YADAIWA HUSSEIN RASHIDI aka (HUSSEIN MACHOZI) KAPOKEA KICHAPO CHA MBWA NA KUPEWA MASAA 24 KUONDOKA NCHINI KENYA

Hussein Machozi
Waswahili wanasema ngoma ikilia sana haikawii kupasuka. Ni hivi karibuni mwanamziki wa Kitanzania wa muziki wa kizazi kipya  Hussein Rashid kwa jina maarufu Hussein Machozi ametokea kuvuma sana huko nchini Kenya kwa vibao kadha motomoto kama ‘ nipe’ na Addicted alivyocheza akishirikiana na mwana dada Size 8 yamemfika ya kumfika baada ya fumanizi.

Habari kutoka kwenye vyombo vya habari vya nchini Kenya zimenukuliwa zikidai kuwa kijana huyu amefumaniwa na Mke wa Mwanasiasa mashuhuri huko jijini Mombasa  Kenya, katika Hoteli ambayo jina halikutajwa na kupokea kichapo na kuamriwa kutoka nchini humo ndani ya saa ishirini na nne.,

“Even though the news could not be confirmed as Hussein Machozi had reportedly been ‘deported’ back to Tanzania and his phone went unanswered, in another hour, a top Mombasa blog posted the piece blaring it with this long catchy headline

“MSANII HUSSEIN MACHOZI APOKEA KICHAPO CHA MBWA NA KUPEWA MASAA 24 KUONDOKA HAPA NCHINI KENYA”. It sounded astonishing, so damning like a fellow caught doing drugs in Singapore.

“Msanii huyu mashuhuri wa bongo flavor leo hii katika hoteli flani ya kitalii hapa jijini Mombasa alijipata matatani baada ya kupatikana akiwa na mke wa kiongozi flani mashuhuri wa hapa nchini. Yasemekana mheshimiwa huyu amekua akimkulia timing Machozi bila mafanikio lakini leo siku arobaini zilitimia kwake msanii huyu mkosa adabu,” read the Blackstar Entertainment update whose Facebook link had been copied to the Pulse editor. In a nutshell, the writer was insinuating that Machozi had been having a secret affair with a top politician’s wife and after learning of it, the politician had been tracking the two all along until this day when he ‘caught them’.

“Msanii huyu alipatikana red handed na mke wa kiongozi huyo kwa kitanda na hapo ndipo masaibu yakamkumba na kuamrishwa aondoke hapa nchini kwa masaa aliopewa,” the dossier concluded and so with an exclamation: “Je, wewe kama shabiki wake wamshauri vipi?”

Some Facebook responses were as hilarious as the reports. One Job Chilibasi reasoned that the news would not stop a steamy affair as ‘watakutana huko bongo’ while Pettie Nashipai added that ‘utamu wa maisha, kipendacho roho dawa...ashapata Hussein, ashapata yake mbona mwamgeuzia?”
Hivyo ndivyo habari za  ‘MTZ ‘ huyu zimevumishwa  katika vyombo hivyo  mbalimali kutoka huko nchini Kenya ambako msanii huyu anavuma. Washabiki wake nchini humo wamefikia kumfananishwa na Mwanamziki mashuhuri wa Kimarekani Curtis Jackson  (aka) 50 cents.

A photo from Shu Omar Yunus in "In a Relationship with Hussein   Machozi"
Kijana huyu mzaliwa wa Manyoni Singida,  mwaka  jana 2013 Agosti 28,  habari zake za kuuaga ukapere zilitangazwa katika mitandao ya kijamii kufunga pingu za maisha na mwadada Shu Yunus Omar raia wa Kenya.

Kutokan na uharaka unaodaiwa ameondokea nao huko Kenya haifahamiki kama kafanikiwa kaondoka na mkewe ama amemuacha huko Kenya.

Tunategemea kupata habari zaidi pale muhusika mwenyewe atakapotoa taarifa za kukanusha tuhuma hizi pale atakapojitokeza kusimulia kilichomsibu huko kwa majirani zetu Kenya.

Tunategemea takuwa ndiyo sivyo maana, tuhuma kama hizi kwa kijana mwiisilamu katika mwezi mtukufu huu akili inakataa kukubaliana nazo.

Shu Yunus Omari
Zaidi ya yote mkewe kwa mwonekano 
Hussein Machozi.
wake  ana vigezo vyote vya kumfanya  mume kutulia ndani na kuacha michepuko.



Kama kweli kachepuka huyo mdada atakuwa si wa kipekee bali ni miss AFRICA.
                     

Kwa uchache haya ndiyo tunayosikia kumkuta Mzee wa 'Binti Kiziwi' 

HAPA pata Kibao  kilichoiteka KENYA NZIMA CHA  'Addicted' UTAKIKUBALI ni kikali ile kwelili kweli.


Hadi tunaiposti habari hii hali ilikuwa bado ni ya kutatanisha kwamba ni kwele au si kweli. 

Hofu ya kwamba ni kweli au si kweli inatokana na tabia iliyojitokeza ya wasanii kutumia vyombo vya hahari kujenga umaarufu wao kwa kukubaliana na vyombo hivi kuwapaka matope na kwa njia hii wanatoka kweli kweli. 


0 comments:

POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza