Na Wewe ni Mmoja wa Hawa Tisa Mpendwa Msomaji Wangu?
Daftari la njano la kuweka kumbukumbu za malengo,changamoto ,utekelezaji na tathimini ya kila siku |
Utafiti umebainisha kuwa watu 9 kati ya kumi
hawatumii kwa ukamilifu uwezo wao wa kiakili katika kijiletea mafanikio.
Mtaalamu wa Fizikia na Hesabu Bwana Einstein ambaye
ni Mmarekani mwenye asili ya Kijerumani alibainisha kwamba tunatumia asilimia
5% tu ya uwezo wetu wa kiakili.
Ukweli huu waweza kugeuzwa sasa hivi kwa kutumia mbinu hii ya kujiuliza
maswali manne kila siku .
Jambo la msingi la kuzingatia
ni kwamba, amini kuwa ukifanyacho leo kinakuletea kesho nzuri au mbaya.
Maswali haya ya kujiuliza kila
siku yako mara mbili. Maswali mawili ya kujiliza mwanzoni mwa siku na mawili ya
kujiuliza mwishoni mwa siku.
Maswali mawili ya kujiuliza
kila unapoianza siku.
1.Nini ninataka leo hii?
Jiulize ni nini unakitaka ? Weka
malengo yako kwa siku hiyo husika. Yaandike kwa kifupi kabisa.Usiweke mambo
mengi unapoanza. Anza na mambo mawili na
ongeza siku zinavyo ongezeka. Andika
malengo yako katika vitenzi majina na usitumie wakati ujao kama nita… Hii husaidia upimaji wa lengo lako.
Kwa mfano waweza kujiwekea
lengo kama hili.
a)
Kusoma barua pepe zangu zote na kuzijibu.
b)
Kufua nguo zote chafu.
2.Zipi
ni changamoto katika kutekeleza malengo ya leo ?
Jiulize
changamoto unazofikiri ziko mbele yako katika utekelezaji wa malengo
uliyojiwekea.Tafuta ufumbuzi wake.
Watu
wanaofanikiwa mara zote hulenga mbali. Jua changamoto zilizo mbele yako kila
siku.
Maswali
mawili ya kujiuliza mwishoni mwa siku.
1.Nimefikia malengo yangu ya
siku ya leo ?
Kuweka malengo na kujua
changamoto hakutoshi.Tathimini ni muhimu ili kujua kama
kuna mafanikio au la.Tathimini husaidia kujua wapi umefanikiwa na wapi
hukufanikiwa na kwa nini? Kwa kujua haya utakuwa katika nafasi nzuri ya kuweka
malengo mazuri yanayotekelezeka.
Jiulize kila siku kama umefanikiwa katika kile ulichotaka?
2. Nimejifunza nini leo?Kupata mafanikio mazuri na kwa
haraka hutokana na kujifunza kwa kila
siku.Tumia muda mfupi kila siku kujiuliza kile ulichojifunza siku hiyo.Laweza kuwa
ni jambo dogo au kubwa cha muhimu ni kutumia hayo maarifa mapya unayoyapata kwa
mafanikio zaidi. Unavyojifunza mapya ndivyo unavyokuwa katika nafasi ya kusonga
mbele zaidi kimaendeleo.
Jiulize kila siku nini umejifunza kwa siku hiyo.
Nakutakia mafanikio.
Nakutakia mafanikio.
0 comments: