Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muunngano wa Tanganyika na Zanzibar Yawa Gumzo kwa Wengi.
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Akikagua Gwaride |
Shereha hizi za Muungano zilifanyika kipindi ambacho Bunge la Katiba lilikuwa likiendelea na mjadala wa kupata katiba mpya.
Kwa sababu ya Sherehe hii na kuanza kwa Bunge la Bajeti bunge hili la Katiba limeahirishwa hadi Agosti 5,2014.
Msisitizo mkubwa katika sherehe hii umekuwa kudumisha na kuuenzi muungano wa nchi zetu hizi mbili,Tanganyika na Zanzibar ambao sasa umefikisha miaka 50.
Raisi Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Joyce Banda Raisi wa Malawi
|
Miongoni mwa Maraisi waliohudhuria ni Raisi Joyce Banda, Raisi wa Malawi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uchumi Kusini mwa Afrika (SADC).
Raisi Uhuru Kenyatta wa Kenya. Raisi Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Pierre Nkuruzinza wa Burudi, Raisi wa Lesoto, Makamu wa Raisi wa Nigeria Mohamed Namand Sambo na Mfalme Mswati wa Tatu wa Swaziland, na wengine wengi kwa kutaja tu hawa wachache.
Nembo iliyobeba kauli mbiu ya sherehe za muungano mwaka huu |
Kauli mbiu ya sikukuu hii mwaka huu ni: ".Utanzania wetu ni Muungano wetuTuulinde, Tuuimarishe na kuudumisha"
Ilifahamika baadae kuwa jina Tanzania lilibuniwa na Mohamed Ikbar na ndiye aliyekuwa mshindi katika hili shindano la kubuni jina Tanzania baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana.
Na jina Tanzania lilianza kutumika rasmi 9.12.1964.
Imedaiwa kuwa tokea kuanzishwa huu Muungano zimekuweko changamoto kadhaa lakini zilizotatuliwa ni chache ikiwemo ya Zanzibar kujiunga na Jumuiya ya EAC na kuwa nchi yenye katiba yake.
Zilizobaki ni zile za Zanzibar kutozwa kodi mara mbili na Umiliki wa mali asili zikiwemo gesi na mafuta.
Raisi Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na Raisi wa Zanzibar Dkt Mohamed Shein |
Raisi alisema hatatoa hotuba bali atatoa shukurani tu kwa kuchelea kuharibu utamu, uzuri na ubora wa maonyesho kwa ujumla wake.
Shukurani zake alizielekeza kwa umahiri wa maonyesho ya halaiki kwa vijana na, mazoezi mbalimbali na kwa walimu wa halaiki na watayarishaji wa kila fani iliyooneshwa na pia kwa waalikwa kwa kuitikia wito.
Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete nkiingia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es saalam |
Hata hivyo kwa kuweka mambo sawa wasemaji wanaohusika na maadhimisho hayo wametetea kuwa si kitu cha ajabu kuoneshsha zana za kijeshi hadharani kama ilivyokuwa.
Walisema nchi nyingi zinafanya maonesho kama hayo haswa katika maadhimisho ya mambo mahususi kama tuliyokuwa nayo.
Wakaongezea kuwa hata kilichooneshwa ni kitu kidogo tu ukichukulia hali halisi ya jeshi letu.
Kwa kujikumbusha sherehe zilivyokuwa tazama video hapo chini.
MUNGU ibariki TANZANIA na WATU wake.
Vyanzo: TBC, ITV na EATV.
0 comments: