Mlipuko wa Kinachodhaniwa ni Bomu, Arusha Night Bar, Jumapili 13, Aprili 2014..

Baadhi ya wananchi waliofika eneo la mlipuko
kutaka kujua na kushuhudia kilichojiri
 (picha na http://arusha255.blogspot.com/
 )
Juzi Jumapili, Aprili 13, 2014 kulitokea mlipuko wa kinachodhaniwa kuwa  ni bomu la kutengeneza  katika baa moja jijini Arusha ambayo ni maarufu kwa maonesho ya mechi za mpira wa miguu  ligi za Ulaya,

Baa hii inaitwa Arusha Night Park au kwa jina maarufu  'Matako Baa' maeneo ya Mianzini, mkoani humo.

Mlipuko huu  umejeruhi zaidi ya watu 20. Wengi wa majeruhi ni wahudumu katika baa hii na wateja waliojazana kushuhudia mechi za soka.ligi ya Ulaya kwenye baa hiyo.

Majeruhi walikimbizwa hospitali za Mt Meru na Dr Mohamed kwa matibabu. Hadi sasa hakuna taarifa rasmi ya mtu aliyepoteza maisha ingawa baadhi ya walionusurika wanashuhudia kuwepo watu waliokatika miguu.

Taarifa ya awali kutoka Jeshi la Polisi inaeleza kuwa bomu hilo ni la kutengenezwa kienyeji baada ya kukuta vipande vya vyuma na misumari eneo la mlipuko.

Aidha taarifa zaidi zinaeleza kuwa bomu hilo lililetwa  kwenye mfuko wa plastiki na mtu asiyejulikana na kuwekwa humo katikati ya mashabiki hao..

Jeshi la Polisi mkoani humo limesema uchunguzi wa kumsaka mtu aliyeweka bomu hilo unaendelea.

Tazama video hii hapa chini kupata maelezo na taarifa zaidi kutoka kwa Mganga wa haspitatli ya Mt Meru,wahudumu na kwa Msemaji wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha


           Mlipuko wa Bomu, Arusha Night Bar, Jumapili 13, Aprili 2014..

0 comments:

POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza