Showing posts with label Habari za Kimataifa. Show all posts
MWANAMME NI KAZI
Katika utafiti wa hivi karibuni, watafiti wamegundua kwamba, wanawake wanawapenda wanaume wasio waoga na mashujaa kuliko wale waoga. Ushujaa wa wanaume ni kigezo kikubwa kwa wanawake kuwapenda marafiki wa kiume wa muda mrefu na muda mfupi. 

Hii inamaanisha kwamba katika urafiki wa kawaida na wa kimapenzi na wa kindoa, wema au ukarimu ulionekana kwamba ni kigezo cha kawaida tu na sio kipaumbele chao.

Tukirudi kwa mababu zetu wa kale walioishi mapangoni, wanawake waliwapenda wanaume shujaa ambao wangeweza kujitoa muhanga kuwalinda wao na watoto wao. Mwanaume ambaye alikuwa na uwezo wa kujitoa muhanga alionekana kuwa na uwezo wa kuwinda bila hofu na kuzama porini kutafuta chakula kwa Ajili ya familia au kutafuta dawa kwa ajili ya matibabu kwa familia yake.

Kikubwa hapa ni ulinzi na usalama. Na hili linawafanya wanawake wengi kuwapenda mabaunsa kwa sababu hih hii ya ulinzi na usalama
Mwanaume mwenye nazo anaonekana kupendwa lakini hapa swala si fedha yake, bali anaonwa kama ndiye anayeweza kuilinda familia. Ukikuta wanawake wanavutiwa na wanaume wenye fedha, usishangae, kwani bado wanaongozwa na  haja yao kuu ya  kuhakikishiwa usalama wao.

Kwa kifupi ni kwamba kinachotafutwa na wanawake ni  amani nausalama.

Siku hizi  fedha imechukua nafasi katika kujihakikishia usalama wetu. Kila kitu siku hizi ni pesa na ndio maana wanawake kwa dhana ile ile ya kujihakikishia usalama wanavutiwa na wanaume wenye nazo.

Sio kwa sababu ya tamaa...... La hasha, ni kutaka kuwa na uhakika na maisha yake na familia yake.
Mwanamume akikosa sifa ya fedha ataangaliwa kwa ujasiri  na uchakarikaji.Kwa haya mwanamke anajua kwamba kwa kushirikiana naye mbeleni maisha yatakuwa mazuri na salama.
Ikitokea kwa mfano kaolewa na mwanaume mzigo au siku hizi huwaita "Dead alive" au mwanaume suruali, jukumu la kutafuta hulishika mwenyewe kwa sababu hamna jinsi na mara nyingi hufanikiwa kuzikamata kwa sababu anafanya hivyo kwa nia na dhamira ya kujihakikishia usalama.
Kama vile wanaume wanavyokosea kuoa kwa kutopiga hesabu zao vizuri katika kuoa vivo hivyo wanawake nao hukosea kwa kudanganyika na zile sifa za mwanaume za muda mfupi bila kuchunguza vizuri zaidi. 

Wapo ambao wakigundua kwamba mwanaume aliyeolewa naye ni mvivu na asiyejali familia anafungasha na kuondoka, lakini wapo ambao wanatafuta suluhu na kuamua kushika hatamu za kuendesha nyumba hawa ni wale wanaoogopa kufanya makosa kwa mara ya pili yaani kuondoka na kuangukia kwa mwanaume mwingine mwenye sifa zisizopendeza. Hawa wanakubali matokeo na kuamua kusimama kama wao, hawayumbishwi na huwakubali wenzi wao kama walivyo.

Wanawake wa aina hii mara nyingi kufanikiwa sana tofauti na wale wanaojipweteka na kubaki wakilalamika. Lakini naomba niseme kuwa wanawake kwa kiasi kikubwa ni mashujaa hawawezi kukaa na kuangalia familia ikianguka kwa sababu mwanaume hawawajibiki. Wengi sana tena kiasi cha kutosha husimama na kushika nyumba kwani wanajua kwamba nyumba ikianguka mara nyingi lawama huwaendea wao.

Pia mwanamke huvutiwa na mwanaume anayejali usalama wa wazazi na ndugu  zake Mwanamke yuko tayari kumpenda mume mwingine nje ya ndoa kama huyu mume ataonesha  upekee katika kuwa chukua wazazi wake.

Kwa mfano wapo wanaume wengi hali zinapokuwa ngumu huzikimbia familia zao na kuzitelekeza hata kwa miaka kadhaa, lakini wakirudi wanakuta familia ipo mbali kimandeleo na watoto wana hali nzuri. Hao ndiyo huitwa wanawake wa shoka. Lakini maendeleo hay0 huwa hayaji hivi hivi, yuko mwanamume aliyependwa badala ya aliyeikimbia familia.

Kwa hiyo swala la uelewa,umaridadi, utanashati katika siyo sifa zinazotazamwa na wanaume bali ni ulinzi na upendo, 

Kwa wanaume vigezo ni utii, na matunzo mazuri. Vitu hivi kwao ni muhimu katika swala zima la kutafuta mwenza. 

 
Naibu Waziri wa fedha na Mbunge wa Iramba Mwigulu 
Lameck Nchemba ndani ya ukumbi wa Nyerere,
chuo cha Mipango mkoani Dodoma

Leo Jumapili ya tarehe 31/05/2015  Naibu Waziri wa fedha na Mbunge wa Iramba Mwigulu  Lameck Nchemba ndani ya ukumbi wa Nyerere,chuo cha Mipango mkoani Dodoma aweka nia yake ya kutaka kuwa Raisi Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kupitia tiketi ya CCM.


Kauli mbiu ya Mwigulu ni ‘Mabadiliko ni Vitendo Wakati ni Sasa.’
Katika hotuba yake Mwigulu alianza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, wazee, ndugu zake, wananchi wake wa Iramba na wananchi wote waliohudhuria hafla hiyo ya kutangaza nia.

Mwigulu pia amempongeza Rais Kikwete kwa kumuamini na kumteua katika nyadhifa mbalimbali.
Amesema ameamua kutangaza nia akiwa mkoani Dodoma ili kuondoa dhana ya ‘ukwetukwetu’ iliyozoeleka miongoni mwa viongozi wengi.


Akaongeza kuwa Dodoma ni makao makuu ya taifa na chama chake ndiyo maana amefanya hivyo.Na akichaguliwa serikali yake itahamia Dodoma.

Aidha Mwigulu ameeleza mambo matatu yaliyomsukuma kutangaza nia kuwa ni pamoja na:
-Kutaka Mabadiliko
-Kujua mbinu za mabadiliko.
-Utayari wa kufanya mabadiliko.

Kiongozi huyo ameeleza jinsi anavyozijua fika shida za Watanzania na umasikini walionao kwani hajausoma kwenye vitabu bali ameuishi.
Mwigulu ameeleza pia alivyobeba zege baada ya kumaliza chuo kikuu na mke wake akiwa mama ntilie akiwapikia yeye na vibarua wengine wa ujenzi.
Mwigulu awa ni wa tatu ndani ya wana CCM walio jitokeza hadi sasa kutangaza nia.

Leo hii hii  nyakati za saa tano asubuhi hapa jijini Mwanza Mheshiwa Wassira alitangaza nia ya kuwa mmoja wa wanaotarajiwa kuteuliwa na CCM  kugombea Uraisi hapo Octoba ndani ya kumbi maarufu hapa  jijini Mwanza.Kauli mbiu yake ikiwa ni Uadilifu mbele na kusisitizia  siasa za uchumi huria ndani ya falsafa ya Ujamaa kupitia ushirika.

Mwigulu yeye katoka na kauli mbiu ya 'Mabadiliko ni vitendo wakati ni huu.' kama nilivyotangulia kuieleza.

Jana kule Arusha ndani ya viwanja vya Shekh Amri Abeid Mheshimiwa Lowassa alikuja na kauli mbiu ya ; "Elmu kwanza."
Mwigulu toka utotoni mwake wazazi wake wanadhihirisha kuwa ameonesha kuwa na kipaji cha uongozi.Hili limeonekana hadi akiwa shuleni,chuo kikuu mpaka sasa.

Mwigulu anawaomba watanzania na wana CCM kumkubali na akaahidi kuwavusha kufikia uchumi wa kipato cha kati.

Amesema tatizo kuu la nchi  ni rushwa, ubadhirifu na kufanya kazi kwa mazoea. Amewahakikishia watanzaniai kwamba hivyo ndivyo vipau mbele vyake  wakimpa ridhaa ya kuliongoza taifa hili.Kwani anayajua matatizo ya watanzania, amejiandaa na nia anayo.

Aidha aliongezea kwa kusema kuwa yeye amebeba ajenda ya wananchi.na alichokieleza kinatokana na ufahamu wake kwa watanzania na wana CCM. na yuko tayari kuwatumikia kwa moyo wake wote na nguvu zake zote.Akisisitiza kuwa umasikini wa watanzania hakuusoma vitabuni bali ameuishi.

Mwigulu na Familia yake
Shida za maji na madawa anasema ameziishi. Akasimulia kisa cha chumba kilichokuwa kikifumgwa sana wakati wa utoto wao ni chumba cha maji na mtoto aliyekuwa anakunywa maji mara kwa mara alionekana kuwa ni mtoto mkorofi.

Aliendelea kudai kuwa hatakuwa na huruma na uvumilivu  kwa wala rushwa na wahujumu uchumi na atazingatia masilahi ya wafanyakazi.
Kuhusu tatizo la ajira amesema kwa kufufua viwanda ambako vijana watafanya kazi kwa 'shift' kwa hatua hii anaamini itapunguza au kuondoa kabisa tatizo la ajira.

Akisisitizia wajibu wa awamu yake,alieleza mafanikio ya awamu zilizotangulia na mafanikio yaliyopatikana katika awamu hizo.

Alisema awamu ya kwanza  ilifanikiwa katika kutafuta uhuru wa taifa hili  na kujenga misingi ya umoja wa kitaifa na ya pili ilibadili mfumo wa uchumi wa nchi hii na kujenga uwezo  wa watanzania kiuchumi na kupunguza serekali kushikilia njia za kiuchumi kwa asilimia mia moja na kuruhusu kusaidiwa.

Kwa awamu ya tatu akasema  ilijenga taasisi na  mifumo ya huduma za kitaifa. Awamu ya nne imejishughulisha na miundo mbinu, Kujenga rasilimali watu na kujenga misingi ya uchumi wa kisasa.

Akieleza kazi za awamu yake alishauri watu kutompima raisi kwa kile alichofanya kwani hakuna zawadi wanayopewa bali wawapime kwa yale wanayotarajia kufanya.
"Raisi wa awamu ya tano atapimwa kwa kile atakachofanya na si kile alichowahi kufanya."akasisitizia.

Akawabainisha wana CCM na watanzania  wote kuwa yeye  akipewa ridhaa ya kuliongoza taifa hili,afanya mambo makuu matatu, kazi ya kwanza na kubwa kulika zote ni kuipeleka nchi kuwa nchi ya  kipato cha kati na wananchi wake kuwa wananchi wa  kipato cha kati. Kazi ya pili akasema ni kujenga taifa linalojitegemea kibajeti. Kazi ya tatu kuwajenga uwezo wa wananchi wa kumiliki uchumi wao wenyewe.

Akakomelea kwa kusema miaka hamsini ya kuwa taifa ombaoba na la watu masiki hali tunazo rasilimali za kututoa hapo sasa basi ni mwisho.

Kuhusu muungano na ulinzi na usalama wa nchi alisema hivyo vitakuwa pia vipaumbele katika serikali yake.

Kama mpenzi wa michezo,suala la michezo hakuliweka kando. Alimalizia kwa kudai kuwa yako mengi ila kutokana na muda hayo yatatosha kumpima kama anafaa au la.

Aliendelea na suala lake ambalo likuwa kama silaha yake ya mapambano, suala la mazoea."Ukichagua kiongozi kwa mazoea atafanya kazi kwa mazoea na mazoea siku zota ni yale yanayomnufaisha mhusika yeye mwenyewe na si kwa masilahi ya wengi."Mara kadaa alirudia kauli hii.

UKUMBI ULIVYOKUWA UMEJAA.
Taarifa zinadai wako watangaza nia zaidi ya thelathini kutoka kwa CCM peke yake bado hatujaanza kusikia kutoka  vyama vingine. Watanzania kazi kwetu kuwasikiliza na kuchambua upi mpunga kwenye kauli za wanaojinadi hawa na zipi ni pumba.
MWIGULI HAKIKA PAMOJA NA VIJINENO VYA HAPA NA PALE YAELEKEA AKAWA CHAGUO LA WENGI.
Dr. Rashidullah Khan, Mwenyekiti wa Baraza Kuu
 la Madawa India (CCIM), New Delhi,  India,
 akimpatia Afisa Mkuu wa kampuni ya madawa ya
 HOOTONE Dr. Sayyed Habib KarimTuzo bora
ya kitaifa kwa ajili ya "Utafiti juu ya dawa ya
tiba ya VVU na UKMWI " katika mkutano mkuu
uliojumuisha wajumbe  wote wa 'India Tibbi Congress'
uliofanyika huko Mumbai Desemba  ya  21, 2013.
Ni muda wa zaidi ya miaka thelathini sasa toka ugonjwa wa Ukimwi utambulike na tafiti nyingi zimefanywa kutoka kona mbalimbali za dunia kuutafutia tiba na kinga pasipo na mafanikio ya kuridhisha.

 Pamoja na tafiti hizo shirika la afya duniani limekuwa likifuatilia kwa karibu jitihada  za tafiti hizi  na pengine kuzisimamia au kuzichangia.

Lakini hali inavyoonekana suala hili kwa upande mmoja limekuwa lina sura ya ushindani ndani yake wa nani awe wa kwanza kuwa kinara wa ugunduzi huu.

Mashirika mengi ya kitafiti ulimwenguni yamekuwa yakitoa taarifa za tafiti zao zikiwa bado hazijaiva..

Majaribio yakuthibitisha dawa na chanjo zilizogunduliwa yamefanywa mengi na matokeo yaliyopokelewa ni mengi lakini cha ajabu tunaambiwa chanjo wala tiba haiko karibu kupatikana.

Lakini matumaini hayapo kwani inadaiwa yanahitajika marekebisho ya mapungufu yanayojitokeza.

Sababu kuu ya kushindikana kupatikana dawa au chanjo ni madai kwamba kirusi cha UKIMWI si aina moja na pia hujibadili badili haraka kwa kujihami na dawa au chanjo zilizopatikana.

Kwa maelezo na majaribio ya Wahindi waliyoyaonesha huenda wakawa wamefuzu.kupata  Dawa yaUKIMWI. Shuhuda za wagonjwa waliopona zinatia matumaini.

Katika ripoti ya utafiti wa Dawa yao ya  Unani Anti-HIV Drug  katika kikao cha kimataifa huko TIANJIN, CHINA tarehe 1-3 Desemba  2006, RIPOTI yao inatia matumaini.

Cha kushangaza ni kwamba hivi ni kwa nini bado WHO iko kimya hadi sasa kwa taarifa nzuri na za kutia matumaini kama hizi.

Kingine cha ajabu zaidi  ni viongozi wa nchi zetu hizi zinzoendelea  na wenye nafasi za kifedha kuzidi kukimbilia India kwa matibabu, Au sababu za kumiminikia kwao huko ni kama zile za kwa babu wa Loliondo.

Kama nasi tungekuwa na  uwezo nadhani hospitali zetu zingefungwa maana wote tungeishia India kama tulivyojazana kwa babu wa Loliondo.

Waswahili wanasema lisemwalo lipo na kama halipo laja.Wahindi hawataishia kutuokoa kwa usafiri wa bajaji bali nadhani watakuja kuwa magwiji wa masuala ya tiba pia.


Kwa  uthibitisho zaidi juu ya uponyaji huu, huu hapa  ushuhuda wa mgonjwa wa ukimwi aliyepona kwa dawa hii.

Aliyeko kutokea kushoto ni  Chief Justice Richard Banda, mkewe akifuatia  Joyce Banda Raisi wa  Malawi. Aliyeketi mbele ni Anjimile mpigisha kura. Wakiwa msitarini kupiga kura  Katika jimbo la Zomba, Malawi, Jumanne,ya Mei 20, 2014 Bi Joyce Banda Alipambana na Wagombea12 Katika Uchaguzi huu.

Rais wa Malawi adai kuwa ni  mahakama pekee ndiyo  iwezayo kuamua mgogoro wa matokeo ya kura nchini humo.


Lilomgwe Malawi  - Rais wa Malawi Joyce Banda alisema jana Alhamisi, 29,Mei 2014 kwamba yuko tetayari kuachia ngazi kama Mahakama Kuu itaridhia kuwa uchaguzi wa wiki iliyopita ambako mpinzani wake anadaiwa kuwa na kura zaidi utarudiwa. 

Mpinzani wake huyu anaonekana ndiye  mshindi.Banda hakubaliani na matokeo kwa kudai kuwa kura zilihesabiwa kwa udanganyifu.

Mahakama Kuu ilitarajiwa kutokana hukumu leo siku ya Ijumaa Hukumu ambayo ingeiwezesha Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC)  kutangaza matokeo ya Mei 20  ambayo mpinzani wa Banda ndiye aliye na uwezekano wa kuwa mshindi, au kurudia zoezi la uhesabuji upya,  mchakato ambao unaweza kuchukua muda wa miezi miwili.

Nchi hii ya kusini mwa Afrika inayokabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi inasubiri uamuzi huu wa kimahakama wa ama Tume itangaze matokeo yaliyopatikana au  kurudia uhesabuji wa kura upya. 

Uanuzi ambao unaweza kuleta ghasia katika uchaguzi huu wa  mfumo wa vyama vingi toka  ule wa chama kimoja uliokuwepo tokea miongo miwili iliyopita.

"Nimewaambia MEC  na wadau kwamba mimi nitaukubali uamuzi wa mahakama, " Banda aliiambia Reuters alipofanya mahojiano nao katika mji mkuu wa Malawi Lilongwe.

"Mimi nilitoa uhuru ili uchaguzi uendeshwe kwa misingi ya haki, uhuru na usawa.Yote haya ni   katika  kutetea haki ya wananchi wa Malawi katika wakati huu muhimu ili  kuhakikisha kuwa kiongozi anayechaguliwa anachaguliwa kwa njia ya haki na kuaminika, " aliongeza.

Uchaguzi ulikumbwa na matatizo mengi. Vifaa vya kupigia kura vilifikishwa vituoni kwa kushelewa  na karatasi nyingine za kupigia kura zilipelekwa kwingine . 

Tume ya Uchaguzi (MEC) ililazimika  kuongeza muda wa  kupiga kura katika baadhi ya maeneo ya mijini ndani ya siku ya pili na uhesabuji wa  awali ulifanyika nje ya muda tena kukiwa na ukosefu wa umeme katika baaddhi ya vituo vya kupigia kura,

Katika siku  nne za awali za uhesabuji  (MEC)Tume ya Uchaguzi ilionesha kuwa Chama cha upinzani cha Democratic Progressive Party (DPP ) kinachoongozwa na Peter Mutharika , ndugu wa marehemu Rais Bingu wa Mutharika kilikuwa  kukiongoza kwa asilimia 42 ya kura zilizopigwa.

Banda, Aliyekuwa Raisi wa kwanza  mwanamke Kusini mwa Afrika, alikuwa akifuatia kwa asilimia 23. 

Uhesabuji wa kura umemalizika lakini Tume bado haijatangaza matokeo.


Taarifa za vyombo vya habari vya nchini Malawi  zinadai kwamba Mutharika bila shaka atachukua ushinda kama hakutakuwepo na urudiaji wa kupiga kura. .

Baada ya kushauriana na vyama viwili vya  upinzani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Bibi Banda aliamuru uchaguzi ufutwe, akitoa sababu za kwamba uchaguzi mzima uligubikwa na  rushwa  udanganyifu na " makosa lufufu ". 

Kisha  akaamuru uchaguzi mpya kufanyika  ndani ya siku 90 lakini alisema yeye hatashiriki kuwa  mgombea ili kuhakikisha uhuru, uwazi, uaminifu na haki vinarejeshwa.

Kurudia uhesabuji.
Mahakama Kuu ilitengua  maamuzi ya Bibi Banda  baada ya DPP kulalamika na kufikisha suala hili Mahakamani na sasa Mahakama inalazimika  kuamua kama matokeo ya uchaguzi yatangazwe au uhesabuji ufanyike tena.

Tume ya Uchaguzi (MEC) imekiri kwamba yalikuwako makosa katika kupiga kura wiki iliyopita ikashauri uhesabuji wa kura urudiwe..

"Wakati niliposema  kuwa huu uchaguzi ulikuwa na ulaghai na mizengwe hakuna mtu aliamini maneno yangu. Lakini leo Najisikia kuhujumiwa na wakosoaji wangu na  nafurahi kuwa hata MEC imeona yale niliyosema na sasa suala hili liko Mahakamani ili kuamua kama uchaguzi urudiwe ama kura zihesabiwe upya," Banda aliiambia Reuters.

"Jukumu langu sasa litakuwa kuhakikisha  kwamba mapenzi ya watu yana heshimiwa na uhuru, usawa, uwazi na kuaminiana kunatimia katika  uchaguzi na hii ndiyo maana  nimetangaza kuwa  sitoshiriki kama uchaguzi utarudiwa," Banda alisema.

Banda alisifika na kupendwa  na wengi alipoingia  madarakani miaka miwili iliyopita, baada ya kifo cha Rais Mutharika, lakini umaarufu wake ulianza kuporomoka pale alipolazimika kuchukua maamuzi makali yakiwa ni pamoja na  kushusha  thamani ya fedha ya nchi yake katika kudhibiti na kuleta  utulivu wa uchumi wa nchi.

Utawala wake pia ukakumbwa na kashfa ya rushwa ya takiribani $ 15,000,000 iliyopewa jina la ' Cashgate 'Kashfa  hii iliibuka baada ya kiasi kikubwa cha fedha kugunduliwa kuwa zimeibwa kwa hila na  maafisa waandamizi wa umma , wafanyabiashara na mabenki.

Banda ,  alisema kwamba atastaafu  siasa na  kujishughulisha na shughuli za kuhudumia jamii, aidha aliongezea kwamba kwa sasa ana imani na Tume ya Uchaguzi (MEC ).
.
"Hata MEC yenyewe inakiri kuwa  yalikuwepo  mapungufu katika uchaguzi huuna  huu ni uthibitisho wa kutosha kuwezesha uhesabuji wa kura isitoshe  na wengine wana unga mkono hoja hii…. Na hili ndilo nililolisema tokea mwanzo, " Banda alijitetea.

Habari nyingine kuhusiana na hii.
====================================
Polisi wa Malawi wapiga mwandamanaji  risasi  katika  jitihada za kuzuia ghasia za waandamanaji wanaotaka  kurudiwa.uhesabuji wa kura.

Lilongwe- Malawi -Polisi wampiga mwandamanaji risasi na kufa leo siku ya Ijumaa baada ya vurugu kati ya Polisin na watu ambao walifunga barabara kwa kuchoma matairi katika kudai uhesabuji tena wa kura za uchaguzi wa Raisi Mei 20, afisa wa polisi alisema.

Taifa hilo maskini la kusini mwa Afrika lilikuwa likisubiri uamuzi wa mahakama ambao  uliotegemewa baadaye leo siku ya  Ijumaa wa Tume ya Uchaguzi Malawi ( MEC ) kuhukumu kurudiwa uchaguzi au uhesabuji wa kura upya.

Waandamanaji katika wilaya ya Mangochi, katika sehemu ya kusini mwa Malawi, walivunja madirisha ya maduka na kuchoma moto matairi kando ya barabara , na hivyo kusababisha polisi kupiga mabomu ya gesi  ya kutoa machozi na risasi za mpira kutawanya vijana hao bila mafanikio..

"Katika vurugu hii mtu mmoja ilipigwa risasi na kufa,Hili lilitokea  polisi wakijaribu kujitetea baada ya kushindwa nguvu na waandamanaji hawa waliokuwa wamejaa hasira, " afisa wa polisi Eliya Kachikuwo aliiambia Reuters.

Pia alisema maafisa wawili wa  polisi walijeruhiwa vibaya katika varangati hili..

Polisi alisema waandamanaji walikuwa wanachama wa Chama cha Watu wa Rais Joyce Banda na Lazaro Chakwera wa Malawi Congress Party , Vyama viwili ambavyo vinadai kurudiwa kwa uhesabuji wa kura.



Google watengeneza miwani yenye uwezo wa kupiga mtu  picha  au kumrekodi  muhusika bila mwenyewe kujua kwa kuiamuru kufanya hivyo (google glass).
Ingawaje teknolojia hii sio mpya,  Kampuni ya Google ndio ya kwanza kuja na teknoloji hii kwa njia ya miwani na kwa njia ya maelekezo.
Teknolojia kama hii Iliyokuwepo hapo awali ilikuwa katika simu za mkononi, vifungo vya nguo , kalamu na  kwenye noti books na iliendeshwa kwa kubonyeza na sio kwa kusema.
 Cha ziada  ni kwamba miwani hii   hufanya kazi nyingi ikilinganishwa na vifaa hivyo vingine.
Inatarajiwa huwenda bidhaa hii ikafanya vizuri sana katika mauzo kuliko bidhaa hizo zingine ingawa bei zake ziko chini ya miwani hii.
Google glass ni rahisi sana kutumia, kama unataka kupiga picha unachotakiwa kusema ni , “OK Glass, take a picture.”
Miwani hii na sehemo zake na umbo lake

Upo kwenye foleni unaona fujo unataka kuchukua video, mwambie Google  Glass naye atakusaidia kuchukua video. “OK Glass, take video.”

Uko mbali  na unataka kuwaonyesha ndugu na marafiki kitu unachokiona wakati huo huo? Google glass inafanya yote haya, inakuja na kitu kama "Skype-style video chat". na kurusha unachotaka kiwafikie.

Umesafiri kwenda kuchukua mzigo China? Google glass itakusaidia  kutafsiri lugha.Umeenda Zanzibar kutembelea majengo ya kitalii na unabaki kushangaa shangaa, uliza Google glass na itakupa maelekezo (tour guide).

Google glass ni kifaa ambacho unaweza kukitumia kurekodi video, kupiga picha, kutafuta habari katika Google, kutafsiri lugha, kutuma taarifa na unaweza fanya yote haya bila kutumia mikono yako (hands free).

Pia chaweza  kutumika katika shughuli za kitabibu.On dakitari huyu akigundua tatizo la mgonjwa wake hata kabla ya kumpeleka maabara kupimwa.



 Cha kusikitisha  hapa ni kwamba kinasikia kiingereza tu.Huwezi kukipa maelekezo kwa  kiswahili.

Uzuri  ni kwamba, ukivaa  miwani hii watu hawajui kama unawarekodi kwenye video au vipi. Hofu  iliyopo ni kwa wabongo walivyo.Wabongo kama kawaida yao hujihami kupigwa picha au kurekodiwa kwenye video, ukivaa Google glass unaweza tolewa baa.


Bei ya miwani hii ni dola elfu moja na mia tano ($1500) kwa hela ya kitanzania kifaa hiki kwa wastani  kitakuwa sh. mil. 2. 2.  Hata hivyo kifaa hiki kinachovaliwa kama miwani, si vyema kutembea nacho kwa sababu  vibaka hawataacha kukuvaa hasa baada ya kujua thamani yake.

Tusubiri Google wakiwezeshe kifaa hiki kiweze elewa kiswahili ndio na sisi tutakifaidi zaidi kwani hapa hamna kubonyeza bonyesha ni kuongea tu. Je ukipata Google glass utatumia kifaa hiki cha kisasa kufanyia nini?

Acha maoni yako.

Chanzo: recode,net
Dr. Joyce Ndalichako_katibu_mtendaji
baraza la mitihani la Taifa.Tanzania.
Na Mwandishi Wetu
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imepitisha uamuzi wa kutotahini tena mtihani wa somo la Dini kuanzia mwaka huu.

 Katika kupitisha uamuzi huo, Wizara ilikutana na taasisi za Kikristo pekee mwezi Machi mwaka huu na baadae kuwapa taarifa Bakwata juu ya maamuzi yaliyofikiwa.

 “Sisi tumefanya tu kupewa taarifa kuwa Serikali imepitisha uamuzi huo, lakini katika kujadili suala hilo hatukufahamishwa, Wizara ilikutana na wadau wa Kikristo pekee.” Amesema afisa mmoja wa Bakwata akielezea juu ya barua waliyoandikiwa na Kamishna wa Elimu juu ya uamuzi huo. 

Afisa huyo akasema kuwa wao kama Bakwata wameshangaa na kushtuka sana.

 Akasema kuwa pamoja na kutoshirikishwa wanakuja kupewa tu taarifa.

Wanashangaa zaidi pale walipopewa taarifa na Kamishna wa Elimu, na kuambiwa jambo hilo liwe siri.

Jambo hili linafanywa “SIRI, je Serikali inataka Waislamu wasiambiwe? Kwanini? Kuna agenda gani? 

Amehoji afisa huyo ambaye hata hivyo hakutaka kutaja jina lake akisema kuwa yeye sio msemaji wa Bakwata. 

Awali taarifa juu ya kikao cha Wakristo na Wizara juu ya mitihani ya dini, zilianza kuvuja kupitia kwa Wakristo waliohudhuria ambao walipokutana na wadau kutoka upande wa Waislamu waliwalaumu ni kwa nini hawakuhudhuria wakasaidiana kupinga uamuzi huo wa Serikali.

 Hata hivyo, wadau hao kutoka Islamic Education Panel waliwafahamisha wadau hao wa Kikristo kuwa wao walikuwa hawakupewa taarifa.

Kufuatia kuvuja kwa taarifa hizo, baadhi ya wajumbe wa Islamic Education Panel walifuatilia jambo hilo Bakwata wakidhani kuwa huenda Bakwata wao walipewa taarifa. Hata hivyo, maofisa wa Bakwata wakasema kuwa nao wanasikia tu, hawakualikwa.

 Kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikitahini masomo ya Dini ya Kiislamu (Maarifa ya Uislamu) na Kikristo (Divinity) katika mitihani ya kidato cha nne na sita na pia katika Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada.

 Kwa upande wa Maarifa ya Uislamu, Wizara imekuwa ikishirikiana na Islamic Education Panel katika kuandaa mihutasari na mitihani kwa ngazi zote hizo.

Vitabu vya mihutasari hiyo, kwa ngazi zote, katika jalada vimewekwa nembo ya Serikali na ile ya Islamic Education Panel na kusainiwa na Kamishana wa Elimu. Hata hivyo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, haikuwaita IEP katika kupitisha uamuzi huo mkubwa na wenye athari kubwa kwa vijana wa Kiislamu na vyuo vya Kiislamu. 

Hivi sasa Vyuo Vikuu kama kile cha Waislamu Morogoro (MUM), pamoja na wanafunzi wa kozi nyingine, huchukua wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na kufaulu Somo la Islamic Knowledge kwa ajili ya kuchukua kozi ya Sheria na Sharia kwa pamoja. Aidha, huchukua pia wanafunzi hao kwa ajili ya kozi ya Masomo ya Dini na Ualimu, yaani BA Islamic Studies and Education. 

Kwa upande mwingine, Chuo Kikuu cha Elimu Zanzibar (Chukwani) na kile cha Tunguu, navyo vinachukua wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na kufaulu somo la Maarifa ya Uislamu kwa ajili ya kozi zao mbalimbali. Vipo pia vyuo vikuu vya Mbale Uganda, Sudan, Uturuki, Malaysia na sehemu nyingine ambapo wana kozi zinazohitaji somo la Maarifa ya Uislamu kama vile Islamic Banking.

Kwa uamuzi huu wa Serikali, ina maana kuwa sasa itakuwa vigumu kwa MUM na Chukwani kupata wanafunzi wenye sifa kwa hiyo huenda vikalazimika kufuta kozi hizo. Hii maana yake ni kuwa uamuzi huu unapunguza idadi ya wanafunzi wa Kiislamu wanaokuwa na sifa za kupata elimu ya juu. 

“Kinachosikitisha ni kuwa Serikali imeamua kukaa na Wakristo pekee kupitisha maamuzi mazito kama haya bila kujali athari yake kwa vijana wa Kiislamu na taasisi za Kiislamu nchini.” Amesema mjumbe mmoja wa Islamic Education Panel akizungumzia suala hilo.

 “Hii ni dharau iliyopitiliza kiwango, Serikali inachukuaje maamuzi kama haya bila kujali kuwa kuna shule za Kiislamu na Vyuo vya Ualimu vya Kiislamu pamoja na Vyuo Vikuu ambavyo vinategemea kupata wanafunzi kutokana na wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita wenye somo la Maarifa ya Uislamu?” Amesema mjumbe huyo wa Islamic Education Panel ambaye hata hivyo hakutaka kutajwa jina lake gazetini.

“Kama Serikali imeona kuna mantiki kujitoa katika kutahini somo hili, kwa nini ifanye kinyemela? Kwa nini isiwashirikishe wadau husika ili kujua, ni utaratibu gani mwingine utafanyika ili vyuo vya Kiislamu vilivyopo visiathirike? Kwa nini wasikae pamoja na Panel? Mbona waliwaita Wakristo? Kitu gani kiliwafanya wakwepe kuwaita Waislamu, ni dharau, UDINI, au kuna agenda ya siri?”

Mdau mmoja wa Kikristo aliyekuwa katika kikao hicho cha Machi kati ya Serikali na wadau wa Elimu wa Kikristo alipoulizwa kuwa katika kikao hicho Serikali imetoa hoja gani ya kufuta mtihani huo alisema kuwa, hakuna jambo lililoelezwa la kujenga hoja madhubuti, lakini yeye binafsi anadhani ni kutokana na masuala ya Waislamu toka walipopinga matokeo ya Islamic mpaka ikabidi Baraza la Mitihani liyabadili.

 Wajumbe wa Islamic Education Panel wanasema kuwa, wakati Waislamu wametimiza matakwa yote ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya kuwa na Mihutasari na vitabu kwa ngazi zote, Wakristo hawakuwa wametimiza matakwa hayo, hawakuwa hata na mihutasari, lakini somo lao lilikuwa likitahiniwa.

Hata hivyo, akasema, hao hao ambao hawakuwa wametimiza matakwa ya Wizara na Baraza la Mitihani, ndio walioitwa kupitisha uamuzi wa Serikali kujitoa katika kutahini mtihani huo. “Waislamu wakilalamika kuwa kuna ubaguzi, udhalilishaji, uonevu na udini, wanaambiwa wanafanya uchochezi, hivi Serikali inaweza kukaa na Waislamu pekee na kufanya maamuzi makubwa yenye kugusa masilahi ya Kanisa Katoliki na Wakristo wote, halafu ifanye tu kuwapelekea taarifa Baraza la Maaskofu juu ya maamuzi hayo?” Alihoji. Wachambuzi wa masuala ya kidini na kijamii nchini wanasema kuwa huenda Serikali imeamua kujitoa katika suala hili ili ipate fursa ya kuweka mkakati mwingine wa kuibuka na somo la dini mseto baada ya kukwama huko nyuma. Hata hivyo wengine wanasema kuwa hii ni moja tu ya mikakati ya kupunguza idadi ya vijana wa Kiislamu wenye sifa za kujiunga na vyuo vikuu.

Wengine wakakumbusha kuwa zilipoanzishwa shule za kwanza za seminari za Kiislamu, Serikali ilitangaza kuwa shule hizo sio shule zinazotambulika. Ni Madrasa. Kwa hiyo wanafunzi wake wakimaliza kidato cha nne wasingepatiwa nafasi za kusoma kidato cha tano katika shule za Serikali. Na kwamba kwa wale watakaomaliza kidato cha sita, wasingechaguliwa kuingia vyuo vikuu na vyuo vingine vya Serikali. Kwa vile isingewezekana kutangaza kuwa wasiotakiwa ni Waislamu pekee, ilibidi tangazo liguse shule zote pamoja na seminari za Kikristo.

Hata hivyo, baadae alilazimika wenyewe kuondoa tena kimya kimya sera hiyo kabla haijafanyiwa kazi, baada ya kuona kuwa watakao athirika zaidi ni vijana wa Kikristo kwa sababu ni taasisi za Kikristo zilizokuwa na shule nyingi za seminari. 

Ni kwa sababu ya matukio kama hayo, baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa huenda kuna agenda ya siri inayowalenga Waislamu na ndio maana waliitwa Wakristo pekee ili waelimishwe kuwa wawe radhi kujitoa muhanga kutofanya mtihani wa ‘Divinity’. 

Kwa upande mwingine huenda hawakuitwa Waislamu kwa kuhofiwa kuwa wangehoji mambo ambayo yasingeweza kupatiwa majibu ya maswali kama; ni utaratibu gani umeandaliwa kuhakikisha kuwa MUM, Chukwani na vyuo vingine vya Kiislamu vyenye kozi za Islamic Studies, Shariah na Islamic Banking, vitapata wanafunzi kulingana na vigezo vya Mamlaka ya Vyuo Vikuu- Tanzania Commission for Universities (TCU). 

Habari kutoka ndani ya Bakwata na Islamic Education Panel zinasema kuwa taarifa kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi juu ya suala hilo, imeeleza kuwa nao Wizara wamefanya kupewa maelekezo na Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu.

Na kwamba Wizara ilitakiwa kukaa na wadau, kwa maana ya taasisi za kidini kuangalia suala hilo. 

Hata hivyo, haikuweza kufahamika kuwa uamuzi wa kutokuwashirikisha Waislamu na badala yake kukaa na Wakristo pekee, ilikuwa ni maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi au ulikuwa uamuzi wa Kamishna wa Elimu. 

Wadadisi wengine wanasema kuwa jambo hili limetokea Baraza la Mitihani (NECTA) na kwamba kama ambavyo Baraza hilo liliona umuhimu wa kuajiri Mchungaji wa kutizama masilahi ya wanafunzi wa Kikristo na kugoma kuajiri Muislamu, ndio mtindo huo huo umetumika katika kuita kikao cha Wizarani.

 Kutokana na hali hiyo, Waislamu kupitia taasisi zao, wamepanga kumuona Katibu Mkuu Kiongozi kupata ufafanuzi juu ya suala hilo.

Na kwa kuwa suala hili linagusa masilahi ya Waislamu wote nchini, litafanyiwa taratibu za kujadiliwa na kupitishiwa maamuzi ya pamoja.

 Hadi jana tukienda mitamboni juhudi za kuwapata wahusika Wizara ya Elimu na NECTA kuzungumzia suala hili, hazikuweza kufanikiwa.


Chanzo; An nuur



Familia za abiria wa ndege iliyotoweka ya Malaysia wakiandamana wakiwa wamebeba mabango.
Licha ya kwamba ni haramu kufanya maandamano ya umma nchini China  familia za abiria wa ndege iliyotoweka ya Malaysia majuma mawili yaliyopita, wamekabiliana na polisi nje ya ubalozi wa Malaysia   leo hii jijini Beijing.

Maandamano ya umma ni haramu nchini China, lakini hadi kufikia watu hawa kupanga maandamano kama haya ni ishara kuwa hawana kilichobakia kuwapa matumaini kabisa.

Wakiwa wamejawa na ghadhabu, na wakiwa na mabango, wanalitaka shirika la ndege la Malaysia mjini Kuala Lumpur kueleza kilichofanyika na kinachoendelea hadi sasa.

 Mabango yalikuwa na maandishi yaliyoandikwa "Save MH370" .Jamaa hawa wa ndugu wanaosadikiwa kupotea na ndege hii, wakiwa na  hasira walikabiliana na polisi na kuwalemea hadi kuingia katika ofisi ya ubalozi huo.

Wakiwa wanafoka kwa hasira kali walisema ..''Tunataka ukweli." huku nyuso na maneno yao yakionesha ishara ya hasira na mfadhaiko wanaoupata kwa kupotelewa na jamaa zao.

Hasira za jamaa hawa zinakuja baada ya waziri mkuu wa Malaysia, Najib Razak kusema udadisi wa data ya Setiliti unaonyesha kuwa safari ya ndege hiyo iliishia baharini Kusini mwa Australia.

Serikali ya China imeomba kuona data hiyo ambayo Malaysia inaiamini kiasi cha kutoa msimamo kama huo..

Hata hivyo kwa sasa msako wa ndege hiyo MH370 umesitishwa  kwa muda kutokana na mawimbi makali baharini

Mataifa mbali mbali yalijitolea kusaidia Malaysia kuitafuta ndege hiyo, juhudi ambazo zililengwa zaidi katika bahari ya Kusini Magharibi mwa mji wa Australia Perth.

Wiki iliyopita China ilidai kuona chombo  kinachodhaniwa kimedondoka kutoka  kwenye ndege hiyo katika maeneo yanayodaiwa ndege hiyo kupotea lakini hadi sasa  uchunguzi huo haujaonesha mafanikio yeyote
 .
Ndege hiyo MH370 ilipotea tarehe  8 Machi, 2014 ilipokuwa njiani kuelekea Beijing kutoka Kuala Lumpar ikiwa imebeba abiria 239 wakiwemo raia 153 wa China.

Maandamano ya umma ni haramu nchini China, lakini hadi kufikia watu hawa wakapanga maandamano kama hayo ni ishara kuwa hawana kilichobakia kuwapa matumaini kabisa.

Wimbi la  matukio ya ajali kubwa za ndega lilikuwa limesahaulika kidogo ila sasa linaanza kutokea na kufanya safari za ndege kutiliwa hofu na wasafiri.
Tunashauri mashirika ya ndege yaongeze  hadhari zaidi  katika katika ndege zao na kwenye viwanja vya ndege.

POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza