.Yule atakayekuwa anabeza juhudi hizi hakika atakuwa ni yule asiyetoridhika kwa lolote na mwenye kujaa tamaa na wivu au uchu wa kitu fulani.Waswahili wanasema asiyeridhika kwa kidogo hata kikubwa hakitamridhisha, Hongera serikali ya awamu ya nne kwa kujali wananchi,
Wananchi wakimiminika eneo hili kushuhudia uzinduzi huu
Ombi kwako Mheshimiwa Magufuli ni kukuomba utukumbuke na sisi wakule Mwanga Mkoani Kilimanjaro kwa barabara ya Kichwa Ng'ombe kupitia Kwakoa Kigonigoni-Butu -Jipe kutokezea Kifaru. Barabara hii ina umuhimu sana kwani itakuwa ni lango la kuunganisha nchi yetu na jirani zetu Kenya ukiacha ile ya Mwanga-Usangi- Ugweno. Pia itasaitia wagonjwa kufika kwenye hospitali hii kubwa inayojenwa hapo Kwakoa ambayo itakuwa ya msaada mkubwa kwa Watanzania na wale kutoka nchi ya jirani Kenya.
Gari la Idara ya Mahakama MEI mosi jijini Mwanza.
SIKU ya Jumatano 25,Juni 2014 mahabusu tisa wa gereza la Wilaya ya Geita mkoani hapo wavua nguo hadharani mbele ya Mahakama ya Wilaya kwa madai ya kucheleweshwa kusikilizwa kwa shauri lao.

Mahabusu aliyechujua nguo jijini MWANZA..
Kutokana na sakata hili uongozi wa serikali kesho yake walilazimika kwenda gerezani hapo kukutana nao.

Maofisa waliowatembelea mahabusu hao walitoka mahakama ya wilaya, ofisi ya mwanasheria wa serikali pamoja na ofisa wa upelelezi wa makosa ya jinai  wa mkoa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juzi, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Geita, Desideric Kamugisha, alisema walilazimika kufanya mazungumzo na mahabusu hao kuhusiana na malalamiko yao ya kutotendewa haki.

Alisema baadhi ya malalamiko hayo ni kucheleweshwa kwa upelelezi wa kesi zao hususani za mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha, huku baadhi ya wafungwa wakidai kuhukumiwa adhabu kubwa zisizolingana na makosa husika na kutokupata fursa ya kukata rufaa.

“Tumekubaliana nao na kuwataka waorodheshe malalamiko yao yote ambayo wameyataja mbele yetu wakiainisha namba ya shauri, mwaka pamoja na mahakama husika.

“Kazi hiyo iliaanza tangu juzi, kwa hiyo matokeo yatapatikana muda si mrefu kuanzia sasa, ili kumaliza kero hii,” alisema.

Kamugisha aliongeza kwamba kwa mujibu wa mwongozo wa kusikiliza kesi kwa mwaka, mahakama inatakiwa kusikiliza mashauri yasiyopumgua 250. 

Kwa mujibu wa kauli yake  alisema, pamoja na uhaba wa mahakimu wamesikiliza kesi 436 tangu Januari hadi Mei mwaka huu.

Alibainisha kuwa   kuna hakimu mmoja tu wa wilaya na wawili wa mahakama ya mwanzo.

Mkuu wa Gereza la Geita, Joseph Mbilinyi, alisema wameanza kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo hayo, ili kuondoa malalamiko hayo.

Wakili wa Serikali Mkoa wa Geita, Mwasimba Hezeroni, alisema kuwa changamoto walizopata walipotembelea gerezani humo watazifanyia kazi kwa muda muafaka, na akataka kila upande utekeleze kazi zake kwa wakati kwa maana ya mahakama, mwanasheria wa serikali pamoja na ofisi ya  upelelezi ya mkoa.

Mahabusu hao walichukua hatua hiyo juzi asubuhi  muda mfupi baada ya kutoka mahakamani bila kesi zao kusikilizwa na kulazimishwa kupanda kwenye Karanding la polisi kurudishwa mahabusu.

Hili ni tukio la pili kutokea kufuatia sakata jingine kama hili lilotokea katika mahakama ya hakimu mkazi hapa jijini Mwanza.Kwa madai kama hayo hayo ya kucheleweshewa kusikilizwa.

Mahabusu aliyechujua nguo jijini ARUSHA
Kule Arusha mwezi Aprili mwaka huu huu mahabusu mmoja, 'alisandura' nguo zake hadhani mbele ya Mahakama jijini humo akiwa na mwenzake wakidai wenzao Dharam Patel (26) na Nivan Patel (20) wanaodaiwa kukamatwa na kete 173 za heroini na misokoto 300 ya bangi, Aprili mwaka huu kuachiliwa ili hali makosa yao ni mamoja.

Tatizo hili la mahabusu kuchujua nguo hadharani tuite ni dalili za uonezi kukithiri hapa nchini ama ni wananchi kujua haki zao au ni nini?Hii yaweza kuwa ni dalili ya jambo baya

Lakini waswahili wanasema panapofuka moto pana moto.Kuwa mahabusu si lazima huyo mhusika kuwa  ni mwenye hatia. Wako waliohukumiwa ikaja bainika kwamba  waliohukumiwa kimakosa lakini walipokata rufaa waliwekwa huru.Parole imewanusuru wengi waliotiwa hatiani kimakosa.

Haki isipotendeka katika jamii ndicho chanzo cha jamii kurudi nyuma kimaendeleo na ni chanzo kikuu cha chuki miongoni mwa wana jamii.Haki tuilinde WATANZANIA kwa maendeleo ya nchi yetu.Upotevu wa haki ni katika jamii ni dalili ya uwepo wa Rushwa iliyokithiri.
Askari zimamoto wakiwa katika jitihada za kuzima moto uliowashwa na Wamachinga ili kuteketeza Msikiti wa Hindu wanaosali Masinga-singa. 
KATIKATI  ya jiji la Mwanza leo Jumatano, Juni 11, 2014  kumekuwa na vurugu toka saa 3:58 asubuhi hadi 8:45 mchana.  

Barabara kuu za katikati ya jiji hili za Kenyatta,  Nyerere, Pamba, Lumumba na Rwegasore   zalikuwa hazikaliki  baada ya mabomu zaidi ya 120 ya  kutoa machozi kulipuliwa na kulifanya eneo zima kunuka harufu ya mabomu hayo na watu kujikuta wakilia ovyo ovyo.

Jeshi la Wananchi (JWTZ) lilitoa askari wa
 “MP” kuimarisha ulinzi katika mabenki,
 ofisi za serikali na maeneo nyeti ili
 kuwezesha shughuli za kila siku kuendelea
Mapema kabisa Jeshi la wananchi lilitoa askari wake wa kijeshi “MP” kuimarisha ulinzi kwenye vitengo vya mabenki, ofisi za serikali na maeneo nyeti ili kutokwaza shughuli za kila siku kuendelea.Lakini pamoja na tahadhari hii hali ilikuwa  ya kutisha.

Mabomu hayo yalilipuliwa maeneo mbalimbali ya mji ikiwemo eneo  maarufu la Makoroboi  kufuatia kuvunjwa kwa vibanda vya machinga jana asubuhi.

Uvunjwaji huu wa vibanda unadaiwa ndio uliyowafanya Wamachinga kucharuke na kuanza mapambano na askari polisi na mgambo wa Jiji huku wakishinikiza wenzao walio kwenye maeneo halali nao waondolewe ili wote waikose Makoroboi.


Baadhi ya Wamachinga wakiwa
 mikononi mwa Jeshi la Polisi
Katika sekeseke hilo wamachinga  zaidi ya 40 wamekamatwa kwa kukiuka sheria za mipango miji.

Hatua hiyo inafuatia maamuzi ya baraza la halimashauri ya Jiji la Mwanza kuondoa wafanya biashara wadogo wadogo almaarufu kama  wamachinga kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria.


Vijana waandamanaji wakifunga barabara
Wakati huo huo walionekana Vijana wakiandamana huku wakifunga barabara. 

Hahari zilizopatikana baadae zilibaini kuwa hao walikuwa wanatumiwa kuzidisha vurugu. 

Haya  yalibainishwa baadae na bwana mmoja aitwae Abdukadri Salim . "Vijana hawa wanatumiwa kufanya vurugu na siyo wamachinga. "Bwana  Abdukadri Salimu alisema.

Mitaa ya Makoroboi na ya pembezoni mwake ilikumbwa na vurugu hizi . Maduka yalifungwa  maeneo haya na ya jirani yake kutokana na vurugu hizi. 

Askari zimamoto walifanikiwa kuzima moto huo uliowashwa na wamachinga ili kuhatarisha usalama wa Msikiti wa Hindu wanaosali Masinga singa. 

 Hii ni kwa sababu walitakiwa kutotandaza bidhaa zao chini au kuegesha kwenye kuta za msikiti huu, na tukio la leo ni la zaidi ya mara mbili kutokea kwa wamachinga  kulikalia eneo hili kwa nguvu.
Oparesheni ofisa wa zima moto,
Sajenti meja Gadafi Masoud
Akiongea na wana habari
Oparesheni ofisa wa zima moto, Sajenti meja Gadafi Masoud  amesema msikiti wa Hindu wanaosali Masinga singa umenusurika kuchomwa moto na machinga hao baada ya magari makubwa mawili ya kikosi chake kuuzima moto uliowashwa na wamachinga kwa lengo la kuuteketeza msikiti huo ulio katika eneo waliloondolewa. Msikiti huu uko eneo la  barabara ya Lumumba  kwenye kona ya kuingia Makoroboi  kupitia msikiti wa Hindu ukitokea barabara ya Nyerere . Sehemu hii Wamachinga waliwasha moto.

 Askari wa jeshi la Polisi Mkoani hapa
wakifanye msako mtaa baada ya mtaa
kuwasaka waanzisha fujo sanjari na
kulinda usalamawa mali za wafanyabiashara
 kwani vurugu hizo ziliambatana na uporaji.
Mbali na mabomu yaliyolipuliwa ili kudhibiti  vurugu hizo ilibidi jeshi la polisi  lifanye msako mtaa baada ya mtaa kuwasaka waanzisha fujo sanjari na kulinda usalama na mali za wafanyabiashara kwani vurugu hizi ziliambatana na uporaji uliofanywa na wezi waliotumia mwanya wa machafuko haya.

Kutokana na mchafuko huu  hata wale Wamachinga walioruhusiwa kufanya biashara hapa Makoroboi kwa kuwa katika maeneo yanayoruhusiwa kuendeshea biashara walishindwa kufungua biashara zao.

Mtawanyiko wa gesi za mabomu haya ya machozi ulisababisha wakati mgumu kwa wengi hususani  wanahabari.

Wakati huo huo Jeshi la polisi likitumia vipaza sauti lilitoa tahadhari ya watu kutosimama kwa makundi.

Tukio hili limetia hasara kubwa kwa kukosekana  kwa huduma toka kweye maduka ya biashara na huduma za usafiri kwa muda, hali ambayo imewapa usumbufu mkubwa wateja wa hapa jijini na wale wa kutoka katika mikoa ya jirani ya Mara, Shinyanga, Kagera, Simiyu na Geita waliohitaji bidhaa katika maduka ya jumla.

Kamanda wa polisi hapa Mkoani Mwanza Valentino Mlowola hakuweza kupatikana kwa kuwa akikuwa katika safari ya kikazi na Christopher Fuime msaidizi wake alidaiwa kuwa katika Oparesheni hii. 


Jeshi la Polisi katika doria
mtaa kwa mtaa
.
Baadhi ya askari ambao hawakutaka  kutajwa majina yao walisema zaidi ya Wamachinga 40 wamekamatwa  kulisaidia jeshi la Polisi kuhusiana na vurugu hizi wa.

Baadhi ya taarifa ambazo hazijathibitishwa bado zinadai kwamba hali hii ya Wamachinga kukaidi amri halali ya kuwataka kuondoka maeneo haya  yasiyo ruhusiwa kuendesha biashara inachochewa na baadhi ya wanasiasa wanaotafuta umaarufu wa kisiasa kupitia mgongo wa wafanyabiashara hawa.
Wakazi wa jiji la Mwanza leo Majira ya saa 4 Asubuhi Waliwekwa njia Panda na Kujawa Hofu kubwa Kufuatia Vikosi vya Askari kanzu, FFU, Askari polisi na Zimamoto Kufanya Zoazi la Kushitukiza la Kusaka Wahalifu ndani ya Majengo Makubwa yenye Msongamano wa Watu.

Sherehe za siku ya mzingira DUNIANI nchini Tanzania zaazimishwa kitaifa leo Alhamisi 5, Juni 2014 hapa Jijini Mwanza.

Kila mwaka ifikapo tarehe 5 Juni, Jumuiya ya Kimataifa inaadhimisha Siku ya Mazingia Duniani kutokana na Azimio la 
Baraza la Umoja wa Mataifa la Mwaka 1972.

Maadhimisho haya  ni kielelezo cha ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira uliofanyika huko Stockholm, nchini Uswis. 

 Leo hii basi Tanzania imeungana na mataifa mengine duniani  kuadhimisha  kilele cha wiki ya mazingira duniani kwa mwaka 2014 kwa ngazi ya mkoa na kitaifa  hapa jijini Mwanza.

Mambo muhimu yaliyofanyika pamoja na kufanya usafi wa mazingira ni  kueleza hatua zilizofikiwa katika uhifadhi wa mazingira kimkoa na kitaifa. 

Kauli mbiu kwa mwaka huu 2014 ni:Tunza Mazingira ili Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.

Jiji la Mwanza kwa mara nyingine limekuwa la kwanza katika usafi likiongoza majiji yote nchini kwa mara ya Tisa mfululizo.

Nayo manisipaa ya Moshi yapoteza nafasi ya kwanza ya ushindi wa usafi katika manisipaa iongozayokwa usafi. Safari hii yajikuta ikishika nafasi ya pili. Manisipaa kinara wa usafi kitaifa mwaka huu ni Manisipaaya Msoma.

Maadhimisho haya  hapa jijini Mwanza yamefanyika kwa staili ya aina yake. Wengi  tumezoea kuona maonesho mbalimbali wakati wa kuadhimisha vilele vya siku kuu kama hizi za kitaifa ndani ya viwanjani.

 Leo hii yamekuweko mabadiliko makubwa. Maonesho haya yamefanyikia katikati ya jiji na kuwaacha wakazi wa jiji hili katika mshangao na taharuki kali kiasi cha baadhi kukimbia wakidhania kulikuweko na ghasia .

Takribani kama muda wa dakika thelathini hivi muda wa saa nne  asubuhi leo wakazi waliokuwepo katikati ya jiji walijikuta wakijiuliza kuna nini? 

Wakaishia kushikwa na butwaa wasijue kilichokuwa kikiendelea huku wengine wakikimbia kujisalimisha kwa kuogopa kuumia.

Tazama hali ilivyokuwa katika picha:


Hali hii ilisababisha magari, pikipiki na watu kusimama kwa muda huku wakiwa wamejaa hofu,wasiwasi na woga. Wengine wakikimbia na baadhi ya wafanyabiashara wakifunga maduka yao wakiihusisha hali hii na ile ya Westgate kule jijini Nairobi nchini Kenya
Gari la zimamoto likiwa kwenye harakati za zoezi zima
Baadhi ya wtuhumiwa wakiwa mikononi mwa askari chini ya ulinzi mkali.
Zoezi la usakaji, kutafuta wahalifu likiendelea  huku  wananchi wakiwa wamebakia kushaanga kinachoendelea.
Asikari wakiwa katika hadhari ya kukabiliana na wahalifu wanaotafutwa muda wowote
Wahalifu wakiwa chini ya ulinzi
Wahalifu wakipelekwa  kituoni  ili hatimae kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kufunguliwa mashitaka.


Mpaka zoezi linamalizika hakuna mwananchi aliyeweza kubaini kuwa tukio hili lilikuwa ni la uigizajitu. Kila mmoja alisimulia kivyake sekeseke zima. Ukweli uliobainika baadae ulidhihirisha kuwa mapango mzima ulikuwa ni kunoa vikosi vya polisi na Zimamoto juu ya kukabiliana na uhalifu kwenye majengo makubwa ya huduma mbalimbali. Ama hakika zoezi lilifanikiwa.
Pamoja na zoezi hili na  yote yaliyojiri kwa siku hii, ikawa nayo ni njia ya kuadhimisha siku hii ya mazingira Duniani.

Aidha,  Siku hii tunaikumbuka kama siku ambayo Azimio la kuunda Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Mazingira Duniani,  UNEP, lilipitishwa. 

UNEP ni chombo pekee cha Umoja wa Mataifa chenye makao makuu yake Barani Afrika, huko Nairobi, Kenya. 

Lengo kubwa katika kuadhimisha siku hii Kimataifa na kitaifa ni kuweka msisitizo katika masuala ya mazingira na kuwapa uwezo wananchi ili wawe mawakala wazuri wa maendeleo endelevu.

 Pili ni kutoa nafasi ya kutafakari kuhusu hali na umuhimu wa utunzaji bora wa mazingira, kuelimishana na kukuza ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za hifadhi na usimamizi wa mazingira yao. 


Kiukweli zoezi hili limepamba sherehe hizi kwa aina yake. Hongera jeshi la polisi kwa kazi nzuri ya kuudhihirishia umma kuwa usalama wao mnaupa kipaumbele cha kwanza kuliko kitu kingine chochote kile.

POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza