Familia za Abiria wa Ndege ya Malaysia Iliyotoweka Waandamana Wakiitaka Kuala Lumpar kutoe Maelezo.


Familia za abiria wa ndege iliyotoweka ya Malaysia wakiandamana wakiwa wamebeba mabango.
Licha ya kwamba ni haramu kufanya maandamano ya umma nchini China  familia za abiria wa ndege iliyotoweka ya Malaysia majuma mawili yaliyopita, wamekabiliana na polisi nje ya ubalozi wa Malaysia   leo hii jijini Beijing.

Maandamano ya umma ni haramu nchini China, lakini hadi kufikia watu hawa kupanga maandamano kama haya ni ishara kuwa hawana kilichobakia kuwapa matumaini kabisa.

Wakiwa wamejawa na ghadhabu, na wakiwa na mabango, wanalitaka shirika la ndege la Malaysia mjini Kuala Lumpur kueleza kilichofanyika na kinachoendelea hadi sasa.

 Mabango yalikuwa na maandishi yaliyoandikwa "Save MH370" .Jamaa hawa wa ndugu wanaosadikiwa kupotea na ndege hii, wakiwa na  hasira walikabiliana na polisi na kuwalemea hadi kuingia katika ofisi ya ubalozi huo.

Wakiwa wanafoka kwa hasira kali walisema ..''Tunataka ukweli." huku nyuso na maneno yao yakionesha ishara ya hasira na mfadhaiko wanaoupata kwa kupotelewa na jamaa zao.

Hasira za jamaa hawa zinakuja baada ya waziri mkuu wa Malaysia, Najib Razak kusema udadisi wa data ya Setiliti unaonyesha kuwa safari ya ndege hiyo iliishia baharini Kusini mwa Australia.

Serikali ya China imeomba kuona data hiyo ambayo Malaysia inaiamini kiasi cha kutoa msimamo kama huo..

Hata hivyo kwa sasa msako wa ndege hiyo MH370 umesitishwa  kwa muda kutokana na mawimbi makali baharini

Mataifa mbali mbali yalijitolea kusaidia Malaysia kuitafuta ndege hiyo, juhudi ambazo zililengwa zaidi katika bahari ya Kusini Magharibi mwa mji wa Australia Perth.

Wiki iliyopita China ilidai kuona chombo  kinachodhaniwa kimedondoka kutoka  kwenye ndege hiyo katika maeneo yanayodaiwa ndege hiyo kupotea lakini hadi sasa  uchunguzi huo haujaonesha mafanikio yeyote
 .
Ndege hiyo MH370 ilipotea tarehe  8 Machi, 2014 ilipokuwa njiani kuelekea Beijing kutoka Kuala Lumpar ikiwa imebeba abiria 239 wakiwemo raia 153 wa China.

Maandamano ya umma ni haramu nchini China, lakini hadi kufikia watu hawa wakapanga maandamano kama hayo ni ishara kuwa hawana kilichobakia kuwapa matumaini kabisa.

Wimbi la  matukio ya ajali kubwa za ndega lilikuwa limesahaulika kidogo ila sasa linaanza kutokea na kufanya safari za ndege kutiliwa hofu na wasafiri.
Tunashauri mashirika ya ndege yaongeze  hadhari zaidi  katika katika ndege zao na kwenye viwanja vya ndege.

0 comments:

POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza