Mazishi ya Gwiji la Muziki Maalim Muhidin Gurumo Yahudhuriwa na Maelfu ya Watu.
![]() | |
Marehemu Muhidin Maalimu Gurumo |
Mauti ya nguli huyu wa muziki wa dansi nchini yalimfika akiwa katika matibabu ya ugonjwa wa moyo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa.
Ugonjwa wa moyo umemsumbua kwa kipindi kirefu.Na huenda ndio uliopelekea hata akatangaza kustaafu shughuli za muziki.
Alipata elimu ya msingi shule ya msingi Sungwi, Masaki Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani huko.
Alisoma madrasa, chuo cha kufundisha elimu ya Dini ya Kiislamu enzi za udogo wake.
Baada ya baba yake kufariki aliacha shule na alichukuliwa na mjomba wake Selemani Sultani Mikole, ambaye wakati huo alikuwa akiishi maeneo ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Gurumo alipoacha shule alianza kupiga muziki na bendi za mitaani alianza na bendi iliyojulikana kama Scock Jazz iliyokuwako mitaa ya Moshi na Kigoma.
Baada ya mwaka mmoja katika bendi hii alijiunga na bendi ya kilimanjaro Chacha ambayo ilikuwa na vyombo vya muziki vya kisasa. Katika bendi hii alitunga vibao vya;Twende Tukalime,Mapenzi Hayana Dawa,Ushirikina ni Sumu na Maendeleo.
Mwaka 1963 alijiunga na Rufiji Jaz Band na hapa alitunga kibao kilichompa umarufu katika muziki wa dansi kijulikanacho kwa jina la Uwezo wa binadamu kufikiri.
Mwaka huo huo alijiunga na Kilwa Jazz Band hapa alitoa vibao vilivyovuma enzi hiyo vya Wewe Mpenzi Naomba Unishauri Kabla Hatujagombana na Siwezi Kukununulia Gari Wakati Hata Baisikeli Sina.
Mwaka 1964 alikuwa miongoni mwa walioanzisha bendi ya Nuta Jazz wakati huo akiwa na kina Ahmed Omary, Mohamed Omary,Epimakus Mkundika na Rashid Abdallah (Wengine wa hai na wengine ni marehemu sasa)
Akiwa Nuta Jazz Bandi alitunga vibao vingi ila hivi viliuma navyo ni Magdalena,Maneno ya Mwalimu Maneno ya Wazee yote Sawa na Rehema Umefeli Shule kwa Sababu Gani.
Baadae Nuta Jazz Bandi iliitwa OTTU Jazz Band kutokana na mabadiliko yaliyotokea kipindi hicho katika vyama vya wafanyakazi nchini.
Akiwa OTTU alitoa vibao vingi ila vilivyovuma sana ni Tenda wema na usia kwa watoto.
Kama Simba walivyo watani wa Yanga katika soka Msondo Ngoma (Baba ya Muziki) watani wao kimziki ni DDC Ochestra Mlimani Park
![]() |
Raisi akimfariji mjane wamarehemu Muhidin Maalim Gurumo |
Pichani Raisi anaonekana akimfariji mjane wa marehemu Muhidin Maalim Gurumo (mwenye shuka nyeupe) na wanafamilia pale alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya April 15, 2014, siku ambayo marehemu alizikwa kijijini kwao Masaki, Kisarawe, Mkoa wa Pwani.
Msafara wa kwenda malaloni uliongozwa na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal.Aidha msafara huu ulianzia nyumbani kwake Mabibo, Makaburi Jijini Dares salaam (kwa jina jingine maarufu la mtaa huu Tabata External )baada ya kutolewa kwa heshima za mwisho na kupokelewa kwa salamu kutoka makundi mbalimbali.
Magari zaidi ya 20 yalianza msafara huu saa 05:15 kwenda Masaki na yalifika kijijini kwake saa 7:10 adhuhuri.
![]() |
Mwili wa marehemu ukipelekwa katika nyumba yake ya milele |
baada ya kuswaliwa mmwili ulipelekwa makaburini ndani ya jeneza tayari kwa maziko.
Baada ya marehemu kuswaliwa kunako saa 07:40 mwili ulipelekwa makaburini hapo karibu na nyumbani kwao hapo hapo Masaki mkabala na ilipo nyumba alikozaliwa.
![]() |
Mwili ukingizwa kaburini |
Kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma Mabela alisema pamoja na Gurumo kujiuzulu muziki walikuwa wote katika bendi ya OTTU hadi pale mauti yalipomfika.
Aliongeza kuwa marehemu akiwa Meneja wa bendi kwa hiyo mauti yamemkuta Gurumo akiwa pamoja naye katika bendi.
Mmoja wa wanamziki hapa nchini amemtaja Marehemu Maalim Muhidini Gurumo kuwa ni Mwalimu wa wanamuziki wengi hapa nchini na kwamba amewainua wanamziki wengi hadi kuwa maarufu katika fani hiyo.
Muhidini Maulidi Gurumo amekuwa katika bendi kadhaa kama ilivyofafanuliwa hapo juu enzi za uhai wake kabla ya kuanzinsha bendi yao ya Msondo Ngoma.
Aliwahi kupigia Bendi ya OSS (Ochestra Safari Sound) na DDC Mlimani Park maarufu kwa jina la mtindo wao wa Ndekule.
![]() |
Mwana muziki King Kiki akiwa na wadau wa muziki. |
Mwanamuziki Ali Choki kiongozi wa bendi ya Extra Bongo ni miongoni mwa wanamziki waliopata ujuzi na kufanya kazi pamoja na Marehemu Gurumo.
Choki anamtaja marehemu kama Mwalimu Mkuu wa Muziki nchini ambaye sasa ametoweka katika ulimwemuzikingu kwa kusema; "Gurumo ni mwanamuziki aliyekaa kwenye 'game' kwa siku nyingi, ninashauri wanamuzuki wa kizazi hiki kufuata nyendo, heshima na mambo mazuri aliyoyaishi. mkongwe huyu katika tasinia ya muzuki"
Aidha mastaa mbalimbali wa tasinia mbalimbali akiwemo JB mmoja wa waingizaji maarufu nchini alisema pengo aliloacha Gurumo litatuchukua kipindi kirefu kuliziba.
Mwanamziki huyu wengi wanadai alitabiri kifo chake kwa yale aliyofanya kabla ya kifo chake,
Akiwa kalazwa aliondoka wodini mara kadhaa akidai kutolewa hasipitalini arudishwe nyumbani kwake. Jingine ni pale alipoagiza agiza wanae siku chache kabla ya kulazwa, waende huko Masaki kusafisha makaburi ya ukoo, Jingine ni lile la kutangaza kuacha kupiga muziki.
![]() |
Diamond Platinum Akimkabidhi Maalimu Gurumo Enzi za Uhai wake Ufunguo wa Gari |
Kitenndo chake hiki cha kutangaza kuacha muziki kilipelekea Diamond Platinum kumpa Gari hasa pale alipolalamika katika mahojiano yake na TBC kuwa anaacha muziki huku akiwa hana kitu cha kujivunia kutokana na tasinia hii ya muziki.
Mwanamziki Gurumo (Kamanda wa muziki ) kama mashabiki wa muziki walivyokuwa wakimwita ilizaliwa mwaka 1940 katika Kijiji cha Masaki Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani na amefariki akiwa na miaka 74..
![]() |
Mjane wa marehemu Guromo |
"Sisi sote tumetoka kwa Allah (SW) na marejeo yetu sote ni kwake" (INNA LILLAIHI WA INAILLAIHI RAJIUUN)
Mungu ilaze roho ya marehemu Gurumo mahali pema peponi
Ona video ya mazishi ya Marehemu Muhidin Maalimu Gurumo ijijini Kwao MASAKI Kisarawe wilaya ya Pwani.(Video imeandaliwa na Global TV)
Source:.bongocelebrity na vyanzo mbalimbali vya habari
0 comments: