INDIA YADAI KUGUNDUA DAWA YA KUTIBU UKIMWI.
Pamoja na tafiti hizo shirika la afya duniani limekuwa likifuatilia kwa karibu jitihada za tafiti hizi na pengine kuzisimamia au kuzichangia.
Lakini hali inavyoonekana suala hili kwa upande mmoja limekuwa lina sura ya ushindani ndani yake wa nani awe wa kwanza kuwa kinara wa ugunduzi huu.
Mashirika mengi ya kitafiti ulimwenguni yamekuwa yakitoa taarifa za tafiti zao zikiwa bado hazijaiva..
Majaribio yakuthibitisha dawa na chanjo zilizogunduliwa yamefanywa mengi na matokeo yaliyopokelewa ni mengi lakini cha ajabu tunaambiwa chanjo wala tiba haiko karibu kupatikana.
Lakini matumaini hayapo kwani inadaiwa yanahitajika marekebisho ya mapungufu yanayojitokeza.
Sababu kuu ya kushindikana kupatikana dawa au chanjo ni madai kwamba kirusi cha UKIMWI si aina moja na pia hujibadili badili haraka kwa kujihami na dawa au chanjo zilizopatikana.
Kwa maelezo na majaribio ya Wahindi waliyoyaonesha huenda wakawa wamefuzu.kupata Dawa yaUKIMWI. Shuhuda za wagonjwa waliopona zinatia matumaini.
Katika ripoti ya utafiti wa Dawa yao ya Unani Anti-HIV Drug katika kikao cha kimataifa huko TIANJIN, CHINA tarehe 1-3 Desemba 2006, RIPOTI yao inatia matumaini.
Cha kushangaza ni kwamba hivi ni kwa nini bado WHO iko kimya hadi sasa kwa taarifa nzuri na za kutia matumaini kama hizi.
Kingine cha ajabu zaidi ni viongozi wa nchi zetu hizi zinzoendelea na wenye nafasi za kifedha kuzidi kukimbilia India kwa matibabu, Au sababu za kumiminikia kwao huko ni kama zile za kwa babu wa Loliondo.
Kama nasi tungekuwa na uwezo nadhani hospitali zetu zingefungwa maana wote tungeishia India kama tulivyojazana kwa babu wa Loliondo.
Waswahili wanasema lisemwalo lipo na kama halipo laja.Wahindi hawataishia kutuokoa kwa usafiri wa bajaji bali nadhani watakuja kuwa magwiji wa masuala ya tiba pia.
Kwa uthibitisho zaidi juu ya uponyaji huu, huu hapa ushuhuda wa mgonjwa wa ukimwi aliyepona kwa dawa hii.
0 comments: