Sakata la Kuwatimua Wafanya Biashara Ndondogo Maeneo Yasiyoruhusiwa Kuanza Tena
Eneo ziunganikiako barabara kuu za jiji hili |
Mkutano huu uliongozwa na Diwani wa kata ya Mahina Mheshimiwa Charles Chinchibela (CHADEMA), ambaye ni Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, alilitoa azimio hili.
Huku akiwatupia lawama nzito nzito baadhi ya viongozi wa mji kwa kuvamia maeneo ambayo yaliyotengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hawa wadogo, alisema wafanyabiashara ndogondogo (machinga) jijini hapa ni kero na kushauri waondolewe kwenye maeneo yasiyotakiwa.
Halmashauri ya jiji tangu mwaka jana, imekuwa ikishirikisha viongozi wa wafanyabiashara wadogo ili kujemga mazingira ya kukuza amani na maelewano kati ya viongozi wa mji na wafanyabiashara hawa.
"Tumekuwa mara nyingi tukilalamika kwa nini wafanyabiashara hawa hawaendi maeneo yaliyotengwa kwa ajili yao kumba baadhi ya viongozi wa mji wamevamia maeneo hayo ," alielezea Mhe. Chinchibela .
Chinchibela, ambaye ni Diwani wa Kata ya Mahina,
Amedai licha ya wafanyabiashara hao kutoiingizia mapato halmashuri hiyo, wanasabaisha msongamano usiokuwa wa lazima katika baadhi ya maeneo mjini hapa.
Mawazo haya yanatofautiana na ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA, ambao hapo awali wamekuwa wakiwashawishi machinga wasihame kwenye maeneo hayo, hali ambayo imekuwa ikisababisha uvunjifu wa amani kila wanapojaribu kuondolewa.
Akitoa mfano , Bw Chinchibela alitaja Sahara kama moja ya maeneo ambayo maofisa wa jiji wameishikilia. Akasema, eneo hilo, lilitengwa kutumika kama Hifadhi ya magari na halmashauri ilikuwa ikipata milioni Sh24 kila mwaka.
"Sasa, eneo hilo kwa sasa halizalishi senti hata moja baada ya kutengwa kwa ajili ya wafanya biashara wadogo ambao hadi kwa sasa hawapo kwenye eneo hili ," alisema Mhe. Chinchibela .
Kwa sasa , kwa mujibu wa diwani huyu, eneo hilo lilikuwa linatumika kinyume cha sheria kwa biashara ya ngono wakati wa usiku. "Hii ni upotevu wa rasilimali za Halmashauri ya mji, " alibainisha.
Mheshimiwa Charles Chinchibela alisema haya hivi karibuni mwezi huu wa Aprili
wakati wa Baraza la Madiwani huku akishangazwa na kutoondolewa kwa machinga hao wakati jiji lilitenga sh. milioni kwa ajili ya kuboresha maeneo wanayotakiwa kuhamia
.
Akijibu , Mhe. Stansilaus Mabula Meya wa Jiji la Mwanza alimtaka diwani kuwasilisha ripoti rasmi katika ofisi yake kwa hatua za haraka badala ya kusubiri hadi mkutano wa madiwani.
Mhe. Mabula alisema kuwa halmashauri ya jiji imetenga baadhi ya maeneo ambayo ni rafiki kibiashara. Maeneo haya ni eneo la kituo cha jumuiya ya Mirongo , eneo la Makoroboi, ukiondoa eneo la kutembea kwa miguu mbele ya msikiti wa Wahindi.
Maeneo mengine ni kituo cha mabasi cha kati ya mji, maarufu kama 'Tanganyika Bus Stand' , Kituo zamani cha mabasi ya Mukuyuni, eneo la barabara ya Vitunguu (dampo ), Asante Moto, barabara ya Pamba chini ya Daraja karibu na (White - pub ), Market Street isipokuwa nje ya picha ya Samaki na kituo cha daladala za Nyegezi.
Alibainisha kuwa maeneo ambayo wafanyabiashara ndogo ndogo hawatakiwi kuendesha shughuli za kibiashara ni kwenye barabara ya Nyerere kutokea Nyamuhongolo njia ya kuingia mji Mwanza karibu na jengo la CCM pande zote, barabara ya Pamba kutokea barabara ya Nyerere pande zote, eneo la barabara kuelekea kanisa la kikatoliki la Bugando kutokea barabara ya Kenyatta .
Mhe. Mawazo, ambaye aliwahi kuwa Naibu Meya, alipinga zoezi la kuwahamisha wafanyabiashara hao kwa kuwashirikisha mgambo wa Jiji.
Mhe, Mawazo pamoja na kutokufafanua sababu za kukataa mgambo wasitumike kwenye zoezi hili wachunguzi wa mambo wanadai huenda anahofu kutokea tena yale. yaliyotokea katika zoezi kama hili siku za nyuma hususani lile la Novemba 2011.
Kwa kumbukumbu za matukio ya nyuma kama hili, rejea ; a).Gsengo. b) jamiiforum
0 comments: