Kweli Diamond Platinum Kadhihirisha Kuwa ni mkali wa wakali,

Dimond Siku Aliyokuwa Akipokea 
zawadi Katika Sindano la KMTA Awads -2014
KWELI kijana Diamond Platinum ni mkali wa wakali, tena ni sukari ya warembo hasa masuperstar wetu wa kike.

Wengine humwiita raisi wa wasafi. Ni kijana huyu huyu ambaye ana 'make headline' kila koona ya Tz na Africa kwa ujumla.. 


"Platinuuuuuum...ebhana jamaa anajua, sio kwamba tu namsifia la hasha..nimepata kusikiliza nyimbo yake mpya hii iliyovuja sijui inaitwa nini vileee sijui kitorondo mwanzoni nilipoona 'title' ya kitorondo nikadharau ndo madudu gani ayo tena jamaa anaimba.


Lakini daah!!!! Namsifu mchizi anajua kusoma nyakati. Anajua ni aina gani ya muziki autoe utakaoendana na nyakati zilizopo.

 Kama mtakumbuka kuna kipindi 'kwaito' zilitamba sana. Mchizi akatupia nyimbo zake za 'style' iyo iyo akakomba mashabiki kibaaao. Saivi 'kwaito' inaishia ivo mchizi kasoma nyakati tena akaibuka na mtindo huu sijui ni mnanda sijui mchiriku mi sielewi, ila 'all in all' nyimbo taamu balaa, 


Nyimbo inachezeka, tena kalenga haswaaaa kuleeee kwa watoto wa uswazi kule kwenye vigodoro ambavyo kila mtu anafahamu siku izi vigodoro ndo mpango mzima. 


Daaah, kwa 'style' hii Diamond atakaa sana kwenye 'peak' ya 'game' hili. 


Wasanii wengine mjifunze kutoka kwake. Someni nyakati." Maneno haya siyo yangu ni ya MKWELI WA MAMBO, mmoja wa wenye kurusha habari kalikali ndani ya Jamii Forum


Maneno yake haya yalipokelewa kwa hisia tofauti tofauti toka kwa wana Jamii Forum. Kama kawaida ya jukwaa hili la JF wako waliomuunga mkono na wako walioponda maneno yake wakidai jamaa ka 'Copy'  na ku 'Paste' kazi ya Nurdin ft Alsay. 


Wakatokea waliodai kuwa si kweli kwa sababu Kitorondo ya Platinum ilitoka kabla ya Kitorondo ya hao wawili.


Ukweli mimi binafsi namuaminia kijana huyu Platinum. Mimi najua Wabongo haya ndio maneno yao ya kila uchwao hasa kwa mtu anayeinukia kimaendeleo.


Nimezisikiliza nyimbo hizi mbili za wasanii hawa ambazo zina jina hili la kufanana la  Kitorondo. 


Wimbo wa Nurdin ft Alsay na Diamond Platinum ni kweli zina jina la kufanana na zimechezwa kwa mahadhi ya kufanana yaliyoko katika mtindo wa Kigodoro.


Hivi ukiitwa Baraka na mwingine akaitwa Bakari ni mzazi yupi hapo kakopi na kupesti kwa mwingine.

Swali la kujiuliza hapa ni mbona tuliwahi kupagawizwa hapa siku si nyingi na muziki wa wanamuziki kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao ulikuwa katika mtindo wa Kwasakwasa na Nzawiza.


Pamoja na hali hiyo iliyotukumba muziki wao hii ulikuwa ukifanana kiasi cha kutoweza kubainisha wimbo wa bendi moja na nyingine.


Istoshe bendi kadhaa hapa nchini zilizovuma zilipiga nyimbo zao kwa mtindo huu huu pia.

Jambo la muhimu hapa ni wanamuziki wetu kwenda na wakati kama alivyodokezea 'Mkweli wa Mambo'.


Hivi mwana muziki aliyepiga muziki wake kwa mtindo wa Kwasakwasa, Hip Hop, Rn B, Rumba, Zuku, Chacha, Mchiriku na kadhalika nani hapo atakuwa kamwiga mwingine.


Hii ni mitindo tu.Yeyote aweza kupiga muziki wake kwa mtindo autakao.Upekee na ubunifu wa msanii uko zaidi katka ujumbe, maudhui na mdundo.


Sasa sikiliza kazi hizi za wasanii hawa na wewe uamue ubishani huu wa  ku 'Copy'  na ku 'Paste.' 


1. Nurdin feat Alsay.
2. Diamond Platinum.

Jikumbushe mambo yalivyokuwa wakati wa (KTMA AWARDS) 

( DIAMOND  PLATNUMZ- KTMA AWARDS)BEST WRITER OF THE YEAR)


0 comments:

POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza