Mwanafunzi wa Shule ya Mwanza Anayedaiwa kuunguzwa Moto na Baba yake Azikwa Leo.

Marehemu Annastazia
Mwanafunzi Anastazia Luckford Magafu azikwa leo  mchana wa tarehe 23. Aprili 2014 huko Rumala Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza baada ya kuagwa na mamia ya wanafunzi wenzake wa Shule ya Sekondari Mwanza na baadhi ya wengine toka shule za jirani.

Binti huyu alilazwa Bugando wiki mbili zilizopita kwa matibabu  ya majeraha  makubwa ya kuunguzwa moto kutokana na ugomvi na baba yake kama ilivyodaiwa hapo awali.

Tarehe 17 Aprili 2014 alifariki  akiwa anaendelea na matibabu  katika Hospitali ya Rufaa Bugando katika mazingira yaliyodaiwa na ndugu waliokuwa wakimuuguza kuwa yalikuwa ya kutatanisha

Madai ya kuwa kifo chake kimetokana na kunyweshwa sumu kama ilivyodaiwa na ndugu aliyekuwa akimuuguza yalisababisha  mwili wa marehemu  kutochukuliwa na wana ndugu kwa kusubiri kufanyiwa uchunguzi kwanza.

Habari za uchunguzi huu bado hazijawekwa wazi ila kwa kuwa wanandugu  sasa wame kubali kuchukua mwili wa marehemu kwa maziko ni ishara kwamba wamepewa majibu waliyoyaridhia.

Mwanzoni walikataa kuuchukua mwili wa marehemu kwa maziko kwa madai hayo ya  kuwa walitaka uchunguzi kufanywa kwanza.

Mmoja wa ndugu hawa alipoulizwa  na mwandika habari hii kueleza matokeo ya uchunguzi, alikataa kusema chochote.

Mwalimu mkuu Msaidizi wa shule ya Mwanza Sekondari Mwl, Naftali Magori akikabidhi rambirambi za wana Mwanza Sekondari  kwa Ndugu wa karibu na Merehemu  alisema.  "Waalimu na wanafunzi wamesikitishwa sana na kifo cha Anna na kuongeza kuwa Merehemu amewaachia wana Mwanza Seko pigo kubwa  kwani hali yake ilikuwa ikitoa matumaini ya kurejea katika kupona."

Mwandishi wa habari hii aliongea na mwalimu wa darasa  la Anna, Mwl.Gloria Swai kuhusu maendeleo ya mwanafunzi  huyu naye alieleza kuwa Mwanafunzi Anna alikuwa mwanafunzi mzuri.

Marehemu Anna alikuwa kidato cha tatu mkondo A cbumba namba mbili, yaani (3A2 Three A two.)

Majonzi haya yamewakuta wana Mwanza seko wakiwa wanajiandaa na Mahafali ya kidato cha nne hapo kesho siku ya Ahamisi.


Wakati msiba huu ukiendelea,shuleni hapo kulikuwa na msiba mwingine.Msiba huu ni  kifo cha mama mzazi wa Mkuu  wa shule hii Mwl,David Nstory.Kilichotokea  leo asubuhi.Shughuli za maziko bado zinaendela Nyumbani kwa Mkuu wa shule hapo hapo maeneo ya Shuleni.
Waalimu na wafanyakazi Mwanza Sekondari wakitoa heshima za mwisho kwa Mwanafunzi wao Anastazia.




Wanafunzi  wa Mwanza Sekondari wakitoa hehima za mwisho kwa Marehemu Annastazia.
BWANA ALITOA BWANA AMETWAA JINA LAKE LITUKUZWE.    RIP Annastazia

0 comments:

POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza