METHALI, NAHAU, NI VIPERA VYA SEMI

Kamusi ni hazina la lugha
METHALI, NAHAU NI VIPERA VYA SEMI.
                (Fasihi Simulizi)
Fasihi simulizi ina tanzu zake na Semi ni moja ya tanzu zake. Utanzu huu nao una VIPERA vyake ambayo ni methali, nahau, misemo, simo, vitanza ndimi, vichezea meno na mgafumbo ambayo hujumuisha vitendawili, chemsha bongo, malumbo na mizungu.

Katika somo hili nitaelezea kwa kifupi maana na kutoa mifano ya Methali na Nahau na kuonesha ukaribu wa nahau, misemo na methali.

Methali na nahau zote ni
 semi zitumiazo lugha fupi fupi na ya mkato.

Methali
Maana.
Methali ni usemi wa kimapokeo, japo zipo methali zinazozaliwa kila wakati na nyingine kufa. ambao unaotumiwa kwa kufumbia jambo kwa maneno ya kawaida bali kwa njia ya mkato huku ukibainisha ukweli au kutolea ushauri kwa kulenga kwa usahihi kile kinachozungumziwa.

Kwa ufupi methali ni kauli inayobeba busara au falsafa za jamii husika.

Mifano ya methali za kimapokeo ni:
i. Pema usijapo pema ukipema si pema tena.
ii. Kozi mwana mandanda kulala njaa kupenda.
iii. Mwenda omo na tezi marejeo ni ngamani.
iv. Mwapiza la nje hupata la ndani.
v. Macho hayana pazia.
vi. Ukilima pakubwa ukivuna pamekwisha.

Mifano ya methali zilizozaliwa hivi karibuni kwa uchache ni:
i. Usiteme 'big G' yako kwa karanga za kuonjeshwa.
ii.Ukilima shamba njiani ujue kulinda ndege.
iii.Ukitaka kujua mwenendo wa mjinga mvishe kilemba.
iv. Kiyoo cha gari hakifungwi katika tairi ya gari
v. Ama kweli kama hujui unakokwenda huwezi kupotea.
 vi. Akimbiaye peke yake siku zote yeye ni mshindi.
vii. Usiku rafikiye ni giza.l

Misemo
Maana
Msemo ni fungu la maneno lenye maana mahsusi lenye  kutoa fundisho ama kuelezea dhana fulani kwa j amii lisilo na kitenzi ndani yake.

Wengi huchanganya misemo na nahau. Tofauti kubwa kati ya tungo hizi ni kitenzi. Nahau huwa na kitenzi lakini msemo hauna kitenzi ndani yake

Ifuatayo ni mifano michache ya misemo ya Kiswahili na maana zake:
i. Mkono wa birika=mchoyo
ii. Sindano na uzi. =ushirikiano au umoja
iii. Kiti moto=nyama ya nguruwe  au misukosuko ya madaraka.
iv. Hamadi kibindoni=akiba uliyo nayo mkononi.
v. Mwana haramu= mtoto wa nje ya ndoa.
vi. Kiwi cha macho= tamaa ya mapenzi.
viii. Mkono mrefu = mwizi
viii. Akali ya watu= watu wachache.
ix. Umti wa watu = watu wengi.

Katika mkutadha wa maongezi aghalabu misemo huongezewa kitenzi na kutenda kazi ya nahau lakini maana hubakia kuwa ile ile ya awali.

Nahau
Maana
Usemi mfupi ulio na kitenzi unaotumia maneno ya kikawaida, lakini yakiwa na maana iliyojificha na iliyotofauti na maana ya maneno hayo.
mfano:
i). Kujikaza kisabuni = kutia bidii,
ii).kuvaa miwani = kulewa,
iii).Kuoga mwaka= kusherehekea kumaliza mwaka kwa salama.

 Zifuatazo ni nahau maarufu za lugha ya Kiswahili. Kila lugha ina nahau zake na kusudio kuu la matumizi ya nahau  ni kuifanya lugha kuwa safi.Neno hili lina asili ya Kiarabu na maana yake ya asili ikiwa ni usafi wa lugha ikimaanisha matumizi sahihi ya lugha.

1 Amekula chumvi nyingi=ameishi miaka.
    mingi
2, Ana mkono wa birika= mtu mchoyo
3.Ametutupa mkono= amefariki, amekufa
4.Ameaga dunia=amekufa, amefariki
5.Amevaa miwani=amelewa
6.Amepiga kite=amependeza
7.Amepara jiko=kaoa
8.Amefumga pingu za maisha=ameolewa
9.Anawalanda wazazi wake =
    kawafanana wazazi wake kwa sura
10. Kawachukua wazazi wake=anafanana
       na wazazi wake kwa sura na tabia.
11.Kawabeba wazazi wake = anawajali na
      kuwatunza wazazi wake.
12. Chemsha bongo = fikiri kwa makini na
       haraka.
13.Amekuwa toinyo=hana pua.
14. Amekuwa popo =amekuwa kigeugeu
15. Ahadi ni deni = timiza ahadi yako
16.Amewachukua wazee wake =
      anawatunza vizuri wazazi
17.Amekuwa mwalimu= yu msemaji sana
18.Amemwaga unga = amefukuzwa kazi
19..Ana ulimu wa upanga=ana maneno
     makali
20.Ameongeza unga = mepanda cheo
21.Agizia risasi = piga risasi
22.Kuchungulia kaburi= kunusurika kifo
23..Fyata mkia= nyamaza kimya
24.Fimbo zimemwota mgongoni=ana
     alama za mapigo ya fmbo mgongoni
25.Hamadi kibindoni= akiba iliyopo
      mkononi]
26.Hawapikiki chungu
       kimoja=hawapatani kamwe
27.Kupika majungu = kumteta mtu kwa
       siri
28.Kumvika mtu kilemba cha ukoka =
      umsifu mtu kwa unafiki
29Kula mlungula /kula rushwa = kupokea
      rushwa
30.Kupelekwa miyomboni = kutiwa au
      kupelekwa jandoni
31.Kujipalia mkaa =  ujitia matatani
32.Kumeza au kumezzea mate = utamani
33.Kumuuma mtu sikio = kumnong'oneza
      mtu jambo la siri
34.Kumpa nyama ya ulimi =
     kumdanganya mtu kwa maneno
     matamu
35.Kumchimba mtu  = kumpeleleza mtu
      siri yake
36.Kutia chumvi  katika mazungumzo  =
      uongea habari za uwongo
37.Vunjika moyo = kata tamaa
38.Kata maini = kutia uchungu
39. Kujikosoa = kujisahihisha
40.Kutia utambi  = kuchochea ugomvi
41.Kumeza maneno  = kutunza siri
      moyoni
42.Kula njama kufanya mkutano wa siri.
43.Kumkalia mtu kitako = kumsema
       au kumsengenya mtu
44.Kupiga mtu vijembe = kumsema mtu
      kwa fumbo
45.Kiinua mgong = malipo ya pongezi ya
      uzeeni bada ya kustaafu kazi
46.Kazi ya majungu = kazi ya kumpatia
      mtu posho
47.Kaza kamba au kaza roho =usikate tamaa
48..Kumwonyesha mgongo = kujificha
49.Kuona cha mtema kuni = kupata
      mateso au kuuliwa kwa kukatwa
      kichwa
50.Maneno ya uwani = maneno yasiyo na
      maana au porojo
51.Mate ya fisi = tamaa kupita kiasi
52.Kata tamaa = vunjika moyo kutokuwa
      na hamu ya jambo fulani.
53. Mbiu ya mgambo = tangazo
54.Mungu amemnyooshea kidole = mungu amemuadhibu
55.Mkubwa jalala = kila  lawama hutupwa kwa mkubwa
56.Mkaa jikoni= mvivu wa kutembea
57.Mungu si Athumani= mungu hapendelei
58.Paka mafuta kwa mgongo wa chupa = danganya
59.Usiwe kabaila  = usichume tokana na jasho la mwingine
60.Usiwe kupe = fanya kazi
61.Usiwe bwanyenye = usichume kwa vitega uchumi vyake.
62. Usiwe na mirija = usinyonye wenzako
63.Utawala msonga= utawala wa wachache
64.Usiwe nyang'au = nchi moja kuifanyia nyingine  ubaya na udhulumati.
65.Usiwe kikaragosi = nchi kuwa kibaraka wa nchi kubwa.
66.Usiwe chui katika ngozi ya kondoo=kujifanya rafiki kumbe ni adui
67.Kutoa ya mwaka =kufanya jambo zuri na la pekee
68.Kumpa mtu ukweli wake = kumwambia mtu wazi ubaya wake.
69.Pua kukaribiana kushikana na uso =kukunja uso kwa hasira
70.Kusema kutoka moyono=kunena kilicho kweli
71.Sina hali= sijiwezi kiuchumi
72.Kupiga uvuvi = kukaa tu bila kazi
73.Kupiga kubwa = kwenda moja kwa moja, kusepa
74.Kumwekea mtu deko = kulipiza  kisasi
Mtu mwenye ndimi mbili = kigeugeu
75.Miamba ya mitishamba =wanga hodari wa kienyeji
76.Kupiga supu = kutegea kazi wengine wafanye
77.Kupiga mali shoka = kugawana  mali au urithi
78. Kula vumbi kuhangaika maisha,  pata tabu kutafuta riziki
79.Mafungulia ng'ombe =muda wa kati ya saa mbili na saa tatu asubuhi.
80.Kutia kiraka =fichia siri
81.Kumlainisha mtu= kumzungumzia mtu maneno matamu mpaka akubali matakwa yako.
82. Kupiga pamba=kuvaa vizuri
83.Kufulia = kuishiwa
84.Umangimeza=uongozi wa kuamrisha watu, udikiteta au uongozi wa imla

Na hizi ni kwa uchache tu, ziko nyingi za zamani na za sasa ambazo sijazielezea kama: kupiga kite, kuondoa kiwi cha macho, kupiga hema, kunawa mikono, nakadhalika.

176 comments:

  1. Maana ya Nyoka na shimo pia ni nahau ila mnisaidie kujua maana yake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pata faida nyingi

      Delete
    2. Kupiga kite inamaana gani

      Delete
    3. Maana ya methali inayosema pampaluma malango wa chuma ukiufungua hauna huruma

      Delete
  2. Zoa matunda
    Je nahau hii inamaana gani

    ReplyDelete
  3. Nini maana ya nahau "kanyaga chelele"?

    ReplyDelete
  4. Nini maana ya kufa kibudu naimba nisaidieni kwa hilo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kufa bila kuchinjwa kwa mnyama anayeliwa.

      Delete
    2. Naomb maana ya chokoza nyuki

      Delete
  5. Nini maana ya nahau:
    Tia moto
    Kaa eda
    Piga kibirizi
    Kichwa kikubwa
    Kazi shows
    Noa lugubrious
    Shika masikio
    Tumbua jaipur
    Kula pona
    Piga maji
    Timua vumbi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mimi ni na jibu swalimoja Piga maji lewa pombe au kunywa kilevi.

      Delete
    2. Nini maana ya Lima kwa miguu

      Delete
    3. Maana ya lima miguu ni kutembea umbali mrefu

      Delete
  6. nini maana ya nahau amepata naizesheni

    ReplyDelete
  7. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  8. naomba unioneshe maana ya piga kibirizi au Nini maana ya nahau hii piga kibirizi? na kidagaa kimemwozea pia na kula mumbi naomba maana ya nahau hizo zote

    ReplyDelete
  9. Nini maana ya lima miguu naomba munisaidie

    ReplyDelete
    Replies
    1. mwenye jib hili anisaidie na mimi

      Delete
  10. Nini maana ya nahau kupiga tarumbeta

    ReplyDelete
  11. Replies
    1. Nini maana ya nahau
      Piga tarumbeta
      Piga risasi
      Kataa katakana

      Delete
  12. Maana ya nahau "piga winda" ni ipi tafadhali

    ReplyDelete
  13. Nahau ya piga ya kumtolea mtu maneno makali ni ipi

    ReplyDelete
  14. Nini maana ya onea here,lia ngora,lilia hali na onea kijicho

    ReplyDelete
  15. Replies
    1. Kukata shauri maana yake ni kuamua jambo fulani.KARIBU TENA

      Delete
  16. Nini maana ya nahau Mtu mropokaji sana

    ReplyDelete
  17. Noa lubu fikiri sana sawa na chemsha bongo

    ReplyDelete
  18. Piga kibirizi tangaza. Kidagaa kimemwozea ameelemewa na jambo.kula mumbi pata shida

    ReplyDelete
  19. Nini maana ya nahau bomu la machozi baridi,
    Lala kifudifudi
    Anakufa huku akining'inia

    ReplyDelete
  20. Replies
    1. Chapa mguu maana yake tembea umbali mrefu

      Delete
  21. Maana ya nahau miyoyo yetu imefinywa nisaidieni please

    ReplyDelete
  22. Maana ya nahau amekuwa paka shume?

    ReplyDelete
  23. Maana ya nahau amekuwa paka shume?

    ReplyDelete
  24. Naomba msaada maana ya nahau hizi:
    1.Amelamba garasha
    2.Amekula bingo
    3.Amekula kishoka
    4.Amekula mabo

    ReplyDelete
  25. Naomba msaada wa nahau hizi:
    1.amelamba garasha
    2.amekula bingo
    3.amekula kishoka
    4.amekula mabo

    ReplyDelete
  26. Naomba maana ya nahau
    Kwenda na maji

    ReplyDelete
  27. Maana ya ukinitia moto ninapaa

    ReplyDelete
  28. Naomba maana ya kondoo si Mali



    ReplyDelete
    Replies
    1. Nisaidieni maana ya nahau inayosema changa bia

      Delete
    2. Namm naombeni maana hii ya nahau isemayo lubu,piga"changa bia",kula mumbi,noa winda na kufa maji

      Delete
  29. Nini maana ya nahau isemayo "kula vichwa"

    ReplyDelete
  30. Changa bia mama yake " shirikiana

    ReplyDelete
  31. Nisaidie maana ya nahau piga hodi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Piga hodi maana yake ni kuomba ufunguliwe.

      Delete
  32. Naomba maana ya nahau amekuwa paka shule

    ReplyDelete
    Replies
    1. Piga winda maana yake ni nini

      Delete
  33. Nini maana ya nahau maji ya
    fufutende

    ReplyDelete
  34. Nini maana ya nahau kata kiu,kufa maji,kufa kikondoo,piga winda

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kufa kikondoo maana yake ni kufa bila kujitetea

      Delete
  35. Naombàaa maana ya nahau hii piga winda

    ReplyDelete
  36. Namba kujua maana ya nahau....ameota miziz

    ReplyDelete
  37. Njni maana ya Nahau "Kunoa lubu"

    ReplyDelete
  38. Nini maana ya Nahau "Kunoa lubu"

    ReplyDelete
  39. Jamaniiii kwa mfano wasukuma,wasambaaana jamaniiii zingne nahau gan wanapenda kutumiaaaa

    ReplyDelete
  40. tafadhali nipe misemo kumi yenye neno kufa

    ReplyDelete
  41. Nini maana ya pangu pangu pakavu tia mchuzi tena

    ReplyDelete
  42. Replies
    1. Ina maana ya kuwa mkaidi na kutotii unchoambiwa

      Delete
  43. Nini maana ya nahau kata mtama

    ReplyDelete
  44. Replies
    1. unga mkono ni kukubaliana na jambo

      Delete
  45. Replies
    1. Nini maana ya nahau piga pande

      Delete
  46. Kuota pembe ina maana gani

    ReplyDelete
  47. Naomba maana ya kata kiu

    ReplyDelete
  48. Maana ya nahau ingia mkenge

    ReplyDelete
  49. Maana ya nahau Ina lubu

    ReplyDelete
  50. Maana ya nahau ona lubu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Maana yake fikiri kwamakin

      Delete
    2. Nisaidieni maana ya chana mbuga

      Delete
    3. Timba Mali ndo Nini

      Delete
    4. Tumia mali kwa fujo

      Delete
  51. Kunoa lubu inamaana gani?

    ReplyDelete
  52. Tii amri ni nahau au tashhisi

    ReplyDelete
  53. Nini maana ya nahau, changa bia ?

    ReplyDelete
  54. unaweza kunisaidia na semi zingine ikiwa na maana

    ReplyDelete
  55. Nini maana ya maji shinda

    ReplyDelete
  56. Kupiga unaa Ina maana Gani?

    ReplyDelete
  57. Nini maana ya changa bia?

    ReplyDelete
  58. Nini maana ya nahau pata naizesheni?

    ReplyDelete
  59. Nini maana ya nahua kichwa maji naomba msaada

    ReplyDelete
  60. Nini maana ya “Kuona cha mtema kuni”

    ReplyDelete
  61. Nini maana ya amepata ashekali

    ReplyDelete
  62. Je ana mkono wa wazi maana yake nini

    ReplyDelete
  63. Naomba msaada maana ya methali ya pampaluma mlango wa chuma ukiufungua hauna huruma

    ReplyDelete
  64. Maana ya nahau lala kifudifudi

    ReplyDelete
  65. Nini maana ya Lima kwa mguu

    ReplyDelete
  66. Nini maan ya nahau punde si punde

    ReplyDelete
  67. Maana ya nahau Vaa cheche ni nini?

    ReplyDelete
  68. Jamani nisaidie maana ya nahau hi kufa kiofisi

    ReplyDelete
  69. Nini maana ya usemi amekuwa fremu

    ReplyDelete
  70. Maana ya piga mbiu

    ReplyDelete
  71. Feckson naomba unisaidie na nahau isemayo piga mbiu

    ReplyDelete
  72. Nini maana ya nahau. Changa bia?

    ReplyDelete
  73. Maana ya sema kwa sauti

    ReplyDelete
  74. Maana ya kunja jamvi

    ReplyDelete
  75. Maana ya piga milundi

    ReplyDelete
  76. Nini ni maana ya change bia

    ReplyDelete
  77. Anakula lakini hashibi maana yake nini

    ReplyDelete
  78. Nini maana ya nahau piga domo msaada

    ReplyDelete
  79. maana ya kata pua

    ReplyDelete
  80. Naomba mnisaidie maana ya nahau kazi ya kijungu jiko

    ReplyDelete
  81. Pnahau piga winda Ina maana ya

    ReplyDelete
  82. Nini maana ya nahau valia njuga

    ReplyDelete
  83. Nini maana piga chenga

    ReplyDelete

POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza