Rais wa Malawi adai kuwa ni mahakama pekee ndiyo iwezayo kuamua mgogoro wa matokeo ya kura nchini humo.
Rais wa Malawi adai kuwa ni mahakama pekee ndiyo iwezayo kuamua mgogoro wa matokeo ya kura nchini humo.
Lilomgwe Malawi - Rais wa Malawi Joyce Banda alisema jana Alhamisi, 29,Mei 2014 kwamba yuko tetayari kuachia ngazi kama Mahakama Kuu itaridhia kuwa uchaguzi wa wiki iliyopita ambako mpinzani wake anadaiwa kuwa na kura zaidi utarudiwa.
Mpinzani wake huyu anaonekana ndiye mshindi.Banda hakubaliani na matokeo kwa kudai kuwa kura zilihesabiwa kwa udanganyifu.
Mahakama Kuu ilitarajiwa kutokana hukumu leo siku ya Ijumaa Hukumu ambayo ingeiwezesha Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) kutangaza matokeo ya Mei 20 ambayo mpinzani wa Banda ndiye aliye na uwezekano wa kuwa mshindi, au kurudia zoezi la uhesabuji upya, mchakato ambao unaweza kuchukua muda wa miezi miwili.
Nchi hii ya kusini mwa Afrika inayokabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi inasubiri uamuzi huu wa kimahakama wa ama Tume itangaze matokeo yaliyopatikana au kurudia uhesabuji wa kura upya.
Uanuzi ambao unaweza kuleta ghasia katika uchaguzi huu wa mfumo wa vyama vingi toka ule wa chama kimoja uliokuwepo tokea miongo miwili iliyopita.
"Nimewaambia MEC na wadau kwamba mimi nitaukubali uamuzi wa mahakama, " Banda aliiambia Reuters alipofanya mahojiano nao katika mji mkuu wa Malawi Lilongwe.
"Mimi nilitoa uhuru ili uchaguzi uendeshwe kwa misingi ya haki, uhuru na usawa.Yote haya ni katika kutetea haki ya wananchi wa Malawi katika wakati huu muhimu ili kuhakikisha kuwa kiongozi anayechaguliwa anachaguliwa kwa njia ya haki na kuaminika, " aliongeza.
Uchaguzi ulikumbwa na matatizo mengi. Vifaa vya kupigia kura vilifikishwa vituoni kwa kushelewa na karatasi nyingine za kupigia kura zilipelekwa kwingine .
Tume ya Uchaguzi (MEC) ililazimika kuongeza muda wa kupiga kura katika baadhi ya maeneo ya mijini ndani ya siku ya pili na uhesabuji wa awali ulifanyika nje ya muda tena kukiwa na ukosefu wa umeme katika baaddhi ya vituo vya kupigia kura,
Katika siku nne za awali za uhesabuji (MEC)Tume ya Uchaguzi ilionesha kuwa Chama cha upinzani cha Democratic Progressive Party (DPP ) kinachoongozwa na Peter Mutharika , ndugu wa marehemu Rais Bingu wa Mutharika kilikuwa kukiongoza kwa asilimia 42 ya kura zilizopigwa.
Banda, Aliyekuwa Raisi wa kwanza mwanamke Kusini mwa Afrika, alikuwa akifuatia kwa asilimia 23.
Uhesabuji wa kura umemalizika lakini Tume bado haijatangaza matokeo.
Taarifa za vyombo vya habari vya nchini Malawi zinadai kwamba Mutharika bila shaka atachukua ushinda kama hakutakuwepo na urudiaji wa kupiga kura. .
Baada ya kushauriana na vyama viwili vya upinzani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Bibi Banda aliamuru uchaguzi ufutwe, akitoa sababu za kwamba uchaguzi mzima uligubikwa na rushwa udanganyifu na " makosa lufufu ".
Kisha akaamuru uchaguzi mpya kufanyika ndani ya siku 90 lakini alisema yeye hatashiriki kuwa mgombea ili kuhakikisha uhuru, uwazi, uaminifu na haki vinarejeshwa.
Kurudia uhesabuji.
Mahakama Kuu ilitengua maamuzi ya Bibi Banda baada ya DPP kulalamika na kufikisha suala hili Mahakamani na sasa Mahakama inalazimika kuamua kama matokeo ya uchaguzi yatangazwe au uhesabuji ufanyike tena.
Tume ya Uchaguzi (MEC) imekiri kwamba yalikuwako makosa katika kupiga kura wiki iliyopita ikashauri uhesabuji wa kura urudiwe..
"Wakati niliposema kuwa huu uchaguzi ulikuwa na ulaghai na mizengwe hakuna mtu aliamini maneno yangu. Lakini leo Najisikia kuhujumiwa na wakosoaji wangu na nafurahi kuwa hata MEC imeona yale niliyosema na sasa suala hili liko Mahakamani ili kuamua kama uchaguzi urudiwe ama kura zihesabiwe upya," Banda aliiambia Reuters.
"Jukumu langu sasa litakuwa kuhakikisha kwamba mapenzi ya watu yana heshimiwa na uhuru, usawa, uwazi na kuaminiana kunatimia katika uchaguzi na hii ndiyo maana nimetangaza kuwa sitoshiriki kama uchaguzi utarudiwa," Banda alisema.
Banda alisifika na kupendwa na wengi alipoingia madarakani miaka miwili iliyopita, baada ya kifo cha Rais Mutharika, lakini umaarufu wake ulianza kuporomoka pale alipolazimika kuchukua maamuzi makali yakiwa ni pamoja na kushusha thamani ya fedha ya nchi yake katika kudhibiti na kuleta utulivu wa uchumi wa nchi.
Utawala wake pia ukakumbwa na kashfa ya rushwa ya takiribani $ 15,000,000 iliyopewa jina la ' Cashgate 'Kashfa hii iliibuka baada ya kiasi kikubwa cha fedha kugunduliwa kuwa zimeibwa kwa hila na maafisa waandamizi wa umma , wafanyabiashara na mabenki.
Banda , alisema kwamba atastaafu siasa na kujishughulisha na shughuli za kuhudumia jamii, aidha aliongezea kwamba kwa sasa ana imani na Tume ya Uchaguzi (MEC ).
.
"Hata MEC yenyewe inakiri kuwa yalikuwepo mapungufu katika uchaguzi huuna huu ni uthibitisho wa kutosha kuwezesha uhesabuji wa kura isitoshe na wengine wana unga mkono hoja hii…. Na hili ndilo nililolisema tokea mwanzo, " Banda alijitetea.
Habari nyingine kuhusiana na hii.
====================================
Polisi wa Malawi wapiga mwandamanaji risasi katika jitihada za kuzuia ghasia za waandamanaji wanaotaka kurudiwa.uhesabuji wa kura.
Lilongwe- Malawi -Polisi wampiga mwandamanaji risasi na kufa leo siku ya Ijumaa baada ya vurugu kati ya Polisin na watu ambao walifunga barabara kwa kuchoma matairi katika kudai uhesabuji tena wa kura za uchaguzi wa Raisi Mei 20, afisa wa polisi alisema.
Taifa hilo maskini la kusini mwa Afrika lilikuwa likisubiri uamuzi wa mahakama ambao uliotegemewa baadaye leo siku ya Ijumaa wa Tume ya Uchaguzi Malawi ( MEC ) kuhukumu kurudiwa uchaguzi au uhesabuji wa kura upya.
Waandamanaji katika wilaya ya Mangochi, katika sehemu ya kusini mwa Malawi, walivunja madirisha ya maduka na kuchoma moto matairi kando ya barabara , na hivyo kusababisha polisi kupiga mabomu ya gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kutawanya vijana hao bila mafanikio..
"Katika vurugu hii mtu mmoja ilipigwa risasi na kufa,Hili lilitokea polisi wakijaribu kujitetea baada ya kushindwa nguvu na waandamanaji hawa waliokuwa wamejaa hasira, " afisa wa polisi Eliya Kachikuwo aliiambia Reuters.
Pia alisema maafisa wawili wa polisi walijeruhiwa vibaya katika varangati hili..
Polisi alisema waandamanaji walikuwa wanachama wa Chama cha Watu wa Rais Joyce Banda na Lazaro Chakwera wa Malawi Congress Party , Vyama viwili ambavyo vinadai kurudiwa kwa uhesabuji wa kura.
0 comments: