Siku ya Mazingira Duniani Yaadhimishwa kwa Namna ya Aina yake Jijini Mwanza.
Sherehe za siku ya mzingira DUNIANI nchini Tanzania zaazimishwa kitaifa leo Alhamisi 5, Juni 2014 hapa Jijini Mwanza.
Kila mwaka ifikapo tarehe 5 Juni, Jumuiya ya Kimataifa inaadhimisha Siku ya Mazingia Duniani kutokana na Azimio la
Baraza la Umoja wa Mataifa la Mwaka 1972.
Maadhimisho haya ni kielelezo cha ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira uliofanyika huko Stockholm, nchini Uswis.
Leo hii basi Tanzania imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha kilele cha wiki ya mazingira duniani kwa mwaka 2014 kwa ngazi ya mkoa na kitaifa hapa jijini Mwanza.
Mambo muhimu yaliyofanyika pamoja na kufanya usafi wa mazingira ni kueleza hatua zilizofikiwa katika uhifadhi wa mazingira kimkoa na kitaifa.
Kauli mbiu kwa mwaka huu 2014 ni:Tunza Mazingira ili Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Jiji la Mwanza kwa mara nyingine limekuwa la kwanza katika usafi likiongoza majiji yote nchini kwa mara ya Tisa mfululizo.
Nayo manisipaa ya Moshi yapoteza nafasi ya kwanza ya ushindi wa usafi katika manisipaa iongozayokwa usafi. Safari hii yajikuta ikishika nafasi ya pili. Manisipaa kinara wa usafi kitaifa mwaka huu ni Manisipaaya Msoma.
Maadhimisho haya hapa jijini Mwanza yamefanyika kwa staili ya aina yake. Wengi tumezoea kuona maonesho mbalimbali wakati wa kuadhimisha vilele vya siku kuu kama hizi za kitaifa ndani ya viwanjani.
Leo hii yamekuweko mabadiliko makubwa. Maonesho haya yamefanyikia katikati ya jiji na kuwaacha wakazi wa jiji hili katika mshangao na taharuki kali kiasi cha baadhi kukimbia wakidhania kulikuweko na ghasia .
Takribani kama muda wa dakika thelathini hivi muda wa saa nne asubuhi leo wakazi waliokuwepo katikati ya jiji walijikuta wakijiuliza kuna nini?
Wakaishia kushikwa na butwaa wasijue kilichokuwa kikiendelea huku wengine wakikimbia kujisalimisha kwa kuogopa kuumia.
Tazama hali ilivyokuwa katika picha:
Gari la zimamoto likiwa kwenye harakati za zoezi zima |
Baadhi ya wtuhumiwa wakiwa mikononi mwa askari chini ya ulinzi mkali. |
Zoezi la usakaji, kutafuta wahalifu likiendelea huku wananchi wakiwa wamebakia kushaanga kinachoendelea. |
Asikari wakiwa katika hadhari ya kukabiliana na wahalifu wanaotafutwa muda wowote |
Wahalifu wakiwa chini ya ulinzi |
Wahalifu wakipelekwa kituoni ili hatimae kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kufunguliwa mashitaka. |
Pamoja na zoezi hili na yote yaliyojiri kwa siku hii, ikawa nayo ni njia ya kuadhimisha siku hii ya mazingira Duniani.
Aidha, Siku hii tunaikumbuka kama siku ambayo Azimio la kuunda Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Mazingira Duniani, UNEP, lilipitishwa.
UNEP ni chombo pekee cha Umoja wa Mataifa chenye makao makuu yake Barani Afrika, huko Nairobi, Kenya.
Lengo kubwa katika kuadhimisha siku hii Kimataifa na kitaifa ni kuweka msisitizo katika masuala ya mazingira na kuwapa uwezo wananchi ili wawe mawakala wazuri wa maendeleo endelevu.
Pili ni kutoa nafasi ya kutafakari kuhusu hali na umuhimu wa utunzaji bora wa mazingira, kuelimishana na kukuza ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za hifadhi na usimamizi wa mazingira yao.
Kiukweli zoezi hili limepamba sherehe hizi kwa aina yake. Hongera jeshi la polisi kwa kazi nzuri ya kuudhihirishia umma kuwa usalama wao mnaupa kipaumbele cha kwanza kuliko kitu kingine chochote kile.
0 comments: