Mwanza Secondari Yapigwa Bao 3-1 na Shule ya Kimataifa ya Isamilo katika Mechi ya Kirafiki.
![]() |
Timu zote mbili Isamilo na Mwanza Sekondari zikiwa kwenye mkao wa picha ya pamoja. |
Jana Ijumaa baada ya swala ya Ijumaa, timu ya walimu Mwanza Sekondari na Shule ya Kimataifa ya Isamilo (Isamilo International School) zote za hapa jiji la Mwanza, zilikuwa na mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu wanaume.
Mchuano huu wa mpira uliozishirikisha timu hizi mbili za shule za sekondari jijini hapa, ulikuwa ni kivutio kikibwa cha kuanzia mapumziko ya mwishoni mwa juma.
Kwenye kinyanganyiro hiki Isamilo iliwachapa Mwanza sekondari bao tatu kwa moja.
Mabao yote yalifungwa kipindi cha kwanza.Goli la kwanza la Isamilo lilifungwa na Mwl.Manda Rafaeli na la pili na Mwl. Peter Kiswaga kwa mkwaju aloupiga akiwa kiasi cha mita 80 hadi langoni mwa goli la ‘ Mwaseco’ na kumbabatiza mlinda lango na mpira kutinga kimiani.
Goli la kufutia machozi la 'Mwaseco' lilifungwa na Mwl. Elias Charles kwa mkwaju alioupokea toka kwa Mwl. David Nestory.
Goli la tatu la Isamilo lililodumu hadi kipenga cha mwisho lilifungwa kipindi hicho hicho cha kwanza na Mwl. Nijel Moye baada ya kizaa zaa kilichotokea langoni mwa goli la ‘Mwaseco’ baada ya mkwaju wa kona ulioletwa langoni na Mwl. Cairl.
Timu ya Mwanza Sekondari iliundwa na kikosi cha walimu wafuatao. Mwl. David Nestory huyu ni mkuu wa shule ya Mwanza Sekondari na alicheza namba 11.
Wengine ni Mwl. Abeli Kalilo ambaye alikiwa nahodha wa timu akicheza nambari 8.
Sanjari nao ni Mwl. Ahmed Hamdan nambari 4 mgongoni , Mwl.Boaz Edward nambari 9, Mwl. Eliasi Charles nambari 10. na mlinda lango wao Mwl. Shata Elia.
Timu hizi zilichezesha wachezaji saba saba. Mchezaji wa saba wa Mwaseco' ni Mwl. Jeremiah Kinshuli aliyevalia jezi namba 7 mgongoni.
Waliokuwa kwenye benchi kwa 'Mwaseco' ni Mwl. Dickson Masomi, Abswamadu Nyenye, Ramadhani Bilali na Vitalius Marisiale.
![]() |
Kikosi kizima cha 'Mwaseco ' Wana 'SOMA MPAKA UFE' na washauri wa timu wakiwa katika pozi la picha ya pamoja |
Safu ya Isamilo iliundwa na Mwl. Appollo aliyekuwa langoni. Mwl. Marx nambari 13, Mwl. Jake nambari 10, Mwl. Nijel Moye nambari 4,Mwl. Cairl nambari 3, Mwl. Peter Kiswaga nambari 14, na Mwl.Manda Rafaeli nambari 7.
Walokuwa benchini kwa upande wa Isamilo ni: Mwl. Joseph Sospeter, Mwl.Godfrey Francis na Mwl. Robert Robert.
Timu zote zilicheza mchezo mzuri wa kistaarabu usio na fujo.Katika kipindi cha pili mpira ulichezwa kwa pasi nyingi na kwa kasi kubwa lakini hakukuwa na timu yeyote iliyoliona lango la mwenzie.
Kwa upande wa timu ya 'Mwaseco' mchezaji Ahmed Hamdani alikuwa ndiye nyota wa mchezo kwa kuidhibiti timu ya Isamilo kuliona lango lao. Hasa kipindi cha pili aliweka juhudi za ziada.
Timu ya Isamilo ilipambwa na walimu wageni. Kati ya wachezaji wao kumi nusu walikuwa wenyeji na nusu nyingine wageni. Hii ni kwa sababu shule hii ni ya kimataifa hivyo ina walimu wazungu wengi.
![]() |
Eliasi Charles mfungaji wa goli la Mwaseko na mfunngaji mwenzie Nigeli Moye wa Isamolo na mgongoni mwao aliya na glovzi mikonono ni mlinzi wa Isamilo Mwl.Appollo' |
Pamoja na kufungwakipindi cha kwanza, kipindi cha pili wana Mwaseco walijihami vilivyo kwa kuelekeza mipira ya hatari kwenye lango la Isamilo na kuwazibiti kuongeza mabao.
Pamoja na makeke yao haya hawakuweza kulipenya lango la Isamilo. Kikwazo chao kikubwa kilikuwa ni mlinda lango wa Isamilo Mwl. Appollo. Hakika mlinda mlango huyu alikuwa nyota kwa timu hii ya Isamilo.Alikuwa akidaka mipira iliyokuwa ni magoli dhahiri.
Hadi kipenga cha mwisho magoli yalikuwa Mwaseco moja na Isamilo tatu.
Kwa wana Mwaseco zaidi ya kufungwa, mchezo huu ulionesha mabadiliko kiasi fulani kwao kwani Ijumaa iliyopita ya tarehe 27 Februari 2015 walicheza na Sekondari ya Bugarika wakachapwa mabao SABA kwa ‘nunge.’
Pale mwishoni mwa mechi nilimuuliza nahodhda wa 'Mwaseco' Mwl. Abeli kalilo kama kwa vichopo hivi vikali viwili mfululizo bado wanayo hamu ya kualika timu nyingine? Naye akalijibu kwamba wanakaribisha maombi toka timu yeyote iliyo tayari kucheza nao huku akionesha hamu ya kuwaalika Shule ya Sekondari Nsumba kwa madai eti Nsumba haina historia ya kuwafunga.
![]() |
Mwl Elibariki Kimei wa 'Mwaseco' na Mwl, wa Isamilo wakiongea na kati yao kijana wa Mwl wa Isamilo akishangilia ushindi wa Isamilo baada ya kipenga cha mwisho. |
0 comments: