WANAWAKE HUVUTIWA NA WANAUME WENYE SIFA IPI?
MWANAMME NI KAZI |
Hii inamaanisha kwamba katika urafiki wa kawaida na wa kimapenzi
na wa kindoa, wema au ukarimu ulionekana kwamba ni kigezo cha
kawaida tu na sio kipaumbele chao.
Tukirudi kwa mababu zetu wa kale walioishi mapangoni, wanawake waliwapenda wanaume shujaa ambao wangeweza kujitoa muhanga kuwalinda wao na watoto wao. Mwanaume ambaye alikuwa na uwezo wa kujitoa muhanga alionekana kuwa na uwezo wa kuwinda bila hofu na kuzama porini kutafuta chakula kwa Ajili ya familia au kutafuta dawa kwa ajili ya matibabu kwa familia yake.
Kikubwa hapa ni ulinzi na usalama. Na hili linawafanya wanawake wengi kuwapenda mabaunsa kwa sababu hih hii ya ulinzi na usalama
Mwanaume mwenye nazo anaonekana kupendwa lakini hapa swala si fedha yake, bali anaonwa kama ndiye anayeweza
kuilinda familia. Ukikuta wanawake wanavutiwa na wanaume wenye fedha,
usishangae, kwani bado wanaongozwa na haja yao kuu ya kuhakikishiwa usalama wao.
Kwa kifupi ni kwamba kinachotafutwa na wanawake ni amani nausalama.
Siku hizi fedha imechukua nafasi
katika kujihakikishia usalama wetu. Kila kitu siku hizi ni pesa na ndio
maana wanawake kwa dhana ile ile ya kujihakikishia usalama wanavutiwa na wanaume
wenye nazo.
Sio kwa sababu ya tamaa...... La hasha, ni kutaka kuwa na uhakika na
maisha yake na familia yake.
Mwanamume akikosa sifa ya fedha ataangaliwa kwa ujasiri na uchakarikaji.Kwa haya mwanamke anajua kwamba kwa
kushirikiana naye mbeleni maisha yatakuwa mazuri na
salama.
Ikitokea kwa mfano kaolewa na mwanaume mzigo au siku hizi huwaita "Dead alive" au mwanaume suruali, jukumu la kutafuta hulishika mwenyewe kwa sababu
hamna jinsi na mara nyingi hufanikiwa kuzikamata kwa sababu anafanya hivyo kwa
nia na dhamira ya kujihakikishia usalama.
Kama vile wanaume wanavyokosea kuoa kwa kutopiga hesabu zao vizuri
katika kuoa vivo hivyo wanawake nao hukosea kwa kudanganyika na zile sifa za
mwanaume za muda mfupi bila kuchunguza vizuri zaidi.
Wapo ambao wakigundua
kwamba mwanaume aliyeolewa naye ni mvivu na asiyejali familia anafungasha na
kuondoka, lakini wapo ambao wanatafuta suluhu na kuamua kushika hatamu za
kuendesha nyumba hawa ni wale wanaoogopa kufanya makosa kwa mara ya pili yaani
kuondoka na kuangukia kwa mwanaume mwingine mwenye sifa zisizopendeza. Hawa
wanakubali matokeo na kuamua kusimama kama wao, hawayumbishwi na huwakubali
wenzi wao kama walivyo.
Wanawake
wa aina hii mara nyingi kufanikiwa sana tofauti na wale wanaojipweteka na kubaki
wakilalamika. Lakini naomba niseme kuwa wanawake kwa kiasi kikubwa ni mashujaa
hawawezi kukaa na kuangalia familia ikianguka kwa sababu mwanaume hawawajibiki.
Wengi sana tena kiasi cha kutosha husimama na kushika nyumba kwani wanajua
kwamba nyumba ikianguka mara nyingi lawama huwaendea
wao.
Pia mwanamke huvutiwa na mwanaume anayejali usalama wa wazazi na ndugu zake Mwanamke yuko tayari kumpenda mume mwingine nje ya ndoa kama huyu mume ataonesha upekee katika kuwa chukua wazazi wake.
Kwa
mfano wapo wanaume wengi hali zinapokuwa ngumu huzikimbia familia zao na
kuzitelekeza hata kwa miaka kadhaa, lakini wakirudi wanakuta familia ipo mbali
kimandeleo na watoto wana hali nzuri. Hao ndiyo huitwa wanawake wa
shoka. Lakini maendeleo hay0 huwa hayaji hivi hivi, yuko mwanamume aliyependwa badala ya aliyeikimbia familia.
Kwa hiyo swala la uelewa,umaridadi, utanashati katika siyo sifa zinazotazamwa na
wanaume bali ni ulinzi na upendo,
Kwa wanaume vigezo ni utii, na matunzo mazuri. Vitu hivi kwao ni muhimu katika swala zima la kutafuta mwenza.
0 comments: