CCM Yashinda kwa Kishindo KALENGA, Yapata Kura Asilimia 79.32
![]() |
Mgimwa akiwa amebebwa na wanachama wa chama chake |
Akiwa ameambatana na mkewe Robby Mgimwa,
Godfrey Mgimwa mgombea katika jimbo hili la Kalenga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi huu mdogo, awabwaga wapinzani wake wawili wa Chadema na Chausata kwa ushindi wa kishindo.
Mgimwa alijizolea ushindi wa kura 22,962 ambazo ni sawa na asilimia 79.32 dhidi ya kura 5,853 ambazo ni sawa na asilimia 20 alizopata Grace Tendega wa Chadema na kura 150 sawa na asilimia 0.52 alizopata Richard Minja wa Chausta.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika uchaguzi huu mdogo wa kumpata Mbunge wa jimbo la Kalenga uliofanyika siku ya jumapili ya tarehe 16, na kuibuka na ushindi huu wa kishindo.
Kwa mujibu wa matokeo haya, Mgombea wa CCM Godfrey Mgimwa ndiye Mbunge mpya wa jimbo la Kalenga akichukua nafasi ya baba yake Mbunge aliyefariki jimboni humo Dr. William Mgimwa.
Chama cha CCM kinaeendeleza mbio zake za kushinda katika chaguzi ndogo na kuwabwaga mahasimu wao chadema.
Msimamizi wa uchaguzi huu Pudensiana Kisaka ambaye ni Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Iringa alimkabidhi juzi hiyo hiyo Godfrey Mgimwa hati yake ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo hili.
Baadae Godfrey akizungumza na waandishi wa habari alisema anakumbuka ahadi zote alizotoa kwa wananchi wa jimbo lake wakati wa kampeni hivyo kilichopo ni kujipanga kuzitekeleza.
"Ahadi zote nilizotoa zitatekelezwa kupitia Ilani ya chama chetu cha CCM. Ninachowataka wananchi wangu ni kuwa na Imani kwani mambo yote hayo yatatekelezwa."Alisema haya akishukuru kwa ushindi aliopata.
Pamoja na kampeni zilizoanza mapema siku tatu kabla zikishirikisha wabunge wengi wa chama hiki na matumizi ya helkopta kulinda kura, Godfrey aliibwaga chini Chadema hata katika kata zilizodaiwa ni ngome ya chama hiki.
Naye Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Nape Nnauye akionesha kufurahia ushindi huu alidai ushindi huu ni ushahidi tosha wa kuonesha kuwa Chama chake bado kinapendwa na ndilo chaguo la watanzania walio wengi.
Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi huu, kura 29,541 ndizo zilizopigwa kati ya kura 71,965 zilizoandikishwa katika daftari la wapiga kura,
CCM imeshinda kwa kura 22,943 dhidi ya kura 5,800 za Chadema na Chausata ikiambukia kura 143 tu.Kura zilizoharibika ni 576 hivyo kura safi zilizotoa matokeo haya zilikuwa 28,965.
Baada ya kumalizika uchaguzi wa kalenga sasa macho yote yanaelekezwa katika jimbo la Chalinze.Huko nako historia itajirudia.Je ridhiwani atapeleka kijiti cha CCM kama CCM inavyotaka?
Vyanzo: Mwl.Msangi na Bongo Today
0 comments: