WAMACHINGA JIJINI MWANZA WALETA KIZAA ZAA NDANI YA JIJI SIKU NZIMA..
Askari zimamoto wakiwa katika jitihada za kuzima moto uliowashwa na Wamachinga ili kuteketeza Msikiti wa Hindu wanaosali Masinga-singa. |
Barabara kuu za katikati ya jiji hili za Kenyatta, Nyerere, Pamba, Lumumba na Rwegasore zalikuwa hazikaliki baada ya mabomu zaidi ya 120 ya kutoa machozi kulipuliwa na kulifanya eneo zima kunuka harufu ya mabomu hayo na watu kujikuta wakilia ovyo ovyo.
Jeshi la Wananchi (JWTZ) lilitoa askari wa “MP” kuimarisha ulinzi katika mabenki, ofisi za serikali na maeneo nyeti ili kuwezesha shughuli za kila siku kuendelea |
Mabomu hayo yalilipuliwa maeneo mbalimbali ya mji ikiwemo eneo maarufu la Makoroboi kufuatia kuvunjwa kwa vibanda vya machinga jana asubuhi.
Uvunjwaji huu wa vibanda unadaiwa ndio uliyowafanya Wamachinga kucharuke na kuanza mapambano na askari polisi na mgambo wa Jiji huku wakishinikiza wenzao walio kwenye maeneo halali nao waondolewe ili wote waikose Makoroboi.
Baadhi ya Wamachinga wakiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi |
Hatua hiyo inafuatia maamuzi ya baraza la halimashauri ya Jiji la Mwanza kuondoa wafanya biashara wadogo wadogo almaarufu kama wamachinga kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria.
Vijana waandamanaji wakifunga barabara |
Hahari zilizopatikana baadae zilibaini kuwa hao walikuwa wanatumiwa kuzidisha vurugu.
Haya yalibainishwa baadae na bwana mmoja aitwae Abdukadri Salim . "Vijana hawa wanatumiwa kufanya vurugu na siyo wamachinga. "Bwana Abdukadri Salimu alisema.
Mitaa ya Makoroboi na ya pembezoni mwake ilikumbwa na vurugu hizi . Maduka yalifungwa maeneo haya na ya jirani yake kutokana na vurugu hizi.
Askari zimamoto walifanikiwa kuzima moto huo uliowashwa na wamachinga ili kuhatarisha usalama wa Msikiti wa Hindu wanaosali Masinga singa.
Hii ni kwa sababu walitakiwa kutotandaza bidhaa zao chini au kuegesha kwenye kuta za msikiti huu, na tukio la leo ni la zaidi ya mara mbili kutokea kwa wamachinga kulikalia eneo hili kwa nguvu.
Oparesheni ofisa wa zima moto, Sajenti meja Gadafi Masoud Akiongea na wana habari |
Askari wa jeshi la Polisi Mkoani hapa wakifanye msako mtaa baada ya mtaa kuwasaka waanzisha fujo sanjari na kulinda usalamawa mali za wafanyabiashara kwani vurugu hizo ziliambatana na uporaji. |
Kutokana na mchafuko huu hata wale Wamachinga walioruhusiwa kufanya biashara hapa Makoroboi kwa kuwa katika maeneo yanayoruhusiwa kuendeshea biashara walishindwa kufungua biashara zao.
Mtawanyiko wa gesi za mabomu haya ya machozi ulisababisha wakati mgumu kwa wengi hususani wanahabari.
Wakati huo huo Jeshi la polisi likitumia vipaza sauti lilitoa tahadhari ya watu kutosimama kwa makundi.
Tukio hili limetia hasara kubwa kwa kukosekana kwa huduma toka kweye maduka ya biashara na huduma za usafiri kwa muda, hali ambayo imewapa usumbufu mkubwa wateja wa hapa jijini na wale wa kutoka katika mikoa ya jirani ya Mara, Shinyanga, Kagera, Simiyu na Geita waliohitaji bidhaa katika maduka ya jumla.
Kamanda wa polisi hapa Mkoani Mwanza Valentino Mlowola hakuweza kupatikana kwa kuwa akikuwa katika safari ya kikazi na Christopher Fuime msaidizi wake alidaiwa kuwa katika Oparesheni hii.
Jeshi la Polisi katika doria mtaa kwa mtaa. |
Baadhi ya taarifa ambazo hazijathibitishwa bado zinadai kwamba hali hii ya Wamachinga kukaidi amri halali ya kuwataka kuondoka maeneo haya yasiyo ruhusiwa kuendesha biashara inachochewa na baadhi ya wanasiasa wanaotafuta umaarufu wa kisiasa kupitia mgongo wa wafanyabiashara hawa.
0 comments: