Showing posts with label Michezo na Burudani. Show all posts
MWANAMME NI KAZI
Katika utafiti wa hivi karibuni, watafiti wamegundua kwamba, wanawake wanawapenda wanaume wasio waoga na mashujaa kuliko wale waoga. Ushujaa wa wanaume ni kigezo kikubwa kwa wanawake kuwapenda marafiki wa kiume wa muda mrefu na muda mfupi. 

Hii inamaanisha kwamba katika urafiki wa kawaida na wa kimapenzi na wa kindoa, wema au ukarimu ulionekana kwamba ni kigezo cha kawaida tu na sio kipaumbele chao.

Tukirudi kwa mababu zetu wa kale walioishi mapangoni, wanawake waliwapenda wanaume shujaa ambao wangeweza kujitoa muhanga kuwalinda wao na watoto wao. Mwanaume ambaye alikuwa na uwezo wa kujitoa muhanga alionekana kuwa na uwezo wa kuwinda bila hofu na kuzama porini kutafuta chakula kwa Ajili ya familia au kutafuta dawa kwa ajili ya matibabu kwa familia yake.

Kikubwa hapa ni ulinzi na usalama. Na hili linawafanya wanawake wengi kuwapenda mabaunsa kwa sababu hih hii ya ulinzi na usalama
Mwanaume mwenye nazo anaonekana kupendwa lakini hapa swala si fedha yake, bali anaonwa kama ndiye anayeweza kuilinda familia. Ukikuta wanawake wanavutiwa na wanaume wenye fedha, usishangae, kwani bado wanaongozwa na  haja yao kuu ya  kuhakikishiwa usalama wao.

Kwa kifupi ni kwamba kinachotafutwa na wanawake ni  amani nausalama.

Siku hizi  fedha imechukua nafasi katika kujihakikishia usalama wetu. Kila kitu siku hizi ni pesa na ndio maana wanawake kwa dhana ile ile ya kujihakikishia usalama wanavutiwa na wanaume wenye nazo.

Sio kwa sababu ya tamaa...... La hasha, ni kutaka kuwa na uhakika na maisha yake na familia yake.
Mwanamume akikosa sifa ya fedha ataangaliwa kwa ujasiri  na uchakarikaji.Kwa haya mwanamke anajua kwamba kwa kushirikiana naye mbeleni maisha yatakuwa mazuri na salama.
Ikitokea kwa mfano kaolewa na mwanaume mzigo au siku hizi huwaita "Dead alive" au mwanaume suruali, jukumu la kutafuta hulishika mwenyewe kwa sababu hamna jinsi na mara nyingi hufanikiwa kuzikamata kwa sababu anafanya hivyo kwa nia na dhamira ya kujihakikishia usalama.
Kama vile wanaume wanavyokosea kuoa kwa kutopiga hesabu zao vizuri katika kuoa vivo hivyo wanawake nao hukosea kwa kudanganyika na zile sifa za mwanaume za muda mfupi bila kuchunguza vizuri zaidi. 

Wapo ambao wakigundua kwamba mwanaume aliyeolewa naye ni mvivu na asiyejali familia anafungasha na kuondoka, lakini wapo ambao wanatafuta suluhu na kuamua kushika hatamu za kuendesha nyumba hawa ni wale wanaoogopa kufanya makosa kwa mara ya pili yaani kuondoka na kuangukia kwa mwanaume mwingine mwenye sifa zisizopendeza. Hawa wanakubali matokeo na kuamua kusimama kama wao, hawayumbishwi na huwakubali wenzi wao kama walivyo.

Wanawake wa aina hii mara nyingi kufanikiwa sana tofauti na wale wanaojipweteka na kubaki wakilalamika. Lakini naomba niseme kuwa wanawake kwa kiasi kikubwa ni mashujaa hawawezi kukaa na kuangalia familia ikianguka kwa sababu mwanaume hawawajibiki. Wengi sana tena kiasi cha kutosha husimama na kushika nyumba kwani wanajua kwamba nyumba ikianguka mara nyingi lawama huwaendea wao.

Pia mwanamke huvutiwa na mwanaume anayejali usalama wa wazazi na ndugu  zake Mwanamke yuko tayari kumpenda mume mwingine nje ya ndoa kama huyu mume ataonesha  upekee katika kuwa chukua wazazi wake.

Kwa mfano wapo wanaume wengi hali zinapokuwa ngumu huzikimbia familia zao na kuzitelekeza hata kwa miaka kadhaa, lakini wakirudi wanakuta familia ipo mbali kimandeleo na watoto wana hali nzuri. Hao ndiyo huitwa wanawake wa shoka. Lakini maendeleo hay0 huwa hayaji hivi hivi, yuko mwanamume aliyependwa badala ya aliyeikimbia familia.

Kwa hiyo swala la uelewa,umaridadi, utanashati katika siyo sifa zinazotazamwa na wanaume bali ni ulinzi na upendo, 

Kwa wanaume vigezo ni utii, na matunzo mazuri. Vitu hivi kwao ni muhimu katika swala zima la kutafuta mwenza. 


Timu zote mbili Isamilo na Mwanza Sekondari zikiwa kwenye mkao wa picha ya pamoja.
Jana Ijumaa baada ya swala ya Ijumaa, timu ya walimu  Mwanza Sekondari na Shule ya Kimataifa ya  Isamilo (Isamilo International School) zote za hapa jiji la Mwanza, zilikuwa na mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu wanaume.

Mchuano huu wa mpira uliozishirikisha timu hizi mbili za shule za sekondari jijini hapa, ulikuwa ni kivutio kikibwa cha kuanzia mapumziko ya mwishoni mwa juma.

Kwenye kinyanganyiro hiki Isamilo iliwachapa Mwanza sekondari bao tatu kwa moja. 

Mabao yote yalifungwa kipindi cha kwanza.Goli la kwanza la Isamilo lilifungwa na Mwl.Manda Rafaeli na la pili na Mwl. Peter Kiswaga kwa mkwaju  aloupiga akiwa kiasi cha mita 80  hadi langoni mwa goli la ‘ Mwaseco’ na kumbabatiza mlinda lango na mpira kutinga kimiani. 

Goli la kufutia machozi la 'Mwaseco' lilifungwa na Mwl. Elias Charles  kwa mkwaju alioupokea toka kwa Mwl. David Nestory.

Goli la tatu la Isamilo  lililodumu hadi kipenga cha mwisho lilifungwa kipindi hicho hicho cha kwanza na  Mwl. Nijel Moye baada ya kizaa zaa kilichotokea langoni mwa goli la ‘Mwaseco’ baada ya mkwaju wa kona  ulioletwa langoni na Mwl. Cairl.

Timu ya Mwanza Sekondari iliundwa na kikosi cha walimu wafuatao. Mwl. David Nestory  huyu ni mkuu wa shule ya Mwanza Sekondari na alicheza  namba 11.

Wengine ni Mwl. Abeli  Kalilo ambaye alikiwa nahodha wa timu akicheza nambari  8. 

Sanjari nao ni Mwl. Ahmed Hamdan  nambari 4 mgongoni , Mwl.Boaz Edward nambari  9, Mwl. Eliasi Charles nambari  10. na mlinda lango wao Mwl. Shata Elia.

Timu hizi zilichezesha wachezaji saba saba. Mchezaji wa saba  wa  Mwaseco' ni Mwl. Jeremiah Kinshuli aliyevalia jezi namba 7 mgongoni. 

Waliokuwa kwenye benchi kwa 'Mwaseco' ni Mwl. Dickson  Masomi, Abswamadu Nyenye, Ramadhani Bilali na Vitalius Marisiale.
Kikosi kizima cha 'Mwaseco ' Wana 'SOMA MPAKA UFE' na washauri wa timu wakiwa katika pozi la picha ya pamoja

 Safu ya Isamilo iliundwa na  Mwl. Appollo aliyekuwa langoni. Mwl. Marx nambari 13, Mwl. Jake nambari 10, Mwl. Nijel Moye nambari 4,Mwl. Cairl nambari 3, Mwl. Peter Kiswaga  nambari 14,  na Mwl.Manda Rafaeli nambari 7. 

Walokuwa benchini kwa upande wa Isamilo ni: Mwl. Joseph Sospeter, Mwl.Godfrey Francis na Mwl. Robert  Robert.

Timu zote zilicheza mchezo  mzuri wa kistaarabu usio na fujo.Katika kipindi cha pili mpira ulichezwa kwa pasi nyingi na kwa kasi kubwa lakini hakukuwa na timu yeyote iliyoliona lango la mwenzie. 

Kwa upande wa timu ya 'Mwaseco' mchezaji Ahmed Hamdani alikuwa ndiye nyota wa mchezo kwa kuidhibiti timu ya Isamilo kuliona lango lao. Hasa kipindi cha pili aliweka juhudi za ziada.

Timu ya Isamilo ilipambwa na walimu wageni. Kati ya wachezaji wao kumi nusu walikuwa wenyeji na nusu  nyingine wageni. Hii ni kwa sababu shule hii ni ya kimataifa hivyo ina walimu wazungu wengi.
Eliasi Charles mfungaji wa goli la Mwaseko na mfunngaji mwenzie Nigeli Moye wa Isamolo na mgongoni mwao aliya na glovzi  mikonono ni mlinzi wa Isamilo Mwl.Appollo'
Pamoja na kufungwakipindi cha kwanza, kipindi cha pili wana Mwaseco walijihami vilivyo kwa kuelekeza mipira ya hatari kwenye lango la Isamilo na kuwazibiti kuongeza mabao.

Pamoja na makeke yao haya hawakuweza kulipenya lango la Isamilo. Kikwazo chao kikubwa kilikuwa ni mlinda lango wa Isamilo Mwl. Appollo. Hakika mlinda mlango huyu alikuwa nyota kwa timu hii ya Isamilo.Alikuwa akidaka mipira  iliyokuwa ni magoli dhahiri.

Hadi kipenga cha mwisho magoli yalikuwa Mwaseco moja na Isamilo tatu.

Kwa wana Mwaseco zaidi ya kufungwa, mchezo huu ulionesha mabadiliko kiasi fulani kwao kwani  Ijumaa iliyopita ya tarehe  27 Februari 2015 walicheza na Sekondari ya Bugarika wakachapwa mabao SABA kwa ‘nunge.’


Pale mwishoni mwa mechi nilimuuliza nahodhda wa 'Mwaseco' Mwl. Abeli kalilo kama kwa vichopo hivi vikali viwili mfululizo bado wanayo hamu ya kualika timu nyingine? Naye akalijibu kwamba wanakaribisha maombi toka timu yeyote iliyo tayari kucheza nao huku akionesha hamu ya kuwaalika Shule ya Sekondari Nsumba kwa madai eti Nsumba haina historia ya kuwafunga.
Mwl Elibariki Kimei wa 'Mwaseco' na Mwl, wa Isamilo  wakiongea na kati yao kijana wa Mwl wa Isamilo
 akishangilia ushindi wa Isamilo baada ya kipenga cha mwisho.
Gotze wonder goal crowns Germany champions
Mario Gotze na 19 kushoto akiwa 
na Thomas Muller na 13 wakifurahia  goli lililommaliza Agentina.
Ujerumani yachukua kombe la dunia kwa mara ya nne huko Rio de Jenairo nchini Brazil kwa kuichapa Agentina bao 1-0 katika michuano ya Ishirini ya kombe la Dunia iliyofanyikia huko  mwaka huu 2014.

Nakifanya Ujerumani kuwa timu ya kwanza ya Ulaya kulichukua kombe hili likichezewa Amerika ya kusini.


Michuano hii ilianza rasmi siku ya Alhamisi 12 Juni, 2014 kwa mchuano kati ya Brazili na Croatia ambako Brazil iliifunga Croatia kwa tabu mabao matatu kwa moja. Brazil  3-1Croatia


Gotze wonder goal crowns Germany champions
Mario Gotze na 19 kushoto akiwa
na Thomas Muller na 13 wakifurahia  goli
Baada ya dakika 90 timu zota zilikuwa sare, Katika dakika ya 113 ndani ya muda wa nyoneza  mchezaji Mario Gotze aliipatia  goli la pekee na la Ushindi.
 Germany 1-0 Argentina     
Wachezaji wa ujeremani wanasubiriwa na kitita cha mamilioni ya Dolla za Kimarekani kama zawadi kwa ushindi huu. 



                               






















Huku Agentina wakisikitika kukosa Ushindi huu watani wao wa jadi Brazil ambao ndiyo wenyeji wa michuano,  kwa kuchapwa mabao Saba kwa moja na Wajerumani kimoyomoyo wamekuwa wanafurahia Agentina kupoteza ushindi.


Brazil ambayo ilitegemewa na wengi kuchukua kombe hili mwaka huu imesikitisha washabiki wake hasa pale ilipopoteza pia ushindi wa nafasi ya Tatu kwa kufungwa na Uholanzi mabao matatu bila 

Kocha wa Timu y Brazili Luiz Filipe Scolari
Wakati Kocha wa Timu ya Brazil  Luiz Felipe Scolari  akisikitika kupoteza kazi mwanzake Louis van Gaal anasherehekea ushindi

Kocha wa Uholanzi Louis Gaal  akipongeza Wachezaji wake
Kuona video BOFYA HAPA







Orodha ya nchi ambazo michuano ya kombe la Dunia limefanyikia tokea kuanza kwake 1930  hadi mwaka 2030.Ifuatayo ni orodha hii.

Orodha ya nchi waandaaji toka 1930- 2022 na nchi iliyochukua kombe hilo kipindi hicho

YearHostWinner
1930 Uruguay Uruguay
1934 Italy Italy
1938 France
1942Cancelled due to World War IINo Winner
1946
1950 Brazil Uruguay
1954  Switzerland West Germany
1958 Sweden Brazil
1962 Chile
1966 England England
1970 Mexico Brazil
1974 West Germany West Germany
1978 Argentina Argentina
1982 Spain Italy
1986 Mexico Argentina
1990 Italy West Germany
1994 United States Brazil
1998 France France
2002 South Korea /  Japan Brazil
2006 Germany Italy
2010 South Africa Spain
2014 BrazilMshindi tunamtegemea.
Bashiri atatokea wapi?
2018 Russia
2022 Qatar
Kutokana na orotha hii BRAZIL imeandaa michuano hii mara mbili hadi sasa na imelichukua kombe hili mara nne ikifuatiwa na Italy na Ujerumani ambazo kila moja imelichukua kombe mara tatu.

Spain ambayo ilikuwa mshindi mtetezi kipindi hiki imekwisha tolewa katika kinyanganyiro hiki.

Swali wewe unatabiri atakayechukua ushindi LEO ni nani?
Timu gani itakuwa mshindi leo kati ya BRAZIL Vs CHILE na COLOMBIA Vs URUGUAY ? CHAGUA
  
pollcode.com free polls 

Leo tarehe 27/06/2014 Timu zilizo katika mzunguko wa kumi na sita hatua ya  pili ni  Brazili  na Chile saa moja jioni na Colombia na  Uruguay saa tano usiku. 

  1. Matches
  2. Groups
  3. 2nd Stage

Brazil
7:00 PM
Chile

Colombia
11:00 PM
Uruguay
Ingia tena kesho kupata matokeo na taarifa nyingine mpya za kombe hili:

POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza