MV Matala yazama katika Ziwa Victoria Katikati ya Visiwa vya Kerebe na Lukolu
.
Jumamosi ya , Aprili 18, 2014\ taarifa za watu 10 kunusurika kufa maji katika ziwa Victoria baada ya meli ya mizigo MV Matala kupinduka na kuzama ikiwa na shehena ya sukari zasikika
Sukari hii ilinunuliwa kutoka katika kiwanda cha sukari Kagera Bukoba na ilikuwa inasafirishwa kuja jijini Mwanza.
Meli hii ambayo inamilikiwa na kampuni ya Mkombozi Fishing and Marine Transport Limited, imezama ikiwa na magunia 5600 ya sukari sawa na tani 280.
Meli hii ni mali ya mfanyabiashara wa jijini Mwanza aitwaye V.H.Shah,
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Gitano Chacha Munanka ameeleza kwamba meli hiyo imezama ikiwa katikati ya visiwa vya Kerebe na Lukolu majira ya saa 10.30 usiku wa kuamkia Jumamosi na kuongeza kwamba hakuna mtu yeyote aliyejepoteza maisha kufuatia tukio hilo.
kituo cha IT na Star TV vimeelezea kuzama kwa meli hii na kongezea kuwa juhudi za wafanyakazi wa kampuni hiyo kuipindua zinaendelea bila mafanikio,
huku baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakisema chanzo cha meli hii kuzama ni kutokana na dhoruba kali .
Watabiri wa hali ya hewa wamekuwa wakitoa ushauri kwa wamiliki wa vyombo vya majini lakini kumekuwa na kutozingatia utabiri unaotolewa na mamlaka hii ya hali ya hewa hapa nchini.
Kungekuwa na mazingatio ya utabiri huu unaotolewa na mamlaka hii huenda kungesaidia kuepusha nchi na maafa haya yanayojitokeza nchini hivi sasa.
Sehemu inayo onekana pichani ni sehemu ya meli iliyozama, ambayo ilianza safari yake ya kutoka Bukoba majira ya saa 7 mchana, ikiwa inaendeshwa na kapteni Erick Lasana.
Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra kanda ya ziwa, imethibitisha kuzama kwa meli hiyo yenye uwezo wa kubeba tani 280 za mizigo na abiria 100.
Sehemu ya meli hii iliyokuwa ikizama |

0 comments: