|
Malkia wa Taarab nchini Tanzania Khadija Omar Kopa |
Jana Asubuhi ya Ijumaa tarehe 9 Mei 2014 Malkia wa Taarab nchini Tanzania Khadija Omar Kopa aliwasili Jijini Mwanza, akiwa ameambatana na The Super Roxx Abdul Misambano Mkali wa wimbo wa Asuu.
Jioni hiyo walitumbuiza kwa mitikisiko ya Pwani katika ukumbi wa Kilimanjaro Night Club , Buzuruga Plaza Nyakato Jijini Mwanza.
|
Malkia wa Taarab nchini Tanzania Khadija Omar Kopa akiwa tu ndio kashuka katika uwanja wa ndege wa jiji la Mwanza asubuhi ya jana (Ijumaa)kwa ajili ya kutoa burudani kwa wakazi wa Mwanza katika ukumbi wa Kilimanjaro Night Club, Buzuruga Plaza Nyakato. |
Chini ni Mzee wa Asuuu. The Super Roxx Abdul Misambano. Kiingilio kilikuwa Sh.elfu kumi (10,000/=) kwa mtu mzima.
Habari zaidi hapo kesho tutakapofahamu ni wapi watakuwa baada ya kutoka hapo Buzuruga.
|
The Super Roxx Abdul Misambano akiwasili katika uwanja wa ndege wa jiji la Mwanza asubuhi ya jana, kwa ajili ya kutoa burudani kwa wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake kwenye usiku wa Mitikisiko ya Pwani katika ukumbi wa Buzuruga Plaza Nyakato jijini Mwanza. Hali ya mapokezi ilikuwa nzuri kwani Mwanza wapenzi wa nyimbo za Pwani ni wengi na kweli ni siku kidogo kwa ugeni kama huu kuja Mwanza. |
0 comments: