Baba Mtu Mzima ( miaka 70) Atuhumiwa Kumwingilia Mbwa (Bestiality )
Mbwwa ni Walinzi na si Wapenzi |
Mkuu wa Polisi (RPC) mkoani hapa Kamanda Robert Boaz amesema Bw. Severin Kessy mtuhumiwa mweye wanawake watatu wa ndoa ameshuhudiwa akifanya kitendo hiki na mbwa tarehe 3 Aprili mwaka huu.
Bwana Boaz alisema kuwa majirani waliitaarifu Polisi juu ya tukio hili lakini walifika wakiwa wamechelewa na mtuhumiwa akawa ametoroka.
Mkuu huyu wa Polisi akiongea na wana habari alisema mbwa aliyefanyiwa kitendo hiki kisicho cha kawaida ni wa kijana ambaye anaishi nyumba moja na mtuhumiwa na imedaiwa pia kwamba majirani wamemshuhudia mtuhumiwa mara kadhaa akimwingilia mbwa huyo siku za nyuma.
Kamanda huyu aliongeza kusema kwamba pamoja na kumsaka mtuhumiwa Bwana Kessy, wataalamu wa tiba wametakiwa kumchunguza mbwa huyu ambaye tokea tukio hili kutokea sehemu zake nyeti zimevimba na anaoneka na hali tofauti na kawaida.
Swali la kujiuliza hapa ni kuwa hivi hii hali kweli ni ya kawaida au ni masuala ambayo yamegubikwa na ushirikina au ni shetani la ngono.
Mkondo wa sheria unapaswa uchukue nafasi yake na ikibainika kwamba mtuhumiwa ana hatia hatua kali zichukuliwe ili kukomesha matukio ya aibu kama haya.
Isitoshe upimaji wa mtu huyu na wake zake unapaswa ufanyike haraka ili kubaini kama wameadhirika kiafiya au la na kama wameathirika matibabu yafanyike mapema.
Chanzo:Daily News online.
0 comments: