MAHABUSU GEITA WALAZIMISHA KUSIKILIZWA KWA KUVUA NGUO.
Gari la Idara ya Mahakama MEI mosi jijini Mwanza. |
SIKU ya Jumatano 25,Juni 2014 mahabusu tisa wa gereza la Wilaya ya Geita mkoani hapo wavua nguo hadharani mbele ya Mahakama ya Wilaya kwa madai ya kucheleweshwa kusikilizwa kwa shauri lao.
Mahabusu aliyechujua nguo jijini MWANZA.. |
Kutokana na sakata hili uongozi wa serikali kesho yake walilazimika kwenda gerezani hapo kukutana nao.
Maofisa waliowatembelea mahabusu hao walitoka mahakama ya wilaya, ofisi ya mwanasheria wa serikali pamoja na ofisa wa upelelezi wa makosa ya jinai wa mkoa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juzi, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Geita, Desideric Kamugisha, alisema walilazimika kufanya mazungumzo na mahabusu hao kuhusiana na malalamiko yao ya kutotendewa haki.
Alisema baadhi ya malalamiko hayo ni kucheleweshwa kwa upelelezi wa kesi zao hususani za mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha, huku baadhi ya wafungwa wakidai kuhukumiwa adhabu kubwa zisizolingana na makosa husika na kutokupata fursa ya kukata rufaa.
“Tumekubaliana nao na kuwataka waorodheshe malalamiko yao yote ambayo wameyataja mbele yetu wakiainisha namba ya shauri, mwaka pamoja na mahakama husika.
“Kazi hiyo iliaanza tangu juzi, kwa hiyo matokeo yatapatikana muda si mrefu kuanzia sasa, ili kumaliza kero hii,” alisema.
Kamugisha aliongeza kwamba kwa mujibu wa mwongozo wa kusikiliza kesi kwa mwaka, mahakama inatakiwa kusikiliza mashauri yasiyopumgua 250.
Kwa mujibu wa kauli yake alisema, pamoja na uhaba wa mahakimu wamesikiliza kesi 436 tangu Januari hadi Mei mwaka huu.
Alibainisha kuwa kuna hakimu mmoja tu wa wilaya na wawili wa mahakama ya mwanzo.
Mkuu wa Gereza la Geita, Joseph Mbilinyi, alisema wameanza kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo hayo, ili kuondoa malalamiko hayo.
Wakili wa Serikali Mkoa wa Geita, Mwasimba Hezeroni, alisema kuwa changamoto walizopata walipotembelea gerezani humo watazifanyia kazi kwa muda muafaka, na akataka kila upande utekeleze kazi zake kwa wakati kwa maana ya mahakama, mwanasheria wa serikali pamoja na ofisi ya upelelezi ya mkoa.
Mahabusu hao walichukua hatua hiyo juzi asubuhi muda mfupi baada ya kutoka mahakamani bila kesi zao kusikilizwa na kulazimishwa kupanda kwenye Karanding la polisi kurudishwa mahabusu.
Hili ni tukio la pili kutokea kufuatia sakata jingine kama hili lilotokea katika mahakama ya hakimu mkazi hapa jijini Mwanza.Kwa madai kama hayo hayo ya kucheleweshewa kusikilizwa.
Mahabusu aliyechujua nguo jijini ARUSHA |
Kule Arusha mwezi Aprili mwaka huu huu mahabusu mmoja, 'alisandura' nguo zake hadhani mbele ya Mahakama jijini humo akiwa na mwenzake wakidai wenzao Dharam Patel (26) na Nivan Patel (20) wanaodaiwa kukamatwa na kete 173 za heroini na misokoto 300 ya bangi, Aprili mwaka huu kuachiliwa ili hali makosa yao ni mamoja.
Tatizo hili la mahabusu kuchujua nguo hadharani tuite ni dalili za uonezi kukithiri hapa nchini ama ni wananchi kujua haki zao au ni nini?Hii yaweza kuwa ni dalili ya jambo baya
Lakini waswahili wanasema panapofuka moto pana moto.Kuwa mahabusu si lazima huyo mhusika kuwa ni mwenye hatia. Wako waliohukumiwa ikaja bainika kwamba waliohukumiwa kimakosa lakini walipokata rufaa waliwekwa huru.Parole imewanusuru wengi waliotiwa hatiani kimakosa.
Haki isipotendeka katika jamii ndicho chanzo cha jamii kurudi nyuma kimaendeleo na ni chanzo kikuu cha chuki miongoni mwa wana jamii.Haki tuilinde WATANZANIA kwa maendeleo ya nchi yetu.Upotevu wa haki ni katika jamii ni dalili ya uwepo wa Rushwa iliyokithiri.
0 comments: