Pata Wimbo katika Mahadhi ya Kisukuma wa BOB HAISA - BHATOJA
Bob Haisa Akiimba Wimbo wa Bahoja |
Wimbo huu Bhatoja ni wimbo wa asili..
Wimbo huu ni maarufu sana na hutumika sana katika shamrashamra za harusi. Wimbo huu huiimbwa na kabila la Wasukuma ambao ni kabila kubwa na maarufu hapa nchini.
Alichofanya Bob Haisa ni kuuboresha kwa kuuongezea vionjo na kuuimba kwa ladha inayovutia lakini isiyoondoa hisia za awali za wimbo wa kale.
Aidha ameuwekea midundo iliyotulia sambamba na kuzingatia maneno husika ya wimbo wa asili.
Ubora huu hakika humvutia hata yule asiyeelewa lugha hii ya kisukuma.
Yeyote ausikiae wimbo huu hakika hubaki akitikisa kichwa au miguu yake kwa utamu.
Bob Haisa kuuweka wimbo huu katika video kumesaidia kuutangaza na kuongeza mvuto wa wimbo huu kwa wengi.
Hii hapa video ya wimbo huu. ili nawe uweze kuhukumu ukweli huu.
Bob Haisa anavibao vingi ambavyo vimempandisha juu katika tasinia hii ya mziki wa kizazi kipya.
Wimbo wake unaoelezea historia ya Tanzania tokea kupata uhuru hadi kufikia miaka hamsini ya Uhuru unatukumbusha mengi sisi watanzania.
Wimbo huu ameuita 'Nasema na weweTanzania'.Hakika ni wimbo wa kuvutia sana.
Nimeona ili uweze kuyahukumu maneno yangu vilivyo nawe sikiliza wimbo huu ili uweze kukubaliana nami au kukataa.
Video ya 'Nasema na weweTanzania' hii hapa
Source: You tube
0 comments: