Mvua za Masika Mwaka huu Zawa Tishio Kubwa Nchini.
Jeshi la Polisi Kikosi cha Uokoaji jana kililazimika kutumia nguvu kuwaokoa wakazi wawili wa Jangwani waliokuwa wamezingirwa na maji wlipokataa kuokolewa |
Mvua za masika zilizoanza kunyesha mwezi Desemba mwaka 2013 hadi kufikia Aprili 2014 katika sehemu nyingi hapa nchini Tanzania zimesababisha madhara yaliowaacha watu katika misiba na mashaka makubwa.
Dar es Salaam: Vifo, uharibifu wa mali, miundombinu na mafuriko, msongamano wa magari, baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam kukimbia makazi yao, wengine kulala kwenye magari na nyumba za wageni yote haya yamewakumba wakazi wa Jiji hili na vitongoji vyake, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa siku ya nne mfululizo hadi sasa.Timu ya waandishi na waokoaji waliofanya uchunguzi maeneo mbalimbali na kushuhudia hali halisi ilivyo, wanaripoti kwambawameshuhudia wanawake na watoto wakiwa nje ya nyumba zao na wengine kuhamia kwenye majengo ya Shule ya Msingi ya Mtakuja.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam alisema jana kuwa walikuwa wakiendelea kukusanya taarifa za maafa ikiwamo vifo alivyosema ni vingi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik alisema kuwa yupo kwenye kikao na hivyo atatoa taarifa zaidi za maafa baadaye.
Ajali ya helkopta:
Hapo mapema wakiwa katika jitihada za kufuatilia janga hili la mafuriko. Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akiwa na Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli,
Mwingine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova, wote hawa walipata ajali wakiwa katika helikopta ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Helikopta hii iligonga ukuta hapo Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam wakati ikitaka kuruka kwenda kukagua madhara ya mafuriko.
Taarifa za ajali hii zilithibitishwa baadae na Mkuu wa Majeshi (CDF), Jenerali Davis Mwamunyange, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik
“Ni kweli kwamba helikopta iliyopata ajali inamilikiwa na JWTZ…Hiyo ni ajali kama ajali nyingine yoyote. Imekuwa ni bahati mbaya wakati inaanza kuruka ikagonga ukuta wa jengo na kushuka chini….Mpaka sasa hatujajua sababu ya ajali hiyo,”Mwamnyange.
Mara:
Gari ikiwa mtaroni |
Gari hili lilikuwa na maofisa wa Wizara ya Uvuvi na Mifugo, waliokuwa katika safari ya kwenda Tarime kikazi.
Kutokana na utelezi na uendeshaji mbovu wa dereva huyu wa 'semi tela' ambayo haikusimama bali ilienda zake bila kujali kilichotokea ilivuruga safari ya maofisa hawa.
Kilichokuwa kinasubiriwa ni kupata watu au gari la kulivuta ili kulitoa katika mtaro huo.
Msaada kutoka wasamaria wema wa hapo Ingirichini Rorya ulisaidia sana kuwatoa kwenye mtaro huu.
Tarifa zilizopatikana baadae zilieleza kwamba waliokuwemo katika gari hilo hawakuumia licha ya gari kuingia maji na kusababisha kupelekwa kwa matengenezo kesho yake.
Tunazipongeza juhudi hizi za wananchi wa Iringichini wilaya ya Rorya na Maofisa wa Uvuvi na Mifugo kwa msaada wao kwani mfano walioonesha ni wa kuigwa.
Tegeta, Boko na Bunju:
Nyumba zikionekana zimefunikwa na maji |
Majirani wa mtoto huyo walisema tofauti na kawaida yao kumtoa mtoto huyo mvua inaponyesha, jana walimsahau na mama yake aliporejea alikuta maiti ya mtoto wake ikielea chumbani.
Katika mvua hizo takribani kaya 180 zimekumbwa na mafuriko huku wakazi wake wakijikuta hawana pa kwenda.
“Mimi nimekuwa hapa tangu Tanu imezaliwa, nyumba yangu imejaa maji nimeshazeeka sina mtu wa kunisaidia, wala sijui wapi nitakwenda. Nomba Serikali inisaidie,”alisema Hussein Ngaoma ambaye ni mjumbe wa nyumba kumi katika eneo hilo.
Naye Husna Ally ambaye pia nyumba yake imekumbwa na mafuriko alisema:
“Nasikitika, maana nimepata hasara kubwa. Mimi ni mfanyabiashara katika eneo hili la Boko, nina duka la kuuzia samani limejaa maji na sijaweza kuokoa chochote. Mzigo wa Sh30 milioni umeharibika wote.”
Pwani-
Daraja la BUNJU lilivyosombwa na maji |
Kukatika kwa daraja hili kumeleta hali iliyosababisha kukosekana kwa mawasiliano ya usafiri kwa watu wanaokwenda na kutoka mikoa ya Kaskazini.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei hali hiyo ilitokea jana saa tatu asubuhi, baada ya mvua kunyesha kupita kiasi na kusababisha mafuriko.
Alisema kuwa daraja hilo ambalo liko mpakani mwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, baada ya mvua kunyesha kwa muda mrefu lilididimia chini na kukata kabisa mawasiliano kati ya Bunju na Dar es Salaam.
Manyara:
Dereva wa NCAA akijinusuru kwa kupanda juu ya mti. |
alisems kuwa Dereva wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) mkoani Arusha, Juma Moshi, amenusurika kufa maji baada ya gari alilokuwa akiliendesha kusombwa na mafuriko katika mto Malera uliopo nje kidogo ya mji wa Karatu kwa kupanda juu ya mti.
Juma alilazimika kutoka kwenye gari hilo aina ya Toyota Land Cruizer SU 36037 lililokuwa limesombwa na mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha kwa umbali wa mita zipatazo 70 kutoka barabarani, alfajiri jana na kujiokoa kwa kupanda juu ya mti wakati akienda mjini Arusha kikazi.
Mkuu wa Idara ya Huduma ya Uhandisi wa NCAA, Isra Missana na wafanyakazi wengine wa mamlaka hiyo wakishirikiana na wakazi jirani wa eneo hilo, walimwokoa dereva huyo saa 12:30 asubuhi.
Na mamia ya wasafiri waliokuwa wakitoka maeneo ya Karatu na watalii toka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwenda mjini Arusha, Dar es Salaam na maeneo mengine nchini jana walikwama kwa muda kuvuka Mto Kirurumo uliokuwa umefurika maji hadi kupita juu ya barabara huku ukiporomosha mawe makubwa kutoka milima ya Mbulumbulu.
Mto huo upo mpakani mwa Wilaya za Monduli na Karatu. Miongoni mwa abiria ni waliokuwa wasafiri kwa mabasi ya Dar Express na Sai Baba kwenda Dar es Salaam.
Pia mamia ya magari yaliyokuwa yakiwasafirisha watalii kutoka hifadhi za taifa yalikuwa miongoni mwa magari mengine mengi yaliyokwama katika eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Felix Ntibenda, akizungumza katika eneo la tukio hilo alisema tatizo la mafuriko katika mto huo limekuwa likijirudia mara kwa mara na serikali inafanya utafiti wa kutafuta ufumbuzi wa kudumu.
Basi likiwa limesombwa na mali ya mto. |
Singida:
Zaidi ya watu arobani wamenusurika kufa kufuatia basi la Bin Ally walilokuwa wakisafiria kutoka Singida mjini kwenda kijiji cha Mtavira wilayani Ikungi kukwama katika ya mto Minyughe.
Basi lilipokwama katika mto Minyughe liltitia katika
mchanga na kisha kusombwa na maji
yaliyotokana na mvua kubwa zinazo endelea kunyesha wilayani humo.
Huko huko Singida taarifa nyingine zilisema kuwa mvua kubwa zilizoanza kunyesha mkoani humo mwezi Desemba mwaka 2013 zimeendelea kuleta maafa baada ya watu watano kuhofiwa kufa maji kutokana na gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji ya mto.
Abiria 16 waliokuwa wakitoka kijiji cha Doromoni kwa kutumia Landrover 110 TDI lenye namba za usajili T.499 ATR, lilisombwa na maji ya mto wakati dereva wake akijaribu kuvuka mto Nzalala.
Kamanda Geofrey akifafanua, amesema walipofika kwenye mto huo abiria hao walimwomba dereva huyo asubiri maji ya mto yapungue ili waweze kuvuka lakini dereva huyo alikataa kwa madai maji ni machache.
“Wakati gari hilo lilipofika katikati ya mto, lilizimika ghafla na wakati huo huo maji ya mto yaliongezeka na kulifunika gari.
Dereva na kondakta waliweza kufanikiwa kutoka na kukimbilia kusikojulikana”
Aidha, amesema abiria 11 waliweza kuokolewa na wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Iramba na watano hadi sasa haijulikani iwapo wamekufa ndani ya landrover au wamesombwa na maji na kupelekwa kusikojulikana.
Katika hatua nyingine, Kamanda Kamwela, alitoa wito kwa madereva wa vyomba vya moto, baiskeli na watembea kwa miguu kuchukua hadhari wakati wa kuvuka mito au mabonde kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Madhara ya kukosa makazi na wengine kulala porini baada ya kukwama magari yao au kusombwa na maji yamekuwa ni ya mara kwa mara kipindi hiki.
Daraja la Dumila |
MAELFU ya abiria na mamia ya magari yakiwemo mabasi yanayosafirisha abiria kwenda kanda ya ziwa, yamekwama katika barabara kuu inayo unganisha mikoa ya Dodoma na Morogoro, katika eneo la Dumila, Wilayani Kilosa baada ya daraja kuu la Dumila kukatika kutokana na mvua kubwa ilionyesha wilayani Kilosa usiku wa kuamkia Januari leo.
Kuvunjika kwa daraja hilo kumesababishwa na mafuriko makubwa na hivyo kusababisha
nyumba na watu kukosa makazi kutokana na
mvua hiyo inayodaiwa kunyesha maeneo ya milimani wilayani Kilosa kusababisha mafuriko.
Mafuriko hayo pia yamesababisha kusombwa kwa nguzo za umeme,
miti mikubwa kukatika na kutanda
barabarani huku shule ya sekondari ya wasichana Dakawa, Chuo cha Veta Dakawa, Mahakama ya Mwanzo Dakawa nazo kuathirika.
Watu wanadaiwa kufa maji huku wengine wakionekana wakiwa
juu ya miti kusubiri kuokolewa.
Hatua za makusudi za kuimarisha miundo mbinu yetu ni la muhimu na pia kuanza kupima makazi salama ya watu kuishi ni jambo lisilokwepeka na la kuzingatia kuanzia sasa.Tuachane na ujenzi wa nyumba kiholela.
Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania.
0 comments: