Pata Wimbo katika Mahadhi ya Kisukuma wa BOB HAISA - BHATOJA

Bob Haisa Akiimba Wimbo wa Bahoja
MSANII wa Muziki wa Bongo Flava nchini Bob Haisa kutoka Kanda ya ziwa mkoani Mwanza hatimaye aachia video ya wimbo  mpya  uitwao BHATOJA aliouimba kwa lugha ya kisukuma.

Wimbo huu Bhatoja ni wimbo wa asili.. 

Wimbo huu ni maarufu sana na hutumika sana katika shamrashamra za harusi. Wimbo huu huiimbwa na kabila la Wasukuma ambao ni kabila  kubwa na maarufu hapa nchini.

Alichofanya Bob Haisa ni kuuboresha kwa kuuongezea vionjo na kuuimba kwa ladha inayovutia lakini  isiyoondoa hisia za awali za wimbo wa kale.

Aidha  ameuwekea midundo iliyotulia sambamba na kuzingatia maneno husika ya wimbo wa asili.

Ubora huu hakika  humvutia hata yule asiyeelewa lugha hii ya kisukuma. 

Yeyote ausikiae wimbo huu hakika hubaki akitikisa kichwa au miguu yake kwa utamu.

Bob Haisa kuuweka wimbo huu katika video  kumesaidia kuutangaza na kuongeza mvuto wa wimbo huu kwa wengi.

Hii hapa video ya wimbo huu. ili nawe uweze kuhukumu ukweli huu.


Bob Haisa anavibao vingi ambavyo vimempandisha juu katika tasinia hii ya  mziki wa kizazi kipya.

Wimbo wake unaoelezea historia ya Tanzania tokea kupata uhuru hadi kufikia miaka hamsini ya Uhuru  unatukumbusha mengi sisi watanzania.

Wimbo huu ameuita 'Nasema na weweTanzania'.Hakika ni wimbo wa kuvutia sana.


Nimeona ili uweze kuyahukumu maneno yangu vilivyo nawe sikiliza wimbo huu ili uweze kukubaliana nami au kukataa. 

Video ya 'Nasema na weweTanzania' hii hapa 




Source: You tube

0 comments:

POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza