Heri ya Pasaka. 
UJUMBE MZITO WA PAPA FRANCIS
Hakuna familia isiyo na mapungufu. Hatuna wazazi wasio na mapungufu, sisi pia si wakamilifu, hatuoi au kuolewa na mtu asiye na mapungufu, kadhalika watoto wetu nao si wakamilifu. Tunayo manung'uniko au malalamiko kila mmoja dhidi ya mwenzake. Tumevunjana moyo na kukatishana tamaa. Kwa hiyo, hakuna ndoa iliyokamilika wala familia iliyoboreka bila kuwa na mazoea au utamaduni wa kusameheana.

Msamaha ni nguzo au msingi wa utulivu wa akili na uhai wa roho zetu. Kama hakuna msamaha, familia inakuwa uwanja wa migogoro na mlipuko wa ugomvi. Panapokosekana msamaha, familia inaugua. Msamaha unahuisha moyo, kwa kusafisha fikra na kuufanya moyo kuwa huru. Binadamu asiyesamehe hana amani moyoni na wala hana urafiki au muunganiko na Mungu.

Maumivu ni sumu inayodhuru na kuua. Hebu kiponye kidonda hicho cha moyo endapo kuna dalili za kujiumiza. Mtu asiyesamehe anajisababishia mwenyewe ugonjwa wa mwili, kiakili na kiroho. Ndiyo maana familia inapaswa kuwa sehemu ya uhai na si kifo; eneo la uponyaji na sio mahali pa magonjwa; jukwaa la msamaha na si la uovu. Msamaha huleta furaha pale uchungu ulipoleta maumivu; huleta uponyaji hata pale ambapo maumivu yalisababisha magonjwa.

Ujumbe huu wa Baba Mtakatifu umfikie kila mmoja wetu leo katika familia yake. Leo basi tuutafakari ujumbe huo muhimu.

Ewe  Mwenyezi Mungu Tusamehe makosa yetu tunayoyajua na yale tusiyoyajua, Aamin.

Muhimu:Kauli hii haimlengi mtu fulani , bali ni mafundisho kwa  mimi mwenyewe  na jamii yote kwa ujumla.
METHALI MIA SITA NA KUMI (610)
1. Aanguaye huanguliwa.
2. Asiye sikia la mkuu, huvunjika guu.
3. Abebwaye hujikaza.
4. Adhabu ya kaburi aijuae maiti.
5. Adui aangukapo, mnyanyue.
6. Adui mpende.
7. Adui wa mtu ni mtu.
8. Afadhali ya Musa kuliko ya Firauna.
9. Ahadi ni deni.
10. Ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke.
11. Akiba haiozi.
12. Akili ni mali.
13. Akili ni nywele kila mtu ana zake.
14. Akili nyingi huondowa maarifa.
15. Akutukanae hakuchagulii tusi.
16. Akipenda chongo huita kengeza.
17. Akufaae kwa dhiki, ndiye rafiki.
18. Akufanyiaye ubaya, mlipe wema.
19. Akupaye kisogo si mwenzio.
20. Akutendaye mtende, mche asiyekutenda.
21. Alisifuye jua, limeuangaza.
22. Aliye juu msubiri chini.
23. Aliye kando, haangukiwi na mti.
24. Aliye kupa wewe kiti (kibao) ndiye aliye nipa mimi kumbi.
25. Aliye kutwika, ndiye atakaye kutua.
26. Akufukuzae hakwambii toka.
27. Aliyekupa mkeka ndiye aliyenipa kumbesa.
28. Amani haipatikani mpaka kwa ncha ya upanga.
29. Ana hasira za mkizi.
30. Anayekuja pasi na hodi, huondoka bila ya kuaga.
31. Angurumapo simba, mcheza ni nani?
32. Aninyimaye mbazi kanipunguzia mashuzi.
33. Apewaye ndiye aongezwaye.
34. Anaejipiga mwenyewe, halii.
35. Asifuye mvuwa imemnyea.
36. Asiye kubali kushindwa si mshindani.
37. Asiye kujua, hakuthamini.
38. Asiye kuwapo na lake halipo.
39. Asiye lelewa na mamae hulelewa na ulimwengu.
40. Asiye na mengi, ana machache.
41. Asiye uliza, hanalo ajifunzalo.
42. Asiyejua maana, haambiwi maana.
43. Atangaye na jua hujuwa.
44. Atangazaye mirimo, si mwana wa ruwari (Liwali).
45. Atekaye maji mtoni hatukani mamba.
46. Avumaye baharini papa kumbe wengi wapo.
47. Baada ya dhiki faraja.
48. Bahari hailindwi.
49. Bamba na waume ni bamba, hakuna bamba la mume.
50. Bandu bandu huisha gogo.
51. Baniani mbaya, kiatu chake dawa.
52. Bendera hufuata upepo.
53. Biashara asubuhi.
54. Bilisi wa mtu ni mtu.
55. Bora kinga kuliko tiba.
56. Bora lawama kuliko fedheha.
57. Bora mchawi kuliko fitina.
58. Biashara asubuhi.
59. Bora nusu shari kuliko shari kamili.
60. Bwawa limeingia ruba.
61. Cha mtu mavi.
62. Chaka la samba, halilali nguruwe.
63. Chamlevi huliwa na mgema.
64. Chanda chema huvikwa pete.
65. Chelewa chelewa, utakuta mtoto si wako.
66. Choko mchokoe pweza, binaadamu hutomuweza.
67. Chombo cha kuzama hakina usukani.
68. Chovya - chovya yamaliza buyu la asali.
69. Chui hakumbatiwi.
70. Chururu si ndo ndo ndo.
71. Dalili ya mvua mawingu.
72. Damu nzito kuliko maji.
73. Daraja livuke ulifikapo.
74. Dawa ya moto ni moto.
75. Daraja ukilibomoa, ujue kuogelea.
76. Dau la mnyonge haliendi joshi, likienda joshi ni matakwa ya Mungu.
77. Dawa ya moto ni moto.
78. Donda ndugu halina dawa.
79. Dua ya kuku haimpati mwewe.
80. Fadhila huna, hata hisani hukumbuki?
81. Fadhila ya nyuki ni moto.
82. Fadhila ya punda ni mateke (mashuz)
83. Fahari ya macho haifilisi duka.
84. Farasi hamuwawezi, tembo mtawalishani?
85. Fata nyuki ule asali.
86. Fimbo ya mbali haiui nyoka.
87. Fumbo mfumbe mjinga, mwerevu huligangua.
88. Funika kombe mwanakharamu apite.
89. Ganda la mua la jana, chungu kaona kivuno.
90. Gome la udi, si la mnuka uvundo.
91. Haba na haba, hujaza kibaba.
92. Haki ya mtu hailiki.
93. Hakuna masika yaso mbu.
94. Hakuna msiba usio na mwenziwe.
95. Hakuna siri ya watu wawili.
96. Hakuna ziada mbovu.
97. Hala hala mti na macho.
98. Hamadi ni ilio kibindoni, na silaha ni iliyo mkononi.
99. Hapana marefu yasio na mwisho.
100. Haraka haraka haina baraka.
101. haraka haraka haina baraka.
102. Haramu yako halali kwa mwenzio.
103. Hasidi hasada.
104. Hasidi mbaya.
105. Hasira, hasara.
106. Hatua ndefu hufupisha mwendo.
107. Hauchi hauchi, unakucha.
108. Hayawi hayawi, mara huwa.
109. Heri kufa macho kuliko kufa moyo.
110. Heri kujikwa kidole kuliko ulimi.
111. Heri nitakula na nini?, kuliko nitakula nini?
112. Heri ya marama kuliko kuzama.
113. Hiari ya shinda utumwa.
114. Hogo halihogoki mpaka kwa hogo jenziwe.
115. Hucheka kovu asiye kuwa na jeraha.
116. Ila ya kikwapa, kunuka pasipo kidonda.
117. Yaliyoopita si ndwele, ganga yajayo.
118. Iliyo jaa ndiyo ipunguzwayo.
119. Imara ya jembe kaingojee shambani.
120. Jambo usilolijua, usiku wa giza.
121. Jina jema hungara gizani.
122. Jini likujualo halikuli likakwisha.
123. Jino la pembe si dawa ya pengo.
124. Jitihada haiondoi kudura.
125. Jitihadi haiondoi kudura.
126. Jogoo la shamba haliwiki mjini.
127. Jungu kuu, halikosi ukoko.
128. Jununu fununu.
129. Kafiri akufaaye, si muislamu asiye kufaa
130. Kafiri akufaye si Isilamu asiyekufa.
131. Kama hujui kufa,tazama kaburi.
132. Kama wewe wasema cha nini, mwezio asema nitakipata lini.
133. Kamba hukatika pabovu.
134. Kanga hazai ugenini.
135. Kawaida ni kama sheria.
136. Kawia ufike.
137. Kazi mbaya siyo mchezo mwema.
138. Kelele za chura hazimzuwii ng'ombe kunywa maji.
139. Kelele za mlango haziniwasi usingizi (Kelele za mlango hazimuudhi mwenye nyumba)
140. Kenda karibu na kumi.
141. Kesho kesho, kesho kiama.
142. Kiburi si maungwana.
143. Kibuzi na kibuzi hununua jahazi.
144. Kichango kuchangizana.
145. Kidole kimoja hakivunji chawa.
146. Kikulacho ki nguoni mwako.
147. Kikushindacho kukila usikitie ila.
148. Kila chombo kwa wimblile.
149. Kila mbwa hubwekea mlangoni kwao.
150. Kila mlango na ufunguwo wake.
151. Kila mtoto na koja lake.
152. Kila mtu huzikwa na kaburi lake.
153. Kila mtu na bahati yake.
154. Kila mwamba ngoma ,ngozi huivuta kwake.
155. Kila mtu hulilia mamae.
156. Kila ndege huruka kwa ubawa wake.
157. Kila shetani na mbuyu wake.
158. Kilimia kikizama kwa jua, huzuka kwa mvua, na kikizama kwa mvua, huzuka kwa jua.
159. Kilio huanza mfiwa ndipo wa mbali wakaingia.
160. Kimya kingi kina mshindo mkubwa.
161. Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.
162. Kingiacho mjini si haramu.
163. Kinyozi hajinyoi.
164. Kinywa ni jumba la maneno.
165. Kipendacho moyo dawa.
166. Kipofu hasahau mkongojo wake.
167. Kipya kinyemi ingawa kidonda.
168. Kisebusebu na kiroho papo.
169. Kisokula mlimwengu, sera nale.
170. Kisokula mlimwengu,sera nale.
171. Kisu kimenifika mfupani.
172. Kitanda usicho kilalia hukijui kunguni wake.
173. Kitumbua kimeingia mchanga.
174. Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua.
175. Kiwi cha yule ni chema cha; hata ulimwengu uwishe.
176. Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
177. Konzi ya maji, haifumbatiki.
178. Konzo ya maji haifumbatiki.
179. Kosa moja haliachi mke.
180. Kozi mwandada, kulala na njaa kupenda.
181. Kuagiza kufyekeza.
182. Kuambizana kuko kusikilizana hapana.
183. Kucha M'ngu si kilemba cheupe.
184. Kuchamba kwingi, kuondoka na mavi.
185. Kufa kufaana.
186. Kufa kwa jamaa, harusi.
187. Kufa kwa mdomo,mate hutawanyika.
188. Kufanaya kosa sio kosa, kosa ni kurudia kosa.
189. Kuishi kwingi, kuona mengi.
190. Kujikwa si kuanguka,bali ni kwenda mbele.
191. Kujikwaa si kuanguka, bali ni kwenda mbele.
192. Kukopa harusi kulipa matanga.
193. Kukopa harusi, kulipa matanga.
194. Kuku havunji yai lake.
195. Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
196. Kula kutamu ,kulima mavune.
197. Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana.
198. Kukopa harusi, kulipa matanga.
199. Kumuashia taa kipofu ni kuharibu mafuta.
200. Kunako matanga kume kufa mtu.
201. Kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake.
202. Kupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma.
203. Kupata si werevu, na kukosa si ujinga.
204. Kupoteya njia ndiyo kujua njia.
205. Kurambaramba ndio kula, kunenepa kwake Mola.
206. Kusikia si kuona.
207. Kutangulia si kufika.
208. Kutoa ni moyo usambe ni utajiri.
209. Kutu kuu ni la mgeni.
210. Kuugua sio kufa.
211. Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi.
212. Kuzima koleo si mwisho wa uhunzi.
213. Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio.
214. Kweli ilio chungu, si uongo ulio mtamu.
215. Kwenda mbio siyo kufika.
216. Kwenye miti hakuna wajenzi.
217. La kuvunda halina rubani.
218. La kuvunda halina ubani.
219. Lake mtu halimtapishi bali humchefua.
220. Leo kwako, kesho kwa mwenzio.
221. Leo ni leo asemayo kesho ni mwongo.
222. Liandikwalo ndiyo liwalo.
223. Lila na fila hazitangamani.
224. Lipitalo, hupishwa .
225. Lisemwalo lipo,ikiwa halipo laja.
226. Lisilo na mkoma, hujikoma lilo.
227. Lisilokuwapo moyoni, halipo machoni.
228. Maafuu hapatilizwi.
229. Macho hayana pazia.
230. Mafahali wawili hawakai zizi moja.
231. Maiti haulizwi sanda.
232. Maji hayapandi mlima.
233. Maji hufuata mkondo.
234. Maji ukiyavuliya nguo huna budi kuyaoga.
235. Maji usiyoyafika hujui wingi wake.
236. Maji ya kifuu, bahari ya chungu.
237. Maji yakijaa hupwa.
238. Maji yakimwagika hayazoleki.
239. Maji yamenifika shingoni.
240. Majuto ni mjukuu.
241. Mali ya bahili huliwa na wadudu.
242. Mama ni mama, hata kama ni rikwama.
243. Mama nipe radhi kuishi na watu kazi.
244. Mambo kunga.
245. Manahodha wengi chombo huenda mrama.
246. Maneno makali hayavunji mfupa.
247. Maneno mazuri humtowa nyoka pangoni.
248. Maneno si mkuki.
249. Mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichika.
250. Masikini akipata matako hulia mbwata.
251. Masikini haokoti,akiokota huambiwa kaiba.
252. Masikini na mwanawe tajiri na mali yake.
253. Maskini hana kinyongo.
254. Mavi usioyala, wayawingiani kuku?
255. Mavi ya kale hayanuki.
256. Mbinu hufuata mwendo.
257. Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
258. Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo.
259. Mchagua jembe si mkulima.
260. Mchagua nazi hupata koroma.
261. Mchagua nazi si mfuaji.
262. Mchakacho ujao,halulengwi na jiwe.
263. Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo.
264. Mchamba kwingi mara ujitia dole.
265. Mcheka kilema hafi bila kumpata.
266. Mchele mmoja mapishi mengi.
267. Mchelea mwana kulia hulia yeye..
268. Mcheza hawi kiwete, ngoma yataka matao.
269. Mcheza kwao hutuzwa.
270. Mcheza na tope humrukia.
271. Mchezea mavi, hayaachi kumnuka.
272. Mchezea zuri, baya humfika.
273. Mchimba kisima hungia mwenyewe.
274. Mchonga mwiko hukimbiza mkono wake.
275. Mchuma janga hula na wakwao.
276. Mchumia juani,hulia kivulini.
277. Mdharau biu, hubiuka yeye.
278. Mdharau mwiba humchoma.
279. Meno ya mbwa hayaumani.
280. Mfa maji haachi kutapatapa.
281. Mfa maji hukamata maji.
282. Mficha uchi hazai.
283. Mfinyazi hulia gaeni.
284. Mfuata nyuki hakosi asali.
285. Mfukuzwa kwao hana pakwenda.
286. Mgaagaa na upwa hali ugari kande.
287. Mganga hajigangi.
288. Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.
289. Mgeni ni kuku mweupe.
290. Mgeni njoo mwenyeji apone.
291. Mgomba haushindwi na mkunguwe.
292. Mgonjwa haulizwi uji.
293. Miye nyumba ya udongo, sihimili vishindo.
294. Mjinga akierevuka mwerevu yupo mashakani.
295. Mjinga mpe kilemba utamuona mwendowe.
296. Mjumbe hauawi.
297. Mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi.
298. Mkamatwa na ngozi ndiye mwizi.
299. Mkamia maji hayanywi.
300. Mkamia maji hayanywi.
301. Mkataa la mkuu huvunjika guu.
302. Mkataa wengi ni mchawi.
303. Mkataa ya Musa hupata ya Firauna.
304. Mke ni nguo, mgomba kupalilia.
305. Mkono moja hauchinji ng'ombe.
306. Mkono moja haulei mwana.
307. Mkono mtupu haulambwi.
308. Mkono usioweza kuukata,ubusu.
309. Mkosa kitoweo humangiria.
310. Mkuki kwa nguruwe, kwa mwanadamu uchungu.
311. Mkulima ni mmoja walaji ni wengi.
312. Mla cha mwenziwe na chake huliwa.
313. Mla cha uchungu na tamu hakosi.
314. Mla kuku wa mwenziwe miguu humwelekea.
315. Mla mbuzi hulipa ngombe.
316. Mla mla leo mla jana kala nini?
317. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
318. Mlala na maiti haachi kulia lia.
319. Mlenga jiwe kundini hajui limpataye.
320. Mlimbua nchi ni mwananchi.
321. Mnyamaa kadumbu.
322. Mnywa maji kwa mkono mmoja,Kiu yake i pale pale.
323. Moja shika, si kumi nenda urudi.
324. Moto hauzai moto.
325. Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
326. Mpanda ngazi hushuka.
327. Mpanda ovyo hula ovyo.
328. Mpemba akipata gogo hanyii chini.
329. Mpemba hakimbii mvua ndogo.
330. Mpende akupendae asiyekupenda achana naye.
331. Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe.
332. Mpofuka ukongweni,hapotewi na njia.
333. Msafiri kafiri.
334. Msafiri masikini ajapokuwa sultani.
335. Msasi haogopi mwiba.
336. Msema kweli hukimbiwa na rafiki zake.
337. Msema pweke hakosi.
338. Mshika kisu, hashiki makalini.
339. Mshale kwenda msituni haukupotea.
340. Mshoni hachagui nguo.
341. Msi bahati, habahatishi.
342. Msi mbele, hana nyuma.
343. Msishukuru mja, hamshukuru Molawe.
344. Msitukane wagema na ulevi ungalipo.
345. Msitukane wakunga na uzazi ungalipo.
346. Mstahimilivu hula mbivu.
347. Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
348. Mtaka lake hasindwi.
349. Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba.
350. Mtaka unda haneni.
351. Mtaka uzuri hudhurika.
352. Mtaka yote hukosa yote.
353. Mtegemea nundu haachi kunona.
354. mtegemea nundu, haachi konona.
355. Mtego bila ya chambo, haunasi.
356. Mtembezi hula miguu yake.
357. Mteuzi heshi tamaa.
358. Mti hauwendi ila kwa nyenzo.
359. Mtondoo haufi maji.
360. Mtoto akililia wembe mpe.
361. Mtoto umleyavyo ndivyo akuavyo.
362. Mtoto wa nyoka ni nyoka.
363. Mtu hakatai mwito,hukata aitwalo.
364. Mtu hujikuna ajipatapo.
365. Mtu huulizwa amevaani ,haulizwi amekulani.
366. Mtumai cha ndugu hufa masikini.
367. Mtumi wa kunga haambiwi maana.
368. Mtumikie kafiri upate mradi wako.
369. Mtupa jongoo hutupa na mti wake.
370. Muhitaji khanithi walau kana rijaali.
371. Muiba yai leo kesho hua mwizi wa ng'ombe.
372. Mume wa mama ni baba.
373. Mungu hamfichi mnafiki.
374. Mungu si asumani.
375. Muonja asali haonji mara moja.
376. Muuza sanda, mauti kwake harusi.
377. Mvua nguo, huchutama.
378. Mvumbika changa hula mbovu.
379. Mvumbika pevu hula mbivu na mvumbika changa hula mbovu.
380. Mvungu mkeka.
381. Mvunja nchi ni mwananchi.
382. Mvuvi ajuwa pweza alipo.
383. Mwacha asili ni mtumwa.
384. Mwamba na wako hukutuma umwambiye.
385. Mwamini Mungu si mtovu.
386. Mwana maji wa kwale kufa maji mazowea.
387. Mwana mkuwa nawe ni mwenzio kama wewe.
388. Mwana simba ni simba.The child of lion is a lion.
389. Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura.
390. Mwana wa mtu ni kizushi, akizuka, zuka naye.
391. Mwanga mpe mtoto kulea.
392. Mwangaza mbili moja humponyoka.
393. Mwanzo kokochi mwisho nazi.
394. Mwanzo wa chanzo ni chane mbili.
395. Mwanzo wa ngoma ni lele.
396. Mwapiza la nje hupata la ndani.
397. Mwekaji kisasi haambiwi mwerevu.
398. Mwenda bure si mkaa bure,huenda akaokota.
399. Mwenda mbio hujikwa kidole.
400. Mwenda omo na tezi marejeo ni ngamani.
401. Mwenda pole hajikwai.
402. Mwenda wazimu hapewi panga.
403. Mwenda wazimu hapoi, bali hupata nafuu.
404. Mwenye haja hwenda chooni.
405. Mwenye kelele hana neno.
406. Mwenye kovu usidhani kapowa.
407. Mwenye kubebwa hujikaza.
408. Mwenye kuchinja hachelei kuchuna.
409. Mwenye kuumwa na nyoka akiona jani hushtuka.
410. Mwenye macho haambiwi tazama.
411. Mwenye mdomo hapotei.
412. Mwenye nguvu mpishe.
413. Mwenye njaa hana miko.
414. Mwenye pupa hadiriki kula tamu.
415. Mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
416. Mwenye shoka hakosi kuni.
417. Mwenye tumbo ni tumbole, angafunga mkaja.
418. Mwenzako akinyolewa wewe tia maji.
419. Mwibaji na watwana, mlifi ni mwungwana.
420. Mwili wa mwenzio ni kando ya mwilio.
421. Mwizi hushikwa na mwizi mwenziwe.
422. Mwomba chumvi huombea chunguche.
423. Mwosha hadhuru maiti.
424. Mwosha huoshwa.
425. Mwosha husitiri maiti.
426. Mzaha,mzaha, mara hutumbuka usaha.
427. Mzazi haachi ujusi.
428. Mzigo usiouweza unaubebea nini?
429. Mzigo Wa mwenzio ni kanda Ia usufi.
430. Mzika pembe ndiye mzua pembe.
431. Mzowea kutwaa, kutoa ni vita.
432. Mzowea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi.
433. Mzungu Wa kula hafundishwi mwana.
434. Nahodha wengi, chombo huenda mrama.
435. Nani kama mama?
436. Natuone ndipo twambe, kusikia Si kuona.
437. Nazi haishindani na jiwe.
438. Nazi mbovu harabu ya nzima.
439. Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu.
440. Ndege mwigo hana mazowea.
441. Ndevu sio shani, hata beberu anazo.
442. Ndugu chungu, jirani mkungu.
443. Ndugu mwui afadhali kuwa naye.
444. Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime, wakipatana chukua kikapu ukavune.
445. Ngoja! ngoja? huumiza matumbo.
446. Ngoma ivumayo haidumu.
447. Ngoma ivumayo haikawii kupasuka.
448. Ngoma ya kitoto, haikeshi.
449. Ng'ombe avunjikapo guu hurejea zizini.
450. Ng'ombe haelemewi na nunduye.
451. Ngombe wa Maskini hazai.
452. Ngozi ivute ili maji. ( Udongo upate uli maji )
453. Nguo ya kuazima, Haistiri matako.
454. Nia njema ni tabibu, nia mbaya huharibu.
455. Nifae na mvua nikufae na jua.
456. Nimekula asali udogoni, utamu ungali gegoni.
457. Nimekupaka wanja, wewe wanipaka pilipili.
458. Nimerejesha kikombe na kisahani chake.
459. Njia ya muongo fupi.
460. Njia ya mwongo ni fupi.
461. Njia ya siku zote haina alama.
462. Nta Si asali; nalikuwa nazo Si uchunga.
463. Nyani haoni kundule, huliona la mwenziwe.
464. Nyani haoni kundule.
465. Nyimbo mbaya haibembelezewi mtoto.
466. Nyimbo ya kufunzwa haikeshi ngoma.
467. Nyongeza huenda kwenye chungu.
468. Nyota njema huonekana asubuhi.
469. Nyumba usiyolala ndani huijui ila yake.
470. Nyumba ya udongo haihimili vishindo.
471. Nzi kufa juu ya kidonda Si haramu. (Jihadi ya nzi, kufa kidondani)
472. Ondoa dari uwezeke paa.
473. Pabaya pako Si pema pa mwenzako.
474. Padogo pako Si pakubwa pa mwenzako.
475. Painamapo ndipo painukapo.
476. Paka akiondoka, panya hutawala.
477. Paka hakubali kulala chali.
478. Paka hashibi kwa wali, matilabaye ni panya.
479. Paka wa nyumba haingwa.
480. Panapo wengi hapaharibiki neno.
481. Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
482. Pele hupewa msi kucha.
483. Pema usijapo pema; ukipema Si pema tena.
484. Penye kuku wengi usimwage mtama.
485. Penye mafundi, hapakosi wanafunzi.
486. Penye mbaya wako, hapakosi mwema wako/na mwema wako hakosi.
487. Penye miti hakuna wajenzi.
488. Penye nia pana njia.
489. Penye urembo ndipo penye urimbo.
490. Penye wazee haliharibiki neno.
491. Penye wengi pana mengi.
492. Penye wengi pana Mungu.
493. Pilipili usoila, wewe inakuwashia nini?
494. Pole pole ndio mwendo.
495. Pwagu hupata pwaguzi.
496. Radhi ni bora kuliko mali .
497. Radhi za wazee, ni fimbo.
498. Sahani iliyofunikwa, kilichomo kimesitirika.
499. Sahau ni dawa ya Waja.
500. Samaki mmoja akioza, huoza wote.
501. Samaki mpinde angali mbichi.
502. Shida haina hodi.
503. Shida huzaa maarifa.
504. Shika! Shika! na mwenyewe uwe nyuma.
505. Shimo Ia ulimi mkono haufutiki.
506. Shoka lisilo mpini halichanji kuni.
507. Si kila king'aacho ni dhahabu.
508. Si kila mwenye makucha huwa simba.
509. Si Mungu mtupu na mkono wa mtu.
510. Sikio halilali na njaa.
511. Sikio halipwani kichwa. (Sikio halipiti kichwa).
512. Sikio Ia kufa halisikii dawa.
513. Siri ya mtungi aijuaye ni kata.
514. Sitaacha kula mkate kwa kuogopa kiungulia.
515. Siku njema huonekana asubuhi.
516. Siku utakayokwenda uchi, ndiyo siku utakayokutana na mkweo.
517. Siku ya kufa nyani, miti yote huteleza.
518. Siku za mwizi, arubaini.
519. Simba mwenda kimya (pole) ndiye mla nyama.
520. Simbiko haisimbuki ila kwa msukosuko.
521. Sio shehe bali ni shehena.
522. Siri ya maiti aijuaye muosha.
523. Sitafuga ndwele na waganga tele.
524. Sitapiki nyongo harudi haramba.
525. Subira ni ufunguo Wa faraja.
526. Sumu mpe paka, mbuzi utamdhulumu.
527. Sumu ya neno ni neno.
528. Tabia ni ngozi ya mwili.
529. Tamaa mbele, mauti nyuma.
530. Taratibu ndio mwendo.
531. Tawi kavu kuanguka si ajabu.
532. Teke Ia kuku halimuumizi mwanawe
533. Tonga si tuwi
534. Tunda jema halikawii mtini.
535. Ucheshi wa mtoto ni anga Ia nyumba.
536. Ujuzi hauzeeki.
537. Uchungu wa mwana, aujue mzazi.
538. Udongo uwahi ungali maji (Udongo upate uli maji)
539. Udugu wa nazi hukutania chunguni (Udugu wa nazi hukutana pakachani)
540. Uji hajauonja, tayari ushamuunguza
541. Ukenda kwa wenye chongo, fumba lako jicho.
542. Ukimpa shubiri huchukua pima.
543. Ukimuiga tembo kunya, utapasuka Makalio.
544. Ukimwamsha alolala utalala weye.
545. Ukinyofoa mnofu, ukumbuke kuguguna mfupa.
546. Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzako kunateketea.
547. Ukiona moshi, chini kuna moto.
548. Ukiona neno, usiposema neno, hutapatikana na neno.
549. Ukiona vinaelea, vimeundwa.
550. Ukiona zinduna, na ambari iko nyuma.
551. Ukistahi mke ndugu, huzai nae.
552. Ukitaja nyoka, shika fimbo mkononi.
553. Ukitaka kula nguruwe, chagua aliye nona.
554. Ukitaka salama ya dunia, zuia ulimi wako.
555. Ukiujua wa mbele, nina ujua wa nyuma.
556. Ukupigao ndio ukufunzao.
557. Ukuukuu wa kamba Si upya wa ukambaa.
558. Ulimi hauna mfupa.
559. Ulimi unauma kuliko meno.
560. Ulipendalo hupati, hupata ujaaliwalo.
561. Ulivyoligema, utalinywa.
562. Umeadimika kama la jogoo.
563. Umegeuka mung'unye waharibika ukubwani.
564. Umejigeuza pweza, unajipalia makaa?
565. Umekuwa bata akili kwa watoto?
566. Umekuwa nguva, huhimili kishindo?
567. Umeruka mkojo unakanyaga mavi.
568. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
569. Unajenga kwa mwenzio na kwako kunaporomoka!!
570. Unakuja juu kama moto wa kifuu.
571. Unamlaumu mwewe, kipanga yuwesha kuku.
572. Ungalijua alacho nyuki, usingalionja asali.
573. Ushikwapo shikamana (Ukibebwa usijiachie).
574. Usiache kunanua kwa kutega.
575. Usiache mbachao kwa msala upitao.
576. Usiache tawi kabla ya kushika tawi.
577. Usiandikie mate na wino ungalipo
578. Usicheze na simba, ukamtia mkono kinywani.
579. Usijifanye kuku mweupe.
580. Usikaange mbuyu ukawaachia wenye meno
581. Usile na kipofu ukamgusa rnkono.
582. Usimgombe mkwezi, nazi imeliwa na mwezi.
583. Usiniache njia panda.
584. Usinikumbushe kilio matangani.
585. Usinipake mafuta kwa nyuma ya chupa.
586. Usinivishe kilemba cha ukoka.
587. Usione simba kapigwa na mvua.
588. Usipoziba ufa utajenga ukuta.
589. Usisafirie nyota ya mwenzio.
590. Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha.
591. Usishindane na Kari; Kari ni mja wa Mungu.
592. Usitukane wagema na ulevi ungalipo.
593. Usitukane wakunga na uzazi 'ungalipo.
594. Utakosa mtoto na maji ya moto.
595. Usiyavuke maji usiyoweza kuyaoga.
596. Utaula na chua kwa uvivu wa kuchagua.
597. Vita havina macho.
598. Vita si lele mama.
599. Vita vya panzi, neema ya kunguru
600. Waarabu wa pemba, hujuana kwa vilemba
601. Wache waseme.
602. Wafadhilaka wapundaka.
603. Wagombanao ndio wapatanao.
604. Watu wanahisabu nazi, wewe unahisabu makoroma.
605. Wapiganapo tembo wawili ziumiazo ni nyasi.
606. Watetea ndizi, mgomba si wao.
607. Wazuri haweshi.
608. Wema hauozi..
609. wengi wape.
610. Zinguo la mtukufu, ni ufito.
Kamusi ni hazina la lugha
METHALI, NAHAU NI VIPERA VYA SEMI.
                (Fasihi Simulizi)
Fasihi simulizi ina tanzu zake na Semi ni moja ya tanzu zake. Utanzu huu nao una VIPERA vyake ambayo ni methali, nahau, misemo, simo, vitanza ndimi, vichezea meno na mgafumbo ambayo hujumuisha vitendawili, chemsha bongo, malumbo na mizungu.

Katika somo hili nitaelezea kwa kifupi maana na kutoa mifano ya Methali na Nahau na kuonesha ukaribu wa nahau, misemo na methali.

Methali na nahau zote ni
 semi zitumiazo lugha fupi fupi na ya mkato.

Methali
Maana.
Methali ni usemi wa kimapokeo, japo zipo methali zinazozaliwa kila wakati na nyingine kufa. ambao unaotumiwa kwa kufumbia jambo kwa maneno ya kawaida bali kwa njia ya mkato huku ukibainisha ukweli au kutolea ushauri kwa kulenga kwa usahihi kile kinachozungumziwa.

Kwa ufupi methali ni kauli inayobeba busara au falsafa za jamii husika.

Mifano ya methali za kimapokeo ni:
i. Pema usijapo pema ukipema si pema tena.
ii. Kozi mwana mandanda kulala njaa kupenda.
iii. Mwenda omo na tezi marejeo ni ngamani.
iv. Mwapiza la nje hupata la ndani.
v. Macho hayana pazia.
vi. Ukilima pakubwa ukivuna pamekwisha.

Mifano ya methali zilizozaliwa hivi karibuni kwa uchache ni:
i. Usiteme 'big G' yako kwa karanga za kuonjeshwa.
ii.Ukilima shamba njiani ujue kulinda ndege.
iii.Ukitaka kujua mwenendo wa mjinga mvishe kilemba.
iv. Kiyoo cha gari hakifungwi katika tairi ya gari
v. Ama kweli kama hujui unakokwenda huwezi kupotea.
 vi. Akimbiaye peke yake siku zote yeye ni mshindi.
vii. Usiku rafikiye ni giza.l

Misemo
Maana
Msemo ni fungu la maneno lenye maana mahsusi lenye  kutoa fundisho ama kuelezea dhana fulani kwa j amii lisilo na kitenzi ndani yake.

Wengi huchanganya misemo na nahau. Tofauti kubwa kati ya tungo hizi ni kitenzi. Nahau huwa na kitenzi lakini msemo hauna kitenzi ndani yake

Ifuatayo ni mifano michache ya misemo ya Kiswahili na maana zake:
i. Mkono wa birika=mchoyo
ii. Sindano na uzi. =ushirikiano au umoja
iii. Kiti moto=nyama ya nguruwe  au misukosuko ya madaraka.
iv. Hamadi kibindoni=akiba uliyo nayo mkononi.
v. Mwana haramu= mtoto wa nje ya ndoa.
vi. Kiwi cha macho= tamaa ya mapenzi.
viii. Mkono mrefu = mwizi
viii. Akali ya watu= watu wachache.
ix. Umti wa watu = watu wengi.

Katika mkutadha wa maongezi aghalabu misemo huongezewa kitenzi na kutenda kazi ya nahau lakini maana hubakia kuwa ile ile ya awali.

Nahau
Maana
Usemi mfupi ulio na kitenzi unaotumia maneno ya kikawaida, lakini yakiwa na maana iliyojificha na iliyotofauti na maana ya maneno hayo.
mfano:
i). Kujikaza kisabuni = kutia bidii,
ii).kuvaa miwani = kulewa,
iii).Kuoga mwaka= kusherehekea kumaliza mwaka kwa salama.

 Zifuatazo ni nahau maarufu za lugha ya Kiswahili. Kila lugha ina nahau zake na kusudio kuu la matumizi ya nahau  ni kuifanya lugha kuwa safi.Neno hili lina asili ya Kiarabu na maana yake ya asili ikiwa ni usafi wa lugha ikimaanisha matumizi sahihi ya lugha.

1 Amekula chumvi nyingi=ameishi miaka.
    mingi
2, Ana mkono wa birika= mtu mchoyo
3.Ametutupa mkono= amefariki, amekufa
4.Ameaga dunia=amekufa, amefariki
5.Amevaa miwani=amelewa
6.Amepiga kite=amependeza
7.Amepara jiko=kaoa
8.Amefumga pingu za maisha=ameolewa
9.Anawalanda wazazi wake =
    kawafanana wazazi wake kwa sura
10. Kawachukua wazazi wake=anafanana
       na wazazi wake kwa sura na tabia.
11.Kawabeba wazazi wake = anawajali na
      kuwatunza wazazi wake.
12. Chemsha bongo = fikiri kwa makini na
       haraka.
13.Amekuwa toinyo=hana pua.
14. Amekuwa popo =amekuwa kigeugeu
15. Ahadi ni deni = timiza ahadi yako
16.Amewachukua wazee wake =
      anawatunza vizuri wazazi
17.Amekuwa mwalimu= yu msemaji sana
18.Amemwaga unga = amefukuzwa kazi
19..Ana ulimu wa upanga=ana maneno
     makali
20.Ameongeza unga = mepanda cheo
21.Agizia risasi = piga risasi
22.Kuchungulia kaburi= kunusurika kifo
23..Fyata mkia= nyamaza kimya
24.Fimbo zimemwota mgongoni=ana
     alama za mapigo ya fmbo mgongoni
25.Hamadi kibindoni= akiba iliyopo
      mkononi]
26.Hawapikiki chungu
       kimoja=hawapatani kamwe
27.Kupika majungu = kumteta mtu kwa
       siri
28.Kumvika mtu kilemba cha ukoka =
      umsifu mtu kwa unafiki
29Kula mlungula /kula rushwa = kupokea
      rushwa
30.Kupelekwa miyomboni = kutiwa au
      kupelekwa jandoni
31.Kujipalia mkaa =  ujitia matatani
32.Kumeza au kumezzea mate = utamani
33.Kumuuma mtu sikio = kumnong'oneza
      mtu jambo la siri
34.Kumpa nyama ya ulimi =
     kumdanganya mtu kwa maneno
     matamu
35.Kumchimba mtu  = kumpeleleza mtu
      siri yake
36.Kutia chumvi  katika mazungumzo  =
      uongea habari za uwongo
37.Vunjika moyo = kata tamaa
38.Kata maini = kutia uchungu
39. Kujikosoa = kujisahihisha
40.Kutia utambi  = kuchochea ugomvi
41.Kumeza maneno  = kutunza siri
      moyoni
42.Kula njama kufanya mkutano wa siri.
43.Kumkalia mtu kitako = kumsema
       au kumsengenya mtu
44.Kupiga mtu vijembe = kumsema mtu
      kwa fumbo
45.Kiinua mgong = malipo ya pongezi ya
      uzeeni bada ya kustaafu kazi
46.Kazi ya majungu = kazi ya kumpatia
      mtu posho
47.Kaza kamba au kaza roho =usikate tamaa
48..Kumwonyesha mgongo = kujificha
49.Kuona cha mtema kuni = kupata
      mateso au kuuliwa kwa kukatwa
      kichwa
50.Maneno ya uwani = maneno yasiyo na
      maana au porojo
51.Mate ya fisi = tamaa kupita kiasi
52.Kata tamaa = vunjika moyo kutokuwa
      na hamu ya jambo fulani.
53. Mbiu ya mgambo = tangazo
54.Mungu amemnyooshea kidole = mungu amemuadhibu
55.Mkubwa jalala = kila  lawama hutupwa kwa mkubwa
56.Mkaa jikoni= mvivu wa kutembea
57.Mungu si Athumani= mungu hapendelei
58.Paka mafuta kwa mgongo wa chupa = danganya
59.Usiwe kabaila  = usichume tokana na jasho la mwingine
60.Usiwe kupe = fanya kazi
61.Usiwe bwanyenye = usichume kwa vitega uchumi vyake.
62. Usiwe na mirija = usinyonye wenzako
63.Utawala msonga= utawala wa wachache
64.Usiwe nyang'au = nchi moja kuifanyia nyingine  ubaya na udhulumati.
65.Usiwe kikaragosi = nchi kuwa kibaraka wa nchi kubwa.
66.Usiwe chui katika ngozi ya kondoo=kujifanya rafiki kumbe ni adui
67.Kutoa ya mwaka =kufanya jambo zuri na la pekee
68.Kumpa mtu ukweli wake = kumwambia mtu wazi ubaya wake.
69.Pua kukaribiana kushikana na uso =kukunja uso kwa hasira
70.Kusema kutoka moyono=kunena kilicho kweli
71.Sina hali= sijiwezi kiuchumi
72.Kupiga uvuvi = kukaa tu bila kazi
73.Kupiga kubwa = kwenda moja kwa moja, kusepa
74.Kumwekea mtu deko = kulipiza  kisasi
Mtu mwenye ndimi mbili = kigeugeu
75.Miamba ya mitishamba =wanga hodari wa kienyeji
76.Kupiga supu = kutegea kazi wengine wafanye
77.Kupiga mali shoka = kugawana  mali au urithi
78. Kula vumbi kuhangaika maisha,  pata tabu kutafuta riziki
79.Mafungulia ng'ombe =muda wa kati ya saa mbili na saa tatu asubuhi.
80.Kutia kiraka =fichia siri
81.Kumlainisha mtu= kumzungumzia mtu maneno matamu mpaka akubali matakwa yako.
82. Kupiga pamba=kuvaa vizuri
83.Kufulia = kuishiwa
84.Umangimeza=uongozi wa kuamrisha watu, udikiteta au uongozi wa imla

Na hizi ni kwa uchache tu, ziko nyingi za zamani na za sasa ambazo sijazielezea kama: kupiga kite, kuondoa kiwi cha macho, kupiga hema, kunawa mikono, nakadhalika.
TIME ya Januari 12, 2004 
Ugonjwa wa sukari umekuwa tishio siku hizi. Ugonjwa huu haushambulii wazee, watoto au vijana tu  bali makundi yote haya yamekuwa yakisumbuliwa na ugomjwa huu.


Tishio hili haliko Tanzania peke yake bali liko ulimwenguni kote Hata hivyo viwango vya kuathirika huweza kutofautiana toka nchi moja na nyingine lakini haipo nchi iwezayo kudai iko salama na tishio la ugonjwa huu.

Ugonjwa huu hauna tiba ila zipo dawa za kumfanya mgonjwa kuishi kwa matumaini na kupunguza athari zitokanazo na ugonjwa huu.

Pamoja na dawa hizi wagonjwa wengi tunashindwa kufuata masharti ya kudhibiti kikamilifu athari zitokanazo na ugonjwa huu katika miili yetu.

HII NI KUTOKANA NA KUTOJUA ATHARI za ugonjwa huu kwetu  PILI KUTOJUA NJIA SAHIHI ZA KUDHIBITI ATHARI HIZI.

Sasa hivi wagonjwa wa sukari tunadanganywa sana na watu kuhusu tiba na kupoteza maelfu ya pesa pasipo na mafanikio.Njia sahihi ni kutumia dawa za hospitali za kuzuia  athari zitokanazo na   ugonjwa huu toka kwa waganga wa mahospitali. Tiba mbadala sahihi  haswa haswa ni vyakula na mazoezi kusaidia hizi  hizi za mahospbinitalini katika kudhibiti athari zitokanazo na ugonjwa huu.

Dawa za hospitalini ziko katika makundi makuu matano.
1.Kwanza zipo za kuchochea kongosho kuzalisha isulin zaidi (Sulfonylureas).
2. Pili ni (Meglitinides) hizi nazo kama kundi la kwanza huishajiisha kongosho kuzalisha insulin
    zaidi
3.Kundi la tatu ni (Biguanides) Hizi hulikataza ini kutoa sukari (glucose) nyingi na husisimua misuli
   kutumia sukari zaidi kutoka katika damu.
4.Kundi la nne linaitwa (Thiazolidinediones) Hizi ni dawa za hivi karibuni tu ambazo huiwezesha
   insulin kusukuma (gulucose) sukari na mafuta kuingia katika misuli kwenda kuzalisha nishati
   mwilini.
5.Kundi la tano ni (Alpha -Glucosidase Inhibitors) hii hufannyia kazi kwenye utumbo mwembamba
   kuzuia mikate na vyakula vya wanga  kubadilishwa kuwa sukari (glucose)

Pili ni vema kujipima kiasi chako cha sukari katika damu  ili kujua kupanda na kushuka kwa sukari katika mwili wako.

Dalili ziashiriazo kuwa na ugonjwa huu za awali ni hizi:
1.Kukojoa mara kwa mara  hasa usiku.
2.Kuona kwa mawengewenge, Macho kupoteza uoni wake wa kawaida.
3.Kuwa na kiu kali isiyoisha.
4.Kuwa na njaa kali kama ya mtoto.
5.Kupoteza uzito kusiko kwa kawaida kwa kipindi kifupi.
6.Kuwa na vidonda visivyopona haraka.
7.Mwili kuchoka kwa hali isiyo ya kawaida.
8.Kupoteza hamu ya tendo la ndoa.
9.Kiuno kuuma hasa ukitaka kusimama.
10.Miguu na mikono kufa ganzi hasa nyakati za asubuhi.
11.Kutopata usingizi mapema na ukilala hutaki kuamka na uamkapo unakuwa umechoka sana.
12.Kupata choo kigumu na huwa hakipatikani kwa wakati wa kawaida.
13.Uzito wa mwili kuongezeka sana na huku huli sana.

Dalili  za ugonjwa huu ni nyingi mno ila za msingi ni hizi hapo juu.Tukiwa wagonjwa wa sukari tunapaswa kushirikiana na kubadilishana uzoefu na njia za kudhibiti athari zake.Hili hakika ni muhimu kulipata kutoka kwa kila mmoja wetu.KUMBUKA UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHDIFU.

Niligundua nina ugonjwa huu toka mwaka 1997 lakini sikuwa na dalili nilizoeleza hapo juu.Tatizo la awali kwangu lilikuwa kuongezeka uzito na kuvimba miguu.Hali hii iliniogopesha nikajihisi  nina tatizo la moyo au figo hivyo nikawaona madakitari na ndipo nilipobainika kuwa nina ugonjwa wa kisukari.

Nilianza kusoma maandiko mbalimbali ya ugonjwa huu na ndipo  nilipo kutana na gazeti la TIME la Januari 12, 2004  gazeti hili lilieleza kwa kina juu ya ugonjwa huu. Waandishi wa makala haya ni Christine Gorman na Kate Noble..Makala yao yalikuwa na kichwa kilichosema "  Why so many are gating Diabetes" Ikiwa na maana KWANINI   KISUKARI KINAWAKUMBA WENGI. Lilikuwa ni swali lilotaka majibu.Humo walieleza kuwa kisuksri hakijapatiwa dawa  kamili na haijulikani kwa hakika  kwanini watu wanakiugua.

Maelezo ya tafiti mbali mbali yalionesha nini chanzo yalitolewa na nini kifanyike kuzuia kupata ugonjwa huu  yalitolewa pia.

Mtindo wa maisha , mazingira  na urithi vilielezwa kuwa ni sababu kubwa za mtu kupata ugonjwa huu.Kwa kawaida kisukari si ugonjwa wa kuambukiza.Ni ugonjwa  ambao mwili unashindwa kutumia sukari kama inavyotakiwa.

Kisukari ni ugonjwa  ambao unaweza  kutambulika kwa namna kuu nne.
1. Kwanza ni kwa njia ya kuangalia kiwango cha sukari  katika damu.Kiwango  sahihi  kisizidi
    m/moll 7  kabla ya kula chochote ndani ya saa 8 hadi 10, Kitaalamu upimaji huu huitwa  FBG
  (Fasting Blood Suger).Kwa kawaida mwili  ukiwa hauna tatizo katika kutumia sukari baada ya
   muda huo lazima sukari katika damu iwe katika kiwango sahihi.Sukari ikiwa zaidi  ya kiwango
   hicho lazima mwili una shida katika kubadili sukari katika damu kuwa nishati.

2. Kipimo cha pili cha kujua mtu ana sukari  au hana ni  (GTT) Glucose Tolerance Test. Kikawaida
    m/moll za mtu asiye na kisukari ni chini ya 7.  Kipimo hiki ni baada ya kula na kutumia sukari,
    Kama baada ya kula na kutumia sukari  kiwango cha sukari katika damu kitaonekana kuwa sukari
    katika damu ni kati ya 7 na 11 m/moll muhusika  atakuwa si mwenye kisukari.

3. Namna ya tatu ya kujua kuwa mtu ana sukari ni kwa njia ya kuona  jinsi 'insulin' inavyogoma
    kufungua 'cell' ili ipokee sukari kutoka katika damu  ikazalishe nishati. Insulin ni homoni
    izalishwayo na kongosho ifanyayo kazi  kama ufunguo wa kufungua mlango.Yaweza ikawa nyingi
    na ya kutosha lakini ikagoma kufungua au ikawa kidogo ikawa haitoshi.Wenye uhaba wa insulini
    mara nyingi ni wale wa aina ya kwanza ya kisukari na wenye nyingi  iliyogoma ni wale wa aina ya
   pili ya kisukari.Kipimo hiki ni kigumu kidogo  katika kupima kisukari kwani  sukari ya mgonjwa
   yaweza kuwa sawa lakini insulini haipo kabisa  ama ipo lakini imegoma kufanya kazi.Kipimo hiki
   kinaitwa (IR) Insulin Resistance.

4 .Namna ya nne ni kuisha kwa sukari mwilini. Hali hii inaitwa (hypoglysomia) Sukari mwilini ikiwa
    chini ya ' mill moll' nne (4) ni hatari hivyo inatakiwa kupandishwa haraka kwa kumpatia mgonjwa
    kitu cha sukari haraka ili kuipandisha.Wagonjwa wengi wa sukari hupoteza maisha sukari yao
    ikishuka sana zaidi ya hapo.

Namna ya kudhibiti ongezeko la sukari ni KUACHA mazoea mabaya ya kunywa pombe kali na za kupitiliza, kula nyama choma kwa wingi, kula chips mayai, kunywa soda sana, kuvuta sigara, kula vyakula viyeyushwavyo haraka tumboni, kutofanya mazoezi na kutunza unene, Ndiyo, wapo wembamba na wana kisukari lakini hatari kubwa ya kupata kisukari iko kwa watu wanene zaidi.Pata maelezo zaidi toka katika clip yangu hii fupi ya dakika saba tu na naomba maoni  yako
Image may contain: 1 person, outdoor

BABU HASSANI SHAGHIRA MTHOO
Eliamini Hassan ALI Salimu Ali Msangi. 
Pata mtiririko wa ukoo wa Salimu Shaghira kutoka kwa BANGALALA kwa Ufupi.
Wasangi ni uzao wa Bangalala aliyetoka huko Kenya sehemu itwayo Usangi miaka mingi iliyopita.Bangalala alizaa watoto wawili Yambii na Mnyatta.
Mnyatta yeye alirudi Kenya.Kwa hiyo habari zake hazijulikani kwa upana.
Yambii akamzaa Mang'a.Mang'a naye akamzaa Ndorokwa.
Ndorokwa akazaa mtoto akamwita jina la baba yake Mang'a. Huyu Mang'a Jr. akamzaa Mahu.
Mahu akamzaa Akavyo..Akavyo akamzaa Kiyanga.
Kiyanga akamzaa Mfuta, Mfuta akazaa watoto wawili Nzano na Setonga.
Sasa hivi nafuatilia uzao wa Setonga.
Yeyote anayejua uzao tokea setonga hadi hapi alipo anipe mtiririko huo.
Wasangi kwa sasa tiko wengi ili uweze kutambulika kuwa wewe ni nani na ni wa baba au ni wa kutoka kwa babuci yupi tunapaswa tuandike majina matatu au zaidi.Jina moja lilkifuatwa na Msang kwa mfano Abdalla Msangi, Ramadhani Msangi, au Adam Msangi halitoshi kukutambulisha kikamilifu.
Sasa, baada ya hilo angalizo, tuendelee na uzao wa Nzano.
Kwa upande wa Nzano yeye alioa wanawake wengi. Kwa jinsi hii akazaa watoto wanne. Ijumbi akiwa ni mtoto wake wa kwanza akifuata Kisarika na Komeja.
Mroki alikuwa mtoto wa nne wa Nzano, na wa mwisho kwa mke wa mwisho.
Ijumbi alizaa ukoo wa kina Senakanga ambao ni kina. Senguji na Bondera.
Komeja akawazaa Mlawa, Mramba, Idhina na Mchaimwa Huyu Mchaimwa alikuwa mwanamke uzao wake ni ukoo wa Saidi Mcholo.
Kisarika akawazaa Kisineni, Nguma,Ishiwa, Mghamba na Kinyonge Kinyonge ukoo wake ni wa kina Chakupewa.
Kisarika, Kisineni, Nguma, Mghamba koo zao ni za kufuatilia sina maeleza yake.
Tukija kwa Mroki mtoto wa Nzano wa mwisho kwa mke mdogo, huyu Mroki alimzaa mtoto mmoja akamwita Mthoo. Mthoo alizaliwa peke yake kama alivyozaliwa baba yake.
Mthoo alizaa watoto watatu Shaghira,Vichike na Nguluma.Vichike alikwa ni mwanamke na alikuwa ndiye mtoto wa kwanza kuzaliwa, akifuatiwa na Shaghira na Nguluma akiwa ni mziwanda.
Shaghira alikuwa mwiisilamu na aliitwa(Ali). Shaghira alizaa watoto wanne Hassaniakiwa wa kwanza akifuatiwa na Salimu, Ibrahimu na Selemani akiwa ndiye wa mwisho kwao.
Salimu akawazaa Ali (Shaghira Jr), Hatibu na Nauche. Huyu ni Nauche ni wa kike na ni kitinda mimba wa babu Salimu aka Kigingi
(Mbishi yakwe Namwai)
Chui aliyezaliwa na Namwai. Namwai ni mama yake.Babu Salimu.Babu Salimu alikuwa akijigamba kwa namna hiyo.
Mimi nimezaliwa na Ali (Shaghira Jr.) Salimu mtoto wa kwanza wa Salimu. Niliitwa Hassani jina la baba mkubwa wa babangu .hivyo mimi ni Hassan Jr
Huyu Hassan ambaye nimeitwa jina lake anaitwa Mthoo jina la babu yake hivyo na mimi ninatwa Mthoo wa tatu. Jina lake jingine la utani (nick name) aliitwa TILISHO.
Na mimi nina watoto Watatu Ali, Riziwani na Hatibu.
Ali ni jina la baba wa babu zangu. Alikuwa kasilimu na alikuwa imamu.
ALI mwanangu ni Ali wa tatu.
HUU NDIO MTI WA UKOO wa Salimu Ali (Shaghira)Mthoo.
KOO NYINGINE HAPO KATIKATI NI ZA KUJAZIA.
SIMULIZI hii nimesimuliwa na Babu Hassan ALi ambaye kwa jina la babu aliitwa Mthoo. Na mimi pia ni Mthoo wa tatu.
Eliamini : Msangi Nawashukuruni nyote mlio like post hii. Kwa kuwa tawi letu limeanzia kwa Nzano, nitaendeleza mtambao wa Wasangi wa tawi hili.Naomba ushirikiano wenu Wasangi wa kwa Nzano na Setonga.
Like · Reply · 1 h
Malaho Omari :Hahahaha weee kaka umenifurahisha sana mimi ni malaho mtoto wa mzee OMARI (SABUNI) wewe tumeachana hapo kwa setonga setonga alimzaa marisa na shanjarika marisa akamzaa Malaho na huyu malaho akamzaa salimu malaho JUMA malaho (babake mshare) Omari malaho...See more
Like · Reply · 1 hr
Eliamini Msangi :VYAKWA KIAMBO TUKO KARIBU SANA NAO, NAMI NITAFUATILIA.wasangi bwana wameenea sana.Omari mshare yule aliyekuwa akiishi Kwakoa.Mzee BONDERA baba yake na JUMANNE NA ERNEST BONDERA.
Chini kushoto ni babu Hassan Ali kulia babu Salimu Ali
Matokeo kidato cha nne mwaka 2016

http://necta.go.tz/matokeo/2016/ftna/index.h

*MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YATOKA*

Baraza la Mitihani nchini(NECTA) latangaza matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2016.
Wavulana wafaulu kwa 73.26% na Wasichana 67%.

*MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YATOKA*

Baraza la Mitihani nchini(NECTA) latangaza matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2016. Wavulana wafaulu kwa 73.26% na Wasichana 67%. Soma

Kujua Shulekidato kumi Bora na kumi za Mwisho bofya link ifuatayo


https://goo.gl/NZWTeW


Nimepoteza   funguo za pikipiki yangu na 'remorte' yake na barua (documents) za kikazi maeneo ya Mkuyuni jijini Mwanza.Yeyote aliyeviokota namwomba anirejeshee. Kunazawadi nzuri. Nipigie kwa Namba+255754366352huu.upotevu umetokea Jumatano ya tarehe. 18-01-2017

Maeneo nilikopita hiyo juzi. Niliipaki pikipiki kwa fundi kwa marekebisho madogo Mkuyuni  Nilichua ufunguo nikapakia daladala   kwenda mijini kwani nilikuwa napeleka form zaHBngu za kustaafu ofisi za PSPF.Nilipotoka PSPF  nilienda Jiji Mwanza kwa kupeleka nakala ya form za form za PSPF nikiwa ofisi za TSD jiji, ndipo nilipobaini upotevu wa funguo  hizo. Nilifuatilia ofisi za PSPF bila mafanikio.Nikafuatilia nilikoacha pikipiki huenda sikuzichomoa nako sikufanikiwa.Nikaamua kubadili 'switch'.

Nikiwa katika harakati za kubadili hiyo 'switch'  nikapigiwa simu kuwa nilipotoa form za PSPF nilisahau juu ya dirisha 'Salary slips' ambazo jioni yake Ida Mangasa jirani yangu aliniletea.

Kasheshe ni hizo nyaraka zangu za kikazi na ufunguo wa 'tank' la mafuta na 'lock' ya pikipiki.

Hizo barua nilikuwa nazo nilipokuwa
nabadili 'switch' hapo Mkuyuni.

Tumaini langu ni kwa wewe mkazi wa Mwanza utakayeusoma ujumbe huu na ukawa umebahatika kuona au kusiki aliyeokota barua hizo au kuona funguo  hizo nisaidie kwa kunirejeshea vitu hivyo kwa kutumia namba ya simu nilotoa hapa ya +255754366352 au ya +255714366352.
Mheshimiwa  Waziri Mkuu Mstaafu  Mhe. Edward Ngoyayi Lowasa ajiunga na UKAWA rasmi mchana huu wa tarehe 28 Julai 2015.

MHE.EDWARD LOWASSA AKARIBISHWA RASMI KUJIUNGA NA UKAWA., MGOMBEA URAIS KUTANGAZWA AGOSTI 4

 Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia (pichani kati) akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar,akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wengine wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),pichani kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe,Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba na wa pili kulia ni Mwenyekitiwa chama cha NLD Dkt.Emmanuel Makaidi.Katika mkutano huo ulizungumzia pia kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Edward Lowassa na Watanzania Wengine wanaotaka kuleta mabadiliko  kuungana kupitia UKAWA ili kuiondoa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MICHUZI MEDIA GROUP. Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano wa viongozi wa Umoja wa UKAWA,uliofanyika mapema leo jijini Dar  Mmoja wa Wahariri wa gazeti la Jamhuri,Deodatusi Balile akitaka ufafanusi kuhusiana na umoja huo wa UKAWA kumkaribisha rasmi Mhe.Lowassa kujiunga na UKAWA,kwenye mkutano wa Wanahabari uliofanyika katika makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar Mmoja wa waandishi mahiri kutoka gazeti la Raia Tanzania,Hafidhi Kidogo aikuliza swali kwa viongozi hao wa UKAWA,kwenye mkutano wa Wanahabari na umoja huo,uliofanyika katika makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar. Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama hicho jijini Dar,akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wengine wa wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),ambapo mkutano huo ulizungumzia pia kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Edward Lowassa na Watanzania Wengine wanaotaka kuleta mabadiliko  kuungana  kupitia UKAWA ili kuiondoa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu,kulia ni Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia na kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe pamoja na Mwenyekitiwa chama cha NLD Dkt.Emmanuel Makaidi (hayupo pichani)  Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama cha CUF,jijini Dar.Mh Mbatia amesema kuwa mtu yoyote ana haki ya kujiunga na UKAWA."Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu,kila chama kilichosajiliwa ni mpinzani kwa mwenzake,watanzania wanahitaji kutengenezewa katiba ambayo itaweka mfumo safi,hivyo mwanzoni mwa mwezi wa nane (wiki ijayo) tutamtangaza  mgombea  wetu kwa mbwembwe,mpaka sasa tumeishapiga hatua ambayo ni nzuri",amesema Mhe.Mbatia katika mkutano huo na Wanahabari.   Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana makao makuu ya chama cha CUF,jijini Dar.Mh Mbatia amesema kuwa mtu yoyote ana haki ya kujiunga na UKAWA."Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu,kila chama kilichosajiliwa ni mpinzani kwa mwenzake,watanzania wanahitaji kutengenezewa katiba ambayo itaweka mfumo safi,hivyo mwanzoni mwa mwezi wa nane (wiki ijayo) tutamtangaza  mgombea  wetu kwa mbwembwe,mpaka sasa tumeishapiga hatua ambayo ni nzuri",amesema Mhe.Mbatia katika mkutano huo na Wanahabari. Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba akipeana mkono na Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe mara baada ya kuzungumza na Waaandishi wa Habari  makao makuu ya chama cha CUF,mapema leo mchana jijini Dar,ambapo kwa pamoja kama UKAWA wamemkaribisha rasmi Mhe.Lowassa kujiunga na umoja huo na kwamba watampa nafasi.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.UMOJA wa  katiba ya Wananchi  nchini (UKAWA) vinamkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa kujiunga katika  na umoja huo pamoja na watanzania wengine katika mapambano ya kuindoa CCM madarakani.


Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Makao Makuu ya Chama cha Wananchi (CUF), kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja huo,Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema wanawalika watanzania wote kujiunga na UKAWA katika kuweza kuleta mabadiliko katika kuhakikisha wanakiondoa Chama cha Mapinduzi (CCM)  katika kuweza kusimamia nchi.
Mbatia amesema kuwa wanamualika Waziri Mkuu  Mstaafu,Edward Lowassa kutokana na kuwa mchapakazi na mfuatilialiaji katika majukumu ambayo anayatoa na uwezo anao katika kusimamia.Amesema  akiingia Lowassa katika umoja huo watashirikiana kwa karibu kutokana na kutambua kuwa ni mhamasishaji  na  ni mtu mwenye kuthubutu.
Aidha amesema kuwa watamsimamisha mgombea  mmoja katika kila nafasi kupeperusha bendera  ya UKAWA katika uchuguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka  huu.

Nae Mwenyekiti wa Chama Cha  Wananchi (CUF),Profesa Ibrahimu Lipumba amesema tuhuma za ufisadi zinazomkabili Lowassa zinatokana na mfumo  uliopo. Amesema  wanatarajia kutaja jina la mgombea Urais Agosti Nne Mwaka  huu  na atapatikana kutokana na taraibu zilizowekwa na umoja huo.
Mbatia hakuweza kuweka wazi kuwa wanamkaribisha Lowassa kujiunga na chama kipi kutokana na ukawa sio chama kilichosajiliwa na msajili wa vyama vya siasa nchini.

Mwenyekiti wa NLD,Dk.Emmanuel Makaidi amesema Lowassa akigombea Urais atamkubali na tuhuma zinazomkabili kiongozi zingekuwa za kweli angepelekwa mahakamani lakini bado yupo na wenye tuhuma wamefikishwa mahakamani .

Katika mkutano wa UKAWA masuali yalilenga kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa kujiunga huko na  tuhuma zake wakati vyama hivyo vilikuwa vikinadi juu ya kutokuwa na usafi na pamoja na uhusikaji katika tuhuma ya mchakato wa  umeme wa dharula kupitia kampuni ya Richmond.


 
Naibu Waziri wa fedha na Mbunge wa Iramba Mwigulu 
Lameck Nchemba ndani ya ukumbi wa Nyerere,
chuo cha Mipango mkoani Dodoma

Leo Jumapili ya tarehe 31/05/2015  Naibu Waziri wa fedha na Mbunge wa Iramba Mwigulu  Lameck Nchemba ndani ya ukumbi wa Nyerere,chuo cha Mipango mkoani Dodoma aweka nia yake ya kutaka kuwa Raisi Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kupitia tiketi ya CCM.


Kauli mbiu ya Mwigulu ni ‘Mabadiliko ni Vitendo Wakati ni Sasa.’
Katika hotuba yake Mwigulu alianza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, wazee, ndugu zake, wananchi wake wa Iramba na wananchi wote waliohudhuria hafla hiyo ya kutangaza nia.

Mwigulu pia amempongeza Rais Kikwete kwa kumuamini na kumteua katika nyadhifa mbalimbali.
Amesema ameamua kutangaza nia akiwa mkoani Dodoma ili kuondoa dhana ya ‘ukwetukwetu’ iliyozoeleka miongoni mwa viongozi wengi.


Akaongeza kuwa Dodoma ni makao makuu ya taifa na chama chake ndiyo maana amefanya hivyo.Na akichaguliwa serikali yake itahamia Dodoma.

Aidha Mwigulu ameeleza mambo matatu yaliyomsukuma kutangaza nia kuwa ni pamoja na:
-Kutaka Mabadiliko
-Kujua mbinu za mabadiliko.
-Utayari wa kufanya mabadiliko.

Kiongozi huyo ameeleza jinsi anavyozijua fika shida za Watanzania na umasikini walionao kwani hajausoma kwenye vitabu bali ameuishi.
Mwigulu ameeleza pia alivyobeba zege baada ya kumaliza chuo kikuu na mke wake akiwa mama ntilie akiwapikia yeye na vibarua wengine wa ujenzi.
Mwigulu awa ni wa tatu ndani ya wana CCM walio jitokeza hadi sasa kutangaza nia.

Leo hii hii  nyakati za saa tano asubuhi hapa jijini Mwanza Mheshiwa Wassira alitangaza nia ya kuwa mmoja wa wanaotarajiwa kuteuliwa na CCM  kugombea Uraisi hapo Octoba ndani ya kumbi maarufu hapa  jijini Mwanza.Kauli mbiu yake ikiwa ni Uadilifu mbele na kusisitizia  siasa za uchumi huria ndani ya falsafa ya Ujamaa kupitia ushirika.

Mwigulu yeye katoka na kauli mbiu ya 'Mabadiliko ni vitendo wakati ni huu.' kama nilivyotangulia kuieleza.

Jana kule Arusha ndani ya viwanja vya Shekh Amri Abeid Mheshimiwa Lowassa alikuja na kauli mbiu ya ; "Elmu kwanza."
Mwigulu toka utotoni mwake wazazi wake wanadhihirisha kuwa ameonesha kuwa na kipaji cha uongozi.Hili limeonekana hadi akiwa shuleni,chuo kikuu mpaka sasa.

Mwigulu anawaomba watanzania na wana CCM kumkubali na akaahidi kuwavusha kufikia uchumi wa kipato cha kati.

Amesema tatizo kuu la nchi  ni rushwa, ubadhirifu na kufanya kazi kwa mazoea. Amewahakikishia watanzaniai kwamba hivyo ndivyo vipau mbele vyake  wakimpa ridhaa ya kuliongoza taifa hili.Kwani anayajua matatizo ya watanzania, amejiandaa na nia anayo.

Aidha aliongezea kwa kusema kuwa yeye amebeba ajenda ya wananchi.na alichokieleza kinatokana na ufahamu wake kwa watanzania na wana CCM. na yuko tayari kuwatumikia kwa moyo wake wote na nguvu zake zote.Akisisitiza kuwa umasikini wa watanzania hakuusoma vitabuni bali ameuishi.

Mwigulu na Familia yake
Shida za maji na madawa anasema ameziishi. Akasimulia kisa cha chumba kilichokuwa kikifumgwa sana wakati wa utoto wao ni chumba cha maji na mtoto aliyekuwa anakunywa maji mara kwa mara alionekana kuwa ni mtoto mkorofi.

Aliendelea kudai kuwa hatakuwa na huruma na uvumilivu  kwa wala rushwa na wahujumu uchumi na atazingatia masilahi ya wafanyakazi.
Kuhusu tatizo la ajira amesema kwa kufufua viwanda ambako vijana watafanya kazi kwa 'shift' kwa hatua hii anaamini itapunguza au kuondoa kabisa tatizo la ajira.

Akisisitizia wajibu wa awamu yake,alieleza mafanikio ya awamu zilizotangulia na mafanikio yaliyopatikana katika awamu hizo.

Alisema awamu ya kwanza  ilifanikiwa katika kutafuta uhuru wa taifa hili  na kujenga misingi ya umoja wa kitaifa na ya pili ilibadili mfumo wa uchumi wa nchi hii na kujenga uwezo  wa watanzania kiuchumi na kupunguza serekali kushikilia njia za kiuchumi kwa asilimia mia moja na kuruhusu kusaidiwa.

Kwa awamu ya tatu akasema  ilijenga taasisi na  mifumo ya huduma za kitaifa. Awamu ya nne imejishughulisha na miundo mbinu, Kujenga rasilimali watu na kujenga misingi ya uchumi wa kisasa.

Akieleza kazi za awamu yake alishauri watu kutompima raisi kwa kile alichofanya kwani hakuna zawadi wanayopewa bali wawapime kwa yale wanayotarajia kufanya.
"Raisi wa awamu ya tano atapimwa kwa kile atakachofanya na si kile alichowahi kufanya."akasisitizia.

Akawabainisha wana CCM na watanzania  wote kuwa yeye  akipewa ridhaa ya kuliongoza taifa hili,afanya mambo makuu matatu, kazi ya kwanza na kubwa kulika zote ni kuipeleka nchi kuwa nchi ya  kipato cha kati na wananchi wake kuwa wananchi wa  kipato cha kati. Kazi ya pili akasema ni kujenga taifa linalojitegemea kibajeti. Kazi ya tatu kuwajenga uwezo wa wananchi wa kumiliki uchumi wao wenyewe.

Akakomelea kwa kusema miaka hamsini ya kuwa taifa ombaoba na la watu masiki hali tunazo rasilimali za kututoa hapo sasa basi ni mwisho.

Kuhusu muungano na ulinzi na usalama wa nchi alisema hivyo vitakuwa pia vipaumbele katika serikali yake.

Kama mpenzi wa michezo,suala la michezo hakuliweka kando. Alimalizia kwa kudai kuwa yako mengi ila kutokana na muda hayo yatatosha kumpima kama anafaa au la.

Aliendelea na suala lake ambalo likuwa kama silaha yake ya mapambano, suala la mazoea."Ukichagua kiongozi kwa mazoea atafanya kazi kwa mazoea na mazoea siku zota ni yale yanayomnufaisha mhusika yeye mwenyewe na si kwa masilahi ya wengi."Mara kadaa alirudia kauli hii.

UKUMBI ULIVYOKUWA UMEJAA.
Taarifa zinadai wako watangaza nia zaidi ya thelathini kutoka kwa CCM peke yake bado hatujaanza kusikia kutoka  vyama vingine. Watanzania kazi kwetu kuwasikiliza na kuchambua upi mpunga kwenye kauli za wanaojinadi hawa na zipi ni pumba.
MWIGULI HAKIKA PAMOJA NA VIJINENO VYA HAPA NA PALE YAELEKEA AKAWA CHAGUO LA WENGI.
Lowassa akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi ya CCM
 mkoa wa Arusha. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM
wa mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole
Jumamosi, Mei,30, 2015
UTANGULIZI:
Ndugu zangu wana-CCM na Watanzania wenzangu,
Hii ni siku muhimu kwangu na kwa nchi yetu. Leo nimeamua kuwaita ili kuwatangazia rasmi Watanzania wenzangu azma yangu ya kutaka kuomba ridhaa ya chama chetu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), niweze kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nasema hii ni siku muhimu kwangu kwa sababu naamini historia yangu itainakili kama ni siku ambayo kwa mara ya pili katika maisha yangu nimejitokeza kuwania kuiongoza nchi yetu kupitia chama chetu. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi hapa nchini nilipojitokeza nikiwa pamoja na Rais Jakaya Kikwete; wakati ule sote tulikuwa wanasiasa vijana. Tulikwenda pamoja kuchukua fomu ndani ya Chama na baadaye tukafanya mazungumzo ya pamoja na waandishi wa habari.Tulileta hamasa kubwa pale tulipofanya jambo ambalo halikuzoeleka kwa Watanzania kwa kutangaza kwamba yeyote atakayepita kati ya wawili sisi basi mwenzake ambaye hatafanikiwa angemuunga mkono.

Ningeweza kujitokeza tena mwaka 2005 lakini nikaamua kwa dhati kabisa kumuunga mkono moja kwa moja Rais Jakaya Kikwete.

 Nikiwa Mwenyekiti wa Kampeni niliwaongoza wenzangu kufanikisha ushindi mkubwa wa mgombea tuliyemuunga mkono na baadaye ushindi mkubwa wa asilimia 80 wa Chama Cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu wa 2005.

Nitaeleza kwa nini nimeamua kujitokeza tena mwaka huu na kwa nini naamini mimi ndiye mtu sahihi wa kuiongoza nchi yetu wakati huu. Mpaka hapa itoshe tu kuwaeleza ni kwa kwa nini naamini leo ni siku muhimu kwangu.

Lakini nasema ni siku muhimu kwa nchi yetu pia. Nasema hivyokwa sababu naamini inajibu wito wa mahitaji ya sasa ya uongozi wa Taifa letu wa kumpata kiongozi imara atakayewaongoza Watanzania kujenga taifa imara. Na hili pia nitalieleza kwa kina.

Hali  ya  Nchi  na  Matarajio  ya  Watu:
Miaka 48 iliyopita katika jiji hili la Arusha, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage alianzisha mchakato wa kujenga taifa huru kiuchumi na kupiga vita maadui umaskini, ujinga na maradhi kwakutumia silaha ya kujitegemea.

Leo hii, wakati taifa likijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu ujao, hatuna budi kutafakari tulikotoka, tulipo na tunapotaka kwenda ili tuweze kubuni upya mikakati ya kuhitimisha azma aliyo kuwa nayo Mwalimu, ili tujenge taifa huru, lenye utulivu, mshikamano, amani na maendeleo.

Nchi yetu hivi sasa inapita katika kipindi kigumu cha mpito katika maeneo yote makuu ya maisha yetu – katika siasa, katika uchumi na katika maisha ya kijamii.

Kisiasa, tumeshuhudia kuongezeka kwa vuguvugu la mfumo wa vyama vingi ambapo ushindani kati ya vyama vya siasa unazidi kuwa mkali na kwa bahati mbaya kufikia sura ya kuonekana kama vile ni mapambano ya watu binafsi badala ya mapambano ya sera na dira ya kuongoza nchi.

Tunashuhudia kuongezeka uhasama binafsi kati ya wanasiasa ndani ya chama kimoja kimoja na pia kati ya wanasiasa wa chama kimoja dhidi ya kingine. Kadiri siku zinavyokwenda, hali inazidi kuzorota na ikiachiwa kuendelea nchi yetu inaweza kujikuta mahali pabaya.

Kukua kwa ushindani ni jambo jema linalokomaza na kurutubisha demokrasia yetu na tukiwa na ushindani wenye afya unaweza kuwa chachu ya kuleta mabadiliko mema kwa wananchi na kupelekea kuongezeka kwa kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi yetu.

Kinyume chake ushindani unaochukua sura ya chuki binafsi au kukomoana na hata kulipizana visasi si ushindani wenye tija na tunapaswa kuutafutia tiba.

Tunahitaji uongozi imara kusimamia kipindi cha mpito kutoka siasa muflisi za aina hii na kuelekea kwenye siasa mpya zinazoimarisha ushindani wenye tija unaojikita katika kushindana katika kuwapatia huduma bora Watanzania.

Kiuchumi, tumeshuhudia ukuaji mzuri na kuongezeka kwa mapato ya ndani ya Serikali na uimarishaji wa mfumo wa uwajibikaji na ulipaji kodi.

 Kwa upande mwengine, Serikali ya Rais BenjaminiMkapa na Rais Jakaya Kikwete imefanya kazi kubwa katika uendelezaji wa sekta ya mafuta na gesi asilia ambapo kiwango kikubwa cha gesi asilia kimegunduliwa.

 Tanzania sasa imekuwa ni miongoni mwa nchi zinazovutia uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo ambayo inatajwa kwamba inaweza kuja kubadilisha kabisa maisha ya Watanzania.

Hata hivyo, kipindi hiki cha mpito kuelekea ujenzi wa uchumi wa kisasa kimeshuhudia kuongezeka kwa hofu na wasiwasi miongoni mwa wananchi kwamba hawatonufaika naukuaji huu wa uchumi na ugunduzi wa utajiri mkubwa wa gesi asilia.

 Kwa upande mwingine, vijana wanataka kuona ukuaji wa uchumi na ugunduzi wa utajiri huo unakwenda sambamba na uzalishaji wa ajira zenye maana ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha yao.

 Niliwahi kusema kwamba tatizo la ukosefu wa ajira likiachiwa bila ya kutafutiwa ufumbuzi imara ni bomu linalosubiri kulipuka.

Vijana wasio na ajira hupoteza matumaini na ni rahisi kughilibiwa kuingiza nchi katika machafuko.Tunahitaji uongozi imara kuweza kuikabili hali hiyo na kuitafutia suluhisho maridhawa.

Kijamii, kipindi cha karibuni tumeshuhudia mabadiliko makubwa ya tabia miongoni mwa raia katika hali ambayo haijawahi kuwa sehemu ya utamaduni wa Watanzania.

 Kumekuwa na ongezeko la kutisha la matukio ya uhalifu linalokwenda sambamba na wananchi kuonyesha wanapoteza imani na taasisi zinazosimamia sheria na usalama na kuamua kujichukulia sheria mikononi mwao.

Kumeripotiwa matukio mengi yakiwemo ya kuvamiwa vituo vya polisi, askari kupigwa na kuporwa silaha, matumizi makubwa ya nguvu katika utatuzi wa migogoro mbalimbali hasa ile ya kijamii, mathalani migogoro ya wakulima na wafugaji, mivutano ya kidini na pia mivutano baina ya viongozi wa dini wenyewe kwa wenyewe na baina ya viongozi wa dini na wale wa Serikali.

 Matokeo yakemshikamano wa taifa nao unaingia majaribuni. Mara nyingine wananchi wanatuuliza viongozi iwapo hii ndiyo nchi tuliyoachiwa na waasisi wetu. Tunahitaji uongozi imara wa kukabiliana na changamoto hizi na kurudisha mshikamano wa taifa letu na watu wake.


Watanzania  Wanataka  Mabadiliko;
Ndugu zangu, mnaweza kujiuliza kwa nini nimeyaeleza yote hayo na yana mahusiano gani na dhamira yangu ya kutangaza nia ya kutaka kuiongoza nchi yetu kupitia CCM?

Nimeyaeleza haya kwa sababu haya na matukio mengine yanayoendelea nchini yamepelekea Watanzania kutaka mabadiliko.

Watanzania wanataka mabadiliko yatakayowawezesha kuzishinda changamoto hizi na kuwaongoza kujenga Taifa imara ambalo kila mwananchi wake anaishi akiwa na uhakika wa mahitaji yake muhimu na papo hapo akijiridhisha kwamba leo yake ni bora kuliko jana yake, na kesho yake itakuwa bora zaidi kuliko leo yake.

 Kwa maneno mengine, Watanzania wanahitaji mabadiliko yatakayowapa uongozi imara unaoweza kuwaongoza kujenga taifaimara. Hii ndio Safari ya Matumaini.

Chama chetu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), na watangulizi wake, TANU na ASP, kimepata bahati ya kuungwa mkono na Watanzania tokea enzi za kupigania uhuru, wakati wa Uhuru wa Tanganyika na Mapinduzi ya Zanzibar, na pia miaka yote tokea Uhuru, Mapinduzi na hatimaye Muungano wetu. Watanzania hawajawahi kushuhudia chama kingine kikiongoza Serikali zetu zaidi ya CCM. Wamekiamini na wanaendelea kukiamini.

 Hata katika yale majimbo machache ya nchi yetu ambayo hatukufanya vizuri katika uchaguzi, ukiangalia kwa undani utaona si kwamba watu wa maeneo hayo wana matatizo na CCM kama Chama bali wana matatizo na baadhi ya viongozi ambao walishindwa kukiwakilisha vyema Chama na kutambua matakwa ya wananchi hao.

Mimi naamini kwamba hata katika kipindi hiki ambapo Watanzania wanaonekana kutaka mabadiliko bado wanaendelea kuamini kwamba watayapata mabadiliko hayo ndani ya CCM.

Lakini kama alivyotupa wasia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi hapa nchini, Watanzania wasipoyapata mabadiliko hayo ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM.

Mimi naamini kwamba CCM tunao uwezo wa kuwapa Watanzania mabadiliko wanayoyataka. Tuwape imani na imani hiyo iwe ni ya dhati na ya ukweli kwamba CCM inao uwezo wa kuwapa uongozi imara wanaouhitaji kwa ajili ya kujenga taifa imara.

Vyama vya siasa vinajumuisha watu na vinaongozwa na watu. Moja ya hulka ya binadamu ni kubadilika kulingana na mahitaji ya mazingira anayoishi.

 Kwa maneno mengine, binadamu ni ‘dynamic’. Kwa sababu hiyo basi, hata vyama vya siasa vinapaswa kuwa ‘dynamic’.

 CCM haijapata kuwa na upungufu wa sifa ya ‘dynamism’. Kwa zaidi ya miongo mitano sasa, CCM (na kabla yake TANU na ASP) iliweza kubadili dira na mwelekeo wake ili kwenda sambamba na mahitaji ya Watanzania ya wakati husika.

Ndiyo maana tumepita katika vipindi tofauti vya mpito kwa mafanikio makubwa licha ya changamoto nyingi zilizotukabili.

Tanzania imeendelea kuwa nchi ya amani licha ya kubadili mfumo wetu wa siasa kutoka ule wa chama kimoja kuja vyama vingi; licha ya kubadili mwelekeo wa uchumi wetu kutoka ule wa dola kumiliki njia zote kuu za uchumi kuja katika uchumi wa soko unaozingatia ushiriki mpana wa Watanzania wa matabaka yote; na hata karibuni kabisa katika mchakato wa kuipatia nchi yetu Katiba mpya.

Tanzania tumeweza kufanya mabadiliko ya uongozi mara nne katika hali ya amani na maelewano, jambo ambalo nchi nyingi za Afrika zimeshindwa.

 Ni imani yangu kwamba tukijikubalisha tunaweza tena kuwapa Watanzania wanachokitaka katika zama hizi za sasa.

 Lakini ni lazima tuoneshe dhamira hiyo kwa dhati ili, kama alivyotuasa Mwalimu Nyerere, Watanzania wasiyatafute mabadiliko hayo nje ya CCM.

Nasisitiza tena kwamba CCM inao uwezo wa kuwapa Watanzania mabadiliko wanayoyataka, lakini pia wananchi wana hiali kuchagua mabadiliko wanayoyataka.

Uongozi  unaohitajika  kuleta  mabadiliko  yanayotakiwa:
Rais Jakaya Kikwete amefanya kazi kubwa katika kipindi chake na kama ambavyo amekuwa akisisitiza mara kwa mara katika hotuba zake za karibuni ni kwamba yeye ametekeleza wajibu wake kwa kuweka misingi imara ya ujenzi wa Taifa la kisasa lenye uchumi madhubuti na unaoweza kukua kwa kasi.

 Amesema anamwachia atakayemkabidhi uongozi wa nchi yetu baada ya yeye kumaliza muda wake kuendeleza pale atakapoachia.

Kwa maoni yangu ili kuifanya kazi hiyo na kuzikabili changamoto nilizozieleza, nchi yetu inahitaji uongozi wenye sifa zifuatazo:

-  Uongozi wenye uthubutu, usioogopa kufanya kufanya maamuzi magumu;
-    Uongozi thabiti na usioyumba;
-    Uongozi makini na mahiri;
-    Uongozi wenye ubunifu na wenye upeo mkubwa;
-   Uongozi utakaozikabili changamoto kifua mbele na siyo kuzikimbia;
-    Uongozi unaoamini katika mfumo shirikishi katika ujenzi wa Taifa;
-    Uongozi unaozingatia muda katika kutekeleza majukumu yake.

Naamini pia kwamba wananchi wanataka Rais ajaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awe na sifa kuu zifuatazo:

-    Aweze kuwaunganisha Watanzania (kukabiliana na viashiria vya migawanyiko ya aina mbali mbali inayoinyemelea Tanzania);

-    Aweze kuja na sera na mikakati ya kuinua uchumi wa Tanzania na kukuza pato la Mtanzania;ikiwemo kupunguza tofauti ya kipato kati ya aliyekuwanacho na wasiokuwanacho;

-     Aweze kuja na sera na mikakati ya kuzalisha ajira kwa vijana wetu;

-     Aweze kutokomeza mianya ya rushwa kwa vitendo;
-    Aweze kuwa mfano wa kuchapa kazi na kuwajibika;
-     Asimamie nidhamu ya matumizi ndani ya Serikali;
-     Aweze kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali;
-     Aweze kutumia fursa yetu ya kijiografia kibiashara

Uongozi  Imara,Taifa  Imara
Naamini kwamba uongozi wa juu wa nchi katika nafasi ya Urais si kazi ya lelemama na unahitaji utashi. Kabla hata ya kutakiwa na wenzako ni lazima kwanza wewe mwenyewe uamini na uwaaminishe wenzio kwamba unao uwezo wa kuwaongoza wananchi wenzako. Na katika hilo, rekodi yako ni lazima izungumze na kulithibitisha hilo.

Binafsi nina hazina ya uzoefu na rekodi njema ya matokeo ya kazi nilizozifanya katika uongozi na utumishi wa umma ndani ya CCM na ndani ya Serikali. Nilianza kazi nikiwa Katibu Msaidizi wa CCM katika mikoa ya Shinyanga, Arusha na Moshi.

 Nimekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu ya CCM. Niliingia Bungeni mwaka 1985 na baadae mzee wangu, Rais Ali Hassan Mwinyi, akaniamini kwa kuniteua kuwa Waziri.

Nimekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Ardhi, Makaazi na Maendeleo ya Miji, Waziri wa Mazingira, Waziri wa Maji na hatimaye Waziri Mkuu.

Miongoni mwa mafanikio ninayojivunia katika uongozi na utumishi wangu, na ambayo Watanzania wanayatambua na naamini wanayathamini, ni pamoja na:

-    Nikiwa Waziri wa Maji chini ya uongozi mahiri wa Rais Mkapa,tulithubutu kushawishi na kuongoza hatua za kukataa kufungika na makubaliano yaliyowekwa na wakoloni ambayo yalikuwa yanazizuia nchi zilizopakana na Ziwa Victoria zisiweze kufaidika ipasavyo na maji ya Ziwa hilo. Leo hii ndugu zangu wa Kanda ya Ziwa wanafaidika na ujasiri wetu katika kukabiliana na suala hilo zito.
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa alieambatana na Mkewe, Mama Regina Lowassa pamoja na wanaCCM wengine.
-    Nikiwa Waziri wa Mazingira, tulipanda miti mingi zaidi kuliko wakati mwingine wowote tokea Uhuru na pia kuwakabili kikamilifu na kuwachukulia hatua waliochafua na kuharibu mazingira.

-    Nikiwa Waziri Mkuu, tulisimamia agizo la Rais Kikwete na kufanikisha utekelezaji wake ndani ya miaka miwili kwa kujenga shule nyingi za sekondari kuliko wakati mwingine wowote tokea Uhuru.

-    Kipindi hicho hicho, tulisimamia agizo la Rais Kikwete la kuanzisha Chuo Kikuu cha Dodoma na kuhakikisha kinakamilishwa kwa wakati. Leo hii Chuo Kikuu hicho ni fahari ya Tanzania.

Tunapomtafuta Rais wa Jamhuri ya Muungano ni lazima tukumbuke kwamba tunamtafuta mtu ambaye atakuwa pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika nchi yetu. Na kwa Chama Cha Mapinduzi tunamtafuta mtu ambaye atakuwa pia Mwenyekiti wa Chama chetu.

Naamini kwa vigezo vyote, nina kila sifa ya kubeba dhamana hizo nzito. Katika mambo ambayo najivunia na sitoyasahau katika historia yangu ni kushiriki kwangu kuilinda nchi yangu pale ilipohitajika.

Nilishiriki kikamilifu katika Vita vya Kagera nikiwa miongoni askari wa mstari wa mbele wa mapambano. Nikiwa Mbunge nilipata heshima ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama. Naamini Watanzania hawatakuwa na wasiwasi wa usalama wao nikiwa Amiri Jeshi Mkuu.

Nimeeleza uzoefu wangu kwenye Chama na huo hauhitaji maelezo zaidi. Ninakijua vyema Chama Cha Mapinduzi kiasi cha kutosha kabisa kukiongoza kama Mwenyekiti wake pale wakati utakapofika.

 Wana-CCM wanajua nikikabidhiwa uongozi, Chama chetu kitakuwa chini ya nahodha madhubuti, mzoefu na asiyeyumba.

Kutokana na rekodi yangu hii, naamini ninazo sifa za kuwaongoza Watanzania wenzangu katika zama mpya za ujenzi wa Taifa la kisasa lenye watu wazalendo walioshikamana na lenye uchumi imara unaomnufaisha kila Mtanzania. Naamini ninao uwezo wa kuwapa Watanzania Uongozi imara kwa ajili ya ujenzi wa Taifa Imara.

Dira  yangu  na  Matarajio  ya  Watanzania
Mfumo tuliojiwekea hapa nchini unaelekeza kila chama cha siasa kinachosimamisha mgombea Urais na kinachowania kuongoza nchi yetu kuja na Ilani ya Uchaguzi ambayo ndiyo inayoweka misingi ya sera zitakazofuatwa na Serikali itakayoongozwa na chama hicho pale kinapopewa ridhaa ya kuongoza nchi.

 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa ni cha kupigiwa mfano katika kutayarisha Ilani bora na ndiyo maana mara zote kimepewa ridhaa ya kuongoza nchi yetu. Tumefanya hivyo tokea enzi za mfumo wa chama kimoja na tumeendelea kufanya vizuri katika mfumo wa kushindanisha sera kupitia vyama vingi.

Najua kwamba Ilani ya CCM ya mwaka 2015 imo katika hatua za mwisho za kukamilishwa na itakapopata baraka za vikao vya Chama itakuwa ndiyo msingi wa utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano itakayochaguliwa Oktoba mwaka huu.

Hata hivyo, naamini pia kwamba mgombea mwenyewe anayetaka ridhaa ya Chama na ya Watanzania kuongoza nchi naye anapaswa kueleza dira yake.

Mimi, baada ya kutafakari kwa kina changamoto tulizo nazo na matarajio na matumaini waliyo nayo Watanzania, naamini kwamba Uongozi imara unaolenga kujenga Taifa imara unapaswa kuwa na dira yenye malengo yafuatayo:

-    Kuimarisha Muungano wetu kwa kuyashughulikia yanayotutenganisha na kuyafanyia kazi ili yasivuruge yale yanayotuunganisha ambayo ni mengi zaidi na makubwa zaidi.

-    Kushughulikia matumizi mabaya ya siasa za udini na ukabila kwa kuimarisha siasa zilizoshiba uzalendo na zenye kutuelekeza kwenye Utanzania wetu.

-    Kujenga uchumi imara na wa kisasa, na ambao ni shirikishi unaomnufaisha kila Mtanzania aliyeko mjini au kijijini. Tunapaswa kubadili hali tuliyo nayo sasa ambapo Kilimo kinaonekana kama kimesahauliwa na wakulima wetu wanaonekana wanakata tamaa.

Wafugaji na wavuvi nao wanahisi sekta zao hazijapewa umuhimu unaostahiki. Tunahitaji kuondokana na hali iliyopo sasa ya kuwa Taifa linalouza malighafi na badala yake kuwa Taifa linalosindika na kusarifu mazao na kutengeneza wenyewe bidhaa zitokanazo na malighafi yake.

Ndani ya miaka mitano ijayo tutahakikishatunaiondolea Tanzania sifa ya kusafirisha malighafi na badala yake kusindika mazao yanayozalishwa hapa nchini kama pamba, kahawa, chai na korosho na kuyaongezea thamani (value addition).Mkakati huu utazalisha ajira nyingi na kuongeza mapato ya fedha za kigeni nchini.

 Tunahitaji kujielekeza kwenye kujenga viwanda na kuleta ajira. Tuna vivutio vingi sana vya utalii lakini bado Tanzania inapitwa na nchi kama Afrika Kusini katika kuingiza idadi kubwa ya watalii.

 Kwa nini nchi kama Dubai iweze kuvutia watalii kwa mamilioni na Tanzania tushindwe? Tunapaswa kukabiliana kikamilifu na hisia zilizopo miongoni mwa wananchi kwamba Tanzania hainufaiki ipasavyo na utajiri wa rasilimali zake nyingi ilizo nazo.

Tutajipanga zaidi kuhakikisha tunanufaika kama nchi na rasilimali zetu kama madini na gesi asilia. Hii ndio Safari ya Matumaini

-    Kukuza kipato cha wananchi na kunyanyua hali za maisha ya watu wetu. Tunapaswa kuhakikisha kuwa ukuaji wa uchumi tunaouzungumzia unamnufaisha Mtanzania aliyeko mjini au kijijini na kwamba hali za Watanzania wa matabaka yote zinanyanyuka na kwamba wanaridhika na kuuona uhalisi wa ukuaji wa maendeleo tunayoyazungumzia.

-    Kuondokana na sifa mbaya ya kuwa Taifa ombaomba. Kwa wingi wa rasilimali tulizo nazo na neema ya ardhi, maziwa, mito na bahari Tanzania tuna kila sababu ya kuacha kuwa ‘bakuli la ombaomba’ na badala yake kuwa ‘mkoba wa neema’ katika Afrika.We can transform our nation from being the begging bowl to become the bread basket of Africa.

- Kujenga mfumo mpya wa elimu unaojielekeza kuwatayarisha vijana wetu waweze kuajirika, kujiajiri na kushindana katika soko la ajira.

Tumepiga hatua kadhaa katika elimu lakini kiwango cha elimu bado ni hafifu. Pamoja na kuwa na shahada (degrees), bado wahitimu wetu hawawezi kushindana kwenye soko la ajira.

Wakati tunazungumzia kuunganisha soko la ajira katika Afrika Mashariki,hatuna budi kujikita kubadili mfumo wetu wa elimu na kuuelekeza kwenye mafunzo ya ufundi na stadi yanayowajenga wahitimu wetu kuwa wabunifu na wenye kujiamini katika kukabiliana na changamoto za maendeleo duniani.

-    Kuhakikisha tunakabiliana ipasavyo na kulipunguza kwa kiasi kikubwa kama si kulimaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama. Ni jambo la kusikitisha kwamba tumezungukwa na mito na maziwa lakini bado watu wetu hawana maji ya kunywa hata ndani ya Dar es Salaam.

-    Kujenga na kusimamia mfumo imara wa kutekeleza sera na sheria tunazozitunga na kuzipitisha kwa lengo la kumtumikia Mtanzania na kumjengea uwezo wa kubadili maisha yake ili tuweze kwenda sambamba na viwango vya kimataifa. Tanzania imepata sera na sheria nzuri sana lakini utekelezaji wake umekuwa hafifu.

Tumekuwa wepesi wa kutunga sera na sheria lakini wazito mno wa kuzitekeleza na kuzisimamia. Uongozi imara wenye kulenga ujenzi wa Taifa imara utahakikisha tunakuwa mfano wa utekelezaji wa sera na sheria tulizo nazo na mpya zitakazotungwa kukabiliana na malengo tuliyojiwekea.

Mambo haya niliyoyaeleza hapa ndiyo yatakayokuwa msingi mkuu wa utendaji wa Serikali nitakayoiongoza pale nitakapopewa ridhaa ya kubeba bendera ya CCM katika nafasi ya Urais na pia nitakapopewa ridhaa ya kuliongoza Taifa letu kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Ramani  ya  Uongozi  Imara  Ninaouamini 9 Leadership Roadmap)
Kama nilivyotangulia kusema, kazi ya kuongoza nchi si lelemama na hasa unapoongozwa na dhamira ya dhati na msukumo wa ndani ya nafsi unaojielekeza kubadilisha maisha ya wananchi wenzako waliokuamini uwaongoze. Kwa vyovyote vile, hiyo haiwezi kuwa kazi ya mtu mmoja. Ni kazi ya pamoja.

 Lakini ili muweze kufanya kazi kama timu moja iliyojipanga kisawasawa kuleta mabadiliko yanayohitajika na ili muweze kweli kutoa Uongozi imara unaojikita kujenga Taifa imara hapana budi kiongozi mkuu anayeongoza timu hiyo aweke ramani anayokusudia kuifuata katika kutoa uongoziimara anaoukusudia yaani ‘Leadership Roadmap’.

Pamoja na kuwa sehemu ya uongozi huko nyuma, kutakuwa na maamuzi na matumaini mapya. Ramani ya uongozi imaraninayokusudia kuutoa kwa wenzangu na ambayo nitaitumia kuiongoza timu yangu katika kuwatumikia Watanzania wenzangu itajikita katika maeneo yafuatayo:

1. Kurejea kwenye Katiba katika kuainisha nia, dhamira na malengo yetu ya kujenga jamii inayozingatia misingi ya demokrasia, udugu na amani. Muhimu katika hili ni kukemea tabia mbaya zinazochochea mfarakano katika jamii kama vile matumizi mabaya ya siasa za udini na ukabila.

Aidha moja ya misingi muhimu ya Katiba ni Muungano wetu. Itakuwa dhamira yangu kuimarisha misingi ya Muungano pamoja na udugu wa damu nahistoria ya ushirikiano iliyojengwa na waasisi wetu, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Amri Abeid Karume na kuyaenzi Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

2. Kujenga fikra mpya za kurejesha kujiamini na kufufua azma ya kujitegemea kama Taifa. Ni dhahiri kuwa pamoja na rasilimali zetu, bado Tanzania ni taifa tegemezi. Bado tunajidanganya kuwa wafadhili watatujengea nchi. Tukumbuke, nchi zinajengwa nawananchi wake.

Nasi pia lazima tujikomboe kifkra na tuondokane na utamaduni wa kuwa tegemezi. Tuanze kwa kujipiga kifua kwa kujiamini kuwa tunaweza kujitegemea na kuijenga Tanzania sisi wenyewe.Kujiamini na kujitegemea ndio uhuru wa kweli.

3. Kujenga uzalendo, uadilifu ikiwa ni pamoja na kuimarisha uwazi katika shughuli zote za serikali na kupambana na rushwa.Watanzania tumepoteza uzalendo kwa kiasi kikubwa. Kuna vitendo vinavyoashiria kuwa hatuipendi tena nchi yetu.

Tunashabikia wizi na rushwa. Inabidi turejee kwenye misingi ya taifa letu misingi ya uadilifu na uzalendo. Tukumbuke kuwa hatuwezi kujenga uchumi wa kisasa kama tutaruhusu rushwa ishamiri.

 Wawekezaji hawataleta mitaji yao kwa wingi kama rushwa itaendelea kutawala katika huduma serikali na wananchi hawawezi kupata huduma bora kama rushwa itaendelea kutawala. Ni lazima tuipinge rushwa kwa vitendo sio maneno.

4. Kujenga Serikali madhubuti, makini na yenye nidhamu inayoendeshwa kwa misingi ya sheria, uwazi na uwajibikaji.Maendeleo ya watu hayawezekani bila serikali kusimamiautekelezaji sera na miradi na kuleta ufanisi katika kutoa huduma na kusimamia maendeleo. Tumekuwa wepesi wa kutunga sera lakini wazito wa kuzitekeleza na kuzisimamia.


5. Kuleta msukumo mpya wa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi katika ujenzi wa uchumi wa kisasa na unaojitegemea. Sekta binafsi ndiyo nyenzo ya uchumi imara. Inazalisha mali, ajira na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa kwa kulipa kodi.

 Ilisekta hii itoe mchango unaotakiwa katika maendeleo ni lazima ifanye kazi na serikali kwa karibu. Tukumbuke, bila uchumi imarahakuna huduma bora!


6. Uwekezaji katika huduma za jamii. Elimu na afya bora, mazingira, makazi safi na maji salama ndiyo mihimili ya maendeleo ya watu.

 Hii inawezekana tu iwapo serikali itakuwa na sera na utashi wa kuutambua uboreshaji wa huduma za jamii kama ndiyo lengo kuu la maendeleo ya nchi. Serikali nitayoiongoza itahakikisha kuwa kila Mtanzania anapata elimu bora na inayogharamiwa na serikali kama mimi na wenzangu tulivyopata.

Wakatitunazungumzia kuunganisha soko la ajira katika Afrika Mashariki, hatuna budi kurekebisha mfumo wetu wa elimu na kuuelekeza kwenye mafunzo ya ufundi na ustadi yanayowajenga wahitimu wetu kuwa wabunifu, wenye kujiamini, wenye uwezo kushindana katika soko la ajira na wa kujiajiri. Napenda kusisitiza kuwa elimu ndiyo muhimili wa maendeleo, ndiyo mkombozi wa kweli wa binadamu. Mimi ni mfano hai wa ukombozi wa elimu.

Elimu ndiyoimenivusha kutoka kijijini kwetu Ngarash na kunipa upeo wa kitaifa. Mama akiwa na elimu atajua umuhimu wa kumpeleka mwanae shule, anapata lishe bora na chanjo stahili na kuwa anaishi katika mazingira safi. Elimu ndilo jibu la umaskini, maradhi na ujinga.Taifa lililo elimika ni taifa lenye maendeleo.

7. Kujenga uchumi shirikishi unaolenga kuondoa umaskini.Mkakati wa kuondoa umaskini Tanzania lazima ujikite kwenye nguzo za ushiriki wa kila Mtanzania katika uchumi wa taifa.

Kwa misingi hii, tukiweza kupunguza umaskini, tutaweza pia kupunguzatofauti za kipato ambazo tukiziacha ziendelee kukua kwa kiasi cha sasa, zinaweza kuhatarisha utulivu na amani katika jamii yetu.Uchumi shirikishi ndio silaha dhidi ya umaskini.

8. Kuimarisha ulinzi wa nchi na usalama wa raia na ujirani mwema.Itakuwa nia yangu kuimarisha misingi iliyojengwa kulinda na kudumisha umoja na amani nchini.

Kadhalika, nitahakikisha kuwa usalama wa mipaka ya Tanzania unaimarishwa kwa misingi ya ujirani mwema na kutanzua migogoro na matatatizo yoyote na nchi jirani, kwa njia ya diplomasia na mazungumzo.
Gari iliyombeba Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa ikipita nje ya uwanja wa Sheih Amri Abeid
, jijini Arusha mapema leo asubuhi wakati akielekea
kwenye ofisi za CCM mkoa wa Arusha.

Hitimisho:
Hii ndiyo misingi na dira ya uongozi wangu. Nachelea kusema kuwa haitakuwa kazi rahisi. Lakini kwa ushirikiano wa kila mmoja na maamuzi magumu, yote yanawezekana.

 Tumeona nchi nyingi zilizosimamiwa na utawala thabiti wa serikali za kimaendeleo zikikabili na kupunguza umaskini katika kizazi kimoja. Kama mataifa mengine yamefanikiwa, tena bila raslimali kama zetu, kwa nini sisi tushindwe?

Tuna kila sababu ya kufanya maamuzi magumu sasa ili kuwajengea Watanzania matumaini mapya ya maendeleo. Naomba nisisitize kuwa katika uongozi wangu hakutakuwa na nafasi ya majungu, na visasi. Hatutaangalia nyuma bali tutasonga mbele kwani ndicho Watanzania wanakitarajiakutoka kwa uongozi uliojengwa kwenye misingi bora.

Ndugu Watanzania:-
Ni maono yangu kuwa siku si nyingi nchi yetu itaanza safari yenye uelekeo wa matumaini na neema tele kwa wananchi.

Ni maono yangu kuwa siku si nyingi sisi kama Watanzania kwa umoja wetu tutajivunia kuishi katika nchi tunayoipenda na inayoendeshwa kwa misingi ya utawala bora, chini ya serikali ya kimaendeleo iliyojengwa kwenye fikra mpya za uzalendo, uadilifu, utendaji na uwajibikaji.

Ni maono yangu kuwa Peke yangu sitaweza, lakini kwa maamuzi magumu na ushirikiano wa kila mmoja wetu ikiwa ni pamoja na wagombea wenzangu ndani ya CCM, inawezekana kuanza safari hii ya Matumaini Mapya.

Kabla ya kumaliza hotuba yangu hii fupi, kuna mambo matatu ningependa kuyaweka wazi hapa.

La kwanza, linahusu msingi wa uongozi ninaouamini na ambao nimeusema mara kadhaa hapa. Msingi huo ni UWAJIBIKAJI.Watanzania wananifahamu mimi si mtu wa maneno, ni mtu wa vitendo. Naamini kwa dhati kabisa kwamba huwezi kuwa na Uongozi imara utakaoweza kusimamia ujenzi wa Taifa imara iwapo huna ujasiri wa kuwajibika. Mimi nimeongoza kwa mfano, na pale ilipobidi, nilikubali kuwajibika na kubeba dhamana ya uongozinilipojiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu.

La pili, mimi si mtu wa visasi. Siamini katika kuangalia ya nyuma. Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Na kwa nini tuangalie nyuma wakati kama taifa tuna kazi kubwa sana mbele yetu inayohitaji kufanywa? Mimi ni Mkristo; najifunza kutoka kwa Bwana Yesu ambaye alipoulizwa: “Nisamehe mara ngapi?” Alijibu, “Samehe mara sabini mara saba”. Nitaenzi na kudumisha utamaduni huu wenye sura ya utu na heshima.

La Tatu, natambua kwamba dhamana ya Urais ni shughuli nzito hasa kwa taifa ambalo lina changamoto nyingi. Nataka niwahakikishie Watanzania wenzangu kwamba afya yangu ni njema kuweza kuwatumikia katika jukumu hili zito. Pamoja na vijineno vinavyosemwa pembeni, mimi mwenyewe ndiye ninayejijua zaidi. Nawahakikishia kuwa nisingekuja hapa leo na kueleza nia yangu hii ingekuwa sina uhakika na afya yangu.

Natoa RAI kwa Chama changu cha CCM, nadhani umefika wakati kwamba tutende tofauti na mazoea, watu wote walioonyesha nia ya kutaka kuongoza, liundwe jopo la madaktari wa ndani na nje ya nchi tupimwe afya zetu, kwa hili najitolea kuwa wa KWANZA KUPIMWA afya yangu

Safari tuianze leo, hatuna kesho nyingine.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

HABARI ZIHUSIANAZO NA HII.

  • Mwanakijiji wa jamii forum na wanao muunga mkono wadai 'LOWASA' Hauziki kwa undani wake  bofia hapa.
  • Kwenye jamii forum hiyo hiyo mjadala wa Raisi yupi kati ya KIKWETE, NYERERE, MWINYI na MKAPA anaongoza kwa kuwapima kwa  criteria za:- 1. Maendeleo ya watu 2. Maendeleo ya Vitu 3. Umoja wa Kitaifa na  4. Muungano wetu. Maoni mbalimbali yametolewawa,kuyapata  kwa undani wake bofia hapa
  • Ushawishi wa wachungaji wazaa matunda.KWA UNDANI pata video hii. 

Pata habari za jijimwanza BURE (weka anuani yako ya barua pepe hapa)

POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza