Malaika BendI ya Muziki wa Dansi ya Dar es salam Yatinga jijini Mwanza.

Chtistian Bella na Ommy Dimpoz katika video ya
                       'Nani kama Mama.'
Mwanza- Bendi ya muziki wa dansi ya Malaika iliyo na masikani yake jijini  Dar es salaam, jana Mei 31 ilikuwa Jijini Mwanza kwa ajili ya kutoa burudani kwa mashabiki wa jiji hili.

Mratibu wa ziara hii, Meneja wa burudani wa Villa Park Resort ya hapa Jijini Mwanza Ramadhani Maganga amesema kwamba, ziara ya Bendi hii imeratibiwa kwa mashirikiano ya  Villa Park Resort na Alpha Hoteli ya mkoani Geita.

Ratiba ya ziara hii ilianza juzi Ijumaa 30,Mei Mjini Geita .

“Wakazi na mashabiki wa Mji huo hakika walishuhudia sauti yenye mvuto ya mwimbaji mahiri Christian Bela wa kundi hili la wana  Malaika bendi lakini pia walipata fursa ya kuzisikia 'live' nyimbo zao na ufundi wa wapigaji vyombo na wacheza 'show' wakali.

Burudani hizi zilipambwa na Rapa mkali 'Totoo ze Bingwa' pale ndani ya Omega Resort,” alisimulia meneja huyu.

Maganga alisema jana Jumamosi ya Mei 31 2014 ilikuwa ni zamu ya wakazi na mashabiki wa Jiji la Miamba ya Mawe (Rock City) ambapo bendi ya Malaika ilitoa burudani ya uhakika ndani ya Villa Park Resort ambapo Bela ambaye hujiita Rais wa Vijana alifanya makubwa.

Christian Bella akiimba wimbo wa 

         'Nani kama Mama'


“Bela aliutambulisha 'live' wimbo wake mpya unaotamba kwa sasa katika Radio, TV na Kumbi za burudani wa “Nani kama Mama”  pia aliwashukuru  mashabiki wa muziki wa dansi kwa kuwaonesha Tuzo yake aliyoipata hivi karibuni ya Kilimanjaro Music Award (KMA) 2014."Meneja wa Villa alifafanua.

Akaongezea kuwa walipokuwa hapo  Villa walisindikizwa na Bendi ya Super Kamanyola ya hapa Jijini Mwanza.

Aidha baada ya kutoka jijini Mwanza, bendi hii ya Malaika inatarajiwa kuhitimisha ziara yake hapa Kanda ya Ziwa kwa burudani ya kufa mtu katika Mji wa kibiashara na Madini wa Kahama.

Huko Kahama wanatarajiwa kupiga muziki katika Ukumbi wa Social Club.

Itakuwa  ni mara yao ya  kwanza kabisa wana Malaika Band kufanya ziara  kama hii Mkoani humo.

Haya wananchi na mashabiki wa muziki wa dansi msikubali kusimuliwa. Fikeni kujionea burudani ya uhakika kutoka kwa wanamuziki wa bendi hii.

Imebainishwa kwamba maeneo yote watakayotoa burudani mashabiki watalazimika kulipia kingilio cha Sh. 10,000/= tu.

Imedhihirishwa kwamba usalama utakuwa wa kutosha.
Ulinzi wa mali za watakaofika ni asilimia 100. 

Inatarajiwa kuwa hakutakuwepo na usumbufu wowote kwa watakaohudhuria burudani hii .

Inasisitizwa kwamba. watoto chini ya miaka 18 hawataruhusiwa kuingia kwenye show hizi.

Pata wimbo huu wa 'Nani kama Mama' hapa.
BOFYA HAPA

0 comments:

POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza