Watu Wanne Wauawa na Wananchi Waliokuwa na Hasira Kali.
![]() |
Mmoja wa walio uliwa akipata kipigo |
Haya yalitokea katika kijiji cha Igwambiti, Kitongoji cha Buhongwa, Kata ya Nyamagana, hapa jijini Mwanza jana asubuhi tarehe 18,March 2014.
Mtendaji wa kata ya Buhongwa Benedict Kabadi alisema alipokea taarifa za kutokea mauwaji haya jana asubuhi na alipofika eneo la mauaji hayo alikuta miili ya watu watatu waliouliwa.
Alidai wananchi walimkamata Joseph Mwita na kumtaka awaoneshe watu anaoshirikiana nao katika wizi.Inadaiwa aliwapeleka hadi kijiji cha Igwambiti katika kata hii na kuwaonesha.
Mtendaji Kabadi anasema watuhumiwa hawa waliuwawa na kundi la watu.Alipofika eneo la tukio walikuwa wameisha ondoka na kuacha miili hiyo hapo.
Baadae ilifahamika kuwa waliouliwa ni Ezekieli Lucas (27),Kusekwa Lucas (25),Masumbuko Kisinza (30) wote wakiwa ni wa kazi wa kijiji hiki cha Igwambiti katika kata hii ya Buhongwa. Wilaya ya Nyamagana na Mfanya biashara ya nyama wa Buhongwa,Mafisi Mwita (30).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola anasema watu watatu wanashikiliwa na jeshi hilo kwa kukutwa na marungu yenye damu.
Akifafanua zaidi alisema tukio hilo lilitokea jana hiyo majira ya saa11.30 alfajiri katika kijiji hicho cha Igwambiti Kata ya Buhongwa.
Chanzo cha mauaji haya inadaiwa ni wizi wa ngo'mbe uliotokea katika kitongoji cha Nyang'omango katika kijiji cha Mtende Tarafa ya Usagara,Wilaya ya Misungwi.
Akikemea hatua hii ya wananchi kujichukulia madaraka mikononi Kamanda Mlowola akihojiwa na kituo cha luninga cha Star, hapa jijini Mwanza alisema uchunguzi juu ya mauaji haya unaendelea ili kubaini wote waliohusika katika mauaji haya.
Hatusemi wezi wa ng'ombe wauliwe wakikamatwa lakini hatua za kukomesha wizi wa ngo'mbe hususani hapa jijini Mwanza umekithiri hivyo tunaliomba jeshi letu la Polisi lione hili kama tatizo katika mkoa wetu na liongeze juhudi za makusudi kukomesha wizi huu.
Chanzo: clouds fm
0 comments: