Tanzania (SCT) Yatwaa Kombe la Dunia la Vijana wa Mitaani- 2014.
![]() |
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kushoto) na Waziri wa Ardhi, Nyumbana Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka wa pili (kulia) wakiwa pamoja na timu hiyo |
Mapema ndani ya wiki la kwanza la mwezi wa nne 2014 Tanzania
iliandika histori baada ya timu ya Watoto wa mitaani Tanzania (SCT) kulitwaa kombe la Dunia la vijana wa mitaani kule Rio de Jeneiro Brazil .
Timu hii ililitwaa kombe
hili kwa baada ya kuichapa timu ya watoto wa mitaani ya Burundi mabao
matatu kwa nunge (3-0).
Timu hii ya Burundi
iliingia fainali katika michuano iliyohusisha vijana 230 toka nchi 19 katika lengo la
kuwaleta watoto katika nchi hizi karibu.
Ushindi huu haukupatikana
kirahisi kwani ulipatikana baada ya timu hii kuzishinda timu nyingine kadhaa zinazosifika katika kandanda duniani kama
vile Argentina
marekani na nyingine .
Hii ni ishara tosha kwamba
vijana hawa wana vipaji na vikiendelezwa wanaweza kuifanya Tanzania kutimiza
ndoto yake ya kuchukua kombe la kandanda la dunia.
Ijumaa ya tarehe 11,Aprili 2014 Timu ya Watoto
wa Mitaani ya Tanzania
iliyotwaa Kombe la Dunia mwaka huu ilitembelea Bunge maalumu la katiba na
kuiomba Serikali kuwasaidia
Juhudi za vijana hawa
zilianza kuonekana mapema toka mwaka 2010 pale walipoingia fainali na India katika michuano kama
hii hii na kushindwa.
Licha ya matatizo mbalimbali yanayowakabili
Watoto hawa wa Mitaani wamethibitisha kwa vitendo kuwa hakuna lisilowezekana kama kutakuwa na nia.
Kinachorudisha juhudi zao nyuma ni kukosa
taasisi au watu wa kuwashika mkono kwa maana ya kuendeleza vipaji vyao.
Kwa hili, tunaipongeza sana Taasisi ya Tanzania Street Children
Sports Academy (TSCSA) ya jijini Mwanza Rais wa kituo hiki Altaf Hirani, na Mkurugenz
wake Yangwe Mtani kwa kuwajumuisha pamoja watoto hawa na kuwashughulisha katika
shughuli mbalimbali zikiwamo za michezo.
“Kupitia michezo kama
hii watoto hawa wanaweza kuonesha vipaji vyao katika kumudu soka na huu ni
mfano halisi kuwa kumbe hawa watoto wa mitaani wanaweza kufika mbali na kufanya
mambo makubwa katika michezo iwapo watasaidiwa.” Rais wa kituo hiki Altaf
Hirani alisema.
Mfungaji bora wa timu hii ya
Watoto wa Mitaani kutoka Mwanza Tanzania, (TSC) ambayo iliibuka mshindi katika
mashindano haya ya Kombe la Dunia la Watoto yaliyofanyika Brazil, mwaka
huu Frank William ameishauri , Serikali na jamii kuwasaidia ili kujiandaa
na mashindano kama haya.
Kauli hiyo ilitolewa leo
mjini Dodoma na
William ambaye pia alikuwa Capteni katika timu hii wakati
walipolitembelea Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma ambapo walipata nafasi ya
kuzungumza na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella
Mukangara pamoja na Naibu wake Juma Nkamia na viongozi wengine mbalimbali
akiwemo waziri mkuu Pinda ambaye aliandaa chakula cha pamoja na watoto hawa.
Alisema siri ya ushindi
wetu ni ushirikiano na kujituma. Hivyo aliomba jamii kuwasaidia watoto
wengi wa mitaani ambao hawana uwezo wa kupata elimu lakini wana vipaji
mbalimbali ili waweze kuvikuza.
Kwa upande wake kipa bora wa
timu hiyo, Emmanue Amos, alishauri Serikal iweze kuwasaidia ili waweze
kushiriki katika mashindano ya mwaka 2018 ya kombe hilo .
Mchezaji mwingine wa timu
hiyo, Denis David aishauri jamii isiwadharau kwa kuwa ni watoto wa mitaani
kwani wanavipaji. Aliitaka jamii kuwekeza katika soka la vijana
kwa sababu baada ya miaka 20 ijayo mchezaji bora atapatikana kwa njia
hiyo.
Naye Kocha wa timu hiyo, Suileiman
Jabir aliwataka wadau mbalimbali kuwasaidia na kuwaendeleza
watoto hawa ambao wengi wameonesha wana vipaji vya sanaa na utamaduni.
Akizungumzia kuhusu mafanikio
ya ushindi kama huu hapo baadae alishauri kuweka mpango wa kutafuta vijana
wenye vipaji ambapo wataviendeleza na kuvikuza kwa kufanya maandalizi ya
kiutalaamu na kiufundi. Jabir aliongeza kuwa
waliwaandaa watoto hawa kisaikolojia ili
waweze kushinda katika mashindano hayo ya kimataifa.
Alishauri saula la
watoto kupewa kipaumbele na kuweka sheria itakayowadhibiti wakina baba wanao
telekeza watoto na kuiasa jamii kuwasaidia watoto pale wazazi au walezi
wanapofariki dunia.
Rais wa timu hii ya Watoto wa
mitaani Altaf Hirani aliiomba Serikali kuwasaidia
kupata kiwanja cha michezo kwa ajili ya watoto hawa jijini Mwanza
au kwenye maeneo mengine ya nchi.
Naye Naibu Waziri wa
Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni Juma Nkamia akizungumzia
kuhusu timu hiyo alisema ameliagiza Shirikisho la Mchezo wa Soka Tanzania
(TFF) kuwa na mpango endelevu wa kuwasaidia watoto.
Wadau mbalimbali nchini kuanzia Serikali,
wanapaswa kuona umuhimu wa kuwasaidia watoto katika maeneo mbalimbali nchini
kuendeleza vipaji walivyojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Ushindi wa Watoto wa Mitaani wa kutwaa Kombe la
Dunia ni kielelezo kwamba Tanzania
imejaliwa vipaji vingi katika michezo, lakini tatizo kubwa limekuwa ni jinsi ya
kuviibua vipaji hivyo na kuviendeleza.
Kinachotakiwa sasa ni Serikali kwa kushirikiana
na taasisi nyingine zisizo za kiserikali kama
TSCSA kubeba jukumu hili na kuhakikisha ndoto za vijana wetu zinatimizwa.
Hongera sana
Watoto wa Mitaani. Mmeipeperusha vyema Bendera ya Tanzania .
Vyanzo: TV, Magazeti na mitandao ya kijamii.
0 comments: