RAIS KIKWETE AWA MIONGONI MWA VIONGOZI BORA AFRIKA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amechaguliwa kuwa Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi katika Maendeleo Barani Afrika kwa mwaka 2013 .
Heshima hiyo kwa Rais Kikwete imetolewa na jarida maarufu la kimataifa la African Leadership Magazine Group na Tuzo la heshima hiyo itatolewa jioni ya leo, Jumatano, Aprili 9, 2014, katika sherehe iliyopangwa kufanyika Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C ikiwa ni pamoja na chakula cha jioni.
Tuzo hiyo ya heshima kubwa hutolewa kwa viongozi wa Afrika ambao hutoa mchango mkubwa zaidi wa kiuchumi na kijamii kila mwaka.
Tunzo hii imetolewa kwa Rais Kikwete kwa mwelekeo wake usiokuwa wa kawaida na wenye mafanikio makubwa kwa masuala ya utawala bora.
Kama kawaida wahenga walisema Nabii hapendwi kwao.Wengi wamejiuliza maswali ya kuonesha kutoridhishwa na uchaguzi huu kwa kujiuliza.
"wanaangalia nini kupata mshindi wa tuzo hii?"
Kwa mtizamo hasi walio nao juu ya raisi wetu kipenzi,wanasema hastahili kwa kudai yafuatayo;
"Tembo wameteketea kwa spidi ya ajabu, Twiga wamepandishwa ndege mchana kweupe, Mauaji na utesaji wa wale wanaopingana na serikali(RIP Mwangosi), Utesaji wa wanaharakati na wadai haki(Kama Dr Ulimboka), Kushamiri kwa biashara ya Madawa ya Kulevya na Deni la Taifa kupanda toka trilioni 4 mwaka 2005 hadi trilioni 23 mwaka 2013 na wanaona bado linazidi kupaa,Wanaona nchi inaweka record ya inflation mwaka 2012/2013."
Mimi nasema hii ni kama ile hadithi ya mwana kondoo na mbweha.
Mwana kondoo alikuwa akinywa maji. Mbweha alikuwa kule maji yatokako na akalalama kuwa mwana kondoo anamchafulia maji.
Mwana kondoo kwa kujitetea akamwambia iweje nikuchafulie maji wakati yanatokea kwako?
Mbweha kwa kujitetea akasema ni mwaka jana uliyachafua.
Mwana kondoo akadai mwaka jana nilikuwa sijazaliwa.Mbweha kuona hana hoja akadai; "Kama si wewe ni mmoja wa jammaa yako."
Hongera Raisi kikwete.Wenye midomo hawachaguliwi la kusema. Hivi na wote waliochaguliwa na shirika hili wote walilihonga au ni vibaraka kama inavyodaiwa?
Rais Kikwete atakuwa mmoja katika orodha ya wapokeaji wa tuzo hii ya Magazine ya Uongozi ya Afrika ya kila Mwaka.
Viongozi waliomtanguli kupata zawadi hii ni, Ernest Bai Koroma Raisi wa Sierra Leone mwaka 2013. Ellen Johnson Sirleaf Rais wa Liberia, James Michel Rais wa Shelisheli na Rais wa zamani wa Ghana John Kuffour
Wengine ni Marehemu Rais John Evans Atta Mills wa Ghana.
Wapokeaji wengine wa zamani waTunzo hii ya Magazine ya Uongozi Afrika ni pamoja na HE, Atiku Abubakar Makamu wa zamani wa Rais wa N igeria; H.E, Xavier Luc Duval Makamu wa Waziri Mkuu wa Mauritius;
Mheshimiwa Donald Kaberuka Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika; Malam Sanusi Lamido Sanusi Gavana wa Benki Kuu ya Nigeria; Alhaji Dikko Inde Abdullahi Comptroller Mkuu wa Huduma za Forodha Nigeria na Dr Mo Ibrahim Kiongozi wa Faundasheni ya Mo Ibrahim na wengine kwa kutaja tu hawa wachache. Mwaka 2012 hakupatikana mshindi.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania na watu wake wote.AMIN
Chanzo:Issa Michuzi, blog.
Hongera Mhe.Dr,.Jakaya Mrisho Kikwete Raisi wa Jamhuri ya
ReplyDeleteMuungano wa Tanzania kwa tuzo ulopata