KAMPENI ZA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA MTAA SWEYA ZAANZA.
![]() |
Kiongozi wa CCM kata, akimkaribisha mgombea kwa tiketi ya CCM, mama Mtalo kunadi sera zake na kuomba kura |
Marehemu Bw. Pius alikuwa kasimama kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM na mgombea mwenanzake Bw. Fred alisimama kwa tiketi ya CHADEMA.
Kwa bahati mbaya Bw. Pius aliugua siku chache kabla ya uchaguzi
na siku hiyo uchaguzi ukifanyika alifariki akiwa katika matibabu hospitali ya Bugando kipindi kura zikiendelea kupigwa.
Siku ya Jumapili ya tarehe 1, Februari 2015 CHADEMA ndio walioanza kulipanda jukwaa na kuanza kunadi sera zao na siku iliyofuata ya Jumatatu tarehe 3,Februari 2015 CCM walilipanda jukwaa kuziweka wazi sera zao.
Hakika safari hii wana Sweya wamekumbwa na changamoto la aina yake tofauti na awali linalotokana na mabadiliko waliyoyafanya wana CCM ya kumsimamisha mgombea mwanamke.
Kwa kura za awali CHADEMA ilikuwa ikiongoza zidi ya CCM katika mtaa huu wa Sweya na walishinda nafasi zote za wajumbe wa mtaa.
Tunachojiuliza ni kumbwa mabadiliko haya yatabadili mwelekeo na msimamo wa wana Sweya wengi waliowapa CHADEMA ushindi wa wajumbe wa serikali ya mtaa?
Bw. Reverian Mtalo akimnadi mgombea wa CCM ambaye pia ni mkewe alisema, anaweza na ameridhia uamuzi wake huo.
"Mke wangu amekua kiongozi katika ngazi mbalimbali kwenye vikundi vya kina mama, vya kijamii na vya kidini na aliponijulisha nia yake hii ya kugombea nafasi hii ya uenyekiti wa mtaa sikuwa na wasiwasi wala shaka yeyote,juu ya uamuzi wake huu na nilimruhusu na naamini anaweza" alisema Bw, Mtalo.
![]() |
Bw, Mtalo akimnadi mkewe. |
Kikundi cha wacheza ngoma na maonesho ya sarakasi kiliingia uwanjani na kuonesha maonesho, ambayo yalizikonga nyoyo za wasikilza kampeni kisawasawa.
![]() |
Kikundi cha burudani 'kikijimwayamwaya' kweye kampeni hizi |
Ukweli ni kwamba kampeni zinaonesha wagombea wa pande zote kuiva kisiasa na kutambua kile wanachokitaka kwani pande zote walimalizia kwa kuomba wananchi kuwapa kura za ndiyo.
Kilichobakia ni uamuzi wa wana sweya ni nani kati ya wagombea hawa kawashawishi kisera na wala sio malumbano ambayo wanaona hayana masilahi kwao.
![]() |
Wana Sweya wakimsikiliza mgombea wa CCM kwa makini |
Baadhi ya wana Sweya walisikika wakidai kuwa wanataka kiongozi wa watu, mchapa kazi na mwenye sera zenye mashiko na suala la Chama si msingi MKUU kwao.
0 comments: