Mama Mzazi wa Mhe. ZITTO KABWE Afariki Dunia Asubuhi ya Leo Jumapili.
Mama Mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, Bi. Shida Salum enzi za uhai wake. Mwaka jana Desemba 2013 alinusurika kifo kwenye ajali mbaya ya gari alipokuwa akienda LINDI. |
Mama Mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, Bi. Shida Salum afarikidunia mapema leo Jumapili, tarehe 01, June 2014 saa 5 asubuhi. akiwa na umri wa miaka 64.
Zitto Kabwe (Mbunge-CHADEMA) amethibitisha kifo cha mama yake kupitia mtandao wa kijamii leo tar 01/06/2014.
Mauti yamemfika akiwa katika hospitali ya AMI iliyoko Msasani
jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa
kansa ya kizazi.
Kwa mujibu wa Zitto, Saida ambaye hadi umauti unamkuta, alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Walemavu nchini, mjumbe wa bunge maalum la katiba na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA.
Zitto Kabwe akiwa na mama yake Shida Salum enzi za uhai wake. |
Mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumatatu Juni 2, huko Mwanga-Kisangani baada ya sala ya mchana (Adhuhuri).
Marehemu Bi. Shida Salum ameacha mume, na watoto 10, wakiume sita na wakike wanne. alisema Zitto.
Arusha:
Kufuatia kifo hiki cha mama Mzazi wa Zitto Zuberi Kabwe; Shida Salum ambaye alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Chama kimetangaza siku tatu za maombolezo
Akiongea na wananchi waliokuwa wamejitokeza kwa wingi mtaa wa balakwenye mkutano wa madiwani na mbunge wa Arusha Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha Mhe. Nanyaro Ephata
alisema si busara kuendelea na mkutano huo huku wakiwa wamempoteza kiongozi wa ngazi ya juu kabisa kwenye maamzi.
Rais wa JYMT, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete alikwenda kumjulia hali wiki kadhaa zilizopita kama ionekanavyo katika picha hapo juu.
Ndege ikiandaliwa tayari kwa kuweza kuingiza mwili wa marehemu mama yake Zitto Kabwe kupelekwa Kigoma kwa Maziko. |
Waheshimiwa wabunge na baadhi ya viongozi wakibeba jeneza lililobeba mwili wa marehemu mama yake Zitto Kabwe, Bi. Shida Salum kuingiza kwenye ndege tayari kwa safari ya kwenda Kigoma kwenye mazishi. |
Prof. Ibrahim Lipumba akijadili jambo na mwenzie baada ya kupakia mwili wa marehemu kwenye ndege kuelekea kigoma kwenye maziko. |
Ewe Mwenyezi Mungu uilaze mahala pema peponi.Sisi sote ni wako na marejeleo yetu ni kwako Aaamiin.
0 comments: