MBWA TISHIO KWA WAKAZI WA SWEYA A NA B AULIWA
Mtoto James Magoti akisaidiwa na kaka yake kuonesha sehemu aliyoumwa |
Mbwa huyu
ameanza kung’ata kuanzia Jumamosi ya tarehe 24, Junuari watoto watatu, James
Magoti, Irene Mashaka na aliyejulikana kwa jina moja la Bahati.
Mbuzi aliyeng’twa ni wa ndugu John Ngugi na
inasemekana aliuliwa hapo hapo na mbwa huyu.
Leo, Jumapili tarehe 25 Januari, 2015, asubuhi, balozi Otieno Kadondi aongoza kundi kubwa la wana Sweya wakiwa wamebeba mikuki, nondo, marungu na magongo kumsaka mbwa huyu.
Mwenyekiti
mteule ndugu Joseph Masome naye hakuwa nyuma, alishiriki zoezi hili la kumsaka
mbwa huyu aliyetokea kuwa tishio la mtaa wote wa Sweya ndani ya siku hizi
mbili.
Hasira za
wananch kwa mbwa huyu zilipanda zaidi pale mbwa huyu alipong’ata watoto wengine
wawili mmoja mtoto wa Bahati ambaye ni bubu na mwingine ambaye jina lake halikupatikana
kwa uhakika lakini ilidaiwa kuwa ni mjukuu wa Marehemu Chacha Kichele.
Baada ya
msako mkali kuzunguka mitaa yote ya Sweya A na Sweya B wanakijiji walifanikiwa
kumtia mikononi huyumbwa na kumuua hapo
hapo.
Katika
harakati za kumsaka mbwa huyu mbwa wengi walionekana kuzagaa ovyo hapa na pale
pasi na kufungiwa ndani kama inavyotakiwa kwa wanaofuga wanyama hawa.
Imefahamika pia
kwamba kumezuka kamtindo ka baadhi ya watu kuwaingiza mbwa kwenye gari na
kwenda kuwatupa sehemu za mbali hususani nje ya mji kwa dhana kuwa hawawezi
kujua njia ya kurudi walikokuwa awali..
Hali hii
inaonesha kuwa mbwa wanafugwa kiholela na wengi wakiwa hawajachanjwa kuwakinga
na ugonjwa wa kichaa cha mbwa (rabies).
Wakati wa
zoezi la kumsaka mbwa huyu, wananchi walisikika wakiilalamikia idara ya mifugo,
jijini Mwanza kwa kushindwa kwake, kutimiza wajibu wake wa kudhibiti ufugaji
holela wa mbwa na kuhimiza uchanjaji wa mbwa kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha
mbwa.
“Gharama ya
kumchanja mtu akinga’twa na mbwa kumkinga na kichaa cha mbwa ni zaidi ya laki
moja.’’Mmoja wa wasakaji wa mbwa huyu alisikika akisema.
Ukweli
unabakia pale pale kuwa gharama za
kumhudumia mtu anapong’atwa ni kubwa zaidi ya hapo haswa ikizingatiwa kuwa jamaa
na majirani huingiwa na hofu na kushindwa kufanya shughuli zao kama kawaida na kwa kuwa kunakuwepo na upoteaji wa muda mwingi
katika kushughulikia matibabu.
Tunaitaka
mamlaka husika kudhibiti kuzagaa kwa
mbwa na paka kiholela, jijini humu hali ambayo hubainishwa kwa kugongwa gongwa mbwa na paka mara kwa mara mabarabarani.
Mbwa aliyeuliwa |
Pamoja na udhibiti
huu ni vyema uchanjaji wa mbwa na paka ukawa unafanywa kila mwaka.
Zoezi hili si
tu kwamba litaleta utulivu bali bado litakuwa
ni njia mojawapo ya kuongeza pato la jiji.
Tatizo hili
laweza kuonekana ni la hapa Sweya lakini laweza kuwa ni kiashiria cha uwepo kwa
tatizo hili sehemu nyingine.
Balozi OTIENO Kadondi aliyehamasisha usakaji wa mbwa huyu aliyekuwa tishio la mitaa miwili ya SWEYA. |
Mwisho wa yote mbwa huyu alifukiwa kwenye shimo refu walochimba wana mtaa na kumfukia.
Wasiwasi ukabakia kwa wale waloumwa na mbwa huyu juu ya kupatiwa matibabu sahihi na pia kuchunguza mwenendo wa mbwa walioumwa na huyu anayedhaniwa kuwa na kichaa.
Ufugaji mbwa kiholela udhititiwa maana ni hatari kwa watu
ReplyDelete