Kidato cha sita Shule ya Sekondari Mwanza Waadhimisha mahafali ya 14 .-2014

Wa tatu toka kulia ni Mgeni rasmi Mwl.Juma Kasandiko ambaye ni Afisa  Elimu wa Wilaya ya Ilemela.  Kulia kwake ni Makamu Mkuu wa shule ya Mwanza Mwl. Naftali Magori na kushoto kwake ni Mwl. Andrew Mtangi Mwakilishi wa M/Kiti wa bodi ya Shule na kushoto kwake ni Mwl. Deosdedit Nsorro, M/kiti wa Ustawi wa jamii Mwanza Sekondari

Jana tarehe 25 Aprili, 2014 Mwl. Juma Kasandiko ambaye ni Afisa Elimu Wilaya ya Ilemela  awa Mgeni Rasmi  kwenye maadhimisho ya  mahafali ya Kumi na nne Kidato cha sita Shule ya Sekondari Mwanza.
Makamu Mkuu wa  Shule Mwl.Naftali Magori Akisoma Risala ya Shule kwa Mgeni Rasmi


Wanafunzi  waliohitimu masomo yao walikuwa 172 kati yao  wasichana wako 91  na wavulana 81.Wahitimu hawa walikuwa katika michepuo ya PCM ,PCB,CBG,HGL,HGK na HKL Kati ya wahitimu hawa hakukuwepo na walio acha shule ama kwa kuhama au kufukuzwa.
Mwl.Andrew Mtangi aliyemwakilisha M/Kiti wa bodi  ya shule

Mwl, Kasandiko aliwahi  kuwa mwalimu wa shule hii miaka ya 1999 na 2002 kabla ya kuhamishiwa Shule ya Sekondri ya Wasichana Nganza.

Pamoja na matatizo yaliyoikabili  jumuiya hii ya wana Mwanza Sekondari kartika wakati huu wa mahafali haya, ya kufiwa na Mwanafunzi wao Annastazia na Mkuu wa shule kufiwa na mama mzazi,  Shule ilishindwa kuahirisha mahafali haya kutokana na hali ya maandalizi yaliyoshirikisha wazazi toka sehemu mbalimbali na matayarisho yaliyokuwa tayari yamekwisha kufanyika.

Kama bahati  jana hiyo hiyo Shule ya Sekondri ya Wasichana Nganza nayo ilikuwa na mahafali ya kidato cha sita ambako  Mgeni wao Rasmi katika mahafali hayo alikuwa ni kiongozi wa juu kutoka Wilaya ya Ilemela.

Kutokana na hali ilivyokuwa shamra shamra zilikuwa si kama zile za miaka yote haswa kwa wenyeji,Hii ni kutokana na  shule kuwa  na misiba ya watu wa karibu sana. Ila kwa mgeni ilikuwa si rahisi kubaini hali hiyo bila kujulishwa. Hakika jumuia hii ilibeba masuala hayo kwa weledi wa hali ya juu sana.
Wahitimu
Katika risala ya wahitimu hawa wa Mwanza, walieleza kuwa shule yao ina uhaba wa vitabu vya kiada ziada na rejea. Aidha walieleza kuwa wana uhaba wa waalimu hasa katika masomo ya sayansi.

Wakieleza matumaini yao katika mitihani ijayo waliahidi kufanya vizuri zaidi kuliko walivvyofanya katika mitihani yao ya Utimilifu (Mock).  Walisema waliongaza kimkoa kwa kuwa na  DivisioN  ONE 36 ,wakasema wataziongeza katika mitihani  hii iliyo mbele yao ya kitaifa.

Makamu Mkuu wa  Shule Naftali Magori ambaye alimwakilisha  Mkuu wa Shule Mwl. Eng.David Nestory. Naye  akimkaribisha  Mjumbe wa bodi ya  shule Mwl.Andrew Mtangi aliyemwakilisha M/Kiti wa bodi  ya shule.Ndugu Mtangi, aliwasisitizia wahitimu kutoridhika na matokeo waliyopata katika mitihani yao ya utimilifu {mock).

Naye Mwl.Andrew Mtangi  aliwambia wahitimu kuwa wana kila sababu ya kushinda na kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini kwa sababu nia ipo, akili wanazo, walimu wanao na afya nzuri wanazo  kwa hiyo akawataka  hilo liwe lengo la kila mmoja wao.

Mgeni rasimi akijibu risala yao aliahidi  kufikisha yale ambayo yako juu ya uwezo wake, kwa mwenye shule ambaye alisema ni Mkurugenzi wa Jiji.Kwa upande wake alisema atatoa rangi kupaka eneo lote la upande wa madarasa.

Akizungumzia jitihada za Serikali katika kipindi hiki cha Matokeo Makubwa Sasa amesema Serikali iko katika mikakati ya kuongeza madarasa kwa vidato vya tana na sita kutokana na ongezeko la wahitimu wa kidato cha nne.Sambamba na hili akaongezea kuwa iko pia katika harakati za kuongeza  mazingira ya kukuza ongezeko la ajira. 

Hatimaye aliwaasa wanafunzI. Aliwataka kusoma kwa bidii na maarifa.Akawaambia  wakienda nyumbani kusubiria matokeo wasibweteke ila wawasaidie wazazi wao kwa shughuli za nyumbani. "Wazazi wanafurahia kumsaidia mtoto anayeonesha utii na adabu kwao."akasisitizia.

Kwa upande wa wazazi aliwakumusha kuwa wana wajibu wa kuwasaidia walimu kwa kuwahoji watoto wa kueleza nini wamejifunza na kuwahimiza kujisomea wakiwa nyumbani badala ya kuwaacha wakajifanyia mambo yao.Pili akawataka kulipa ada kwa wakati na kutoa michango wanayotakiwa kutoa ili kuboresha zoezi zima la kupata mahitaji ya  kufundishia  na kujifunzia.

Katika utoaji vyeti kwa wahitimu alianza kutoa vyeti vya  vilabu na makundi ya viongozi bora,usafi, nidhamu,  michezo na taaluma Alianza na wale walijitokeza kitaaluma.


  • Waliojitokeza kitaaluma kwa kuongoza katika somo  na somo analo onekana kufanya vizuri ni:
  • Mohamedi Salimini - Geography
  • Khadija Yusufu Ngonyani - English/ Swahili
  • Fatuma Ramadhani - Literature in English
  • Miraji Nasibu Omary  - Physics /Ad .Maths
  • Mabia Nduta  - Chemistry
  • Erick Warioba Benjamini - Biology
  • Justin John Danstan  - Maths
  • Irine Soka  - General Studies.
Katika kusherehekea Wahitimu walikaa katika vyumba vya madarasa. Vimba hivi vilipambwa na huko wahitimu walisherehekea na ndugu na jammaa zao. Vifuatavyo ni vyumba baadhi tu vilivoandaliwa kwa ajili hiyo ambavyo tulivitembelea .


Chumba cha kina Mary Musa -PCB, Edina Kimala -CBG, Naomi Masabi  -PCM, Jacline James-  pcm  na Herieti Bayona -PCM

Hiki nacho ni miongoni mwa vyumba ila kwa bahati mbaya wahusika hawakuwepo kueleza wao ni kina nani.

Chanzo cha Habari: Na MWANDISHI wetu.


0 comments:

POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza