GOOGLE NA MIWANI YA KIJASUSI IJIENDESHWAYO KWA MAELEKEZO. TEKNOLOJIA
Google watengeneza miwani yenye uwezo wa kupiga mtu picha au kumrekodi muhusika bila mwenyewe kujua kwa kuiamuru kufanya hivyo (google glass).
Ingawaje teknolojia hii sio mpya, Kampuni ya Google ndio ya kwanza kuja na teknoloji hii kwa njia ya miwani na kwa njia ya maelekezo.
Teknolojia kama hii Iliyokuwepo hapo awali ilikuwa katika simu za mkononi, vifungo vya nguo , kalamu na kwenye noti books na iliendeshwa kwa kubonyeza na sio kwa kusema.
Cha ziada ni kwamba miwani hii hufanya kazi nyingi ikilinganishwa na vifaa hivyo vingine.
Inatarajiwa huwenda bidhaa hii ikafanya vizuri sana katika mauzo kuliko bidhaa hizo zingine ingawa bei zake ziko chini ya miwani hii.
Google glass ni rahisi sana kutumia, kama unataka kupiga picha unachotakiwa kusema ni , “OK Glass, take a picture.”
Miwani hii na sehemo zake na umbo lake |
Upo kwenye foleni unaona fujo unataka kuchukua video, mwambie Google Glass naye atakusaidia kuchukua video. “OK Glass, take video.”
Uko mbali na unataka kuwaonyesha ndugu na marafiki kitu unachokiona wakati huo huo? Google glass inafanya yote haya, inakuja na kitu kama "Skype-style video chat". na kurusha unachotaka kiwafikie.
Umesafiri kwenda kuchukua mzigo China? Google glass itakusaidia kutafsiri lugha.Umeenda Zanzibar kutembelea majengo ya kitalii na unabaki kushangaa shangaa, uliza Google glass na itakupa maelekezo (tour guide).
Google glass ni kifaa ambacho unaweza kukitumia kurekodi video, kupiga picha, kutafuta habari katika Google, kutafsiri lugha, kutuma taarifa na unaweza fanya yote haya bila kutumia mikono yako (hands free).
Pia chaweza kutumika katika shughuli za kitabibu.On dakitari huyu akigundua tatizo la mgonjwa wake hata kabla ya kumpeleka maabara kupimwa.
Cha kusikitisha hapa ni kwamba kinasikia kiingereza tu.Huwezi kukipa maelekezo kwa kiswahili.
Uzuri ni kwamba, ukivaa miwani hii watu hawajui kama unawarekodi kwenye video au vipi. Hofu iliyopo ni kwa wabongo walivyo.Wabongo kama kawaida yao hujihami kupigwa picha au kurekodiwa kwenye video, ukivaa Google glass unaweza tolewa baa.
Bei ya miwani hii ni dola elfu moja na mia tano ($1500) kwa hela ya kitanzania kifaa hiki kwa wastani kitakuwa sh. mil. 2. 2. Hata hivyo kifaa hiki kinachovaliwa kama miwani, si vyema kutembea nacho kwa sababu vibaka hawataacha kukuvaa hasa baada ya kujua thamani yake.
Tusubiri Google wakiwezeshe kifaa hiki kiweze elewa kiswahili ndio na sisi tutakifaidi zaidi kwani hapa hamna kubonyeza bonyesha ni kuongea tu. Je ukipata Google glass utatumia kifaa hiki cha kisasa kufanyia nini?
Acha maoni yako.
Chanzo: recode,net
0 comments: