Namna ya kuondosha Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume na Kike.

Kitunguu saumu
 Tatizo la nguvu za kiume na kike linakuwa kwa kasi sana siku hizi!
 Hali halisi ya tatizo la nguvu za wanawake  na wanaume linawasumbua wanaume  na wanaweke wengi kiasi cha kuwafanya baadhi kuachana na wenza wao.

Kinachoweza kuwaokoa wanaume  na wanawake kutoka kwenye hali hii ni kuzingatia masharti ya wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja na kula vyakula vya asili na kufanya mazoezi.

Pili chunguza chanzo cha tatizo kwa kuwaona madakitari ili kujua nini chanzo cha taizo.Tatizi la kukosa nguvu za kiume au kwa mwanamke kukosa hamu ta tendo la ndoa hutokana na sababu kuu mbili.

Sababu ya kwanza ni ile ya kuonekana (Phisical reasons) kama magonjwa, kazi na madawa ya kulevya.

Sababu ya pili hutokana na msongo wa mawazo (Psychology reasons) kama hasira, hofu, na kutojiamini au vitisho.
 Sababu hizi zimekuwa zikiongezeka sana katika jamii  kutokana na watu kuzidi kuiga mitindo ya maisha ya kigeni.

Watanzania msile sana chips mayai, chips kuku, nyama choma, juice na soda na pombe. Acha kabisa kuvuta sigara kama u mvutaji wa sigara au kama u mnywaji wa pombe za kupita kiasi.

Achana na  vyakula vya kukaangwa na mafuta. Kula vyakula vya kuchemshwa na maji na usinywe pombe na vinywaji vitamu vyenye sukari., Kunyweni maji madafu na togwa.

Tuepuke kufanya kazi zaidi ya saa 8 kila siku.Pata usingizi wa kutosha usiopungua saa nane kila siku.

Tupumzishe akili zetu weekends kwa kukaa nyumbani  ama kutembelea sehemu za  vivutio ili kuburudisha akili walao mara moja kwa mwezi.

Matatizo ya kutosimamisha na  kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake na wanaume mara nyingine hutokana na kufanya kazi sana.

Sababu nyingine ya kisaikolojia ni msongo wa mawazo, kula vyakula vya sukari na vya mafuta sana

Sababu nyngine ni magonjwa ya sukari, kansa, moyo, figo, presha, kuvimba tezi za uzazi, ukimwi  na magonjwa mengine mengi kwa kutaja tu haya machache.

Mwone dakitari ujue chanzo cha tatizo lako. Ukosefu wa nguvu za kiume au hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake si ugonjwa bali ni dalili ya ugonjwa fulani ulioko mwilini mwako.

Ili uweze kuudhibiti tatizo hili ni vemz kujua kwanza ugonjwa usababishao tatizo hili. Ukiutibu, utakabili tatizo lako hilo la ukosefu wa nguvu za kijinsia.

Namna ya kujikinga na tatizo hili;
Pamoja na kufanya mazoezi  ya mwili ya mara kwa mara, njia nzuri ya kujikinga na tatizo hili ni kula  mlo uliokamilika ulio na virutubisho vihitajikavyo mwilini.

Ili kupata virutubisho hivi tunapaswa kula vyakula vikiwa katika  uasilia wake. Hakikisha mlo wako unakuwa unatokana na nafaka, matunda, majani, mikunde, mizizi, mbegu, samaki na nyama haswa vikiwa havijafanyiwa usanidi.

Vyakula hivi vinapaswa kuliwa vikiwa kwenye  uasili wake na siyo  baada  ya kukobolewa au kufanyiwa usanidi kiwandani.

Kula matunda na  mboga za majani kila siku.
Mboga za majani kama ; kisamvu, majani ya kunde, matembele, sukuma wiki, mlenda, , majani ya maharage, bamia, bilinganya, ngogwe na mchicha,  vitunguu maji na vitunguu saumu, hivi si vyakula tu bali pia ni dawa.

Hakikisha unapata vyakula hivi kwa wingi.

Kitunguu saumu kimetumika miaka mingi kama dawa ya kuzui na kutibu mradhi  na hali mbalimbali. 

Kitunguu  hiki  kina madini mchanganyiko ya salfa ambayo hukifanya kuwa na harufu kali. 'Alicin' ikiwa ni moja ya mchanganyiko huu ina nguvu  ya kupambana na virusi, bakteria, fangasi na  seli  kali (radical cells)

Kitunguu hiki ni chanzo cha kuaminika cha 'selenium' na 'allicin' Pamoja na 'viini mimea tiba'(phytochemicals) vingine  kama 'ajoene', 'alliin', nk.


Viini mimea tiba hivi hukifanya kitunguu swaumu kuwa  na uwezo wa  kuondoa athari kwenye mzunguko wa damu, mfumo wa chakula, mfumo wa fahamu, kupunguza shinikizo la damu,  kuondoa sumu mwilini na mengine mengi. 


Nyama inapendwa na wengi lakini nyama nzuri ni ile iliyokaushwa. Kama ni kuku  awe ni wa kienyeji kwani yeye hakuzwi kwa madawa. Epuka samaki waliovuliwa kwa sumu.


Kumbuka afya bora hujengwa haiji yenyewe.Na hakuna maradhi yasiyo na tiba.Tatizo ni kutojua tiba husika ya ugonjwa.

0 comments:

POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza