Mkazi Mmoja Maeneo ya Butimba Tambuka Reli Ang'oa Dirisha la Nyumba ya Jirani.
Mbwa aliyekutwa na mpiga picha akijitafutia chakula jalalani (Picha na Mwl.Msangi E.H.) |
Ilikuwa ni siku ya Alhamisi, tarehe 20 Marrch 2014 majira ya Mchana wiki iliyopita, kundi kubwa la watoto wa ButimbaTambuka -Reli mtaa wa Kanyerere.Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza walikuwa wakimshambulia mbwa.
Kwa mafimbo,magongo na mawe watoto hawa walimshambulia mbwa huyu kwa lengo la kumuua kwa kumdhania ana kichaa cha mbwa kwa hali dhoofu aliyokuwa nayo.
Tendo hili lilitokea katika moja ya barabara za kitongoji hiki cha Butimba Tambuka- Reli.
Akimsimulia mwandishi wa kisa hiki, Mratibu wa Elimu kata ya Butimba Ndugu Rogasian N, Mrema alisema habari hii ilipatikana ofisini kwake wakati wakisimuliwa kisa kingine kama hiki cha kijana kukimbizwa na mbwa na kugonga mti kwa kichwa maeneo hayo hayo ya Tambuka-Reli.
Katika kisa hiki inasemekana kijana alipogonga mti kwa kichwa mbwa aliyekuwa anamkimbiza alipoona hivyo akaogopa kuwa kama atagongwa naye hivyo itakuwa hatari kwake hivyo akajiondokea.
Kwa kisa hiki cha kung'oa dirisha . Mwenyekiti wa kitongoji hiki cha Butimba Tambuka Reli kilikotokea Ndugu Leonard Malisa ambaye ni Ndugu wa Bwana Mshiu Dominic aliyekimbizwa, alisema Bwana Dominic Mshiu akiwa njiani kuelekea nyumbani aliona kundi la watoto wakimshambulia mbwa kwa kusudio la kumuuwa.
Bwana Mshiu hakujishughulisha nao akajipitia kwenda alikokuwa akielekea . Mara alishitukia mbwa anamkimbilia.Wengi wanahisi mbwa huyu alikuwa anatafuta msaada kwake.
Naye kuona mbwa anakuja mbio kwake akaogopa na kuongeza kasi kumkimbia. Mbwa naye akaongeza kasi ili asiachwe kwa wale watoto walio kuwa wakimpiga.
Bwana huyu alipoona mbwa anamkaribia.akaongeza mbio huku akipiga kelele za kuomba msaada.
Pamoja na mbio hizi bado mbwa alikuwa karibu sana naye .
Kwa kuona hawezi kumwacha kwa mbio mbwa huyu, alipokaribia nyumba ya mama mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Mama Kanyerere. bila hodi huku akipiga yowe aliingia ndani ya nyumba hii.
Alipoingia na mbwa naye akaingia. Kuona hivyo akaingia chumbani.Mbwa hakuchelewa haraka haraka kabla hajarudishia mlango wa chumba mbwa naye huyo chumbani.
Kuona hivyo Bwana Mshiu Dominic akapiga ngumi dirisha la chumba hicho na kutoka nalo.Akiwa nje bado akaona kama haitoshi hiyo kwa usalama zaidi akapanda juu ya mti wa mwembe uliokuwa hapo karibu.
Mama mwenye nyumba kwa sasa inasemekana anadai dirisha lake likarsbatiwe ama kama sivyo anatishia kumfungulia bwana Dominic mashitaka.
Habari ambazo hazijathibitishwa zadai ni kwamba mbwa huyu ameuliwa kwa kwa hofu kwamba huenda anaweza kuleta madhara kwa wakazi wa eneo hili.
Kwa upande mwingine wanadai mbwa huyu hakuwa na kichaa bali alikuwa anatafuta nusura toka kwa bwana Mshiu, kwani kama alikuwa akitaka kumuuma asingeshindwa kwa vile alikuwa anamkaribia mno kiasi ambacho asingeshindwa kumuuma kama hilo ndiyo lilikuwa kusudio lake.
Tukio hili lapaswa liwe fundisho kwa jamii.Ufugaji holela wa mbwa unatakiwa kukomeshwa.TuwafungIe mbwa vibandanI nyakati za mchana. Mbwa wasiachwa na wanaozagaa ovyo wauliwe.Isitoshe idara ya mifugo inapaswa kufanya juhudoi kuchanja mbwa wote na mbwa anayeonekana kuzagaa auliwe.
Kinga ni bora kuliko tiba.
0 comments: