Showing posts with label Habari za Jiji. Mahusiano. Show all posts
..
Taarifa ya matokeo ya uchaguzi katika vijiji vya Mlandizi leo tr 15.10.2017 kama ifuatavyo
1.kitongoji gwata mjini. Waliojiadikisha 248. WalioPiga kura 161. iriyo haribika 1. Ccm 151. Chadema 9.
2.kijiji lukenge. Waliojiandikisha 487. Walio piga kura 436. Zilizo haribika 3. Ccm 333. Chadema 100
3.Kijiji Gumba. Waliojiandikisha 290. Walio piga kura 250.zilizo haribika 4. Ccm 220. Chadema 26.
4. Kitongoji Cha Midizini ZILIZOPIGWA 143,ZILlZO HARIBIKA 3,CCM 78,CUF 62,WALIOANDIKISHWA 156.
5. Mwenyekiti wa kijiji Misufini, waliojiandikisha 233, waliopiga kura 222,zilizoharibika 2,CCM 127 na CHADEMA 91
6. Ngeta: Waliojiandikisha 354: waliopiga kura 314 zilizoharbika 2 CCM 188 CHADEMA 124
7. Kitongoji cha Mkarambati Waliojiandikisha 62 waliopiga kura 60 ccm Kura 22 chadema kura 38. 

Taarifa hii toka kwa 
Beatrice Condrad TANURU LA FIKIRA
MWANAMME NI KAZI
Katika utafiti wa hivi karibuni, watafiti wamegundua kwamba, wanawake wanawapenda wanaume wasio waoga na mashujaa kuliko wale waoga. Ushujaa wa wanaume ni kigezo kikubwa kwa wanawake kuwapenda marafiki wa kiume wa muda mrefu na muda mfupi. 

Hii inamaanisha kwamba katika urafiki wa kawaida na wa kimapenzi na wa kindoa, wema au ukarimu ulionekana kwamba ni kigezo cha kawaida tu na sio kipaumbele chao.

Tukirudi kwa mababu zetu wa kale walioishi mapangoni, wanawake waliwapenda wanaume shujaa ambao wangeweza kujitoa muhanga kuwalinda wao na watoto wao. Mwanaume ambaye alikuwa na uwezo wa kujitoa muhanga alionekana kuwa na uwezo wa kuwinda bila hofu na kuzama porini kutafuta chakula kwa Ajili ya familia au kutafuta dawa kwa ajili ya matibabu kwa familia yake.

Kikubwa hapa ni ulinzi na usalama. Na hili linawafanya wanawake wengi kuwapenda mabaunsa kwa sababu hih hii ya ulinzi na usalama
Mwanaume mwenye nazo anaonekana kupendwa lakini hapa swala si fedha yake, bali anaonwa kama ndiye anayeweza kuilinda familia. Ukikuta wanawake wanavutiwa na wanaume wenye fedha, usishangae, kwani bado wanaongozwa na  haja yao kuu ya  kuhakikishiwa usalama wao.

Kwa kifupi ni kwamba kinachotafutwa na wanawake ni  amani nausalama.

Siku hizi  fedha imechukua nafasi katika kujihakikishia usalama wetu. Kila kitu siku hizi ni pesa na ndio maana wanawake kwa dhana ile ile ya kujihakikishia usalama wanavutiwa na wanaume wenye nazo.

Sio kwa sababu ya tamaa...... La hasha, ni kutaka kuwa na uhakika na maisha yake na familia yake.
Mwanamume akikosa sifa ya fedha ataangaliwa kwa ujasiri  na uchakarikaji.Kwa haya mwanamke anajua kwamba kwa kushirikiana naye mbeleni maisha yatakuwa mazuri na salama.
Ikitokea kwa mfano kaolewa na mwanaume mzigo au siku hizi huwaita "Dead alive" au mwanaume suruali, jukumu la kutafuta hulishika mwenyewe kwa sababu hamna jinsi na mara nyingi hufanikiwa kuzikamata kwa sababu anafanya hivyo kwa nia na dhamira ya kujihakikishia usalama.
Kama vile wanaume wanavyokosea kuoa kwa kutopiga hesabu zao vizuri katika kuoa vivo hivyo wanawake nao hukosea kwa kudanganyika na zile sifa za mwanaume za muda mfupi bila kuchunguza vizuri zaidi. 

Wapo ambao wakigundua kwamba mwanaume aliyeolewa naye ni mvivu na asiyejali familia anafungasha na kuondoka, lakini wapo ambao wanatafuta suluhu na kuamua kushika hatamu za kuendesha nyumba hawa ni wale wanaoogopa kufanya makosa kwa mara ya pili yaani kuondoka na kuangukia kwa mwanaume mwingine mwenye sifa zisizopendeza. Hawa wanakubali matokeo na kuamua kusimama kama wao, hawayumbishwi na huwakubali wenzi wao kama walivyo.

Wanawake wa aina hii mara nyingi kufanikiwa sana tofauti na wale wanaojipweteka na kubaki wakilalamika. Lakini naomba niseme kuwa wanawake kwa kiasi kikubwa ni mashujaa hawawezi kukaa na kuangalia familia ikianguka kwa sababu mwanaume hawawajibiki. Wengi sana tena kiasi cha kutosha husimama na kushika nyumba kwani wanajua kwamba nyumba ikianguka mara nyingi lawama huwaendea wao.

Pia mwanamke huvutiwa na mwanaume anayejali usalama wa wazazi na ndugu  zake Mwanamke yuko tayari kumpenda mume mwingine nje ya ndoa kama huyu mume ataonesha  upekee katika kuwa chukua wazazi wake.

Kwa mfano wapo wanaume wengi hali zinapokuwa ngumu huzikimbia familia zao na kuzitelekeza hata kwa miaka kadhaa, lakini wakirudi wanakuta familia ipo mbali kimandeleo na watoto wana hali nzuri. Hao ndiyo huitwa wanawake wa shoka. Lakini maendeleo hay0 huwa hayaji hivi hivi, yuko mwanamume aliyependwa badala ya aliyeikimbia familia.

Kwa hiyo swala la uelewa,umaridadi, utanashati katika siyo sifa zinazotazamwa na wanaume bali ni ulinzi na upendo, 

Kwa wanaume vigezo ni utii, na matunzo mazuri. Vitu hivi kwao ni muhimu katika swala zima la kutafuta mwenza. 
Heri ya Pasaka. 
UJUMBE MZITO WA PAPA FRANCIS
Hakuna familia isiyo na mapungufu. Hatuna wazazi wasio na mapungufu, sisi pia si wakamilifu, hatuoi au kuolewa na mtu asiye na mapungufu, kadhalika watoto wetu nao si wakamilifu. Tunayo manung'uniko au malalamiko kila mmoja dhidi ya mwenzake. Tumevunjana moyo na kukatishana tamaa. Kwa hiyo, hakuna ndoa iliyokamilika wala familia iliyoboreka bila kuwa na mazoea au utamaduni wa kusameheana.

Msamaha ni nguzo au msingi wa utulivu wa akili na uhai wa roho zetu. Kama hakuna msamaha, familia inakuwa uwanja wa migogoro na mlipuko wa ugomvi. Panapokosekana msamaha, familia inaugua. Msamaha unahuisha moyo, kwa kusafisha fikra na kuufanya moyo kuwa huru. Binadamu asiyesamehe hana amani moyoni na wala hana urafiki au muunganiko na Mungu.

Maumivu ni sumu inayodhuru na kuua. Hebu kiponye kidonda hicho cha moyo endapo kuna dalili za kujiumiza. Mtu asiyesamehe anajisababishia mwenyewe ugonjwa wa mwili, kiakili na kiroho. Ndiyo maana familia inapaswa kuwa sehemu ya uhai na si kifo; eneo la uponyaji na sio mahali pa magonjwa; jukwaa la msamaha na si la uovu. Msamaha huleta furaha pale uchungu ulipoleta maumivu; huleta uponyaji hata pale ambapo maumivu yalisababisha magonjwa.

Ujumbe huu wa Baba Mtakatifu umfikie kila mmoja wetu leo katika familia yake. Leo basi tuutafakari ujumbe huo muhimu.

Ewe  Mwenyezi Mungu Tusamehe makosa yetu tunayoyajua na yale tusiyoyajua, Aamin.

Muhimu:Kauli hii haimlengi mtu fulani , bali ni mafundisho kwa  mimi mwenyewe  na jamii yote kwa ujumla.


Image may contain: 1 person, outdoor

BABU HASSANI SHAGHIRA MTHOO
Eliamini Hassan ALI Salimu Ali Msangi. 
Pata mtiririko wa ukoo wa Salimu Shaghira kutoka kwa BANGALALA kwa Ufupi.
Wasangi ni uzao wa Bangalala aliyetoka huko Kenya sehemu itwayo Usangi miaka mingi iliyopita.Bangalala alizaa watoto wawili Yambii na Mnyatta.
Mnyatta yeye alirudi Kenya.Kwa hiyo habari zake hazijulikani kwa upana.
Yambii akamzaa Mang'a.Mang'a naye akamzaa Ndorokwa.
Ndorokwa akazaa mtoto akamwita jina la baba yake Mang'a. Huyu Mang'a Jr. akamzaa Mahu.
Mahu akamzaa Akavyo..Akavyo akamzaa Kiyanga.
Kiyanga akamzaa Mfuta, Mfuta akazaa watoto wawili Nzano na Setonga.
Sasa hivi nafuatilia uzao wa Setonga.
Yeyote anayejua uzao tokea setonga hadi hapi alipo anipe mtiririko huo.
Wasangi kwa sasa tiko wengi ili uweze kutambulika kuwa wewe ni nani na ni wa baba au ni wa kutoka kwa babuci yupi tunapaswa tuandike majina matatu au zaidi.Jina moja lilkifuatwa na Msang kwa mfano Abdalla Msangi, Ramadhani Msangi, au Adam Msangi halitoshi kukutambulisha kikamilifu.
Sasa, baada ya hilo angalizo, tuendelee na uzao wa Nzano.
Kwa upande wa Nzano yeye alioa wanawake wengi. Kwa jinsi hii akazaa watoto wanne. Ijumbi akiwa ni mtoto wake wa kwanza akifuata Kisarika na Komeja.
Mroki alikuwa mtoto wa nne wa Nzano, na wa mwisho kwa mke wa mwisho.
Ijumbi alizaa ukoo wa kina Senakanga ambao ni kina. Senguji na Bondera.
Komeja akawazaa Mlawa, Mramba, Idhina na Mchaimwa Huyu Mchaimwa alikuwa mwanamke uzao wake ni ukoo wa Saidi Mcholo.
Kisarika akawazaa Kisineni, Nguma,Ishiwa, Mghamba na Kinyonge Kinyonge ukoo wake ni wa kina Chakupewa.
Kisarika, Kisineni, Nguma, Mghamba koo zao ni za kufuatilia sina maeleza yake.
Tukija kwa Mroki mtoto wa Nzano wa mwisho kwa mke mdogo, huyu Mroki alimzaa mtoto mmoja akamwita Mthoo. Mthoo alizaliwa peke yake kama alivyozaliwa baba yake.
Mthoo alizaa watoto watatu Shaghira,Vichike na Nguluma.Vichike alikwa ni mwanamke na alikuwa ndiye mtoto wa kwanza kuzaliwa, akifuatiwa na Shaghira na Nguluma akiwa ni mziwanda.
Shaghira alikuwa mwiisilamu na aliitwa(Ali). Shaghira alizaa watoto wanne Hassaniakiwa wa kwanza akifuatiwa na Salimu, Ibrahimu na Selemani akiwa ndiye wa mwisho kwao.
Salimu akawazaa Ali (Shaghira Jr), Hatibu na Nauche. Huyu ni Nauche ni wa kike na ni kitinda mimba wa babu Salimu aka Kigingi
(Mbishi yakwe Namwai)
Chui aliyezaliwa na Namwai. Namwai ni mama yake.Babu Salimu.Babu Salimu alikuwa akijigamba kwa namna hiyo.
Mimi nimezaliwa na Ali (Shaghira Jr.) Salimu mtoto wa kwanza wa Salimu. Niliitwa Hassani jina la baba mkubwa wa babangu .hivyo mimi ni Hassan Jr
Huyu Hassan ambaye nimeitwa jina lake anaitwa Mthoo jina la babu yake hivyo na mimi ninatwa Mthoo wa tatu. Jina lake jingine la utani (nick name) aliitwa TILISHO.
Na mimi nina watoto Watatu Ali, Riziwani na Hatibu.
Ali ni jina la baba wa babu zangu. Alikuwa kasilimu na alikuwa imamu.
ALI mwanangu ni Ali wa tatu.
HUU NDIO MTI WA UKOO wa Salimu Ali (Shaghira)Mthoo.
KOO NYINGINE HAPO KATIKATI NI ZA KUJAZIA.
SIMULIZI hii nimesimuliwa na Babu Hassan ALi ambaye kwa jina la babu aliitwa Mthoo. Na mimi pia ni Mthoo wa tatu.
Eliamini : Msangi Nawashukuruni nyote mlio like post hii. Kwa kuwa tawi letu limeanzia kwa Nzano, nitaendeleza mtambao wa Wasangi wa tawi hili.Naomba ushirikiano wenu Wasangi wa kwa Nzano na Setonga.
Like · Reply · 1 h
Malaho Omari :Hahahaha weee kaka umenifurahisha sana mimi ni malaho mtoto wa mzee OMARI (SABUNI) wewe tumeachana hapo kwa setonga setonga alimzaa marisa na shanjarika marisa akamzaa Malaho na huyu malaho akamzaa salimu malaho JUMA malaho (babake mshare) Omari malaho...See more
Like · Reply · 1 hr
Eliamini Msangi :VYAKWA KIAMBO TUKO KARIBU SANA NAO, NAMI NITAFUATILIA.wasangi bwana wameenea sana.Omari mshare yule aliyekuwa akiishi Kwakoa.Mzee BONDERA baba yake na JUMANNE NA ERNEST BONDERA.
Chini kushoto ni babu Hassan Ali kulia babu Salimu Ali


Timu zote mbili Isamilo na Mwanza Sekondari zikiwa kwenye mkao wa picha ya pamoja.
Jana Ijumaa baada ya swala ya Ijumaa, timu ya walimu  Mwanza Sekondari na Shule ya Kimataifa ya  Isamilo (Isamilo International School) zote za hapa jiji la Mwanza, zilikuwa na mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu wanaume.

Mchuano huu wa mpira uliozishirikisha timu hizi mbili za shule za sekondari jijini hapa, ulikuwa ni kivutio kikibwa cha kuanzia mapumziko ya mwishoni mwa juma.

Kwenye kinyanganyiro hiki Isamilo iliwachapa Mwanza sekondari bao tatu kwa moja. 

Mabao yote yalifungwa kipindi cha kwanza.Goli la kwanza la Isamilo lilifungwa na Mwl.Manda Rafaeli na la pili na Mwl. Peter Kiswaga kwa mkwaju  aloupiga akiwa kiasi cha mita 80  hadi langoni mwa goli la ‘ Mwaseco’ na kumbabatiza mlinda lango na mpira kutinga kimiani. 

Goli la kufutia machozi la 'Mwaseco' lilifungwa na Mwl. Elias Charles  kwa mkwaju alioupokea toka kwa Mwl. David Nestory.

Goli la tatu la Isamilo  lililodumu hadi kipenga cha mwisho lilifungwa kipindi hicho hicho cha kwanza na  Mwl. Nijel Moye baada ya kizaa zaa kilichotokea langoni mwa goli la ‘Mwaseco’ baada ya mkwaju wa kona  ulioletwa langoni na Mwl. Cairl.

Timu ya Mwanza Sekondari iliundwa na kikosi cha walimu wafuatao. Mwl. David Nestory  huyu ni mkuu wa shule ya Mwanza Sekondari na alicheza  namba 11.

Wengine ni Mwl. Abeli  Kalilo ambaye alikiwa nahodha wa timu akicheza nambari  8. 

Sanjari nao ni Mwl. Ahmed Hamdan  nambari 4 mgongoni , Mwl.Boaz Edward nambari  9, Mwl. Eliasi Charles nambari  10. na mlinda lango wao Mwl. Shata Elia.

Timu hizi zilichezesha wachezaji saba saba. Mchezaji wa saba  wa  Mwaseco' ni Mwl. Jeremiah Kinshuli aliyevalia jezi namba 7 mgongoni. 

Waliokuwa kwenye benchi kwa 'Mwaseco' ni Mwl. Dickson  Masomi, Abswamadu Nyenye, Ramadhani Bilali na Vitalius Marisiale.
Kikosi kizima cha 'Mwaseco ' Wana 'SOMA MPAKA UFE' na washauri wa timu wakiwa katika pozi la picha ya pamoja

 Safu ya Isamilo iliundwa na  Mwl. Appollo aliyekuwa langoni. Mwl. Marx nambari 13, Mwl. Jake nambari 10, Mwl. Nijel Moye nambari 4,Mwl. Cairl nambari 3, Mwl. Peter Kiswaga  nambari 14,  na Mwl.Manda Rafaeli nambari 7. 

Walokuwa benchini kwa upande wa Isamilo ni: Mwl. Joseph Sospeter, Mwl.Godfrey Francis na Mwl. Robert  Robert.

Timu zote zilicheza mchezo  mzuri wa kistaarabu usio na fujo.Katika kipindi cha pili mpira ulichezwa kwa pasi nyingi na kwa kasi kubwa lakini hakukuwa na timu yeyote iliyoliona lango la mwenzie. 

Kwa upande wa timu ya 'Mwaseco' mchezaji Ahmed Hamdani alikuwa ndiye nyota wa mchezo kwa kuidhibiti timu ya Isamilo kuliona lango lao. Hasa kipindi cha pili aliweka juhudi za ziada.

Timu ya Isamilo ilipambwa na walimu wageni. Kati ya wachezaji wao kumi nusu walikuwa wenyeji na nusu  nyingine wageni. Hii ni kwa sababu shule hii ni ya kimataifa hivyo ina walimu wazungu wengi.
Eliasi Charles mfungaji wa goli la Mwaseko na mfunngaji mwenzie Nigeli Moye wa Isamolo na mgongoni mwao aliya na glovzi  mikonono ni mlinzi wa Isamilo Mwl.Appollo'
Pamoja na kufungwakipindi cha kwanza, kipindi cha pili wana Mwaseco walijihami vilivyo kwa kuelekeza mipira ya hatari kwenye lango la Isamilo na kuwazibiti kuongeza mabao.

Pamoja na makeke yao haya hawakuweza kulipenya lango la Isamilo. Kikwazo chao kikubwa kilikuwa ni mlinda lango wa Isamilo Mwl. Appollo. Hakika mlinda mlango huyu alikuwa nyota kwa timu hii ya Isamilo.Alikuwa akidaka mipira  iliyokuwa ni magoli dhahiri.

Hadi kipenga cha mwisho magoli yalikuwa Mwaseco moja na Isamilo tatu.

Kwa wana Mwaseco zaidi ya kufungwa, mchezo huu ulionesha mabadiliko kiasi fulani kwao kwani  Ijumaa iliyopita ya tarehe  27 Februari 2015 walicheza na Sekondari ya Bugarika wakachapwa mabao SABA kwa ‘nunge.’


Pale mwishoni mwa mechi nilimuuliza nahodhda wa 'Mwaseco' Mwl. Abeli kalilo kama kwa vichopo hivi vikali viwili mfululizo bado wanayo hamu ya kualika timu nyingine? Naye akalijibu kwamba wanakaribisha maombi toka timu yeyote iliyo tayari kucheza nao huku akionesha hamu ya kuwaalika Shule ya Sekondari Nsumba kwa madai eti Nsumba haina historia ya kuwafunga.
Mwl Elibariki Kimei wa 'Mwaseco' na Mwl, wa Isamilo  wakiongea na kati yao kijana wa Mwl wa Isamilo
 akishangilia ushindi wa Isamilo baada ya kipenga cha mwisho.
Kiongozi wa CCM  kata,
akimkaribisha mgombea kwa tiketi
ya CCM, mama Mtalo kunadi
sera zake na kuomba kura
Uchanguzi wa mwenykiti wa mtaa Sweya ulioahirishwa  kutokana na kufariki Bw. Pius Masome aliyekuwa mmoja wa wagombea kiti hicho kupitia CCM utarudiwa hapo Jumapili ijayo ya tarehe 8, Februari 2015.

Marehemu Bw. Pius alikuwa kasimama kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM na mgombea mwenanzake Bw. Fred alisimama kwa tiketi ya CHADEMA.

Kwa bahati mbaya Bw. Pius aliugua siku chache kabla ya uchaguzi
na siku hiyo uchaguzi ukifanyika alifariki akiwa katika matibabu hospitali ya Bugando kipindi kura zikiendelea kupigwa.

Siku ya Jumapili ya tarehe 1, Februari 2015 CHADEMA ndio walioanza kulipanda jukwaa na kuanza kunadi sera zao na siku iliyofuata ya Jumatatu tarehe 3,Februari 2015 CCM  walilipanda jukwaa kuziweka wazi sera zao.



Hakika safari hii wana Sweya wamekumbwa na changamoto la aina yake tofauti na awali linalotokana na mabadiliko waliyoyafanya wana CCM ya kumsimamisha mgombea mwanamke.

Kwa kura za awali  CHADEMA ilikuwa ikiongoza zidi ya CCM katika mtaa huu wa Sweya na walishinda nafasi zote za wajumbe wa mtaa.

Tunachojiuliza ni kumbwa mabadiliko haya yatabadili mwelekeo na msimamo wa wana Sweya wengi waliowapa CHADEMA ushindi wa wajumbe wa serikali ya mtaa?

Bw. Reverian Mtalo akimnadi mgombea  wa CCM ambaye pia ni mkewe alisema, anaweza na ameridhia uamuzi wake huo.

"Mke wangu amekua kiongozi katika ngazi mbalimbali kwenye vikundi vya kina mama, vya kijamii na vya kidini na aliponijulisha nia yake hii ya kugombea nafasi hii ya uenyekiti wa mtaa sikuwa na  wasiwasi wala shaka yeyote,juu ya uamuzi wake huu na nilimruhusu na naamini anaweza" alisema Bw, Mtalo.  
Bw, Mtalo akimnadi mkewe.
Shangwe na nderemo zilirindima kiwanjani humo pale Bw, Mtalo alipouliza swali,"Wanawake mnaweza hamuwezi?"

Kikundi cha wacheza ngoma na maonesho ya sarakasi kiliingia uwanjani na kuonesha maonesho, ambayo yalizikonga nyoyo za wasikilza kampeni kisawasawa.
Kikundi cha burudani 'kikijimwayamwaya' kweye kampeni hizi

Ukweli ni kwamba kampeni zinaonesha wagombea wa pande zote kuiva kisiasa na kutambua kile wanachokitaka kwani pande zote walimalizia kwa kuomba wananchi kuwapa kura za ndiyo.

Kilichobakia ni uamuzi wa wana sweya ni nani kati ya wagombea hawa kawashawishi kisera na wala sio malumbano ambayo wanaona hayana masilahi kwao.
Wana Sweya wakimsikiliza mgombea wa CCM  kwa makini

Baadhi ya wana Sweya walisikika wakidai kuwa wanataka kiongozi wa watu, mchapa kazi na mwenye sera zenye mashiko na suala la Chama si msingi MKUU kwao.

Mtoto James Magoti  akisaidiwa 
na kaka yake kuonesha
 sehemu aliyoumwa
Watoto watano, mbuzi na mbwa wa Justine Mwenula wang’atwa katika mitaa ya Sweya A na B Nyegezi, viunga vya Jiji la Mwanza na mbwa anayeshukiwa kuwa na kichaa.

Mbwa huyu ameanza kung’ata kuanzia Jumamosi ya tarehe 24, Junuari watoto watatu, James Magoti, Irene Mashaka na aliyejulikana kwa jina moja la Bahati.

 Mbuzi aliyeng’twa ni wa ndugu John Ngugi na inasemekana aliuliwa hapo hapo na mbwa huyu.

Leo, Jumapili  tarehe 25 Januari, 2015, asubuhi, balozi Otieno Kadondi aongoza kundi kubwa la wana Sweya wakiwa wamebeba mikuki, nondo, marungu na magongo kumsaka mbwa huyu.

Mtoto Bahati na majeraha ya meno ya mbwa mgongoni.
Mwenyekiti mteule ndugu Joseph Masome naye hakuwa nyuma, alishiriki zoezi hili la kumsaka mbwa huyu aliyetokea kuwa tishio la mtaa wote wa Sweya ndani ya siku hizi mbili.

Hasira za wananch kwa mbwa huyu zilipanda zaidi pale mbwa huyu alipong’ata watoto wengine wawili mmoja mtoto wa Bahati ambaye ni bubu na mwingine ambaye jina lake halikupatikana kwa uhakika lakini ilidaiwa kuwa ni mjukuu wa Marehemu Chacha Kichele.

Baada ya msako mkali kuzunguka mitaa yote ya Sweya A na Sweya B wanakijiji walifanikiwa kumtia mikononi huyumbwa  na kumuua hapo hapo.

Katika harakati za kumsaka mbwa huyu mbwa wengi walionekana kuzagaa ovyo hapa na pale pasi na kufungiwa ndani kama inavyotakiwa kwa wanaofuga wanyama hawa.

Imefahamika pia kwamba kumezuka kamtindo ka baadhi ya watu kuwaingiza mbwa kwenye gari na kwenda kuwatupa sehemu za mbali hususani nje ya mji kwa dhana kuwa hawawezi kujua njia ya kurudi walikokuwa awali..


Wana kijiji katika harakati za kumsaka mbwa nwenye kichaa 
Hali hii inaonesha kuwa mbwa wanafugwa kiholela na wengi wakiwa hawajachanjwa kuwakinga na ugonjwa wa kichaa cha mbwa (rabies).

Wakati wa zoezi la kumsaka mbwa huyu, wananchi walisikika wakiilalamikia idara ya mifugo, jijini Mwanza kwa kushindwa kwake, kutimiza wajibu wake wa kudhibiti ufugaji holela wa mbwa na kuhimiza uchanjaji wa mbwa kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha mbwa.

“Gharama ya kumchanja mtu akinga’twa na mbwa kumkinga na kichaa cha mbwa ni zaidi ya laki moja.’’Mmoja wa wasakaji wa mbwa huyu alisikika akisema.
Ukweli unabakia pale pale  kuwa gharama za kumhudumia mtu anapong’atwa ni kubwa zaidi ya hapo haswa ikizingatiwa kuwa jamaa na majirani huingiwa na hofu na kushindwa kufanya shughuli zao kama kawaida na  kwa kuwa kunakuwepo na upoteaji wa muda mwingi katika kushughulikia matibabu.

Tunaitaka mamlaka husika kudhibiti kuzagaa kwa  mbwa na paka kiholela, jijini humu hali ambayo hubainishwa kwa kugongwa gongwa mbwa na paka mara kwa mara mabarabarani.


Mbwa aliyeuliwa 
Pamoja na udhibiti huu ni vyema uchanjaji wa mbwa na paka ukawa unafanywa kila mwaka.

Zoezi hili si tu kwamba litaleta utulivu bali  bado litakuwa ni njia mojawapo ya kuongeza pato la jiji.

Tatizo hili laweza kuonekana ni la hapa Sweya lakini laweza kuwa ni kiashiria cha uwepo kwa tatizo hili sehemu nyingine.


Balozi OTIENO Kadondi  aliyehamasisha usakaji wa 
mbwa huyu aliyekuwa tishio la mitaa miwili ya SWEYA.
Mwisho wa yote mbwa huyu alifukiwa kwenye shimo refu walochimba wana mtaa na kumfukia.

Wasiwasi ukabakia kwa wale waloumwa na mbwa huyu  juu ya kupatiwa matibabu sahihi na pia  kuchunguza mwenendo wa mbwa walioumwa na huyu anayedhaniwa kuwa na kichaa.

'Wananzengo' wakishuhudia akifukiwa
aridhini mbwa aliyekuwa tishio kwao







POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza