TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) KWA MUJIBU WA SHERIA MWAKA - 2014

Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa wakitoa
 salamu ya heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu
 Dr Jakaya Mrisho Kikwete katika maadhimisho
 ya Miaka 50 ya Jeshi hilo.
  

AWAMU YA     KWANZA. 

VIJANA 20,000 WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA 2014 KUJIUNNGA NA JKT KWA  MUJIBU WA SHERIA  KATIKA VIKOSI MBALIMBALI KUANZIA 01.JUNI 2014.

UTARATIBU 

 

  • AWAMU YA KWANZA; VIJANA 20,000 WATARIPOTI KWENYE MAKAMBI YA MAFUNZO YA JKT KUANZIA TAREHE 01 JUNI 2014 NA KUANZA RASMI MAFUNZO YAO TAREHE 08 JUNI 2014 NA KUMALIZA TAREHE 04 SEPTEMBA 2014. ORODHA YAO ITAANZA KUONEKANA KWENYE WEBSITE YA JKT TAREHE 11 MEI 2014 KUANZIA SAA NNE (4) ASUBUHI.
  • AWAMU YA PILI; VIJANA 14450 WATARIPOTI KWENYE MAKAMBI YA MAFUNZO YA JKT KUANZIA TAREHE 11 SEPTEMBA 2014 NA KUANZA RASMI MAFUNZO TAREHE 18 SEPTEMBA 2014 NA KUMALIZA TAREHE 17 DESEMBA 2014. ORODHA YAO ITAANZA KUONEKANA KWENYE WEBSITE YA JKT TAREHE 15 MEI 2014 KUANZIA SAA KUMI (10) JIONI.
  • KIJANA YEYOTE MWENYE ULEMAVU UNAOONEKANA ARIPOTI KATIKA KAMBI YA MAFUNZO YA RUVU JKT (832 KIKOSI CHA JESHI).
  • VIJANA WOTE WANATAKIWA KUWA NA VYETI VYA KUMALIZA KIDATO CHA SITA ( LEAVING CERTIFICATE).
  • INASISITIZWA VIJANA WARIPOTI KWENYE MAKAMBI WALIOPANGIWA NA SIO KUJA MAKAO MAKUU YA JKT. 
  • IMETOLEWA NA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA.
Leo Alhamisi tarehe  08 Mei 2014 07:26.

Majina ya vijana wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa Sheria AWAMU ya  KWANZA. Zifuatazo ni kambi na Majina ya awamu hii ya kwanza kuanzia ---  A- M)..


 Muhimu sana,  soma !!!


ORODHA YA VIJANA KIDATO CHA SITA WANAOKWENDA JKT MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA KWANZA IMEFANYIWA MAREKEBISHO KAMA IFUATAVYO:-
  • VIJANA 1200 WAMEONDOLEWA KUTOKA KIKOSI CHA RUVU NA KUPELEKWA VIKOSI VYA MAKUTUPORA, MAFINGA NA WACHACHE VIKOSI VINGINE.

  • MAREKEBISHO MACHACHE PIA YAMEFANYIKA KATIKA VIKOSI MBALIMBALI.

  • KUTOKANA NA MAREKEBISHO HAYO VIJANA WANASISITIZWA KUHAKIKI TENA MAJINA YAO KATIKA ORODHA MPYA ILIYOPO KWENYE TOVUTI HII.

    VIJANA WOTE AMBAO HAWAJAPANGWA AWAMU YA

    KWANZA, WAMEPANGIWA AWAMU YA PILI NA 

    ORODHA YAO ITAWEKWA KWENYE TOVUTI HII MUDA

     WOWOTE KUANZIA SASA.


    IMETOLEWA NA MAKAO MAKUU YA JKT



    Bofia KAMBI ambako herufi tatu za kwanza za jina lako zipo kujua ni wapi umepangwa.          
                                                                                                 Majina  kuanzia   

    Bofia KAMBI sehemu ziliko herufi tatu za kwanza za jina lakokupata kambi yako.



    Kumbukia enzi hizo wabunge wlipojiunga na JKT, toka kushoto ni Halima Mdee, Ester Bulaya na mwisho kulia ni
     Neema Hamid wakiwa mafunzoni Mwaka - 2013.

    MAFUNZO YANA FAIDA.

    Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Umoja wa Vijana wa CCM, Mkoa wa Mara, Ester Bulaya, alisema kuwa anashukuru kupata mafunzo ya kijeshi, kwani yamemjenga kwa kiasi kikubwa.

    “Japo ni kazi lakini tunatamani muda uongezwe, maana wiki tatu zilikuwa fupi, program ni nyingi, kwa hiyo tukatakiwa kufanya kwa pamoja,” alisema Bulaya kisha akaongeza: “Imenijenga kweli, najiona mkakamavu mwenye uwezo zaidi wa kutumikia wananchi.”


    Kwa upande wa Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, alisema: “Natamani kila mtu awe anapitia mafunzo ya JKT, maana siyo tu yanakujenga kiukakamavu, bali pia yanakupa uzalendo na ari ya kuwatumikia wananchi.”


    Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee akinyolewa nywel
    KUHUSU VIPARA. 

    Mbunge mwingine alisema: “Walichotuweza ni ile tunaripoti tu, tunanyolewa vipara halafu ndiyo taratibu nyingine zinafuata. 
    Kama wangekuwa wanatuonesha picha ya kile kitakachofanyika 
    kabla ya kutunyoa, wengi wetu tungetimka mapema.

    “Tatizo unanyolewa halafu ndiyo unapelekwa kupimwa ukimwi, sasa ukikataa kupima na una kipara chako, mtaani utarudi vipi? Hata kunyoa, wengine tuliingia na rasta, lakini wakatupiga upara wa wembe harakaharaka bila hata kungoja kuzifumua.”

    VIJANA WOTE AMBAO HAWAJAPANGWA AWAMU YA KWANZA, WAMEPANGIWA AWAMU YA PILI NA ORODHA YAO ITAWEKWA KWENYE TOVUTI HII MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.
    • Nakutakia mafunzo mema.

    0 comments:

    POLL

    Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
      
    pollcode.com free polls 

    TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

    Name

    Email *

    Message *

    Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza