Pata Habari Toka Magazeti Mbalimbali Toka Hapa Nchini na ya Kimataifa.

TUMIA MUDA WAKO WA
 MAPUMZIKO KWA
KUJISOMEA  ILI KUONGEZA 

MAARIFA NA KUJIBURUDISHA
Soma magazeti uyatakayo kupitia blog hii ya Jiji Mwanza. 

FUATA MAELEKEZO.







  • Soma hadithi  IFUATAYO iitwayo KIKULACHO..Kuipata hadithi hii bofya hapa.Sehemu ya kwanza. KilulachO

  •  Pata utangilizi wa kitabu hiki.kwa MAAELEZO ZAIDI WASILIANA NAMI kwa anuani zilizopo.
Kitabu hiki kinapatikana bado  katika mfumo wa PDF kwani hakijachapishwa bado.










Soma Utanguluzi wa kitabu hiki na toa maoni yako kwa kutumia barua pepe ehmsangi@gmail.com 
BOFIA HAPA KUPATA UTANGULIZI HUU.











0 comments:

Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muunngano wa Tanganyika na Zanzibar Yawa Gumzo kwa Wengi.

Raisi  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Akikagua Gwaride


Sherehe za Miaka Hamsini ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar  zilizoadhimishwa tarehe 26.04.2014 zilipambwa kwa Halaiki na .maonyesho ya ndege za kivita,wimbo wa wanamziki 50 toka vikundi mbalimbali na Maonesho mbalimbali katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es saalam.

Shereha hizi za Muungano zilifanyika kipindi ambacho Bunge la Katiba lilikuwa likiendelea na mjadala wa kupata katiba mpya. 

Kwa sababu ya Sherehe hii na  kuanza kwa Bunge la Bajeti bunge hili la Katiba limeahirishwa hadi Agosti 5,2014.

Msisitizo mkubwa katika sherehe hii umekuwa  kudumisha na kuuenzi muungano wa nchi zetu hizi mbili,Tanganyika na Zanzibar ambao sasa umefikisha miaka 50.

                      Raisi Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Joyce Banda Raisi wa Malawi
Sherehe hii imehudhuriwa na Maraisi,Mabalozi na viongozi  mbalimbali wa mashirika ya kimataifa wa hapa nchini na nje ya nchi. 

Miongoni mwa Maraisi waliohudhuria ni Raisi Joyce Banda, Raisi wa Malawi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa  Jumuiya ya Uchumi Kusini mwa Afrika (SADC).

Raisi Uhuru Kenyatta wa Kenya. Raisi Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Pierre Nkuruzinza wa Burudi, Raisi wa Lesoto, Makamu wa Raisi wa Nigeria Mohamed  Namand Sambo na Mfalme Mswati wa Tatu wa Swaziland, na wengine wengi kwa kutaja tu hawa wachache.
Nembo iliyobeba kauli  mbiu ya sherehe za muungano mwaka huu

Kauli mbiu ya sikukuu hii mwaka huu ni: ".Utanzania wetu ni Muungano wetuTuulinde, Tuuimarishe na kuudumisha"

Ilifahamika baadae kuwa jina Tanzania lilibuniwa na Mohamed Ikbar na ndiye aliyekuwa mshindi katika hili shindano la kubuni jina Tanzania baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana. 

Na jina Tanzania lilianza kutumika rasmi 9.12.1964.

Imedaiwa kuwa tokea kuanzishwa huu Muungano zimekuweko changamoto kadhaa lakini  zilizotatuliwa ni chache ikiwemo ya Zanzibar kujiunga na Jumuiya ya EAC na kuwa nchi yenye katiba yake.

Zilizobaki ni zile za  Zanzibar kutozwa kodi mara mbili na Umiliki wa mali asili zikiwemo gesi na mafuta.

Raisi Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na Raisi  wa Zanzibar Dkt Mohamed Shein

Raisi alisema hatatoa hotuba bali atatoa shukurani tu  kwa kuchelea kuharibu utamu, uzuri na ubora wa maonyesho kwa ujumla wake.

 Shukurani zake alizielekeza kwa umahiri wa maonyesho ya halaiki kwa vijana  na, mazoezi mbalimbali na kwa walimu wa halaiki  na watayarishaji wa kila fani iliyooneshwa na pia kwa waalikwa kwa kuitikia wito.


Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete  nkiingia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es saalam
Lakini minong'ono imesikika ikidai maonyesho ya  zana za kijeshi  hayakuwa yanastahili kuoneshwa kwa namna yalivyo oneshwa kwani yaliashiria kutishia zadi ya kufurahisha.

Hata hivyo kwa kuweka mambo sawa wasemaji wanaohusika na maadhimisho hayo wametetea kuwa si kitu cha ajabu kuoneshsha zana za kijeshi hadharani kama ilivyokuwa.

Walisema nchi nyingi zinafanya maonesho kama hayo haswa katika maadhimisho ya mambo mahususi kama tuliyokuwa nayo.

Wakaongezea kuwa hata kilichooneshwa ni kitu kidogo tu ukichukulia hali halisi ya jeshi letu.

Kwa kujikumbusha sherehe zilivyokuwa tazama video hapo chini. 

MUNGU ibariki TANZANIA na WATU wake.



Vyanzo: TBC, ITV  na EATV.



0 comments:

Kidato cha sita Shule ya Sekondari Mwanza Waadhimisha mahafali ya 14 .-2014

Wa tatu toka kulia ni Mgeni rasmi Mwl.Juma Kasandiko ambaye ni Afisa  Elimu wa Wilaya ya Ilemela.  Kulia kwake ni Makamu Mkuu wa shule ya Mwanza Mwl. Naftali Magori na kushoto kwake ni Mwl. Andrew Mtangi Mwakilishi wa M/Kiti wa bodi ya Shule na kushoto kwake ni Mwl. Deosdedit Nsorro, M/kiti wa Ustawi wa jamii Mwanza Sekondari

Jana tarehe 25 Aprili, 2014 Mwl. Juma Kasandiko ambaye ni Afisa Elimu Wilaya ya Ilemela  awa Mgeni Rasmi  kwenye maadhimisho ya  mahafali ya Kumi na nne Kidato cha sita Shule ya Sekondari Mwanza.
Makamu Mkuu wa  Shule Mwl.Naftali Magori Akisoma Risala ya Shule kwa Mgeni Rasmi


Wanafunzi  waliohitimu masomo yao walikuwa 172 kati yao  wasichana wako 91  na wavulana 81.Wahitimu hawa walikuwa katika michepuo ya PCM ,PCB,CBG,HGL,HGK na HKL Kati ya wahitimu hawa hakukuwepo na walio acha shule ama kwa kuhama au kufukuzwa.
Mwl.Andrew Mtangi aliyemwakilisha M/Kiti wa bodi  ya shule

Mwl, Kasandiko aliwahi  kuwa mwalimu wa shule hii miaka ya 1999 na 2002 kabla ya kuhamishiwa Shule ya Sekondri ya Wasichana Nganza.

Pamoja na matatizo yaliyoikabili  jumuiya hii ya wana Mwanza Sekondari kartika wakati huu wa mahafali haya, ya kufiwa na Mwanafunzi wao Annastazia na Mkuu wa shule kufiwa na mama mzazi,  Shule ilishindwa kuahirisha mahafali haya kutokana na hali ya maandalizi yaliyoshirikisha wazazi toka sehemu mbalimbali na matayarisho yaliyokuwa tayari yamekwisha kufanyika.

Kama bahati  jana hiyo hiyo Shule ya Sekondri ya Wasichana Nganza nayo ilikuwa na mahafali ya kidato cha sita ambako  Mgeni wao Rasmi katika mahafali hayo alikuwa ni kiongozi wa juu kutoka Wilaya ya Ilemela.

Kutokana na hali ilivyokuwa shamra shamra zilikuwa si kama zile za miaka yote haswa kwa wenyeji,Hii ni kutokana na  shule kuwa  na misiba ya watu wa karibu sana. Ila kwa mgeni ilikuwa si rahisi kubaini hali hiyo bila kujulishwa. Hakika jumuia hii ilibeba masuala hayo kwa weledi wa hali ya juu sana.
Wahitimu
Katika risala ya wahitimu hawa wa Mwanza, walieleza kuwa shule yao ina uhaba wa vitabu vya kiada ziada na rejea. Aidha walieleza kuwa wana uhaba wa waalimu hasa katika masomo ya sayansi.

Wakieleza matumaini yao katika mitihani ijayo waliahidi kufanya vizuri zaidi kuliko walivvyofanya katika mitihani yao ya Utimilifu (Mock).  Walisema waliongaza kimkoa kwa kuwa na  DivisioN  ONE 36 ,wakasema wataziongeza katika mitihani  hii iliyo mbele yao ya kitaifa.

Makamu Mkuu wa  Shule Naftali Magori ambaye alimwakilisha  Mkuu wa Shule Mwl. Eng.David Nestory. Naye  akimkaribisha  Mjumbe wa bodi ya  shule Mwl.Andrew Mtangi aliyemwakilisha M/Kiti wa bodi  ya shule.Ndugu Mtangi, aliwasisitizia wahitimu kutoridhika na matokeo waliyopata katika mitihani yao ya utimilifu {mock).

Naye Mwl.Andrew Mtangi  aliwambia wahitimu kuwa wana kila sababu ya kushinda na kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini kwa sababu nia ipo, akili wanazo, walimu wanao na afya nzuri wanazo  kwa hiyo akawataka  hilo liwe lengo la kila mmoja wao.

Mgeni rasimi akijibu risala yao aliahidi  kufikisha yale ambayo yako juu ya uwezo wake, kwa mwenye shule ambaye alisema ni Mkurugenzi wa Jiji.Kwa upande wake alisema atatoa rangi kupaka eneo lote la upande wa madarasa.

Akizungumzia jitihada za Serikali katika kipindi hiki cha Matokeo Makubwa Sasa amesema Serikali iko katika mikakati ya kuongeza madarasa kwa vidato vya tana na sita kutokana na ongezeko la wahitimu wa kidato cha nne.Sambamba na hili akaongezea kuwa iko pia katika harakati za kuongeza  mazingira ya kukuza ongezeko la ajira. 

Hatimaye aliwaasa wanafunzI. Aliwataka kusoma kwa bidii na maarifa.Akawaambia  wakienda nyumbani kusubiria matokeo wasibweteke ila wawasaidie wazazi wao kwa shughuli za nyumbani. "Wazazi wanafurahia kumsaidia mtoto anayeonesha utii na adabu kwao."akasisitizia.

Kwa upande wa wazazi aliwakumusha kuwa wana wajibu wa kuwasaidia walimu kwa kuwahoji watoto wa kueleza nini wamejifunza na kuwahimiza kujisomea wakiwa nyumbani badala ya kuwaacha wakajifanyia mambo yao.Pili akawataka kulipa ada kwa wakati na kutoa michango wanayotakiwa kutoa ili kuboresha zoezi zima la kupata mahitaji ya  kufundishia  na kujifunzia.

Katika utoaji vyeti kwa wahitimu alianza kutoa vyeti vya  vilabu na makundi ya viongozi bora,usafi, nidhamu,  michezo na taaluma Alianza na wale walijitokeza kitaaluma.


  • Waliojitokeza kitaaluma kwa kuongoza katika somo  na somo analo onekana kufanya vizuri ni:
  • Mohamedi Salimini - Geography
  • Khadija Yusufu Ngonyani - English/ Swahili
  • Fatuma Ramadhani - Literature in English
  • Miraji Nasibu Omary  - Physics /Ad .Maths
  • Mabia Nduta  - Chemistry
  • Erick Warioba Benjamini - Biology
  • Justin John Danstan  - Maths
  • Irine Soka  - General Studies.
Katika kusherehekea Wahitimu walikaa katika vyumba vya madarasa. Vimba hivi vilipambwa na huko wahitimu walisherehekea na ndugu na jammaa zao. Vifuatavyo ni vyumba baadhi tu vilivoandaliwa kwa ajili hiyo ambavyo tulivitembelea .


Chumba cha kina Mary Musa -PCB, Edina Kimala -CBG, Naomi Masabi  -PCM, Jacline James-  pcm  na Herieti Bayona -PCM

Hiki nacho ni miongoni mwa vyumba ila kwa bahati mbaya wahusika hawakuwepo kueleza wao ni kina nani.

Chanzo cha Habari: Na MWANDISHI wetu.


0 comments:

Mwanafunzi wa Shule ya Mwanza Anayedaiwa kuunguzwa Moto na Baba yake Azikwa Leo.

Marehemu Annastazia
Mwanafunzi Anastazia Luckford Magafu azikwa leo  mchana wa tarehe 23. Aprili 2014 huko Rumala Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza baada ya kuagwa na mamia ya wanafunzi wenzake wa Shule ya Sekondari Mwanza na baadhi ya wengine toka shule za jirani.

Binti huyu alilazwa Bugando wiki mbili zilizopita kwa matibabu  ya majeraha  makubwa ya kuunguzwa moto kutokana na ugomvi na baba yake kama ilivyodaiwa hapo awali.

Tarehe 17 Aprili 2014 alifariki  akiwa anaendelea na matibabu  katika Hospitali ya Rufaa Bugando katika mazingira yaliyodaiwa na ndugu waliokuwa wakimuuguza kuwa yalikuwa ya kutatanisha

Madai ya kuwa kifo chake kimetokana na kunyweshwa sumu kama ilivyodaiwa na ndugu aliyekuwa akimuuguza yalisababisha  mwili wa marehemu  kutochukuliwa na wana ndugu kwa kusubiri kufanyiwa uchunguzi kwanza.

Habari za uchunguzi huu bado hazijawekwa wazi ila kwa kuwa wanandugu  sasa wame kubali kuchukua mwili wa marehemu kwa maziko ni ishara kwamba wamepewa majibu waliyoyaridhia.

Mwanzoni walikataa kuuchukua mwili wa marehemu kwa maziko kwa madai hayo ya  kuwa walitaka uchunguzi kufanywa kwanza.

Mmoja wa ndugu hawa alipoulizwa  na mwandika habari hii kueleza matokeo ya uchunguzi, alikataa kusema chochote.

Mwalimu mkuu Msaidizi wa shule ya Mwanza Sekondari Mwl, Naftali Magori akikabidhi rambirambi za wana Mwanza Sekondari  kwa Ndugu wa karibu na Merehemu  alisema.  "Waalimu na wanafunzi wamesikitishwa sana na kifo cha Anna na kuongeza kuwa Merehemu amewaachia wana Mwanza Seko pigo kubwa  kwani hali yake ilikuwa ikitoa matumaini ya kurejea katika kupona."

Mwandishi wa habari hii aliongea na mwalimu wa darasa  la Anna, Mwl.Gloria Swai kuhusu maendeleo ya mwanafunzi  huyu naye alieleza kuwa Mwanafunzi Anna alikuwa mwanafunzi mzuri.

Marehemu Anna alikuwa kidato cha tatu mkondo A cbumba namba mbili, yaani (3A2 Three A two.)

Majonzi haya yamewakuta wana Mwanza seko wakiwa wanajiandaa na Mahafali ya kidato cha nne hapo kesho siku ya Ahamisi.


Wakati msiba huu ukiendelea,shuleni hapo kulikuwa na msiba mwingine.Msiba huu ni  kifo cha mama mzazi wa Mkuu  wa shule hii Mwl,David Nstory.Kilichotokea  leo asubuhi.Shughuli za maziko bado zinaendela Nyumbani kwa Mkuu wa shule hapo hapo maeneo ya Shuleni.
Waalimu na wafanyakazi Mwanza Sekondari wakitoa heshima za mwisho kwa Mwanafunzi wao Anastazia.




Wanafunzi  wa Mwanza Sekondari wakitoa hehima za mwisho kwa Marehemu Annastazia.
BWANA ALITOA BWANA AMETWAA JINA LAKE LITUKUZWE.    RIP Annastazia

0 comments:

Tanzania (SCT) Yatwaa Kombe la Dunia la Vijana wa Mitaani- 2014.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kushoto) na 
Waziri wa Ardhi, Nyumbana Maendeleo ya
 Makazi,Profesa Anna Tibaijuka wa pili (kulia)
wakiwa pamoja na timu hiyo
Mapema ndani  ya wiki la kwanza la mwezi  wa nne 2014 Tanzania iliandika histori baada ya timu ya Watoto wa mitaani Tanzania  (SCT) kulitwaa kombe la Dunia  la vijana wa mitaani kule Rio de Jeneiro Brazil.

Timu hii ililitwaa kombe hili kwa baada ya kuichapa timu ya watoto wa mitaani ya Burundi mabao matatu kwa nunge (3-0).

Timu hii ya Burundi iliingia fainali katika michuano iliyohusisha  vijana 230 toka nchi 19 katika lengo la kuwaleta watoto katika nchi hizi karibu.

Ushindi huu haukupatikana kirahisi kwani ulipatikana baada ya timu hii kuzishinda timu nyingine  kadhaa zinazosifika katika kandanda duniani kama vile Argentina  marekani na nyingine .  

Hii ni ishara tosha kwamba vijana hawa wana vipaji na vikiendelezwa wanaweza kuifanya Tanzania kutimiza ndoto yake ya kuchukua kombe la kandanda la dunia.

 Ijumaa ya tarehe 11,Aprili 2014 Friday, April 11, 2014Timu ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania iliyotwaa Kombe la Dunia mwaka huu ilitembelea Bunge maalumu la katiba na kuiomba Serikali kuwasaidia

Juhudi za vijana hawa zilianza kuonekana mapema toka mwaka 2010 pale walipoingia fainali na India katika michuano kama hii hii na kushindwa.
Licha ya matatizo mbalimbali yanayowakabili Watoto hawa wa Mitaani wamethibitisha kwa vitendo kuwa hakuna lisilowezekana kama kutakuwa na nia.
 Kinachorudisha juhudi zao nyuma ni kukosa taasisi au watu wa kuwashika mkono kwa maana ya kuendeleza vipaji vyao.
Mkurugenzi wa Timu ya Watoto wa
 Mitaani (TSCSA), Mutani  Yangwe akisalimiana
 na Makamu wa pili  wa Rais wa Zanzibar,
Balozi Seif Ali Iddi mjini Dodomamara baada ya  timu  hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba
Kwa hili, tunaipongeza sana Taasisi ya Tanzania Street Children Sports Academy (TSCSA) ya jijini Mwanza Rais wa kituo hiki Altaf Hirani, na Mkurugenz wake Yangwe Mtani kwa kuwajumuisha pamoja watoto hawa na kuwashughulisha katika shughuli mbalimbali zikiwamo za michezo.
“Kupitia michezo kama hii watoto hawa wanaweza kuonesha vipaji vyao katika kumudu soka na huu ni mfano halisi kuwa kumbe hawa watoto wa mitaani wanaweza kufika mbali na kufanya mambo makubwa katika michezo iwapo watasaidiwa.” Rais wa kituo hiki Altaf Hirani alisema.

 Mfungaji bora wa  timu hii ya Watoto wa Mitaani kutoka  Mwanza Tanzania, (TSC) ambayo iliibuka mshindi katika mashindano haya ya Kombe la Dunia la  Watoto yaliyofanyika Brazil, mwaka huu  Frank William ameishauri , Serikali na jamii kuwasaidia ili kujiandaa na mashindano kama haya.

Kauli hiyo ilitolewa leo mjini Dodoma na  William  ambaye pia alikuwa Capteni katika timu hii wakati walipolitembelea Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma ambapo walipata nafasi ya kuzungumza na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara pamoja na Naibu wake  Juma Nkamia na viongozi wengine mbalimbali akiwemo waziri mkuu Pinda ambaye aliandaa chakula cha pamoja na watoto hawa.

Alisema  siri ya ushindi wetu ni ushirikiano na kujituma. Hivyo  aliomba jamii kuwasaidia watoto wengi wa mitaani ambao hawana uwezo wa kupata  elimu lakini wana vipaji mbalimbali ili waweze kuvikuza.

Kwa upande wake kipa bora wa timu hiyo, Emmanue  Amos, alishauri Serikal iweze kuwasaidia ili waweze kushiriki katika mashindano ya mwaka 2018 ya  kombe  hilo.

Mchezaji mwingine wa timu hiyo, Denis David aishauri jamii isiwadharau kwa kuwa ni watoto wa mitaani kwani wanavipaji. Aliitaka jamii kuwekeza katika  soka la vijana  kwa  sababu baada ya miaka 20 ijayo mchezaji bora atapatikana kwa njia hiyo.

Naye Kocha wa timu hiyo, Suileiman Jabir aliwataka wadau  mbalimbali  kuwasaidia na  kuwaendeleza watoto hawa ambao wengi wameonesha wana  vipaji vya sanaa na utamaduni.

Akizungumzia kuhusu mafanikio ya ushindi kama huu hapo baadae  alishauri kuweka mpango wa kutafuta vijana wenye vipaji ambapo wataviendeleza na kuvikuza kwa kufanya maandalizi ya kiutalaamu na kiufundi. Jabir aliongeza kuwa waliwaandaa  watoto hawa kisaikolojia ili waweze kushinda katika mashindano hayo ya kimataifa.

Alishauri saula la watoto kupewa kipaumbele na kuweka sheria itakayowadhibiti wakina baba wanao telekeza watoto na kuiasa jamii kuwasaidia watoto pale wazazi au walezi wanapofariki dunia. 

Rais wa timu hii ya Watoto wa mitaani  Altaf Hirani aliiomba Serikali kuwasaidia kupata kiwanja  cha michezo  kwa ajili ya watoto hawa jijini Mwanza au kwenye  maeneo mengine ya nchi. 

 Naye Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni Juma Nkamia akizungumzia kuhusu timu hiyo alisema ameliagiza Shirikisho la Mchezo wa Soka  Tanzania (TFF) kuwa na mpango endelevu wa kuwasaidia watoto.
Wadau mbalimbali nchini kuanzia Serikali, wanapaswa kuona umuhimu wa kuwasaidia watoto katika maeneo mbalimbali nchini kuendeleza vipaji walivyojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Ushindi wa Watoto wa Mitaani wa kutwaa Kombe la Dunia ni kielelezo kwamba Tanzania imejaliwa vipaji vingi katika michezo, lakini tatizo kubwa limekuwa ni jinsi ya kuviibua vipaji hivyo na kuviendeleza.
Kinachotakiwa sasa ni Serikali kwa kushirikiana na taasisi nyingine zisizo za kiserikali kama TSCSA kubeba jukumu hili na kuhakikisha ndoto za vijana wetu zinatimizwa.
Hongera sana Watoto wa Mitaani. Mmeipeperusha vyema Bendera ya Tanzania.

Vyanzo: TV, Magazeti na mitandao ya kijamii.




0 comments:

Mazishi ya Gwiji la Muziki Maalim Muhidin Gurumo Yahudhuriwa na Maelfu ya Watu.

Marehemu Muhidin Maalimu Gurumo
Mazishi ya gwiji la muziki wa dansi  nchini Muhidin Maalimu Gurumo, aliyefariki Jumapili Aprili 13, 2014  na kuzikwa siku ya  Jumatano tarehe 15 Aprili 2014  kijijini kwake  Masaki Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani yahudhuriwa na maelfu ya watu.

Mauti ya nguli huyu wa muziki wa dansi nchini yalimfika akiwa katika matibabu ya ugonjwa wa moyo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa.

Ugonjwa wa moyo umemsumbua kwa kipindi kirefu.Na huenda ndio uliopelekea hata  akatangaza kustaafu shughuli za muziki.

Alipata elimu ya msingi shule ya msingi Sungwi, Masaki Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani huko.

Alisoma madrasa, chuo cha kufundisha elimu ya Dini ya Kiislamu enzi za udogo wake.
Baada ya baba yake kufariki aliacha shule na  alichukuliwa na mjomba wake  Selemani Sultani Mikole, ambaye wakati huo alikuwa akiishi maeneo ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

Gurumo alipoacha shule  alianza kupiga muziki na bendi za mitaani alianza na bendi iliyojulikana kama Scock Jazz iliyokuwako mitaa ya Moshi na Kigoma.

 Baada ya mwaka mmoja katika bendi hii alijiunga na  bendi ya kilimanjaro Chacha ambayo ilikuwa na vyombo vya muziki vya kisasa. Katika bendi hii alitunga vibao vya;Twende Tukalime,Mapenzi Hayana Dawa,Ushirikina ni Sumu na Maendeleo.

Mwaka 1963 alijiunga na Rufiji Jaz Band na hapa alitunga kibao kilichompa umarufu katika muziki wa dansi kijulikanacho kwa jina la Uwezo wa binadamu kufikiri.

Mwaka huo huo alijiunga na Kilwa Jazz Band hapa alitoa vibao vilivyovuma enzi hiyo vya Wewe Mpenzi Naomba Unishauri Kabla Hatujagombana na Siwezi Kukununulia Gari Wakati Hata Baisikeli Sina.

Mwaka 1964 alikuwa miongoni mwa walioanzisha   bendi ya Nuta Jazz wakati huo akiwa na kina Ahmed Omary, Mohamed  Omary,Epimakus Mkundika na Rashid Abdallah (Wengine wa hai na wengine  ni marehemu sasa)

Akiwa Nuta Jazz Bandi alitunga vibao vingi ila hivi viliuma navyo ni Magdalena,Maneno ya Mwalimu Maneno ya Wazee yote Sawa na Rehema Umefeli Shule kwa Sababu Gani.
Baadae Nuta Jazz Bandi iliitwa OTTU Jazz  Band kutokana na mabadiliko yaliyotokea  kipindi hicho katika vyama vya wafanyakazi nchini.

Akiwa OTTU  alitoa vibao  vingi  ila vilivyovuma sana ni Tenda wema na usia kwa watoto.
Kama Simba walivyo watani wa Yanga katika soka Msondo Ngoma  (Baba ya Muziki) watani wao kimziki  ni DDC Ochestra Mlimani Park

Raisi akimfariji mjane wamarehemu Muhidin Maalim 
Gurumo
Mapema JIONI  baada ya maziko Raisi  Mhe. Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alifika nyumbani kwa marehemu kutoa rambirambi na mkono wa pole.

Pichani Raisi anaonekana akimfariji mjane wa marehemu Muhidin Maalim Gurumo (mwenye shuka nyeupe) na wanafamilia pale alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya April 15, 2014, siku ambayo marehemu alizikwa kijijini kwao Masaki, Kisarawe, Mkoa wa Pwani.

Msafara wa kwenda malaloni uliongozwa na Makamu wa Rais  Dk. Mohamed Gharib Bilal.Aidha msafara huu ulianzia nyumbani kwake Mabibo, Makaburi Jijini Dares salaam (kwa jina jingine maarufu la mtaa huu Tabata External )baada ya  kutolewa kwa heshima za mwisho na kupokelewa kwa salamu kutoka makundi mbalimbali.

Magari zaidi ya 20 yalianza msafara huu saa 05:15  kwenda Masaki na yalifika kijijini kwake  saa 7:10 adhuhuri.

Mwili wa marehemu ukipelekwa
katika nyumba yake ya milele
Kabla ya Mwili wa Gurumo kupelekwa malaloni, ulipelekwa kwanza  msikitini kuswaliwa na
baada ya kuswaliwa mmwili ulipelekwa makaburini  ndani ya jeneza tayari kwa maziko.

Baada ya marehemu kuswaliwa  kunako  saa 07:40 mwili ulipelekwa makaburini  hapo  karibu na nyumbani kwao   hapo hapo Masaki mkabala na ilipo nyumba alikozaliwa.

Mwili ukingizwa kaburini
Makaburini Kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma Saidi Mabela na ndugu wa marehemu waliingia kaburini kuulaza mwili wa Marehemu Gurumo kwenye nyumba yake ya milele.

Kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma Mabela alisema pamoja na Gurumo kujiuzulu muziki walikuwa wote katika bendi ya OTTU  hadi pale mauti yalipomfika.

Aliongeza kuwa marehemu akiwa Meneja wa bendi kwa hiyo mauti yamemkuta Gurumo akiwa pamoja naye  katika  bendi.

Mmoja wa wanamziki hapa nchini amemtaja  Marehemu Maalim Muhidini Gurumo kuwa ni Mwalimu wa wanamuziki wengi hapa nchini na kwamba  amewainua wanamziki wengi hadi kuwa maarufu katika fani hiyo.

Muhidini Maulidi Gurumo amekuwa katika bendi kadhaa kama  ilivyofafanuliwa  hapo juu enzi za uhai wake kabla ya kuanzinsha bendi yao ya Msondo Ngoma.

 Aliwahi kupigia Bendi ya OSS (Ochestra Safari Sound) na DDC Mlimani  Park maarufu kwa jina la mtindo wao wa Ndekule.

Mwana muziki King Kiki akiwa na wadau wa muziki.
Mwana muziki King Kiki alimweleza Gurumo kuwa ni mwanamuziki  aliye kuwa na kipaji cha kipekee katika utunzi.Alisema alikuwa na uwezo wa kutunga wimbo hapo hapo na kuimba akaongezea  kuwa  ni  yeye aliyebuni mitindo ya Ndekule na Msondo.

Mwanamuziki  Ali Choki kiongozi wa bendi ya Extra Bongo ni miongoni mwa wanamziki waliopata ujuzi na kufanya kazi pamoja na Marehemu Gurumo.

Choki anamtaja marehemu kama Mwalimu Mkuu wa Muziki nchini ambaye sasa ametoweka katika ulimwemuzikingu kwa kusema; "Gurumo ni mwanamuziki aliyekaa kwenye 'game' kwa siku nyingi, ninashauri wanamuzuki wa kizazi hiki kufuata nyendo, heshima na mambo mazuri aliyoyaishi. mkongwe huyu katika tasinia ya muzuki"

Aidha mastaa mbalimbali wa tasinia mbalimbali akiwemo  JB mmoja wa waingizaji  maarufu nchini alisema pengo aliloacha Gurumo litatuchukua kipindi kirefu kuliziba.

Mwanamziki huyu wengi wanadai  alitabiri kifo chake kwa yale aliyofanya  kabla ya kifo chake,  

Akiwa kalazwa aliondoka wodini mara kadhaa akidai  kutolewa hasipitalini arudishwe nyumbani kwake. Jingine ni pale alipoagiza agiza wanae siku chache kabla ya kulazwa, waende huko Masaki kusafisha makaburi  ya ukoo, Jingine ni lile la kutangaza kuacha kupiga muziki.
Diamond Platinum Akimkabidhi Maalimu Gurumo
Enzi za Uhai wake Ufunguo wa Gari

Kitenndo chake  hiki cha kutangaza kuacha  muziki kilipelekea Diamond Platinum kumpa Gari hasa pale alipolalamika katika mahojiano yake na TBC kuwa anaacha muziki huku akiwa hana kitu cha kujivunia kutokana na tasinia hii ya muziki.

Mwanamziki  Gurumo (Kamanda wa muziki ) kama mashabiki wa muziki walivyokuwa wakimwita  ilizaliwa mwaka 1940 katika Kijiji cha Masaki Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani na amefariki akiwa na miaka 74..

Mjane wa marehemu Guromo
Marehemu Maalim Muhidin Gurumo alioa na  ana watoto, wajukuu na vitukuu. Pia alikuwa ni mwanachama wa  Klabu ya Simba tangu 1964.

"Sisi sote tumetoka kwa Allah (SW) na marejeo yetu sote ni kwake" (INNA LILLAIHI WA INAILLAIHI RAJIUUN)

Mungu ilaze roho ya marehemu Gurumo mahali pema peponi

Ona video ya mazishi ya Marehemu Muhidin Maalimu Gurumo ijijini Kwao MASAKI Kisarawe wilaya ya Pwani.(Video imeandaliwa na Global TV)




Source:.bongocelebrity  na vyanzo mbalimbali vya habari

0 comments:

MV Matala yazama katika Ziwa Victoria Katikati ya Visiwa vya Kerebe na Lukolu

.
Sehemu ya meli hii iliyokuwa ikizama
 Jumamosi ya , Aprili 18, 2014\ taarifa za watu 10 kunusurika kufa maji katika ziwa Victoria baada ya meli ya mizigo MV Matala kupinduka na kuzama ikiwa na shehena ya sukari zasikika

Sukari hii ilinunuliwa kutoka katika kiwanda cha sukari Kagera Bukoba na  ilikuwa inasafirishwa  kuja jijini Mwanza.

Meli hii ambayo inamilikiwa na kampuni ya Mkombozi  Fishing and Marine Transport Limited, imezama ikiwa na magunia 5600 ya sukari sawa na tani 280.

 Meli  hii ni mali ya mfanyabiashara wa jijini Mwanza aitwaye V.H.Shah,

Mkurugenzi wa kampuni hiyo Gitano Chacha Munanka ameeleza kwamba meli hiyo imezama ikiwa katikati ya visiwa vya Kerebe na Lukolu majira ya saa 10.30 usiku wa kuamkia Jumamosi na kuongeza kwamba hakuna mtu yeyote aliyejepoteza maisha kufuatia tukio hilo.

kituo cha IT  na Star TV vimeelezea  kuzama kwa meli hii na kongezea kuwa juhudi za wafanyakazi wa kampuni hiyo kuipindua zinaendelea bila mafanikio,

huku baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakisema chanzo cha meli hii kuzama ni kutokana na dhoruba kali .

Watabiri wa hali ya hewa wamekuwa wakitoa ushauri kwa wamiliki wa vyombo vya majini lakini kumekuwa  na kutozingatia utabiri unaotolewa na mamlaka hii ya hali ya hewa hapa nchini.

Kungekuwa na mazingatio ya utabiri huu unaotolewa na mamlaka hii huenda kungesaidia  kuepusha nchi na maafa haya yanayojitokeza nchini hivi sasa.



Sehemu inayo onekana  pichani ni sehemu ya meli iliyozama, ambayo ilianza safari yake ya kutoka Bukoba majira ya saa 7 mchana, ikiwa inaendeshwa na kapteni Erick Lasana.
Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra kanda ya ziwa, imethibitisha kuzama kwa meli hiyo yenye uwezo wa kubeba tani 280 za mizigo na abiria 100.

0 comments:

Fununu za Kuwanasa Walio Tega Bomu Arusha Night Park Bar Zapatikana.

Askai wakifanya doria eneo la tukio.
VYOMBO  vya Usalama vinachunguza picha za kamera za usalama (CCTV)  za baa ya Arusha Night Park, muda mfupi kabla ya na baada ya bomu kulipuka.

Bomu hili lililojjeruhi watu  wapatao 20, lililipuka ndani ya baa hii maarufu mkoani Arusha, Jumapili, Aprili 13, 2014 saa 1:30 usiku, wakati wateja wakiangalia mechi ya  soka, Ligi kuu ya Uingereza, kati ya timu za Chelsea na Swansea

Taarifa toka vyanzo kadhaa zinadai kuwa tayari makechero wa polisi kwa kushirikiana na wale wa Idara ya Usalama wa Taifa wanachunguza sehemu ya matukio ya picha hizo, kabla  na baada ya bomu hilo kulipuka.

Habari zinaeleza kuwa sehemu ya picha hizo zinaonesha watu wawili waliokuwa na mfuko mweusi wakiingia na  kuweka mfuko huo katika moja ya sehemu za baa hiyo na muda mfupi baadaye mlipuko ukatokea.

Aidha  kitu kinachodhaniwa pia kuwa ni bomu kiligundulika katika baa ya Washington iliyopo jirani na kituo kikuu cha mabasi madogo katikati ya jiji la Arusha siku hiyo hiyo, usiku wa saa tano.

Akizungumzia tukio hilo katika mkutano wake na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Isaya Mungulu alieleza kuwa makechero wanaendelea kuchunguza picha za kamera za usalama katika baa hiyo.

“Uwezekano wa tukio hilo kunaswa na kamera za usalama ni mkubwa sana na tunaweza kuwatambua wahusika hata kwa sura zao kwa sababu picha zinaonesha watu wawili wakiweka mfuko mweusi na baada ya muda mlipuko ukatokea,” alisema.

Alipotakiwa kusema nini kinafuatia kwa  kupatikana kwa kielelezo kama hicho alikuwa na haya ya kusema.

“Ni kweli tumechukua matukio yote yaliyorekodiwa na kamera hiyo ya usalama lakini bado tuko katika hatua za mwanzo za uchunguzi wetu, hatuwezi kwa sasa kutangaza hadharani hatua tuliyofikia,”alisema Mungulu.

Kuhusu jeshi hilo kushindwa kuwakamata watuhumiwa katika matukio ya milipuko ya awali iliyotokea Arusha, Mungulu alisema. "Hata wahalifu na walioko nyuma ya matukio haya ni werevu na wana akili za kukwepa mkono wa dola, ila tutawatafuta na kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria  pale tutakapowatia mikononi.".

Tukio la Jumapili ya Aprili 13,2014  saa 1:30 usiku ni  la nne tokea kuwepo na kulipuka  kwa mabomu hapo jijini Arusha.

Tukio la kwanza lilikuwa la bomu  lililolipuka na kumjeruhi vibaya usoni aliyekuwa Katibu wa Bakwata Mkoani Arusha Abdulkarim Njonjo ambalo pia lilibainika kuwa ni bomu la kutengenzwa kienyeji.

Tukio la pili mwezi Mei mwaka jana bomu la mkono lilirushwa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Olasit ambapo waumini watatu walipoteza maisha na wengi kujeruhiwa vibaya. Balozi wa Vatican nchini Askofu Fransesco Padilla na Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha Josephat Lebulu  ingawa walikuwepo katika mkutano huu.hawakupata madhara yoyote.

Rejea tukio hili ambalo bado lko mwenye kumbukumbu za wengi.kwa njia ya video  kama lilivyoripotiwa na ITV.

Tukio lingine la tatu ni la bomu kurushwa katika mkutano wa kampeni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika viwanja vya Soweto ambapo watu wanne walifariki dunia na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa.

Hadi sasa  hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa na hakuna  kikundi chochote kile kilichowahi kutangaza au kudai  kuhusika katika matukio yote haya.

Kinachotushangaza na kutupigisha butwaa ni kwamba ni kwa nini Arusha ambako nchi na mataifa yanapaona ni sehemu tulivu na yenye vivutio vya kitalii vingi kuwa eneo la shabaha kwa washambuliaji hawa?

Tunaomba uchunguzi uongezeke  kuwabaini wahalifu hawa kwa kuliongezea jeshi la Polisi jijini Aruha nguvu za ziada toka Makao makuu ya Polisi nchini kwani hili sasa linapaswa kuchukuliwa kama janga la kitaifa.

0 comments:

Phytonutrients;. Their sources, Kinds and Their Potential Health Effects to Our Bodies

Some foods from which  phyto-nutrients are obtained

Phytonutrients.

Plant foods contain thousands of natural chemicals. These are called phytonutrients or phytochemicals."Phyto" refers to the Greek word for plant. These chemicals help protect plants from germs, fungi, bugs,virus, and other threats.
 Phytonutrients are what give the skins of fruits and vegetables their flavor, scent and color. They consist of a variety of naturally formed chemicals that protect plants from fungi, germs, virus  and other threats in nature. In short they are plants natural defense system against environmental damage.
Fruits whole grains,nuts, beans tea and vegetables contain phytonutrients.

Phytonutrients doesn't  play the role of vitamins and minerals that plant foods contain. in to our bodies but when we eat or drink phytonutrients, they help us prevent diseases and keep our bodies working properly.
There are more than 25,000 phytonutrients  found in plant foods. Here we are going to take a look at  six important phytonutrients and foods in which we can find them – as well as their potential health effects to our bodies.
              I.Carotenoids
            II.Ellagic acid
         III.Flavonoids
          IV.Resveratrol
            V.Glucosinolates
          VI.Phytoestrogens

Carotenoids

More than 600 carotenoids provide yellow, orange, and red colors in fruits and vegetables.
Carotenoids act as antioxidants in your body. This means they tackle harmful free radicals that damage tissues throughout your body.
The types of carotenoids that may have other health benefits include:
a.     Alpha – carotene
b.    beta-carotene
c.      beta - cryptoxanthin. 
d.    Lycopene. 
e.      Lutein and
f.       zeaxanthin. 
Alpha - carotene, beta-carotene, and beta - cryptoxanthin. Your body can convert all of these to vitamin A. This vitamin helps keep your immune system working properly, and it's needed for eye health. Yellow and orange foods like pumpkins and carrots are good sources of alpha- and beta-carotene.
These also contain beta - cryptoxanthin, as do sweet red peppers.
Lycopene. This gives red or pink color to: Tomatoes, Watermelon, and Pink grapefruit
Lycopene has been linked to a lower risk of prostate cancer.
Lutein and zeaxanthin. These may help protect you from cataracts and age-related macular degeneration, which are two types of eye problems.
Good sources of these phytonutrients are greens such as: Spinach, Kale, Collards

Ellagic Acid

Ellagic acid is found in a number of berries and other plant foods, especially:
a.                 Strawberries
b.                 Raspberries
c.                  Pomegranates
Ellagic acid may help protect against cancer through several different ways. For example, it may cause cancer cells to die. And it may help your liver neutralize cancer-causing chemicals in your system.

Flavonoids

A large number of phytonutrients fall into the flavonoid category. They are found in a variety of plant foods.
The types of flavonoids include:
a.                 Catechins. 
b.                 Hesperidin. 
c.                  Flavonols
Catechins. Green tea is a good source of catechins. The drink of catechins may help prevent certain types of cancer.
Hesperidin. Found in citrus fruits, this flavonoid works as an antioxidant. It can reduce inflammation in the body. It may also help reduce the risk of cancer.
Flavonols. Quercetin is a well-studied type of flavonol. It is found in: Apples, Berries Grapes, Onions
It might help reduce people's risk of asthma, certain types of cancer, and coronary heart disease.

Resveratrol

Resveratrol is found in: Grapes, Purple grape juice, Red wine
It acts as an antioxidant and anti-inflammatory.
Some research suggests that resveratrol might reduce the risk of heart disease and cancer. And it may help extend people's life span.
Glucosinolates
Glucosinolates: These are natural components of many pungent plants such as mustard, cabbage Cauliflower, Broccoli and horseradish.
 The pungency of those plants are due to mustard oils produced from glucosinolates when the plant material is chewed, cut or otherwise damaged Cruciferous vegetables contain vitamins, minerals, other nutrients  and chemicals known as glucosinolates.
Cruciferous vegetables are rich in nutrients, including several carotenoids (beta-carotene, lutein, zeaxanthin); vitamins C, E, and K; folate; and minerals. They also are a good fiber source.  
In addition, cruciferous vegetables contain a group of substances known as glucosinolates, which are sulfur-containing chemicals. These chemicals are responsible for the pungent aroma and bitter flavor of cruciferous vegetables.
During food preparation, chewing, and digestion, the glucosinolates in cruciferous vegetables are broken down to form biologically active compounds such as indoles, nitriles, thiocyanates, and isothiocyanates (1). Indole-3-carbinol (an indole) and sulforaphane (an isothiocyanate) have been most frequently examined for their anticancer effects.
Indoles and isothiocyanates have been found to inhibit the development of cancer in several organs in rats and mice, including the bladder, breast, colon, liver, lung, and stomach (2, 3). Studies in animals and experiments with cells grown in the laboratory have identified several potential ways in which these compounds may help prevent cancer:
They help protect cells from DNA damage, They help inactivate carcinogens,They have antiviral and antibacterial effects,They have anti-inflammatory effects,They induce cell death (apoptosis),They inhibit tumor blood vessel formation (angiogenesis) and tumor cell migration (needed for metastasis).
Studies in humans, however, have shown mixed results.

Phytoestrogens
Phytoestrogens are naturally occurring estrogenic compounds in a variety of plant foods such as beans, seeds, and grains. 

 Their chemical structure resembles estrogen.

Phytoestrogens acting as estrogen mimics may affect the production and/or the breakdown of estrogen by the body, as well as the levels of estrogen carried in the bloodstream.

These mimics can either have the same effects as estrogen or block estrogen's effects.  These compounds are generally weak estrogens, in comparison to real estrogen, synthetic estrogen (HRT), and xenoestrogens.

Anyone who is experiencing estrogen dominance problems will likely want to avoid phytoestrogens where possible as they will only contribute to the problem.

Women who do not have estrogen dominance issues and desire to supplement with estrogen due to lowered levels from menopause or hysterectomy may find consuming some phytoestrogens to be beneficial.
Which foods contain phytoestrogens?
More than 300 foods have been shown to contain phytoestrogens. The three chemical classes of phytoestrogens are Isoflavonoids, Lignans and Coumestans -

Isoflavonoids:- Isoflavonoid phytoestrogens are found in beans from the legume family; soybeans and soy products are the major dietary source of this type of phytoestrogens.  The isoflavonoid extracts from soy are known as genistin, diadzein, and glycitin.
Lignans: - Lignan phytoestrogens are found in high fiber foods such as cereal brans and beans; flaxseeds contain large amounts of lignans, but some studies say that it can have a positive effect on estrogen dominance. 
Coumestans: - Coumestan phytoestrogens are found in various beans such as split peas, pinto beans, and lima beans. Alfalfa and clover sprouts are the foods with the highest amounts of coumestans.
Following are some of the strongest phytoestrogen containing substances: Soy, Black Cohosh, Chasteberry, Dong Quai, Red Clover, Caffeine
What are the benefits of consuming phytoestrogens?

 It has already been shown that soya beans, with their ingredients genistein and daidzein from the isoflavonoid group, have protective effects on hormone-caused diseases.

 

Attention:

 Xenoestrogens and Phytoestrogens

We are constantly assaulted by estrogens in our environment from the food we eat and the chemicals we use.  Estrogen mimickers in the form of chemicals (xenoestrogens), and foods and plants (phytoestrogens), mimic the action of estrogen produced in cells and can alter hormonal activity.

It is important for all of us to be aware of the effects of estrogens in our 
environment. 

It should be of particular interest for anyone dealing with an estrogen dominance  condition such as uterine fibroid tumors, fibrocystic breasts, glandular dysfunction, hair loss, weight gain, and depression, to name just a few.

Evidence is steadily growing that xenoestrogens and other hormone mimicking substances are implicated in a wide range of human and wildlife health problems. 

Estrogen dominance from these environmental hormone disrupters are causing an imbalance of female hormones, creating a host of estrogen dominance symptoms.
Girls and boys are reaching puberty too early as a result of these disrupters.  

Additionally, xenoestrogens produce hormonal stimuli that contributes to inappropriate growth of mammary tissue cells, resulting in a problem society is calling “man boobs.” 

 Some theorize that estrogen dominance in men is contributing to hair loss, atherosclerosis, prostrate problems, lowered libido, and impotency. 

Xenoestrogens

Xeno literally means foreign, therefore xenoestrogens means foreign estrogens. Some of the 70,000 registered chemicals for use in the United States have hormonal effects in addition to toxic effects. 

The synergistic effects of exposure to many xenoestrogens are well documented, but largely unknown.  These substances can increase the estrogen load in the body over time, and are difficult to detoxify through the liver.

 This further compounds the problem of estrogen dominanceTo gain a perspective on how much exposure of chemicals is occurring, the NIH's National Institute of Environmental Health Sciences and the Centers for Disease Control and Prevention have launched a study of blood and urine samples to determine the amount of exposure that Americans have to environmental estrogens. 

 The CDC will measure approximately 50 environmental estrogens in 200 persons to determine levels of exposure to the population.

Among the more familiar chemicals that will be tested for are: insecticides parathion and DDT and its metabolites; herbicides; fungicides; plant and fungal estrogens; and industrial chemicals such as cadmium, lead, mercury, PCBs and dioxins.
Byproducts of the plastic and pesticide industries—called organochlorines—are one of the largest sources of xenoestrogens.

These compounds, also used in dry cleaning, the bleaching of feminine hygiene products and the manufacture of plastics ranging from yogurt containers to baby bottles, have been shown to exert hormone-disrupting effects. What's more, organochlorines are known to accumulate in fatty human tissue and fluid such as breasts and breast milk.

 Caution dictates that women should try to eliminate these external estrogen sources through diet, supplements and lifestyle changes.

Plastics in our lives also expose us to the chemical bisphenol A, a breakdown product of polycarbonate, widely used in many plastics. 

Bisphenol A, found in the lining of many food cans and juice containers, escapes when polycarbonate is subjected to high temperatures.

The estrogenic effects of bisphenol A became clear when men working in the plastics industry developed breasts after chronically inhaling the chemical in dust.

Other bad news from scientists have suggested that environmental estrogens might be reducing sperm counts in men and causing breast cancer, fibroids and other reproductive diseases in women.

Xenoestrogens can be found in many of our meats and dairy products in the form of chemicals and growth hormones that are given to the animals. These can be quite powerful, and should be avoided where possible.
The information below makes suggestions to avoid substances that contain xenoestrogens. These substances can increase the estrogen load in the body.
  • Avoid all pesticides, herbicides, and fungicides. Wash your food well to rid the pesticides. Bathe the washed food in a produce wash or ozonated water for 20 minutes before cooking.
  • Have a good water filter for your source of water.
  • Use only organic based whole foods when you can. Buy hormone free meats and dairy products where possible.
  • Avoid plastic goods - they leach into the environment.
  • Do not microwave food in plastic containers, and especially avoid the use of plastic wrap to cover food for microwaving.
  • Use glass or ceramics whenever possible to store food.
  • Do not leave plastic containers, especially your drinking water, in the sun.
  • If a plastic water container has heated up significantly, throw it away - do not drink the water either.
  • Don't use fabric softeners as it puts petrochemicals right on your skin.
  • Use a simple laundry and dish detergent with less chemicals.
  • Use organic soaps and toothpastes. Avoid fluoride.
  • Avoid creams and cosmetics that have toxic chemicals and estrogenic ingredients such as parabens and stearal konium chloride. Switch to more natural products. Cheap brands usually have more toxic ingredients.
  • Avoid nail polish and nail polish removers.
  • Use only naturally based perfumes. Most perfumes are petrochemically based.
  • Avoid surfactants found in many condoms and diaphragm gels.
  • Avoid new carpet - it can give off noxious fumes.
  • Avoid X-rays as much as possible.
  • Be aware of noxious gas such as that from copiers and printers, carpets, fiberboards, etc. Computer monitors can emit a high level of electromagnetic force (EMF). Read about the Aulterra Neutralizer for preventing EMF damage.


0 comments:

POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza