|
MV TEMESHA |
Waziri wa Ujenzi
Dkt. John Pombe Magufuli leo hii Jumatano ya tarehe 9 julai 2014, majira ya saa tatu asubuhi azindua kivuko kitakachofanya kazi kama daladala ya kusafirisha abiria kupitia majini kwa lengo la kukabiliana na msongamano wa magari jijini hapa kutokana na kuwa na njia moja tu ya kuingia na kutoka katika jiji hili.
Kivuko hiki kijulikanacho kwa jina la MV TEMESHA injini yake ina 'horse power' kubwa ambayo itakiwezesha kwenda kasi na kuweza kubeba kwa wakati mmoja mzigo wa tani 65 ambao ni sawa na abiria 80 na magari madogo madogo sita.
|
Kikundi cha Ngoma kikitoa Burudani katika Uzinduzi huu |
Kivuko hiki ambacho uzinduzi wake unafanywa leo hii hapa Sweya, Nyegezi nje kidogo ya jiji la Mwanza kinatarajiwa kufanya safari zake kuanzia wiki ijayo ambazo zitanzia Luchelele, kupitia Sweya, Butimba, mkuyuni, Igogo, Mjini hadi Kirumba, lengo likiwa ni kupunguza foleni za magari jijini hapa cha kufurahisha zaidi ni kwamba, imedaiwa wanafunzi watasafiri bure alimradi tu wawe na vitambulisho.
|
Dk.John Pombe Magufuli Akiteta na Wenyeji wake
|
Kabla ya ufunguzi wa kivuko hiki Dk.John Pombe Magufuli alitoka katika kukagua mradi wa barabara ya kutoka Usagara hadi Kisesa mkoani humu kwa lengo lile lile la kupunguza msongamano wa magari katika jiji hili. Barabara hii ni ya urefu wa kilometa 16.7 na inajengwa kwa kiwango cha lami.
Barabara hii na kivuko hiki hakika vitawezesha ufikaji katika kona yeyete ile katika jiji hili kwa wepesi zaidi.
Habari toka wizara hii zimeeleza pia kwamba kesho, Waziri huyu ambaye ni mmoja wa Mawaziri wanopigiwa mfano miongoni mwa Mawaziri wachache wachapaka kazi na hodari katika nchi hii ataenda mkoani Mara kukagua barabara ya Makutano - Nata na Mugumu yenye urefu wa kilomita 50.
|
Mkuu wa mkoa akitoa neno katika ufunguzi huu |
Aidha kesho hiyo hiyo anatarajiwa kuzindua kivuko kingine cha MV MARA huko Mkoani Mara kitakachofanya safari zake kati ya Iramba na Majita na baada ya uzinduzi huu atafanya mkutano wa hadhara eneo la mwibara ikiwa ni sehemu ya kufanya ukaguzi wa mradi wa barabara ya Nyamuswa- Bunda-Kisorya. na Nansio yenye urefu wa kilomita 51.
Imedawa pia kuwa serikali katika azma yake ya kupunguza kero za usafiri kwa wananchi wake inatarajia kuanzisha kivuko kingine kama hivi huko jijini Dar es salaam kitakachofanya safari kati ya Dar es salaam na Bagamoyo.
|
Wananchi wakibadilishana hili na lile kabla ya uzinduzi |
Kweli hizi ni juhudi za wazi za serikali hii ya awamu ya nne katika kuwajali wananchi wake.Yule atakayekuwa anabeza juhudi hizi hakika atakuwa ni yule asiyetoridhika kwa lolote na mwenye kujaa tamaa na wivu au uchu wa kitu fulani.Waswahili wanasema asiyeridhika kwa kidogo hata kikubwa hakitamridhisha, Hongera serikali ya awamu ya nne kwa kujali wananchi,
|
Wananchi wakimiminika eneo hili kushuhudia uzinduzi huu |
Ombi kwako Mheshimiwa Magufuli ni kukuomba utukumbuke na sisi wakule Mwanga Mkoani Kilimanjaro kwa barabara ya Kichwa Ng'ombe kupitia Kwakoa Kigonigoni-Butu -Jipe kutokezea Kifaru. Barabara hii ina umuhimu sana kwani itakuwa ni lango la kuunganisha nchi yetu na jirani zetu Kenya ukiacha ile ya Mwanga-Usangi- Ugweno. Pia itasaitia wagonjwa kufika kwenye hospitali hii kubwa inayojenwa hapo Kwakoa ambayo itakuwa ya msaada mkubwa kwa Watanzania na wale kutoka nchi ya jirani Kenya.
0 comments: