MV Matala yazama katika Ziwa Victoria Katikati ya Visiwa vya Kerebe na Lukolu

.
Sehemu ya meli hii iliyokuwa ikizama
 Jumamosi ya , Aprili 18, 2014\ taarifa za watu 10 kunusurika kufa maji katika ziwa Victoria baada ya meli ya mizigo MV Matala kupinduka na kuzama ikiwa na shehena ya sukari zasikika

Sukari hii ilinunuliwa kutoka katika kiwanda cha sukari Kagera Bukoba na  ilikuwa inasafirishwa  kuja jijini Mwanza.

Meli hii ambayo inamilikiwa na kampuni ya Mkombozi  Fishing and Marine Transport Limited, imezama ikiwa na magunia 5600 ya sukari sawa na tani 280.

 Meli  hii ni mali ya mfanyabiashara wa jijini Mwanza aitwaye V.H.Shah,

Mkurugenzi wa kampuni hiyo Gitano Chacha Munanka ameeleza kwamba meli hiyo imezama ikiwa katikati ya visiwa vya Kerebe na Lukolu majira ya saa 10.30 usiku wa kuamkia Jumamosi na kuongeza kwamba hakuna mtu yeyote aliyejepoteza maisha kufuatia tukio hilo.

kituo cha IT  na Star TV vimeelezea  kuzama kwa meli hii na kongezea kuwa juhudi za wafanyakazi wa kampuni hiyo kuipindua zinaendelea bila mafanikio,

huku baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakisema chanzo cha meli hii kuzama ni kutokana na dhoruba kali .

Watabiri wa hali ya hewa wamekuwa wakitoa ushauri kwa wamiliki wa vyombo vya majini lakini kumekuwa  na kutozingatia utabiri unaotolewa na mamlaka hii ya hali ya hewa hapa nchini.

Kungekuwa na mazingatio ya utabiri huu unaotolewa na mamlaka hii huenda kungesaidia  kuepusha nchi na maafa haya yanayojitokeza nchini hivi sasa.



Sehemu inayo onekana  pichani ni sehemu ya meli iliyozama, ambayo ilianza safari yake ya kutoka Bukoba majira ya saa 7 mchana, ikiwa inaendeshwa na kapteni Erick Lasana.
Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra kanda ya ziwa, imethibitisha kuzama kwa meli hiyo yenye uwezo wa kubeba tani 280 za mizigo na abiria 100.

0 comments:

POLL

Which structure of government do you prefer to be implemented in Tanzania?
  
pollcode.com free polls 

TOA MAONI YAKO HAPA (NI BURE)

Name

Email *

Message *

Copyright © 2014 Hii Wiki jijini Mwanza